Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Friday 18 December 2015

SALAAM ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA



Mimi Adam Alphonce Kivenule, kwa heshima na taadhima, naomba nitumie fursa hii kuwatakia Heri ya Christmas  na Mwaka Mpya 2016.

Najua ni kwa neema za Mungu tu ndio maana nimepata fursa ya kuundika ujumbe huu wa kuwatakia kila kheri katika mwisho huu wa mwaka 2015.

Natumaini, Mungu awabariki wote.

Asanteni,

Adam Kivenule
0713 270364
kivenule@gmail.com

Ndugu Mwinuka (kushoto) na Ndugu Adam Kivenule (kulia)
 

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA 11 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)


Adam Kivenule, Katibu Mkuu-KAUKI

Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa kushirikiana na Kanda ya Nduli, kwa heshima kubwa unapenda kuwajulisha ndugu, jamaa, marafiki na Wana Ukoo wote, umeanza maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika Kijijini Nduli, Mkoani Iringa, tarehe 2 had 3 Julai, 2016.

Kwa taarifa hii, tunaomba Viongozi wote wa KAUKI na Viongozi wa Kanda, kuanza kujiandaa kwa Mkutano huo muhimu. Sambamba na hilo, Viongozi wa KAUKI waendelee kuratibu maandalizi ya Mkutano kwa kusambaza taarifa na kuweka mikakati imara ya kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI unafanikiwa. Wadau wakuu wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI ni Viongozi wa Kanda kwa kushirikiana na ndugu wote.

Ikumbukwe kuwa, mwaka huu (2015), Mkutano wa Mkuu wa KAUKI uliopangwa ufanyika Kijijini Irore, Mkoano Iringa, umeshindwa kufanyika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Maana nyingine Kanda ya Irore bado inayo nafasi nyingine ya kuandaa Mkutano Mkuu wa 12 wa KAUKI, 2017. Kwa hiyo wana Irore na sehemu zote za Igominyi mnaombwa kuanza kufanya maandalizi ya mkutano wenu, sambamba na maandalizi ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Nduli mwakani.

Kuna mambo mengi muhimu yanaweza kufanyika kama sehemu muhimu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika Kijijini Nduli:
1. Kila ndugu kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI na kuhakikisha kuwa unafanikiwa. Kila mwana ukoo anaweza kujitoa kwa chochote kile ambacho kitasaidia kufanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI.
2. Ndugu wenye uwezo kujitolea ili kufanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI. Kuna wana Ukoo ambao wamejiajili na wana vipato vya uhakika. Tunaomba kwa moyo wa upendo wasaidie kuandaa mkutano huu. Pia kuna ndugu ambao wameajiliwa na wana vipato vizuri. Tunaomba wachukue jukumu la kusaidia kugharama za maandalizi ya Mkutano huo.
3. Wana Ukoo wa Kanda ya Nduli na Kanda nyingine ambazo zina fursa ya ardhi, wanaweza kulima angalau nusu ekari kwa lengo la kupanda mazao ambayo yatatumika kwa ajili ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI. Mazao ambayo yanaweza kupandwa ni pamoja na Mahindi, Maharage, Viazi na mazao mengine ya nafaka.
4. Kuhamasishana na kuhimizana ndugu na wana ukoo miongoni mwetu ili kuendelea kuwa na moyo wa kupendana, kushirikiana na kusaidiana; na pia kuwa pamoja katika masuala yote yanayohusu ndugu na ukoo kwa ujumla kwa faida yetu wote.
Matarajio ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika tarehe 2 – 3 Julai, 2016, Kijijini Nduli.
Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI unatarajia yafuatayo:
1. Kuendelea kuboresha Kitabu cha Wana Ukoo kwa kujaza taarifa mbalimbali za ndugu (Clan Organization Tree).
2. Kuwafahamisha wana ukoo, Historia na Chimbuko la Ukoo. Hususani Ukoo wa Kivenule.
3. Mwingiliano wa Ukoo wa Kivenule na Koo nyingine uliopelekea kuwepo kwa Ukoo wa Kivenule.
4. Kufanya tathmini ya mipango mbalimbali ya KAUKI tuliyojiwekea kwa miaka kadhaa.
5. Kutathmini changamoto na vikwazo mbalimbali vinavyoukabili Umoja wetu.
6. Yatakayojiri katika Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika tarehe 2 – 3 Julai,

