Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Wednesday, 7 August 2013

CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE



Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule- Karibu Usome

CHIMBUKO NA HISTORIA YA
UKOO WA KIVENULE


Toleo la Kwanza - 2013 (Imeboreshwa)





Kwa mawasiliano:
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
Kando ya Barabara ya Hifadhi ya Ruaha
Sanduku la Posta 193
Kidamali, Iringa
Simu: +255 713 270364 (Katibu Mkuu-KAUKI)
Barua-pepe:     kauki2006@gmail.com
                                   kivenule@gmail.com
                                   tagumtwa.kauki@gmail.com
Blogu: http://www.kauki-kauki.blogspot.com


UTANGULIZI

UKOO NI NINI?
Ukoo ni muungano wa familia kadhaa zenye utambulisho fulani. Unaweza kuwa utambulisho wa jina, alama au mwelekeo mmoja. Utambulisho wowote kati ya hizo nilizotaja, unaufanya ukoo utambulike miongoni mwa jamii mbalimbali. Mara nyingi utambulisho ambao huufanya ukoo utambulike baina ya jamii za Kiafrika ni Jina. Pamoja na jina, halikadhalika kuna tunu (values) mbalimbali ambazo huheshimiwa na ukoo husika na jamii kwa ujumla.

Tunu hubeba mambo mengi, ikiwa ni pamoja na miiko, maadili, heshima, vyakula na tamaduni. Sambamba na tunu, pia kuna Mila na Desturi, ambazo huzingatiwa sana katika masuala ya kijamii, mfano wakati wa kuoa au kuoza, misiba, sherehe za jadi mfano matambiko na masuala ya kimila.

Ukoo wa Kivenule ni mmojawapo wa koo nyingi kubwa zilizopo katika Himaya ya Uhehe katika Mkoa wa Iringa. Ukoo wa Kivenule ulianza kutambulika toka Karne ya 18. Historia inaonesha kuwa Ukoo huu asili yake ni kutoka kwa Wabena-Manga, waliopo Kusini mwa Mji wa Iringa; yaani maeneo ya Mufindi na Njombe. Ni mchanganyiko wa Wahehe na Wabena wanaojulikana kama Wabena-Manga.

Wahehe ni moja kati ya makabila makubwa hapa Tanzania ambalo kiasili linaishi katika Wilaya za Kaskazini mwa Mkoa wa Iringa, yaani Iringa Vijijini, Iringa Mjini, Kilolo na Mufindi. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinazopatikana na kutafitiwa, inasemekana kuwa ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji; yaani Wahehe wenye Asili ya Ungazija. Pengine hata ile sababu ya kuzika wafu wao wakielekea mashariki inapewa uzito.

Lugha ya Kabila hili ni Kihehe na limegawanyika kiasi fulani katika lahaja (matamshi) tofauti tofauti kutokana na maeneo ambayo huzungumzwa. Inafanana kimatamshi na kimaana na lugha ya Kibena iliyopo wilayani Njombe. Pamoja na Wabena wanaohesabika kuwa zaidi ya watu milioni moja. Wengi wao ni wafuasi wa Ukristo, hasa wa Kanisa Katoliki (Jimbo Katoliki la Iringa). Kihistoria Wahehe ni maarufu kwa jinsi walivyopambana na Wajerumani walioteka maeneo yao, kama katika mapigano ya Lugalo mwaka 1891. Kiongozi wao alikuwa Chifu Mkwawa.

Katika kuenzi na kutunza tunu za asili za Uhehe, Ukoo wa Kivenule hauli nyama ya Mbawala (kwa lugha ya Kihehe Mato/Imato). Imani kubwa imejengeka miongoni mwa jamii ya Ukoo wa Kivenule kuwa kula Mbawala ni kuvunja miiko ya Ukoo ambayo iliyowekwa na Waasisi wetu (Babu zetu). Mara mwanaukoo anapokiuka miiko hii na kula nyuma ya Mbawala (Imato) basi huweza kufikwa na matatizo mbalimbali, mfano kudhurika afya yake. Mara nyingi huwapata matatizo kama ya kuvimba miguu na pengine kuoza kabisa.

Tunu nyingine ambazo Ukoo wa Kivenule unazienzi kama zilivyo koo nyingine katika Uhehe ni Miitikio (Midikiso). Tunu hii huutambulisha Ukoo wa Kivenule miongoni mwa Koo za Wahehe. Mwitikio (Mwidikiso) wa Ukoo wa Kivenule ni 'MLIGO'. Mwitikio huu hutumika katika maeneo mbalimbali mfano katika salamu, kuapa (kufanya viapo) na pia kujitofautisha na koo nyingine. Miitikio (Midikiso) huutambulisha Ukoo wa Kivenule katika koo nyingine katika ardhi ya Uhehe.

CHIMBUKO LA UKOO WA KIVENULE
Historia ya Chimbuko la Ukoo wa Kivenule limetoka mbali zaidi hata kabla ya Jina la sasa la KIVENULE kupatikana. Utafiti unaonesha kuwa BABU NYAKUDIRA BALAMA ndiye aliyemzaa BABU KANOLO BALAMA. Hapa tunauangalia Ukoo wa Balama. Hali kadhalika, BABU KANOLO BALAMA, akamzaa BABU MTENGELINGOMA BALAMA. Maelezo haya yote tunayoyazungumzia ni katika Karne ya 17 kabla ya kuja kwa BABU TAGUMTWA BALAMA, ambaye aliuleta Jina la KIVENULE.

BABU MTENGELINGOMA BALAMA ndiye Baba Mzazi wa TAGUMTWA BALAMA. Wakati huu Babu Tagumtwa Balama alikuwa hajaenda kwenye Vita za LIGALU.

