Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Umoja wa Ukoo wa Kivenule-KAUKI

KAUKI NI NINI?




Nembo ya KAUKIKAUKI  ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi Desemba 17-18, 2005 Kijijini Kidamali, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa. Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianzishwa mwezi Februari 06, 2005 Jijini Dar es Salaam kwa kufanya Mkutano Mkuu wa Kwanza. Harakati nyingine za maandalizi zilielekezwa upande wa Kidamali, Ilole na Nduli. Kwa upande wa Kidamali, Mkutano wa kwanza wa maandalizi ya Mkutano Mkuu ulifanyika mwezi Mei ambapo wajumbe toka Dar es Salaam walisafiri kwenda huko ili kufanya majadiliano, kuchagua viongozi wa kuunda kamati ya maandalizi na pia kuhamasisha.

KAUKI, pia ni jina la Katiba na pia Umoja wa Wanaukoo wa Kivenule, ambalo lilipitishwa na pia kukubaliwa kutumika na jumuiya nzima iliyoshiriki Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule. Lengo kuu la KAUKI limebaki pale pale, ikiwa ni kujaribu kwa kila hali kutumia ujuzi na maarifa, kuinua uwezo wa kielimu, kiuchumi, kijamii na kimaisha, kwa wanajamii wanaunda umoja huo, kwa kutumia rasimali mbalimbali zinazopatika katika nchi ya Tanzania na hususani katika maeneo wanayoishi.

KAUKI imeundwa ili kukidhi mahitaji ya jamii iliyounda umoja huu, kwa kushirikisha mawazo, fikra, ujuzi na maarifa ya kila mwanaukoo, katika mikutano mikuu na mikutano midogo midogo, ambayo huandaliwa na wanaukoo wenyewe. Kwa kukutana pamoja, fikra za kujenga, ujuzi, uzoefu na maarifa, huunganishwa pamoja na kisha kupanga mikakati mbadala ya kuweza kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika mkutano huo.

MIPANGO YA KAUKI

KAUKI inajikita kujiimarisha katika ngazi zote za kiutendaji, kiuendeshaji na kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kielimu, kisiasa, kimaendeleo, kimabadiliko na kimapinduzi. Baadhi ya mikakati ambayo ni muhimu kuzingatiwa ni pamoja na:

KAUKI kuwa na ofisi yake Kijijini Kidamali na pia sehemu nyingine za Kanda ambapo wanaukoo wanadhani ni muhimu kuwa na ofisi.
  1. Suala na pili ni kupata usajiri ili tuwe na fursa ya kufanya shughuli kubwa zaidi.
  2. KAUKI kuwa na sanduku lake la posta.
  3. Kuwa na Akaunti katika Benki yeyote. Suala na akaunti limo ndani ya Katiba na kinachotakiwa ni utekelezaji tu.
  4. KAUKI kuwa na vitendea kazi mfano Kompyuta, Printa, Simu, Meza na Viti.
  5. KAUKI kuanza kutoa elimu mbalimbali kwa wadau wake.
  6. KAUKI kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ambayo itawasadia wanajamii.
  7. KAUKI kuwa na kitengo cha Utaalam wa Kitaaluma na Kiujuzi ambacho kitafanya shughuli za kuiletea fedha KAUKI, pamoja na miradi mbalimbali. za ndani ya nchi na nje kwa kutumia teknolojia ya kisasa yaani tovuti na webusaiti.
  8. Kuchapisha kitabu toleo la kwanza cha Umoja wa Ukoo wa Kivenule kwa kipindi cha mwaka 2008 – 2009.

 Imeandaliwa na
 



Adam Kivenule

Katibu wa KAUKI

No comments:

Post a Comment