Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Monday 29 October 2012

Mikasa ya Soko Kuu la Mwanjelwa

Ni mwaka wa tatu sasa toka Soko la Mwanjelwa lianze kujengwa upya baada ya ajali ya moto iliyowapatia hasara kubwa wafanyabiashara wa Mbeya kwa kuunguliwa bidhaa na mazao mbalimbali ya biashara, yaliyokuwemo katika soko hilo.

Wengi wao walitarajiwa kuwa ujenzi wa soko ungeenda haraka kutokana na umuhimu na mahitaji makubwa ya soko hili kwa wakazi wa Mbeya, mikoa ya karibu na nchi jirani za Zambia na Malawi.

Hali imekuwa tofauti kwa sababu sasa ni mwaka wa tatu tangu ujenzi uanze huku shauku kubwa kwa wafanyabiashara ikilitaka liishe mapema na waingie kuendeleza biashara zao.

Mkoa wa Mbeya ni Jiji linalokua kwa kasi na matarajio wengi kuboreka kwa miundo mbinu na masoko ya biashara kama kichocheo cha uchumi.

Je, pamoja na jitihada mpya ya kulijenga soko hili, je litaweza kumudu majanga ya moto ambayo yamekuwa yakilikumba soko hilo mara kwa mara. Hili ndilo swali kubwa ambalo linapaswa kuulizwa na kila mmoja wetu mpenda maendeleo. Tusubili tuone mara baada ya kukamilika na kuanza kutumika.

Zifuatazo ni baadhi ya picha zilizopigwa kuonesha ujenzi wa Soko la Mwanjelwa ukiendelea....









The Wonder of Mount Kilimanjaro







































Mount Kilimanjaro

Resources Abundance Versus Poverty Paradox



Tanzania is a resource-rich country with abundant gold (2,222 tones of proven reserves), natural gas (33 trillion cubic feet of proven reserves), uranium (35.9 million pounds of proven reserves), coal (1.5 billion tones of proven reserves), diamond 50.9 million carat of proven reserves), to mention only a few extractive resources in the country. Tanzania had since 2009 implemented EITI during which the country has produced two reports; February 2011, and Jun 2012. The latter awaits EITI International Secretariat Review.









Wise Words



When something serious is going on silence is a lie, if you know the truth and you keep quiet you are a liar too. If you do not know your right you have no right. Tanzanians we do not need good infrastructure anymore we need justice first.

Friday 19 October 2012

POLISI CHANZO CHA AJALI NYINGI ZA BARABARANI



Sio washauri wazuri, wamejikita kwenye rushwa tu



Nimekuwa nikitafakari mlolongo wa ajali ambazo zimekuwa zikipurura maisha ya watu katika eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya kwa wiki sasa, tokea ajali mbaya iliyogharimu maisha ya watu zaidi ya kumi wiki iliyopita. Ni masikitiko makubwa kwa sababu watu wale hawakupaswa kuondoka mapema hivi. Hata ule usemi wa mipango ya Mungu nashindwa kukubaliana nao kulingana mazingira ya ajali hiyo.

Kwa wale mnaopenda kuperuzi habari mbalimbali zinazotokea hapa nchini, mtakumbuka kuwa, siyo ajali ya mara ya kwanza kutokea katika eneo hilo, huku ikihusisha mlolongo wa magari na wafu bila hata serikali kutoa suluhu la wimbi la ajali ambazo zinaendelea kutokea katika eneo hilo.

Si ajabu ukasikia ari na amri ya kuwasihi wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kununua vipuri bora na vya kisasa na pengine kuwasisitiza kununua magari yenye ubora! Lakini huku nyuma, wenye mamlaka ya udhibiti wa ubora wa bidhaa mbalimbali mfano binadhaa na vyakula (Tanzania Bureau of Standard-TBS) au wale wenzetu wanaosisitiza ubora wa huduma katika tasnia ya dawa na vyakula (Tanzania Food and Drugs Authority-TFDA) ambao juzi juzi tu wamerasimisha dawa feki za ARV zitumiwe na ndugu zetu wanaopunguza makali ya VVU, na kisha kuendelea kusisitiza kuwa siyo dawa feki. Hii dhiyo taswira halisi ya Tanzania tuliyonayo sasa.