Kwa Asili, Ukoo wa Balama na baadaye Kivenule ni maarufu kama Wapiganaji wa Vita. Ukoo wa Balama (Kivenule) ulikuwa hodari sana katika vita vya msituni ambavyo viliwahusisha Babu zetu akina TAGUMTWA. Enzi hizo za Mababu zetu vita za Koo na Kabila zilipiganwa maeneo mengi ya himaya ya Uhehe kwa lengo la kupata mali, mifugo na heshima.

Babu TAGUMTWA BALAMA (KIVENULE) ndiye aliyewazaa Babu TAVIMYENDA KIVENULE na Babu KALASI KIVENULE. Ikumbukwe kuwa, jina halisi la ukoo wa Kivenule ni BALAMA. Kama ilivyokwisha julikana katika mada zilizowasilishwa katika Mikutano Mikuu Tisa ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), ambapo ilielezwa kuwa, neno KIVENULE linamaanisha sifa ya kuwa jasiri Vitani na hasa katika kutumia silaha za Mishale na Mikuki yaani kwa Lugha Asilia ya Kihehe “KUMIGOHA”.  Yaani kwa maana nyingine LIGALU yenye maana ya Kwihoma ImigohaKuhoma Vatavangu au Kuvenula Avatavangu. LIGALU maana yake Vita. Kuhoma maana yake Kuchoma na Migoha maana yake Mikuki. Venula maana yake ua, fyeka maadui.
LIGALU ndiyo iliyochangia kuzaliwa kwa jina la Ukoo la KIVENULE. KIVENULE maana yake ni Ushujaa kutokana na Shabaha ya Mikuki.

KUVENULA likiwa na maana halisi ya kuwa na shabaha ya kuwaangamiza maadui kwa kutumia silaha ya Mishale na Mikuki. Babu zetu akina TAGUMTWA BALAMA walilidhihirisha hili katika Vita na Watavangu na hivyo kusababisha kuzawadiwa kwa jina la KIVENULE kama jina la sifa kutokana na ushujaa katika Vita.

Tagumtwa Balama asili yake ni kutoka katika Ukoo wa Balama. Sifa kubwa ya Tabu Tagumtwa, alikuwa ana Shabaha sana ya Mikuki katika uwanja wa Vita. Alikuwa hakosei shabaha (target) na hivyo hupelekea kuwaangamiza na kuwaua sana maadui. Wakati akiwamaliza/fyeka/kuwaua adui zake kwa Mikuki, Wakuu wa Vita (Vatavangu) walikiita kitendo hicho 'KUVENULA'. Taarifa za Tagumtwa kuua (Kuvenula) adui zake katika uwanja wa vita, zilizagaa kila mahali na hivyo kupelekea Wakuu (Viongozi) wa Vita (Vatavangu) kumzawadia Jina la KIVENULE, kama jina la sifa na heshima kwa kuwa shujaa wa Vita.

Ikumbukwa kuwa asili ya Ukoo wa Kivenule ni kutoka katika ukoo wa BALAMA (MWIBALAMA). Hawa ni ndugu wa karibu wa Kivenule kabisa na hawapaswi kuoana. Koo za Mwibalama zinapatikana maeneo mengi katika Mkoa wa Iringa hususani katika Wilaya  za Mufindi, Iringa Vijijini, Iringa Mjini na Kilolo; hali kadhalika kama ilivyo ukoo wa kina Mwakivenule.

TAGUMTWA KIVENULE alifia katika uwanja wa mapambano (vita) na mwili wake haukuweza kupatikana. Kama zilivyo koo za machifu au watu maarufu miili yao ilikuwa haizikwi. Baada ya kufa iliegemezwa kwenye miti mikubwa na kuliwa na wanyama. Wakija watu wasiukute mwili basi huamini kuwa mwili umechukuliwa na Mungu.

KUKUA NA KUZAGAA KWA UKOO WA KIVENULE
Kwa mujibu wa taarifa mbalimblai za kitafiti ambazo zimekuwa zikifanyika toka mwaka 2005 hadi sasa 2013; kupitia mikutano mbalimbali ya KAUKI; zinabainisha kuwa, BABU NYAKUDIRA BALAMA  alimzaa BABU KANOLO BALAMA. Hali kadhalika BABU KANOLO BALAMA alimzaa MTENGELINGOMA BALAMA. BABU MTENGELINGOMA BALAMA ndiye aliyemzaa Tagumtwa Balama (Kivenule).

Baada ya hapo, tunaona sasa Kizazi cha TAGUMTWA KIVENULE kinaanza kujitokeza. Hii ilikuwa ni Karne ya 18. TAGUMTWA KIVENULE alizaa watoto wawili (2).  Bado utafiti unafanyika kumfahamu Mama wa watoto hawa. Watoto wa Tagumtwa Kivenule walikuwa ni TAVIMYENDA KIVENULE na KALASI KIVENULE. Kwa mujibu wa taarifa kadhaa tulizonazo kwa sasa; hawa ni vinara wa Ukoo wa Kivenule ulioenea maeneo mbalimbali hapa Tanzania.

Tavimyenda Kivenule na Kalasi Kivenule katika harakati za kutafuta maisha walifika katika eneo la Kalenga, mahali alipoishi Mkwawa na kukutana na na Mwamyinga, aliyekuwa mfugaji maarufu katika eneo la Ulefi huko Magubike, Iringa Vijijini. Tavimyenda Kivenule alibahatika kupata kazi kwa Mwa-Myinga baada ya kuombwa kwenda kumwangalizia mifugo yake huko Magubike, huku akimwacha mwenzake Kalasi pale Kalenga.

Kalasi Kivenule yeye hakupata fursa hiyo ya kazi na hivyo akaamua kuelekea eneo Irore katika Wilaya Iringa Vijijini (kwa sasa Kilolo) kutafuta maisha. Huu ukawa ni mwanzo wa kugawanyika kwa watoto hawa wawili wa Tagumtwa Kivenule.

Tavimyenda Kivenule akielekea upande wa Magharibi mwa Mji wa Iringa na Kalasi alielekea upande wa Mashariki mwa Mji wa Iringa.

