Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Friday 18 December 2015

SALAAM ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA



Mimi Adam Alphonce Kivenule, kwa heshima na taadhima, naomba nitumie fursa hii kuwatakia Heri ya Christmas  na Mwaka Mpya 2016.

Najua ni kwa neema za Mungu tu ndio maana nimepata fursa ya kuundika ujumbe huu wa kuwatakia kila kheri katika mwisho huu wa mwaka 2015.

Natumaini, Mungu awabariki wote.

Asanteni,

Adam Kivenule
0713 270364
kivenule@gmail.com

Ndugu Mwinuka (kushoto) na Ndugu Adam Kivenule (kulia)
 

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA 11 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)


Adam Kivenule, Katibu Mkuu-KAUKI

Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa kushirikiana na Kanda ya Nduli, kwa heshima kubwa unapenda kuwajulisha ndugu, jamaa, marafiki na Wana Ukoo wote, umeanza maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika Kijijini Nduli, Mkoani Iringa, tarehe 2 had 3 Julai, 2016.

Kwa taarifa hii, tunaomba Viongozi wote wa KAUKI na Viongozi wa Kanda, kuanza kujiandaa kwa Mkutano huo muhimu. Sambamba na hilo, Viongozi wa KAUKI waendelee kuratibu maandalizi ya Mkutano kwa kusambaza taarifa na kuweka mikakati imara ya kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI unafanikiwa. Wadau wakuu wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI ni Viongozi wa Kanda kwa kushirikiana na ndugu wote.

Ikumbukwe kuwa, mwaka huu (2015), Mkutano wa Mkuu wa KAUKI uliopangwa ufanyika Kijijini Irore, Mkoano Iringa, umeshindwa kufanyika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Maana nyingine Kanda ya Irore bado inayo nafasi nyingine ya kuandaa Mkutano Mkuu wa 12 wa KAUKI, 2017. Kwa hiyo wana Irore na sehemu zote za Igominyi mnaombwa kuanza kufanya maandalizi ya mkutano wenu, sambamba na maandalizi ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Nduli mwakani.

Kuna mambo mengi muhimu yanaweza kufanyika kama sehemu muhimu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika Kijijini Nduli:
1. Kila ndugu kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI na kuhakikisha kuwa unafanikiwa. Kila mwana ukoo anaweza kujitoa kwa chochote kile ambacho kitasaidia kufanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI.
2. Ndugu wenye uwezo kujitolea ili kufanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI. Kuna wana Ukoo ambao wamejiajili na wana vipato vya uhakika. Tunaomba kwa moyo wa upendo wasaidie kuandaa mkutano huu. Pia kuna ndugu ambao wameajiliwa na wana vipato vizuri. Tunaomba wachukue jukumu la kusaidia kugharama za maandalizi ya Mkutano huo.
3. Wana Ukoo wa Kanda ya Nduli na Kanda nyingine ambazo zina fursa ya ardhi, wanaweza kulima angalau nusu ekari kwa lengo la kupanda mazao ambayo yatatumika kwa ajili ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI. Mazao ambayo yanaweza kupandwa ni pamoja na Mahindi, Maharage, Viazi na mazao mengine ya nafaka.
4. Kuhamasishana na kuhimizana ndugu na wana ukoo miongoni mwetu ili kuendelea kuwa na moyo wa kupendana, kushirikiana na kusaidiana; na pia kuwa pamoja katika masuala yote yanayohusu ndugu na ukoo kwa ujumla kwa faida yetu wote.
Matarajio ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika tarehe 2 – 3 Julai, 2016, Kijijini Nduli.
Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI unatarajia yafuatayo:
1. Kuendelea kuboresha Kitabu cha Wana Ukoo kwa kujaza taarifa mbalimbali za ndugu (Clan Organization Tree).
2. Kuwafahamisha wana ukoo, Historia na Chimbuko la Ukoo. Hususani Ukoo wa Kivenule.
3. Mwingiliano wa Ukoo wa Kivenule na Koo nyingine uliopelekea kuwepo kwa Ukoo wa Kivenule.
4. Kufanya tathmini ya mipango mbalimbali ya KAUKI tuliyojiwekea kwa miaka kadhaa.
5. Kutathmini changamoto na vikwazo mbalimbali vinavyoukabili Umoja wetu.
6. Yatakayojiri katika Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika tarehe 2 – 3 Julai,

