Mkutano Mkuu wa 14 wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) ulifanya uchambuzi wa Vizazi 6 vya Balama vilivyopelekea kuzaliwa kwa Jina la Ukoo wa Kivenule.
Mtafiti na Mchambuzi wa Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule, Ndugu William Sigatambule Tavimyenda Kivenule aliwajulisha washiriki wa Mkutano huo (Wanaukoo wa Kivenule) kuwa Vizazi 6 vya Balama vilivyoleta jina la sasa la KIVENULE, vinajumuisha: Mwinyisambusa Balama, Mtengelingoma Balama, Kanolo Balama, Nyakudila Balama, Mnyarungemba Balama na Mwigingili Balama.
Hapa chini ni Chati inayoonesha Vizazi 6 vya Ukoo wa Mwibalama.