Historia inabainisha kuwa pamoja na Babu hawa kugawanyika kutokana na utafutaji wa maisha, mahusiano na ushirikiano baina yao haukuvunjika. Babu zetu waliendelea kushirikiana na kutembelea licha ya ukoo kukua na kuwa mkubwa sana.

KIZAZI CHA TAVIMYENDA KIVENULE
Katika Karne ya 19 hadi 20, Kizazi cha Tavimyenda Kivenule kilizaliwa na kuzagaa katika maeneo ya Ulefi, Magubike na Mlafu, Wilaya ya Iringa Vijijini, Iringa Mjini na maeneo mengine mkoani Iringa.

Taarifa tulizonazo kupitia tafiti tunazofanya, hali inaonesha kuwa, Babu Tavimyenda alikuwa na wake watatu (3), ambao ni:
1.     Bibi         Mkami          Sekabogo
2.     Bibi         Senosa
3.     Bibi         Pili              Mvemba

Mke wa kwanza wa Tavimyenda Kivenule aliolewa akiwa na mtoto; aliyejulikana kama Bibi Sikimbilavi Semabiki. Kwa mke huyu wa Kwanza Sekabogo, Tavimyenda alizaa nae watoto wanne (4); ambao ni:
1.     Babu       Kavilimembe          Kivenule
2.     Babu       Mgaifaida               Kivenule
3.     Babu       Sigatambule           Kivenule
4.     Babu       Hussein                 Kivenule (Bado yupo hai)

Kwa Mke wa Pili Bibi Senosa, Babu Tavimyenda akizaa nae watoto watatu (3); ambao ni:
1.     Babu       Abdallah                Kivenule
2.     Bibi         Sigungilimembe      Kivenule
3.     Bibi         Malibora                Kivenule

Watoto hawa wa Bibi Senosa waliishi maeneo ya Kihesa katika Mji wa Iringa.

Kwa upande wa mke wa Tatu wa Bibi Pili Mvemba; Babu Tavimyenda alizaa mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la BIBI MGASI KIVENULE aliishi eneo la Ulefi. Baada ya kufariki amezikwa Mlafu. Babu Tavimyenda Kivenule amezikwa katika eneo la Ulefi.

Bibi SIKIMBILAVI alikuwa mtoto wa kufikia wa Bibi MKAMI SEKABOGO. Bibi SIKIMBILAVI aliolewa na Ukoo wa Mgoda na kubahatika kupata watoto wanne (4) ambao ni:
1.     Mama wa Kitatambe
2.     Salia       Maneno        Mgoda
3.     Galamale Mgoda
4.     William    Mgoda

Baada ya hapo kizazi hiki kimeendelea kukua hadi hivi sasa Karne ya 21. **Angalia Chati kuonesha Muundo wa Ukoo wa KIVENULE**

KIZAZI CHA KALASI KIVENULE
Kwa upande wa Kalasi Tagumtwa Kivenule, kizazi hiki kilienea maeneo ya Nduli, Mgongo, Itagutwa, Kigonzile, Igominyi na Irore. Taarifa zinaonesha kuwa, Babu Kalsi Kivenule alikuwa na wake wawili (2); yaani:
1.     Bibi         Semsakwa              Mnonikilwa
2.     Bibi         Mnyamtage            Sekindole

Bibi Semsakwa Mnoni Kirwa kwa Babu Kalasi Kivenule alizaa watoto wawili (2) ambao ni:
1.     Bibi Cheilaje Nginasambula Kivenule
2.     Gingilemesa Kivenule

Kwa bahati mbaya hakuna taarifa zozote za hawa watoto wawili wa Kalasi.
Kwa upande wa Bibi Mnyamtage Sekindole, Babu Kalasi Kivenule alizaa mtoto mmoja ambaye ni Salamalenga Kahengula Kivenule. Bibi Mnyatage Sekindole awali alikuwa ameolewa kwa Mwa-Mhumba na kuzaa nae mtoto mmoja aliyeitwa Bibi Mganga Semhumba na baadaye kufariki. Baada ya hapo aliolewa na Kalasi ambapo pia alizaa mtoto mmoja tu anayefahamika kwa jina la Salamalenga Kahengula Kivenule. * Angalia watoto wa Kahengula katika Chati ya Muundo wa Ukoo wa Kivenule*

Kuna taarifa nyingi kutoka kwa Babu Tavimyenda Kivenule na Kalasi Kivenule. Mwingiliano wa koo nao unaonesha simulizi hizi. Kwa upande wa Tavimyenda mke wa Kwanza Bibi Mkami Sekabogo alikuwa na mtoto wa kufikia, aliyejulikana kwa jina la Bi Sikimbilavi Semabiki. Hatujapata taarifa rasmi kuhusiana na kizazi cha Bibi huyu, kama ilivyotokea kuwa Sipanganakumtwa Mwilongo Regina Sematagi aliyekuwa mtoto wa kufikia Bibi Semkonda mke wa Salamalenga Kahengula Kivenule.

Sipanganakumtwa Mwilongo Regiona Sematagi amesaidia kueneza kizazi cha Ukoo wa Mnyavanu. Taarifa zaidi na ukoo wa Mnyavanu upo katika Chati ya Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule.**

TABIA YA KIZAZI CHA TAVIMYENDA NA KALASI KIVENULE KUOA WAKE WENGI
Ukoo wa KIVENULE hususani kizazi cha Babu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule ulikuwa na tabia tofauti pengine na vizazi vya sasa. Tabia ya kizazi hiki cha Tavimyenda na Kalasi ilikuwa ni kuoa wake wengi. Kwa mfano Babu Tavimyenda pekee alikuwa na wake watatu. Hali kadhalika Babu Kalasi naye alioa wake wawili.