Imeandaliwa na kusambazwa na:

Katibu Mkuu (Adam Alphonce Kivenule)
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
Mobile: 0713 270364
            kivenule@gmail.com




Wednesday 16 December 2015

KUMBUKUMBU YA MAHAFALI YA KUAGANA WABUNGE MWAKA 2015

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa wabunge pale walipohitimu masomo yao kwa kufanya mahafali ya kuagana wao wenyewe na wanachuo wenzao, yaliyofanyika katika chuo hicho. Kwa kutambua ushirikiano wao katika maisha ya chuo hapo, wabunge na wanachuo walipiga picha mbalimbali kama sehemu ya kumbukumbu. 

Zifuatazo ni picha za kumbukumbu katika mahafali hayo:
 
Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika ngazi za ukumbi wa mikutano wa Auditorium


Mhe. Mwinuka na Ndugu Kivenule katika picha ya pamoja

Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzao

aheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzao

Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzao katika ngazi za ukumbi wa Auditorium

Waheshimiwa Wabunge wakiingia ukumbini

Waheshimiwa Wabunge wakiwa Morogoro Road

Mhe. Mwinuka na Kivenule wakitoka jengo la Utawala wa Chuo hicho
Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzao

MATUKIO YA KUKUMBUKANA NA BAADHI YA WANACHUO WENZANGU

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa Wabunge (viongozi wa wanachuo) pale walipofanya sherehe ya kuagana huku wakiwashirikisha wanachuo wenzao. Sherehe hiyo haikuweza kuwaalika viongozi wa Serikali ya Wanachuo kwa kile kilichodaiwa kutowajibika ipasavyo katika utendaji wao, pamoja na malalamiko kadhaa ambayo yalielekezwa kwenye uongozi huo.

Mwadili wa Chuo alikuwa mmoja wa waalikuwa na alihutubia warsha hiyo, huku akipiga picha ya pamoja na Wabunge. 

Yafuatayo ni matukio katika picha:
Waheshimiwa Wabunge wakiwa wamesimama mbele ya Ukumbi uliopo katika Library ya Chuo hicho.

Waheshimiwa Wabunge wakiwa na Mgeni Rasmi, Mhe. Mwadili wa Chuo (aliyechuchuma na baadhi ya wabunge) katika bustani ya Chuo

Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja, katika garden ya Chuo

Waheshimiwa Wabunge: Kutoka kushoto ni Emanuel Sulle, Jose Mniko (Spika) nyuma, tatu nyuma, Mwinuka, Rajabu, David, Adam Kivenule, Malunguja na James

Waheshimiwa Wabunge wakiongozana na Mgeni Rasmi (Mwadili wa Wananchuo) kuingia katika ukumbi wa sherehe

Wednesday 2 December 2015

Kuhusu UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

Kuhusu UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

FASILI YA KAUKI

KAUKI ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii inayounda umoja huu; hususani katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga, maradhi na utegemezi.

 

Kuanzishwa kwa KAUKI kuliambatana na maandalizi yaliyojumuisha mikutano zaidi ya 10 ya mashauriano iliyofanyika sehemu mbalimbali Jijini Dar es Salaam na Kidamali, Iringa.

 

Dira ya KAUKI

Kuwa na jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa kujitegemea.

 

Maono ya KAUKI

Kujengeana uwezo kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia mafunzo, kongamano, mijadala na mikutano ili kuboresha maisha.

 

Malengo ya KAUKI

Lengo Kuu

Kuinua na kuboresha maisha ya wanaukoo wa Kivenule, kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa kutumia ujuzi, maarifa na raslimali zinazotunguka.

 



--
Adam Kivenule
P.O. Box 3255,
Dar es Salaam
Mob. +255 713 270364
E-mail: kivenule@gmail.com / KAUKI2006@gmail.com
Blog: www.adamkivenule.blogspot.com
Twitter: www.twitter.com/kivenule

Sunday 29 November 2015

Wise words

He will choose you, disarm you with his words, and control you with his presence. He will delight you with his wit and his plans. He will show you a good time but you will always get the bill. He will smile and deceiveyou, and he will scare you with his eyes. And when he isthrough with you, and he willbe through with you, he will desert you and take with himyour innocence and your pride. You will be left much sadder but not a lot wiser, and for a long time you will wonder what happened and what you did wrong. And if another of his kind comes knocking on your door, will you open it?-From an essay signed "A psychopath in prison

Thursday 26 November 2015

Dondoo 10 muhimu sana kwa walezi /Wazazi na Wazazi watarajiwa wote

Dondoo 10 muhimu sana kwa walezi /Wazazi na Wazazi watarajiwa wote

1. Mkanye mtoto wako wa kike na hata wa kiume kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.

2. Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.

3. Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao "Mchumba", "Mke wangu" au "Mme wangu".

4. Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu na wengine wana maambukizi....

5. Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwendakwa mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.

6. Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.

7. Mwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za sirimwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo.

8. Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.

9. Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.

10. Usipende kumruhusu mwanao kulala na housegirl au houseboy au mgeni. Huwezi jua tabia za watu na wanayomtendea usiku!!!!

AROBAINI YA MAREH. LILIAN IGNAS KIVENULE


AROBAINI (40) YA MAREHEMU LILIAN IGNAS KIVENULE

Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya familia ya Ignas Kivenule na Mme wake Mareh. Lilian Kivenule, inatumia fursa hii kuwafahamisha ndugu, marafiki na jamaa wa karibu, kuwa Arobaini ya ndugu yao mpendwa itakuwa tarehe 05 Desemba 2015.

 

Arobaini hiyo inatarajiwa kufanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu, Buyuni – Chanika, Mkoani Dar es Salaam. KAUKI na Familia ya Ignas Kivenule kwa pamoja, wanawaomba ndugu, jamaa, marafiki na umma kwa ujumla kujumuika nao siku hiyo.

 

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe, AMINA.

 

Imetolewa na kusambaza na:

 

Adam Kivenule

Katibu Mkuu – Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)


--
Adam Kivenule
P.O. Box 3255,
Dar es Salaam
Mob. +255 713 270364
E-mail: kivenule@gmail.com / KAUKI2006@gmail.com
Blog: www.adamkivenule.blogspot.com
Twitter: www.twitter.com/kivenule

Thursday 5 November 2015


TANZIA

Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya wana ukoo wa Ukoo wa Kivenule, inatoa pole na masikitiko kwa msiba wa ndugu yao Lilian Ignas Kivenule, aliyefariki usiku wa tarehe 31 Oktoba 2015 na kuzikwa siku ya tarehe 02 Oktoba katika Makaburi yaliyopo Buyuni Chanika, mkoani Dar es Salaam.


Kuondoka kwa Lilian Kivenule kumeacha pengo kubwa kwa ukoo wa Kivenule, hususani familia yake na wazazi wake. Ni kifo cha ghafla na hakikutegemewa.


Kama Ukoo na KAUKI tunasema hiyo ni mipango ya Mungu. Kilichobaki ni kumwombea ili aweze kupumzika kwa amani.

Rest in Peace Lilian..

Kama wana Ukoo na KAUKI kwa ujumla, ndugu, jamaa na marafiki tutakukumbuka daima.

Asante,

Imetolewa na:

Adam Alphonce
Katibu - Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)


