UGIMBI/KOMONI KIBURUDISHO MURUA CHA KABILA LA WAHEHE

Ugimbi au Komoni hunywewa Vilabuni, mashambani na majumbani kwa watu wa rika mbalimbali, mfano watoto, watu wazima na watoto ikibidi. Pia ugumbi/komoni hutumika kama kiburudisho kwenye misiba, sherehe na mikutano. Ugumbi kama vinywaji vingine, huwa na wapenzi wake. Mtu yupo tayari kukataa kunywa, soda, bia, au Ulanzi na kuamua kutumia Ugimbi au Komoni.
Ugimbi au maarufu Komoni huwapo na watu maalum waliojaliwa kuonja Ladha ya Ugimbi kama ni Mtamu au la. Hawa waonja Ugimbi hujipatia umarufu kutokana na kuonja kwao pombe hii. Na mara nyingi hupewa fursa ya kuonja Ugimbi/Komoni sehemu mbalimbali.
Ugimbi ukishapatikana baada ya kuchujwa, machicha yake huhifidhiwa kwa matumizi mengine ya kupata Kileo kinachofanana na Ugumbi. Machicha ya Ugimbi hulowekwa na maji kwa muda kadhaa na kisha huchujwa vizuri. Yale male yanayopatikana baada ya kuchunjwa hayo machicha, hujulikana kama MACHORO. Ladha na thamani ya machoro hutugea ubora wa Komoni au Ugimbi uliokuwa umepikwa mwanzo.

Makala hii itaendelea wiki ijayo. Hapo juu ni picha ya Babu ambaye anajiburudisha na Ugimbi. Je unajua hii ni lita ngapi? Pia jiulize, machicha ya pombe yakichujwa bado yanaweza kutumika kama Pombe karibu Iringa ujaribu?
Kipindi kijacho, tutaangalia makala nyingine ya Pombe inayoitwa, Kihambule na namna inavyoandaliwa? Usisahau kuwa pia kuna Ulazi, Wanzuki na mengine mengi.

No comments:
Post a Comment