Hali hii ya kuwa na mke zaidi ya mmoja walirithi watoto wao. Kwa mfano watoto watatu wa kiume wa Babu Tavimyenda waliozaliwa kwa Bibi Mkami Se-Kabogo walioa wake wawili hadi watatu. Mtoto wa kwanza wa Babu Tavimyenda Kivenule aliyejulikana kama Kavilimembe Kivenule alikuwa na wake wawili (2). Mtoto wa tatu wa Bibi Mkamai Sekabogo, aliyejulikana kwa jina la Sigatambule Matesa Kivenule, alikwa na wake watatu. Hali kadhalika mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo anayejulikana kama Hussein Kivenule alikuwa na wake wawili. Mtoto pekee wa Pili wa Bibi Mkami hakubahatika kuwa na familia; na alijiita jina la kujinyanyapaa "Mgaifaida" Kivenule.

Sambamba na tabia ya Ukomo wa Kivenule kuoa mke zaidi ya moja; pia kuna utamaduni uliojitokeza kwa baadhi ya watoto wa Bibi Mkami Sekabogo kuoa dada na mdogo wake. Hili linajidhihirisha kwa wake wawili wa Babu Kavilimembe Kivenule ambao walikuwa ni Bibi Sikumwendinguluvi Sekusiga (Bi Mkubwa) na Bibi Gakumwalia Sekusiga (Bi Mdogo).

Hali kadhalika kwa mtoto wa tatu wa Bibi Mkami Sekabogo; Babu Sigatambule Matesa Kivenule alioa wake watatu, ambapo wake wawili wakubwa, 'Bibi Sikumwendinguluvi Singaile (Bi Mkubwa) na Bibi Nyanyilemale Singaile (Bi Mdogo wa Pili); na wa tatu aliitwa Bibi Pangulimale Setwanga.

Mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo Hussein Kivenule, yeye alioa wake wawili kutoka familia tofauti. Wake zake waliitwa Bibi Yimilengeresa Semsisi (Bi Mkubwa) na Bibi Dalika Setala (Bi Mdogo). Kwa upande wa watoto Kalasi Kivenule, mtoto wake Salamalenga Kahengula Kivenule naye alioa wake watatu; ambao ni Bibi Semkonda, Bibi Semfilinge na Bibi Nyangali.

Hatujapata taarifa rasmi za watoto wa Kalasi kutoka kwa mke wake Bibi Semsakwa Mnonikilwa ambao ni Cheilaje Nginasambula Kivenule na Gingilemesa Kivenule. Kwa upande wa Kahengula yeye alioa kutoka katika familia tofauti.

UZAO WA BABU KAVILIMEMBE, MGAIFAIDA, SIGATAMBULE NA HUSSEIN KIVENULE
Babu Kavilimembe Kivenule aliishi eneo la Magubike, Wilaya ya Iringa Vijijini, huku akipakana na Ulefi upande wa Kaskazini, Idete na Ibogo upande wa Magharibi. Akiwa ameoa wake wawili wa familia moja, Babu Kavilimembe alibahatika kupata watoto sita (6).

Kwa upande wa mke wa kwanza Bibi Sikumwendinguluvi Sekusiga; Mzee Kavilimembe Kivenule alipata watoto wafuatao:
1.     Elizabert           Kivenule
2.     Dalikimale         Kivenule
3.     Sandra              Kivenule
4.     Pangalasi          Kivenule

Na kwa mke mdogo Bibi Gakumwalia Sekusiga, Mzee Kavilimembe alipata watoto wawili ambao ni:
1.     Salikuvaganga   Kivenule
2.     Francis              Kivenule

Watoto hao wa Babu Kavilimembe wengi wao waliishi maeneo ya Ulefi na Magubike. Baadhi yao walihamia maeneo mengine kama Nzihi, ukiacha wale waliokuwa watumishi wa serikali wakaenda kuishi maeneo mbalimbali. Babu Kavilimembe amezikwa eneo la Magubike, Iringa Vijijini.

Kwa upande wa Babu Mgaifaida (Yakobo) Kivenule, yeye hakubahatika kupata familia. Mgaifaida alikuwa na ulemavu ambao ulimfanya ashindwe kutembea katika hali ya kawaida. Muda mwingi aliishi eneo la Ulefu kabla ya sehemu kubwa ya Ukoo wa Kivenule kuhamia sehemu ya Mlafu. Baada ya kufariki, alizikwa Mlafu.

Babu Sigatambule Matesa Kivenule alikuwa ni mtoto wa tatu wa Tavimyenda Kivenule kwa Bibi Mkami Sekabogo. Babu Sigatambule aliishi Ulefi, akahamia Mlafu na baadaye Kidamali. Babu Sigatambule ndiye aliyehakikisha Ukoo wa Kivenule unapata eneo la Mlafu huku akipambana na Wagiriki. Walowezi na wawekezaji katika zao la Tumbaku.

Babu Sigatambule Kivenule katika uhai wake alibahatika kuoa wake watatu (3); huku wake zake wawili wakitoka katika familia moja ya ukoo wa Singaile. Wake zake hawa wakubwa waliitwa Bibi Sivangumhavi Singaile na Bibi Nyanyilimale Singaile. Mke wa Tatu wa Babu Sigatambule aliitwa Bibi Pangulimale Setwanga. Wote waliishi Mlafu na baadaye wake zake kuhamia eneo Kidamali baada yeye kufariki.

Wake zake wawili Bibi Nyanyilimale Singaile na Bibi Pangulimale Setwanga bado wapo hai na wanaishi Kidamali mpaka leo.