Thursday 6 August 2015

MakalaLowassa tusamehe tuliokuhukumu, nikiwamo mimi Fred Mpendazoe

Toleo la 4175 Aug 2015

NIMEONA ni vema niandike makala hii baada ya kupigiwa simu nyingi sana na wasomaji wa Raia Mwema baada ya Edward Lowassa kuhamia Chadema. Wengi wameomba maoni yangu na wengine uchambuzi.Katika makala hii mimi nitaeleza maoni yangu tu. Nilikuwa nimeanza kuandika makala juu ya tabia ya unafiki ya wana CCM ambao kila mara hunukuu maandikokadhaa ya Hayati Mwalimu Nyerere kwenye hotuba zao kwenye majukwaa na mikutano ya kisiasa lakini ukiwaambia wahame CCM wanakataa kata kata. Mimi nilikuwa najiuliza hawa wanamuenzi vipi.Wakati wa huduma ya Nabii Issa ilipokuwa inafikia ukingoni, siku moja Nabii Issa alikamatwa akawekwa gerezanikutokana na mpango uliokuwa umeandaliwa kwa muda mrefu na mafarisayo na masadukayo ambao wengi wao walikuwa ni viongozi wa dini.Kwa kifupi, falsafa za Nabii Issa zilikuwa zinapingana na mwenendo wa mafarisayona masadukayo wakati ule. Humo gerezani au rumande Nabii Issa alikutana na Barnaba ambaye alikuwa amefungwa kwa ajili ya tuhuma za wizi au ufisadi.Kama ilivyokuwa desturi wakati ule, Pilato alitakiwa atoe hukumu kwa Nabii Issa. Pilato aliangalia tuhuma za Nabii Issa na alibaini tuhuma hazikuwa na ushahidi, hivyo akataka amwache huru. Pilato aliwauliza wale watu waliokuwa wamekusanyika kwamba amwachie nani kati ya Barnaba na Nabii Issa. Umati uliokuwepo pale ukiongozwa na mafarisayo na masadukayo walipiga kelele kwa nguvu, wakisema amwachie Barnaba! Hivyo, Barnaba akatolewa gerezani kwa shinikizo la umati wa watu.Sababu iliyosababisha mafarisayo na masadukayo na Wayahudi wengine wamtake Pilato amwachie Barnaba ambaye walikuwa wanajua ni mwizi au fisadi ni tabia yao ya unafiki. Tunaambiwa mafarisayo na masadukayo walikuwa na elimu ya kutosha, elimu ya dini na elimu ya kawaida.Pia walijihesabia haki ya kupitiliza. Tatizo kubwa la mafarisayo na masadukayo ilikuwa unafiki, yaani kuishi maisha ambayo yalikuwa tofauti na walivyokuwa wakihubiri na tofauti na elimu waliyokuwanayo. Walikuwa ni wanafiki kupindukia.Mafarisayo walikuwa wakipita barabani wakisali sala ndefu ili waonekane. Kwenye masinagogi walikaa viti vya mbele. Walipotoa sadaka makanisani, walitoa fedha nyingi kwa kuonekana ili wasifiwe.Walipokuwa wakisali, walisali kwa sauti kubwa ili maneno yao yasikike, walipangilia sala zao vizuri kwa ufasaha ili wasifiwe. Lakini, maisha halisi ya mafarisayo na masadukayo yalikuwa ni machafu, yaliyojaa ufisadi. Mahubiri ya Nabii Issa yaliwakasirisha sana mafarisayo na masudukayo kwani aliwekawazi unafiki wao.Walikataa mahubiri yake. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu kuu ya kumtaka Barnaba atolewe gerezani na kumkataa nabii Issa. Lakini kwa kumkataa nabii Issa, Israel inasumbuka mpaka leo.Ndani ya CCM, kuna kundi la wana CCM wazee ambao wanatambua kwamba CCM imefika mwisho, imechoka, imekosa mwelekeo na imepoteza sifa na heshima ya kuendelea kuongoza nchi. Wana CCM hawa wamekuwepo ndani ya CCM toka wakati wa hayati Mwalimu Nyerere.Wanatambua tofauti ya CCM ya leo na CCM ya Nyerere. Wazee hawa katika majukwaa mbalimbali wanaikosoa sana CCM na serikali yake. Je ni nini tofauti ya wana CCM hawa na mafarisayo wa Uyahudi waliomtoa Barnaba gerezani?Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kuwaambia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, na baadhi ya wazee ninaowazungumzia walikuwepo nanukuu "Watanzania wanataka mabadiliko. Wasipoyapata, wasipoyaona ndani ya CCMwatayatafuta nje ya CCM". Baada ya kuwaambia maneno haya, wajumbe wengi wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwemo wazee wetu walishangilia sana.Sijui kwa nini walishangilia, kwani tafsiri yamaneno haya ni kwamba kama CCM itashindwa kuleta mabadiliko basi Watanzania watayatafuta mabadiliko hayokwenye vyama vya upinzani. Aidha, HayatiMwalimu Nyerere aliwahi kusema, na wazee hawa walikuwepo "Bila CCM madhubuti nchi itayumba".Ni bayana kwamba CCM ya leo siyo imara tena. Na ni dhahiri nchi yetu imeyumba kutokana na uongozi legelege wa CCM. Kwani chama legelege huzaa serikali legelege.Ninaamini pasipo shaka yoyote Nyerere angekuwepo leo asingekuwa mwana CCM.Angekuwa upinzani au raia asiye mwanachama wa chama cha siasa. Lakini siyo CCM ya leo. Lakini, wazee hawa kila mara huwa wanasema wanamuenzi Mwalimu Nyerere. Lakini tujiulize, kwa lipi?Wanamuenzi kwa kuendelea kuwa wanachama wa CCM iliyochoka na kuacha misingi yake? Wanamuenzi kwa kuendeleakuwa wanachama wa CCM na serikali yakeinayonyanyasa wakulima na wafanyakazi?.Ikiwa CCM si madhubuti tena wanategemea nini tena wakati ni bayana mabadiliko hayataletwa na CCM? Au nao wazee hawa ni mafarisayo wa Uyahudi? Au wanayoyahubiri kwenye majukwaa si yale wanayoyaishi? Ipo siku waliyoyaficha kwa siri sana yatakuwa hadharani. Lakini ninawasihi wazee wetu, njia ya heshima ya kumuenzi Mwalimu Nyerere siyo kubaki CCM. Nawasihi watoke CCM.Ninafahamu kwamba tuna mitazamo tofauti ya mawazo. Dhamira zetu pia hazilingani na hatuna sare za mawazo kwa wakati wote. Nitumie mfano kufafanua suala la wale ambao wamebaki ndani ya CCM ambayo imeyumba hususani wazee waliofanya kazi na Nyerere.Tunamfahamu Musa kwenye Maandiko Matakatifu. Inaelezwa kuwa alipokuwa mtu mzima alikataa kuitwa mwana wa binti Farao, akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na wana wa Israeli kuliko kujifurahisha kwa kitambo kwenye Ikulu ya Farao, ambaye alikuwa anawanyanyasaWaisraeli na ndugu zake. Musa aliondoka kwa Farao, ikulu iliyojaa neema.Ndani ya CCM kumechafuka. CCM na seriklai yake inawanyanyasa Watanzania. Ni jambo la kushangaza kuona wazee waliofanya kazi na Hayati Mwalimu Nyerere wanaona fahari gani kuendelea kukaa kwenye chama ambacho kimeacha misingi yake.Wengine wameendelea kubaki humo na mnawasikia wakipiga kelele kwamba wanaonewa. Ni rahisi kwa mtu yeyote kufikiria kwamba maslahi yao binafsi ni muhimu kuliko kuwatetea wananchi. Msanii maarufu wa Ufaransa, Cocteau, aliwahi kusema: "Ni hulka ya jamii nyingi kunyamazisha sauti huru za wapenda haki. Kwanza, zitajaribu kukushambulia kwa kukupiga. Hilo likishindikana kukunyamazisha, zitajaribu kukuua kwa kukuwekea sumu. Hilo, nalo, likishindikana, zitamalizia kwa kukumwagia sifa, heshima, tuzo na vyeo".Inawezekana tuzo na vyeo ndiyo sababu ya kuendelea kubaki CCM. Wako wapi leo wapambanaji 11 wa ufisadi mliowasikia mwaka 2008 na 2009? Wengine ni mawaziri, wengine ni manaibu waziri, wengine ni viongozi kwenye CCM.Ni nini tofauti yao na mafarisayo wa Uyahudi waliomtoa Barnaba gerezani?. Lakini pia wapo waliondelea na mapambano.Lowassa alikuwa mwana CCM aliyekulia na kutumia muda mwingi wa maisha yakeakiwa CCM. Lowassa aliipenda CCM na aliipigania. Namfafananisha Lowasaa na Saul Mwebrania, msomi wa kupindukia aliyekuwa anaupenda mfumo wa kiutawala wa wakati huo na akaupigania kama Lowassa alivyoipigania CCM na serikali yake.Kwa kifupi, Sauli alikuwa ni mmoja wa viongozi ambao walikuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa sera na mipango ya serikali ikiwemo kuhakikisha wafuasi wa Yesu au Wakristo wanadhibitiwa na hata kuangamizwa.Siku moja Sauli akiwa katika kutekeleza maagizo ya kuwatesa Wakristo alikutana na muujiza ambao