Jina lake halisi anaitwa William Henry Gates, III ingawa wengi wanamjua zaidi kama Bill Gates. Kwa mujibu wa Mtandao wa Forbes na Jarida la Bloomberg Billionaires List, Bill Gates ndiye tajiri namba moja duniani kwa mwaka 2014.
Yafuatayo ni mambo kumi ambayo huyajui (au unayajua lakini nakukumbusha) kuhusu bilionea huyu.
1. Kwa mara ya kwanza, alitangazwa kuwa bilionea mwaka 1987, akiwa na umri wa miaka 32 tu, akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.25.
2. Bill Gates alianza utundu wa kuchezea vifaa vya kielektroniki akiwa na umri wa miaka 13. Amewahi kusimamishwa masomo kwa kuharibu kompyuta shuleni.
3. Licha ya kufaulu kwa kiwango kikubwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Havard, Bill Gates alisoma kwa kipindi kifupi tu, akaacha chuo na kuelekeza nguvu kwenye kubuni programu za kompyuta.
4. Kabla hajaoa, Bill Gates amewahi kuingia kwenye orodha ya mabachela wasafi zaidi na wanaojua kutunza nyumba zao.
5. Amelelewa katika maadili ya kidini, alianza kupelekwa kanisani na wazazi wake tangu akiwa mdogo na anaendelea kufanya hivyo mpaka sasa. Ni Mkatoliki.
6. Watu wake wa karibu huwa wanamlalamikia mara kwa mara kutokana na tabia yake ya kutopokea simu akipigiwa au kutumiwa meseji. Hata mkewe huJmlaumu kwa tabia hii.
7. Amewahi kukamatwa na kutupwa selo kutokana na kukutwa na hatia ya kuendesha gari kwa spidi kubwa.
8. Ni shabiki mkubwa wa wasanii Bruno Mars na Lady Gaga. Anaweza kuuimba wimbo wote wa I Wanna be a Billionaire wa Bruno Mars.
9. Amepanga kwamba akifa, wanaye watatu wasirithi hata senti tano yake, badala yake utajiri wote ugawiwe kwa watu maskini. Anasisitiza kuwa lazima wanaye wajitafutie fedha zao.
10. Eti anachukia kuwa tajiri kwa sababu anashindwa kuishi maisha yake halisi. Anatamani kuwa mtu wa kawaida.