Watoto wa Babu Sigatambule Kivenule ni hawa wafuatao:
Kwa Bibi Sivangumhavi Singaile (Mke Mkubwa):
1.     Gidagumhindi    Cecilia          Kivenule
2.     Semyamba        Khadija        Kivenule
3.     Sivinitu             Alphonce      Kivenule
4.     Kadungu           William         Kivenule
5.     Fibumo             Xavery         Kivenule
6.     Mlagile              Anyesi          Kivenule
7.     John                                   Kivenule

Bibi Nyanyilimale Singaile (Mke wa Pili)
1.     Mgulwa             Agnes          Kivenule
2.     Luhanage          Ponsiano      Kivenule
3.     Mgendwa          Eusebio        Kivenule
4.     Msinziwa          Daniel          Kivenule
5.     Kanolo              Edward        Kivenule

Mke wa Tatu wa Bibi Pangulimale Setwanga
1.     Conjeta            Kivenule
2.     Pyela                Kivenule
3.     Faustino           Kivenule
4.     George             Kivenule
5.     Carolina           Kivenule

Babu Sigatambule Kivenule alifariki mwaka 1995 na kuzikwa eneo la Mlafu, Kidamali - Iringa. Hali kadhalika mke wake Mkubwa Bibi Siwangumhavi Singaile Mwilumbwa alifariki dunia mwaka 1999 na kuzikwa eneo hilo hilo la Mlafu.

Mzee Hussein Tavimyenda Kivenule alikuwa ni mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo. Yeye aliishi eneo la Ulefi na baadaye Mlafu. Hatimaye alihamia tena Magubike. Babu Hussein Kivenule hadi anafariki dunia Juni 26, 2013 anakadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 113 kwa mujibu wa taarifa na tafiti ambazo tunazo.

Babu Hussein Tavimyenda Kivenule ameshiriki kikamilifu katika Vita vya Pili ya Dunia. Wakati anashiriki vita hiyo alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 44. Amepigana vita maeneo mbalimbali mfano Burma, India na Ulaya. Kwa sasa ana upofu wa macho ambao anasema ulisababishwa na Baruti. Hali kadhalika anakiri kuwa kuendelea kuwa hai ni kwa sababu alipigana upande wa Mwingereza. Anakiri vita ndiyo iliyomsababishia upofu pengine asingekuwa na hali aliyonayo kwa sasa.

Mzee Hussein Kivenule alioa wake wawili na kubahatika kupata watoto kumi na tatu (13). Kwa mke wake wa kwanza Bibi Yimilengeresa Semsisi. Babu Hussein alipata watoto wafuatao:
1.     Nyakudila          Benjamin      Kivenule
2.     Sekiyavile          Modesta       Kivenule
3.     Dominicus                            Kivenule
4.     Emmanuel                            Kivenule
5.     Luciana                                Kivenule
6.     Ajendina                             Kivenule

Kwa upande wa mke wa pili wa Bibi Dalika Setala, Mzee Hussein Kivenule alipata watoto wafuatao:
1.     Kabogo Bernadi           Kivenule
2.     Sembata Josephine      Kivenule
3.     Necia                         Kivenule
4.     Batromeo                   Kivenule
5.     Brandino                    Kivenule
6.     Tavina                        Kivenule
7.     Masikitiko                   Kivenule

Asilimia kubwa ya familia ya Babu Hussein Kivenule inaishi maeneo ya Vijiji vya Magubike, Idete na Ibogo ambavyo vipo jirani kabisa na barabara ya kwenda Hifadhi ya Wanyama ya Ruaha, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.

Mke wa pili wa Babu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule, alijulikana kwa jina la BIBI SENOSA. Bibi huyu alibahatika kupata watoto watatu (3) waliojulikana kwa majina yafuatayo:
1.     Babu Abdallah             Kivenule
2.     Bibi Sigungilimembe    Se-Kivenule
3.     Bibi Malibora               Se-Kivenule

Tafiti za awali zinazofanywa na KAUKI zinaonesha kuwa kizazi cha Bibi SENOSA kiliishi maeneo ya Mkimbizi eneo la Kihesa, Wilaya ya Iringa Mjini, Mkoani Iringa. Tafiti zinaendelea kubainisha kuwa Babu Abdallah Tavimyenda Kivenule hakubahatika kupata familia. Na baada ya kufariki alizikwa katika makaburi ya Mlafu, Kidamali - Iringa Vijijini.

KAUKI bado inaendelea na jitihadi za kutafiti kuhusiana na Bibi Sigungilimembe na Bibi Malibora, ambazo zinaonesha kuwa wao waliishi maeneo ya Mkimbizi Kihesa, na hata baada ya kufariki walizikwa huko huko. Hapajakuwepo na taarifa rasmi kuhusiana na uzao wao, pamoja na vifo vyao. KAUKI inaandaa mpango wa kutuma ujumbe kwenda kufuatilia taarifa za ndugu hawa.

Mke wa Tatu wa Babu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule alijulikana kwa jina la BIBI PILI SE-MVEMBA. Bibi huyu aliishi eneo la Ulefi, Magubike, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa. Bibi Se-Mvemba alibahatika kupata mtoto moja tu aliyejulikana kwa jina la BIBI MGASI SE-KIVENULE.

Bibi Mgasi Tavimyenda Sekivenule alizaliwa akiwa mtoto pekee wa KIKE kwa Babu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule. Bibi MGASI KIVENULE aliolewa katika Ukoo wa akina KIGERESO na kubahatika kupata watoto sita (6). Watoto hao ni:
1.     Gisapa              Kigereso
2.     Sinatoga           Kigereso
3.     Mtogapawene    Kigereso
4.     Chesilemungu    Kigereso
5.     Ronjino            Kigereso
6.     Cecilia              Kigereso

Baadhi ya ukoo wa akina KIGERESO wanapatikana katika maeneo ya Nyamihuu, Igangimali na Kinyamlewa, kando ya barabara ya kwenda Hifadhi ya Wanyama ya Ruaha, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa. Baada ya kufariki, BIBI MGASI KIVENULE alizikwa eneo la MLAFU, Kidamali -Iringa.