matokeo yake ulisababisha Sauli abadili msimamo na hatimaye akawa moja ya wahubiri wakuu wa injili ambayo alikuwa akiipinga. Kwa neema ya Mungu, Sauli aliweza kubadilika.Wakati wa kumkaribisha Lowassa Chadema, Mwenyekiti wa Chadema alisema ilikuwa si kazi rahisi kumshawishi Lowassa kujiunga na Chadema. Kwa maoni yangu nasema Lowassa kuhamia Chadema ni kwa neema ya Mungu na binadamu yeyote asije kujisifu.Nawakumbusha tena, ndani ya CCM kuna kundi la wana CCM wazee ambao wanatambua kwamba CCM imefika mwisho, imechoka, imekosa mwelekeo imepoteza sifa na heshima ya kuendelea kuongoza nchi.Wana CCM hawa wamekuwepo ndani ya CCM tangu wakati wa hayati Mwalimu Nyerere. Wanatambua tofauti ya CCM ya leo na CCM ya Nyerere. Wazee hawa katika majukwaa mbalimbali wanaikosoa sana CCM na serikali yake, lakini ukiwaambia ondokeni huko hawaelewi wanasema watafia humo.Ukiwauliza kwa nini wanasema wanamuenzi Mwalimu. Ukiwauliza kwa lipi? Hawana la kujibu. Naamini ipo siku Neema aliyoipata Lowassa nao wataipata na hatimaye wataihama CCM na hapo watakuwa wanamuenzi Mwalimu kwa uhalisia.Sauli alipoanza kuihubiri injili aliyokuwa akiipinga awali watu wengi walishangaa sana na hata baadhi ya Wakristo walimnyanyapaa. Ndivyo ilivyo kwa Lowassa. Wapo wana Chadema hawakubaliani na Lowassa kuhamia Chadema. Wanalalamika. Lakini tukumbuke kwamba kule mbinguni huwa ni sherehe mwenye dhambi mmoja akibadilika.Malaika mbinguni hawalalamiki kwa mwenye dhambi kuhama kutoka ufalme wa giza kwenda ufalme wa Mungu, hushangilia. Lowassa amebadilika, wana Chadema tumpokee.Lowassa kuhama CCM ni muujiza, ni kwa neema sawa na Sauli wa Tarso kuiamini injili aliyoipinga. Hata kama alikuwa mchafu kiasi gani, yeye ameikana CCM na mambo yake yote, tumpokee. Kumbukeni,Sauli aliyewatesa Wakristo ndiye ambaye ameandika nyaraka nyingi na kuwafanya Wayahudi wengi waiamini Injili.Sauli ambaye alikuja kuitwa Paulo alifanyakazi kubwa zaidi kuliko mitume walioanza na Yesu. Biblia inasema wa kwanza atakuwa wa mwisho, na Katiba ya Chadema inasema mwanachama wa Chadema aliyeingia miaka 20 iliyopita na aliyejiunga mwezi mmoja wote wana haki sawa, hivyo kama Lowassa anazo sifa za kuipatia Chadema ushindi agombee urais na wanachadema tumuunge mkono.Namfahamu Lowassa kwa muda mrefu, nimefanya kazi naye kwa miaka minane pale Wizara ya Maji. Ana sifa moja kuu, ni jasiri. Nilikuwa mbunge wakati alipopata kashfa ya Richmond.Niliiamini Ripoti ya Kamati Teule ya Bungeiliyoongozwa na Dk. Felix Mwakyembe Mwakyembe kama Watanzania wengine walivyoamini na kumhukumu. Lowassa ameeleza hahusiki, aliwajibika kisiasa.Tumwamini. Marafiki za Lowassa watakaohamia Chadema wafanye ungamo lao na wapimwe imani yao.Lowassa ana kazi moja kubwa inayohitaji neema tena. Anatakiwa kuwasamehe kwa dhati wote waliomhukumu na mmoja waoni mimi kwa makala zangu kali. Lakini pia Lowassa amshukuru Mungu kwa Kamati Kuu ya CCM kuliondoa jina lake, kwani hapo ndipo mpango wa Mungu ulikuwa unatimia kwa yeye kuwa mgombea urais jambo ambalo lisingewezekana ndani ya CCM.Kumbukeni Josefu aliuzwa utumwani Misrina kaka zake. Josefu aliumia sana. Lakini ilibidi awasamehe kaka zake waliofanya mpango wa kumuuza. Lakini Josefu ilibidi auzwe utumwani ili aje kuwa Waziri Mkuu wa Misri. Lowassa amepitia misukosuko na mambo mengi magumu sana, ninaamini ni kwa ajli ya kuandaliwa kwa kuwatumikia Watanzania. Jina la Lowassa liliondolewa na watu waliokuwa ni wa karibu na yeye, marafiki zake, viongozi wenzake. Dhahabuili iwe na thamani kubwa hupitishwa kwenye tanuru la moto mkali.Naiona ndoto aliyonayo Lowassa ya kuwa rais inatimia. Tumuunge mkono.