Imeandaliwa na kusambazwa na:

Katibu Mkuu (Adam Alphonce Kivenule)
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
Mobile: 0713 270364
            kivenule@gmail.com




Wednesday 16 December 2015

KUMBUKUMBU YA MAHAFALI YA KUAGANA WABUNGE MWAKA 2015

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa wabunge pale walipohitimu masomo yao kwa kufanya mahafali ya kuagana wao wenyewe na wanachuo wenzao, yaliyofanyika katika chuo hicho. Kwa kutambua ushirikiano wao katika maisha ya chuo hapo, wabunge na wanachuo walipiga picha mbalimbali kama sehemu ya kumbukumbu. 

Zifuatazo ni picha za kumbukumbu katika mahafali hayo:
 
Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika ngazi za ukumbi wa mikutano wa Auditorium


Mhe. Mwinuka na Ndugu Kivenule katika picha ya pamoja

Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzao

aheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzao

Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzao katika ngazi za ukumbi wa Auditorium

Waheshimiwa Wabunge wakiingia ukumbini

Waheshimiwa Wabunge wakiwa Morogoro Road

Mhe. Mwinuka na Kivenule wakitoka jengo la Utawala wa Chuo hicho
Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzao

MATUKIO YA KUKUMBUKANA NA BAADHI YA WANACHUO WENZANGU

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa Wabunge (viongozi wa wanachuo) pale walipofanya sherehe ya kuagana huku wakiwashirikisha wanachuo wenzao. Sherehe hiyo haikuweza kuwaalika viongozi wa Serikali ya Wanachuo kwa kile kilichodaiwa kutowajibika ipasavyo katika utendaji wao, pamoja na malalamiko kadhaa ambayo yalielekezwa kwenye uongozi huo.

Mwadili wa Chuo alikuwa mmoja wa waalikuwa na alihutubia warsha hiyo, huku akipiga picha ya pamoja na Wabunge. 

Yafuatayo ni matukio katika picha:
Waheshimiwa Wabunge wakiwa wamesimama mbele ya Ukumbi uliopo katika Library ya Chuo hicho.

Waheshimiwa Wabunge wakiwa na Mgeni Rasmi, Mhe. Mwadili wa Chuo (aliyechuchuma na baadhi ya wabunge) katika bustani ya Chuo

Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja, katika garden ya Chuo

Waheshimiwa Wabunge: Kutoka kushoto ni Emanuel Sulle, Jose Mniko (Spika) nyuma, tatu nyuma, Mwinuka, Rajabu, David, Adam Kivenule, Malunguja na James

Waheshimiwa Wabunge wakiongozana na Mgeni Rasmi (Mwadili wa Wananchuo) kuingia katika ukumbi wa sherehe

Wednesday 2 December 2015

Kuhusu UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

Kuhusu UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

FASILI YA KAUKI

KAUKI ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii inayounda umoja huu; hususani katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga, maradhi na utegemezi.

 

Kuanzishwa kwa KAUKI kuliambatana na maandalizi yaliyojumuisha mikutano zaidi ya 10 ya mashauriano iliyofanyika sehemu mbalimbali Jijini Dar es Salaam na Kidamali, Iringa.

 

Dira ya KAUKI

Kuwa na jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa kujitegemea.

 

Maono ya KAUKI

Kujengeana uwezo kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia mafunzo, kongamano, mijadala na mikutano ili kuboresha maisha.

 

Malengo ya KAUKI

Lengo Kuu

Kuinua na kuboresha maisha ya wanaukoo wa Kivenule, kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa kutumia ujuzi, maarifa na raslimali zinazotunguka.

 



--
Adam Kivenule
P.O. Box 3255,
Dar es Salaam
Mob. +255 713 270364
E-mail: kivenule@gmail.com / KAUKI2006@gmail.com
Blog: www.adamkivenule.blogspot.com
Twitter: www.twitter.com/kivenule