UZAO WA SALAMALENGA KAHENGULA KIVENULE
BABU SALAMALENGA KAHENGULA KIVENULE alikuwa ni mtoto pekee wa kiume wa BABU KALASI TAVIMYENDA KIVENULE kwa Mke wake wa Pili BIBI MNYAMTAGE SEKINDOLE. BABU KAHENGULA pia ni KAKA wa BIBI MGANGA SEMHUMBA, aliyekuwa mtoto pekee kwa MWAMHUMBA, aliyefariki mara tu baada ya kumzaa BIBI MGANGA SE-MHUMBA kwa Sekindole.

BIBI MGANGA  aliolewa kwa MWALAMBA SAMBAGI, ambapo alibahatika kuzaa nae watoto kadhaa ambao ni:
1.     Lyamturo          Sambagi
2.     Mtemelavanu     Sambagi

Kuhusiana na watoto wengine wa Ukoo wa akina SAMBAGI ambapo timu ya Utafiti ya KAUKI bado inaendelea kutafuta taarifa zao. Ukoo wa akina SAMBAGI unapatikana zaidi katika maeneo ya WELU, yaliyopo karibu kabisa na KALENGA-Iringa, hali kadhalika kuzunguka eneo la TOSAMAGANGA na IPAMBA, Iringa.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa baadhi ya Ukoo wa SAMBAGI walilelewa na BABU yao KAHENGULA SALAMALENGA KIVENULE. KAUKI ipo katika mchakato wa kuendelea kutafiti zaidi taarifa mbalimbali za ukoo huu kwa kutuma ujumbe wake eneo la WELU - Iringa.

Historia inaonesha kuwa Babu Salamalenga Kahengula Kivenule alikuwa ameoa  wake watatu ambao ni:
1.     Bibi Semkonda
2.     Bibi Semfilinge
3.     Bibi Nyangali

Babu Salamalenga Kivenule anapomuoa Bibi Semkonda alimkuta na mtoto wa kufikia Sipanganakumtwa Mwilongo Regina Sematagi. Kwa wake zake hawa watatu, Babu Salamalenga alibahatika kupata watoto kumi na tatu (13). Kwa Bibi Semkonda alibahatika kupata watoto wafuatao:
1.     Pangayena        Kivenule
2.     Jonas               Kivenule
3.     Samwel             Kivenule
4.     Galasamaneno   Kivenule
5.     Daud (William)   Kivenule
6.     Barton              Kivenule

Kwa mke wa pili Bibi Semfilinge, Babu Salamalenga alizaa nae watoto 3 ambao ni:
1.     Chogavanu                 Kivenule
2.     Munguatosa                Kivenule
3.     Mwilimilisa                 Kivenule

Na kwa mke wa tatu Bibi Nyangali, Babu Salamalenga alizaa nae watoto wanne (4) ambao ni:
1.     Tindasulanga              Kivenule
2.     Sigongola                   Kivenule
3.     Shaban                      Kivenule
4.     Gungamesa                 Kivenule
Historia inaonesha kuwa baadhi ya akina Bibi waliolewa kwa Babu zetu akina Kivenule walikuja na watoto wa kufikia. Hili tunaliona kwa Bibi Mkami Sekabogo ambapo wakati anaolewa na Babu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule, alikuja na mtoto aliyejulikana kama BIBI SIKIMBILAVI SEMABIKI. Hali kadhalika, ulezi wa watoto wa kufikia katika Ukoo wa Kivenule, uliendelea kwa upande wa Irore, ambapo tunaona kuwa BIBI SEMKONDA anapoolewa na Babu Kahengula Salamalenga Kivenule, alikuwa tayari ameshapata mtoto anayejulikana kama SIPANGANAKUMTWA MWILONGO REGINA SEMATAGI.

Bibi huyu MWILONGO, aliolewa katika Ukoo wa Mwa-MNYAVANU na kufanikiwa kupata watoto sita (6) ambao ni:
1.     Albert               Mnyavanu
2.     Teresia             Mnyavanu
3.     Alphonsina        Mnyavanu
4.     Helena             Mnyavanu
5.     Simon              Mnyavanu
6.     Michael             Mnyavanu

MWINGILIANO NA KOO NYINGINE KATIKA HIMAYA YA UHEHE
Zaidi ya Koo mbalimbali 50 zinachangamana na Ukoo wa Kivenule. Hii ni kutoka Karne ya 18 ambapo kizazi hiki kilianza kujitambua na kujikusanya. Baadhi ya Koo ambazo zimechangamana na ukoo huu ni pamoja na koo za:

1.     Kabogo
2.     Kamtawa
3.     Katowo
4.     Kigereso
5.     Kindole
6.     Kisumbe
7.     Kiteve
8.     Kitu
9.     Kusiga
10. Lawa
11. Luhwavi
12. Lupola
13. Madembwe
14. Manimu
15. Matagi
16. Mabiki
17. Mdongwe
18. Mfilinge
19. Mgoda
20. Mhapa
21. Mhumba
22. Mkeng'e
23. Mkonda
24. Mnonikirwa
25. Mnyavanu
26. Msisi
27. Mtono
28. Mvemba
29. Myalla
30. Ngeng'ena
31. Ngolo
32. Ngwenga
33. Ngweta
34. Nyakunga
35. Nyangali
36. Nyangalima
37. Twanga
38. Nzala
39. Sambagi
40. Senosa
41. Setala
42. Singaile
43. Utenga
44. Kalinga
45. Sungu
46. Mgimwa
47. Nyamika
48. Nongele

NAMNA YA KUHIFADHI KUMBUKUMBU ZA KAUKI
Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule, ni muhimu sana kwa kizazi cha sasa na kijacho; na pia ni mwendelezo wa ukusanyaji wa taarifa mbalimbali zinazohusiana na Ukoo wa KIVENULE; na pia kuzisambaza kwa jamii inayounda KAUKI. Mada hizi husaidia kuziboresha taarifa za Ukoo wa Kivenule zilizotangulia, kupitia taarifa mpya ambazo zinakuwa zimekusanywa kupitia mjumbe mmoja moja na Mikutano Mikuu ya KAUKI inayoendelea kufanyika kila mwaka.  Hali kadhalika, mada hii husaidia kurithisha Historia na Chimbuko la Ukoo wa Kivenule kwa kizazi cha sasa na baadaye; na pia kuweka mantiki ya dhana nzima kuhusiana na kuwepo kwa tunu zinazoheshimika na ukoo; na taarifa kadhaa zinazohusiana na Ukoo wa Kivenule na namna ya kuzihifadhi.

