MZEE PONSIANO SIGATAMBULE
TAVIMYENDA KIVENULE AFARIKI DUNIA
Siku ya Ijumaa, ya tarehe 10 Agosti 2012, nyakati za asubuhi, ilikuwa ni siku ya ni masikitiko makubwa kwa Ukoo wa Kivenule, watoto na familia yake kwa ujumla, baada ya kupata taarifa ya kifo cha Mzee Ponsiano (Luhanage) Sigatambule, Tavimyenda Kivenule, kilichotokea katika Hospitali ya Misheni ya Ipamba, inamilikiwa na Kanisa Katoliki. Hospitali hiyo ipo njiani kuelekea Tosamaganga na Kalenga, Katika Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.
Historia yake ni ndefu, lakini kwa kifupi, Marehemu Ponsiano Kivenule alizaliwa yapata miaka 69 iliyopita huko Mlafu, Kijijini Kidamali. Katika uhai wake alifanya kazi kama Mwalimu na pia kama Bwana Mifugo. Pia katika uhai wake amekuwa akiishi Kijijini Kidamali huku akishirikiana na wenzake katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Baada ya kutokea kwa msiba huo, Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), kwa niaba ya Wana-KAUKI wote kutoka Kanda ya Kidamali, Magubike, Nduli, Irore, Mufindi na Dar es Salaam, na wanaukoo kwa ujumla, uliwatangazia taarifa hizo za Msiba Mkubwa wa Mzee Ponsiano Sigatambule Tavimyenda Kivenule.
Pia taarifa hiyo, iliyotangazwa na Mwenyekiti wa KAUKI, ilisema Mazishi ya Marehemu yatafanyika Kijijini Kidamali, Siku ya Jumamosi ya tarehe 11 Agosti, 2012, katika Makaburi ya Mlafu, mnamo saa 7 mchana.
Marehemu Ponsiano Kivenule ameacha wake wanne na watoto. Pia kama Wana-KAUKI, tumeachiwa pengo ambalo haliwezi kuzibika kutokana na mchango wake mkubwa katika uanzilishi wa KAUKI na pia michango yake katika Mikutano mbalimbali ya KAUKI ambayo amekuwa akihudhuria.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.
Imeandaliwa na Kusambazwa na:
Adam Alphonce Kivenule
No comments:
Post a Comment