Kama wenye mamlaka wanakiuka maadili ya taaluma zao na maadili ya kazi na kuendelea kuangamiza Taifa, je kwa huyo mmiliki wa vyombo vya usafirishaji, anayesutwa anunue vifaa/vipuri bora kwa ajili ya magari afanyeje? Ni dhahiri kama nchi tupo katika janga kubwa la kuendelea kuathirika na majanga mbalimbali ya kibinadamu.

Ukimwuliza mkazi wa Mbalizi kuhusiana na wimbi la ajali ambazo zinatokea katika eneo hili, atakuambia kuwa jambo la kawaida kwa sababu ni kila wakati na kila mwaka ajali mbaya na za kutisha zimendelea kushuhudiwa zikitokea mahali hapo.

Lakini tujiulize, kuna yeyote asiyejua changamoto za miundombinu katika Mabonde ya Ufa. Kwa mfano eneo la Senkeke na Salanda katika Mkoa wa Singida; safu ya milima ya Lukumbulo barabara ya kwenda Songea; Mlima Kitonga mkoani Iringa, Wami Pwani na Nyang’olo Mtera, Iringa. Je, kuna yeyote ambaye hujui kuwa katika kingo za bonde la ufa huwa na miinuko na miteremko mikali ambayo huathiri miundo mbinu ya barabara na reli? Ni dhahili kwa wanataaluma na wakandarasi wanayafahamu haya. Sijui kama wenzetu polisi, hususani wale wa kitengo cha usalama barabara kama hufikiria tatizo la miundombinu katika maeneo yaliyopitiwa na bonde la ufa.

Lakini pia kuna tatizo Kubwa la mlolongo na mlundikano wa matuta barabarani (makubwa na madogo, yenye mtetemo mkubwa sana na wa kati, yenye ncha kali na  umbo lisiloeleweka) ambayo yameendelea kuharibu magari pamoja na vipuri vyake. Ni kwa bahati mbaya gari iliyohusika imeteketea kabisa. Pengine tungeweza kuona athari za matuta katika vipuri vya gari hilo toka lilipoanza safari yake hapa jijini Dar es Salaam. Mathalani, mifumo ya breki si imara kama wengi wetu tunavyodhani. Ipo macho ‘Sensitive’, inaitika haraka ‘responsive’ na inawajibika ipasavyo ‘reactive’ pale inapoposwa kufanya kama inaelekezwa. Kupita kwenye tuta za kina umbile kunachangia kwa kiasi kikubwa kuvuga mifumo ya breki kwa kusababu kupasuka kwa mirija (pipes) za upepo au vinginevyo ambayo inahusika na mifumo ya breki, pengine ndiyo ikawa chanzo cha ajali nyingi zinazoendelea kutokea. Kwa kifupi, ajali za matatizo ya mifumo ya breki kwa magari makubwa imekuwa ikiongezeka mara kwa mara.

Mimi binafsi nilishuhudia kwa macho yangu busta za upepo wa breki kwa matairi ya nyuma kwenye basi zikipasuka pale Mbuga ya Wanyama Mikumi, baada ya basi kukanyaga matuta na hivyo kusababisha gari kukosa breki. Na safari iliishia pale kwa sababu kulikuwa hamna namna nyingine. Kuna mifano mingi ambayo imenikuta mwenyewe ikiwemo nyingine kuchomoka kwa boti upande wa kushoto wa gari ndogo na hivyo kupelekea breki kupatikana kwa shida.

Pengine wenzetu hufikiria zaidi kukamata, kutisha na kupokea rushwa tu, na si mambo ya kitaalam. Tukubaliane kuwa sera yao ni kushurutisha tu. Sioni mantiki ya sababu zao za kila mara inapotokea ajali, ‘uzembe wa dereva’, ‘mwendo kasi’.

Mazingira ya ajali ya Mbalizi, kwa asilimia 90 linasababishwa na miundombinu finyu (yaani inayobana) ambayo haiwezi hata kidogo kumpa fursa, dereva wa gari ya aina yeyote ambaye atapatwa na tatizo la mifumo ya breki ya gari kushindwa kufanya kazi. Ni dhahiri kabisa, kama breki zitashindwa kufanya kazi, huna jinsi kulingana na barabara ilivyo na mazingira halisi ya kuweza kujiokoa. Tofauti na miinuko mingine kama Kitonga ambapo mara nyingi maderera wameweza kujiokoa kwa kuparamia gema ambazo zipo karibu mno na barabara.