Katika mkakati wa kuhakikisha kuwa Taarifa Muhimu za Ukoo wa Kivenule zinahifadhiwa, Wana-KAUKI walipendekeza yachongwe Mawe yenye Majina ya Marehemu ambapo tutayaweka katika Makaburi. Sababu ya msingi ya kuchonga mawe ni kuwa siyo rahisi kufutika au kupotea.

Mkakati mwingine mahsusi wa kuhifadhi Taarifa na Historia ya Ukoo wa KIVENULE ni kuziweka katika Maandishi hususani Vitabu ambavyo vitasambwa kwa wanaukoo wote na kuweza kujisomea.

Hali kadhalika, mkakati maalum wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information Communication Technology-ICT) imeanza kutumika kwa lengo kuzitunza na kusambaza taarifa mbalimbali zinazohusiana na KAUKI na Ukoo wa Kivenule kwa ujumla. Kwa mfano mpaka sasa tuna Blogu zifuatazo ambazo zimesheheni taarifa za KAUKI na Ukoo wa KIVENULE  kwa ujumla:
http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com
http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.kauki-kauki.blogspot.com

Kwa bahati mbaya Blogu yenye anuani: www.tagumtwa.blogoak.com hatuwezi kuweka tena taarifa za KAUKI kwa sasa kwa sababu ya matatizo ya kiufundi yaliyo nje ya uwezo wetu. Ila tunaweza kupata taarifa mbalimbali ambazo zilikuwa tayari zimeshawekwa. Na kwa taarifa tu za kufurahisha, mpaka mwishoni mwa mwaka jana (2012), tulikuwa na watu karibu milioni 2 waliokuwa wametembelea/kuzifungua na kusoma taarifa zilizomo kwenye blogu yetu. Ni masikitiko makubwa kwetu kwa sababu blogu hii ilipata hitilafu ya kiufundi kutokana na wezi wa mtandao kujaribu kuiiba. Pamoja na jitihadi za kujaribu kuirudisha bado hazijafanikiwa. Ila binafsi naipigania kwa kuendelea kuihangaikia ili iweze kurudi tena.

Hali kadhalika Blogu binafsi ya Ndugu Adam Alphonce Kivenule ambaye pia ni Katibu Mkuu wa KAUKI, inatunza na kusambaza taarifa mbalimbali za KAUKI. Blogu hiyo inaitwa:
http://www.adamkivenule.blogspot.com

KAUKI pia katika mkakati wake kuhifadhi taarifa mbalimbali za Ukoo wa Kivenule imefungua Ukurasa wa Facebook. Anuani yake ni:
http://www.facebook.com/tagumtwa-kauki

Katika ukurasa wa facebook, taarifa mbalimbali za KAUKI huwekwa, pamoja na taarifa za mikutano, misiba, sherehe na hata salaam miongoni mwa wana-ukoo na hata watu wengine ambao ni marafiki zetu.

Au unaweza kutafuta tagumtwa-kauki katika ukurasa wa Google na kupata taarifa mbalimbali za KAUKI, Tagumtwa, Magubike, Kivenule, Kidamali na mambo mengine mengi.

Hali kadhalika, katika Mtandao wa Twitter pia KAUKI inapatikana kupitia jina la Babu yetu Tagumtwa.
http://www.twitter.com/tagumtwa
Hali kadhali taarifa za KAUKI zipo katika mfumo wa video na zimewekwa katika mtandao kupitia anuani zifuatazo:
http://www.youtube.com/tagumtwa-kauki
http://www.youtube.com/kivenule

Taarifa mbalimbali kuhusiana na video zilizochukuliwa katika matukio ya Wana-KAUKI zitaonekana, japo siyo nyingi. Matumizi ya video ndio kwanza tunajaribu na hata video zake hazina ubora sana kutokana na kukosekana kwa kamera za kisasa.

Katika suala la kuwasiliana na KAUKI, kuna anuani nyingi ambazo zimesajiliwa kwenye mtandao kama mkakati wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano; ambazo unaweza kuzitumia kutupatia taarifa au kuomba taarifa kutoka kwetu. Nazo ni barua-pepe (e-mail) zifuatazo:
tagumtwa@gmail.com
kivenule@gmail.com
tagumtwa-kauki@gmail.com
tagumtwa@yahoo.com
kauki2006@gmail.com

TAFSIRI ZA MAJINA MBALIMBALI YALIYOPO KATIKA UKOO WA KIVENULE
Kidagamhindi      Heka heka za kukimbia kodi wakati wa mkoloni
Tunyahindi          Kupigwa pigwa na wakoloni
Mwanitu              Alizaliwa kweusi (kwa kutumia lung’ali). Kuwasha moto ili kupata                      mwanga kwa kutumia kuni au aina fulani ya nyasi. Mara nyingi                         ving’ali vinakuwa vinazimika.
Kadungu              Kuwa na Dungu kubwa (kuwa na kitovu kikubwa)
Kibumo                Mvefi (Mtu anayelialia)
Mlagile                Alizaliwa wakati Bibi yake hayupo. Wakati anaonyeshwa Bibi yake                    akisema Mlagile  akaitwa Mlagile.
Fatamali              Alifuata mali
Yamkopita           Bibi alipomzaa mtoto wa kwanza na kisha kufariki, akapata jina                        la ya Mkopite

Luhanage            Wakati Bibi anazaa watoto wanakufa, alipomzaa mtoto na                               akaugua sana basi akaitwa Luhanage. Luhanage maana yake ni                         kuugua sana.
Mgendwa             Alizaliwa kwa taabu. Alizaliwa kwa waganga wa kienyeji kwa                           tabu wakiwa safarini
Msinziwa   
Kanolo                 Wakati ameugua, anapiga ramli huki akitembea kwa waganga.
Yimilengeresa     Mzee Babu Husein alichukuliwa kwenye Vita ya Pili ya Dunia.                            Wahindi walikufa sana na Waingereza wakashinda Vita.