Barabara ya mbalizi ni mteremko mkali, usio na kingo au kizuizi chochote cha kumwezesha dereva kujiokoa zaidi ya kuendelea kuifuata barabara mpaka hapo atakapoweza kusimama salama au kinyume chake. Nina mfano mdogo tu ambapo siku ya Jumamosi ya tarehe 06 Oktoba 2012, basi la Bajeti likiwa linaelekea Dar es Salaam, dereva wake aliweza kuliokoa lisitumbukia bondeni katika eneo la Kitonga baada ya breki zake kushindwa kufanya kazi na kulielekeza kwenye gema ambazo abiria wote walipona. Hapa ni Kitonga, lakini ingekuwa ni Mbalizi, tungesikia maafa mengine tena.

Kwa nini nasema ajali nyingi zinachangiwa na polisi wetu? Nina sababu za msingi. Wakati magari aina ya toyota land cruizer mwaka juzi yaliporipotiwa kupata ajali mfululizo, wachunguzi wa masuala ya ajali ya magari huko Marekani, waliweza kubaini tatizo la kimakenika katika mifumo ya breki na peda za breki katika magari hayo. Na kwa maana hiyo walimjulisha mmiliki wa kiwanda kinachotengeneza magari hayo kuhusiana na tatizo hilo, aliahidi magari yote ya modeli hiyo yarudishwe na pia kulipa fidia kwa wale wote ambao waliathirika.

Siamini kama Tanzania nasi tulikuwa katika mkumbo wa magari hayo mabovu na pengine hatukuchukua hatua zozote muhimu kukabiliana na tatizo hilo. Sikuona sababu ya mwendo kasi na uzembe imetajwa katika ajali nyingi zilizotokea ambazo zilihusisha magari hayo ya Toyota Land Cruizer.

Tofauti na wenzetu hao weupe kutoa sababu za msingi na kisomi, kwetu sisi sababu za ajali ambazo zinafahamika ni mwendo kasi na uzembe. Na cha ajabu zaidi, nilisikia Kamanda wa Polisi wa Mbeya akisema wanamtafuta Dereva wa gari iliyohusika katika ajali hiyo ili wamhoji. Sijui kama alifariki au vinginevyo lakini sioni mantiki. Wao kama polisi, wanaojiita Wataalam, wanasemaje kuhusiana na ajali hiyo, kwa kuhusianisha na ajali nyingi ambazo zimetokea katika maeneo hayo.

Nasema kama nchi tuna janga la taaluma na weledi katika kushughulikia majanga yanayotokea katika nchi yetu. Sidhani kama akili ndogo inaweza kutawala akili kubwa. Ajali ni akili kubwa na tunapaswa kutumia akili kubwa zaidi kutatua akili kubwa iliyopo ya wimbi na ongezeko la ajali za barabarani.

Kwa mtazamo wangu, ufinyu wa miundo mbinu katika mlima huo ndiyo chanzo cha ajali zote ambazo zimetokea katika eneo hili. Jambo la msingi ni kupanua miundombinu na pia kuwepo barabara za dharura kwa magari ambayo yanakuwa yamepata tatizo kufeli kwa mifumo ya breki. Barabara hizo za dharura inabidi ziwe wazi muda wote na zitumike kwa dharura tu. Udongo ni wa bure. Raslimali tunazo, kinachopaswa kuchuliwa ni hatua tu. Pengine mnasubiri mpaka kiongozi wa juu wa serikali apoteze uhai katika eneo hilo ndio mchukue hatua za kuboresha miundombinu. Nadhani damu za watanzania dagaa haziwaumi na ndiyo maana hamchukua hatua za makusudi kuondoa tatizo hilo.

Imeandaliwa na:

Adam Kivenule

Friday 12 October 2012

NGUVU YA MABADILIKO NI DHAHIRI KATIKA MKOA WA ARUSHA

Movement for Change M4C
Nguvu ya mabadiliko ni dhahiri katika Mkoa wa Arusha kama inavyojidhihirisha katika kesi ya kupinga kuvuliwa Ubunge kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Godbless Lema. Angalia picha zifuatazo.