Misamiti ya Lugha ya Kihehe
Mhisive                  Binamu
Nyavana                Degedege
Ligalu                    Vita
Watavangu             Wakubwa (Wakuu wa Nchi) kabla ya Ukoloni

KWA TAARIFA NA MAWASILIANO NA:
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) unatoa wito kwa Wana-ndugu, Wana-Ukoo, Jamii inayopenda kukuza utamaduni wa mtanzania, mashirika na taasisi mbalimbali za umma na kijamii, kuziangalia kazi zetu na pia kutupatia msaada pale inabidi. Hizi ni hatua tu za awali lakini bado tunaendelea na mkakati wa kutafuta taarifa nyingi zaidi kuhusiana na jamii yetu na Kabila la Wahehe kwa Ujumla.
Mpaka mwezi Desemba 2013, angalau sura ya Kitabu inaweza kuonekana kama Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema atatupatia uhai na afya njema.

Kwa taarifa na mawasiliano unaweza kutufikia kupitia.
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
Kando ya Barabara ya Hifadhi ya Ruaha
Sanduku la Posta 193
Kidamali, Iringa
Simu: +255 713 270364 (Katibu Mkuu-KAUKI)
Barua-pepe:        kauki2006@gmail.com
                            kivenule@gmail.com
                            tagumtwa.kauki@gmail.com
Blogu:        http://www.kauki-kauki.blogspot.com
                  http://www.tagumtwa.blogoak.com
                  http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com

Twitter:      https://twitter.com/kivenule
Facebook: https://www.facebook.com/kivenule

ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA WALIMU KWA NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA YATANGAZWA

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO  YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA   MWAKA 2013/2014

 MAELEKEZO MUHIMU:

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa tarehe 15/08/2013.

Fomu ya maelekezo (joining instruction) itatumwa kwa mhusika kupitia anuani yake. Aidha, fomu hizi zinapatikana pia kwenye tovuti hii  kwa kubofya katika link ya Chuo husika. 
Wanafunzi wanatakiwa kufika Vyuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
1. Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania kidato cha NNE na SITA kulingana na kozi husika;
2. Ada ya muhula wa kwanza sh.100,000/= au ya mwaka sh. 200,000/=;
 3. Sare ya Chuo kulingana na maelekezo ya Chuo husika; na
4. Fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi.

Mkuu wa Chuo anatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa Chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na SI vinginevyo.

Usajili wa waliochaguliwa kujiunga na Vyuo utafungwa tarehe 25/08/2013 saa 12.00 jioni.
 



Tuesday, 23 July 2013

Makabila Ya Tanzania



Orodha ya Makabila ya Tanzania
Kuna matatizo kwenye majina kadhaa katika orodha hii, kwasababu mbalimbali. Orodha hii inatokana na orodha ya Ethnologue ya lugha za Tanzania, pamoja na tovuti nyingine. Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya makabila ni majina ya lugha au lahaja badala ya makabila, na labda majina mengine yaliandikwa vibaya. Juu ya hivyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema kwamba kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vinavyo mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii za aina tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha lugha zao.

Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani. Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi kutoka vita katika nchi za jirani. Ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Arabia au Uhindi.

Waalagwa (pia wanaitwa Wasi),wanatokea Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa. Lugha yao ni Chasi. Waakiek,Waarusha,Waassa,

 Wabembe ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kigoma, Wilaya ya Kigoma Vijijini. Lugha yao ni Kibembe.

, Wabena ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Njombe.Lugha yao ni Kibena

, Wabende ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Mpanda. Lugha yao ni Kibende,

Wabondei ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Tanga, karibu na Milima ya Usambara. Lugha yao ni Kibondei.

, Wabungu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Chunya. Lugha yao ni Kibungu.

Waburunge ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa. Lugha yao ni Kiburunge

, Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo. Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia Mashariki Tarakea, Rombo hadi magharibi ya Kilimanjaro Siha, Machame. Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Marangu, Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo, Wa-Uru, na Wa-Siha.

• Lugha ya Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kimarangu, Ki-Old Moshi,Kikibosho, Kimachame, Kikirua na Kisiha. Lugha hizi zinakaribia kufanana kulingana na jinsi makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Ki-Old Moshi kinafanana na Kikirua, ambacho nacho kinafanana kidogo na Kimarangu. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.

Majina ya Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo. Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.

Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.

Wadatooga (pia huitwa Wataturu, Wamang'ati au Wabarabaig) ni kabila la Tanzania wanaoishi katika mikoa ya Manyara na Singida. Lugha yao ni Kidatooga

Wadigo ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Tanga, hasa kwenye mji wa Tanga. Pia wako Kenya wanapoishi upande wa Kusini wa mji wa Mombasa. Katika Kenya huhesabiwa kati ya mijikenda. Lugha yao ni Kidigo.

, Wadoe ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo. Lugha yao ni Kidoe.

, Wafipa ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Rukwa, hasa katika wilaya za Sumbawanga na Nkansi. Lugha yao ni Kifipa.

, Wagogo (mmojawao anaitwa Mgogo) ni kabila la Tanzania ya kati, wenyeji wa mikoa ya Dodoma na Singida. Lugha yao ni Cigogo (kwa Kiswahili hutamkika Kigogo).

Dini ya wengi wao ni Ukristo, hasa wa madhehebu ya Anglikana, halafu wa Kanisa Katoliki. Historia ya Wagogo inaweza kuelezeka kwa kuangalia yafuatayo: Utawala wa jadi, nyumba za asili, chakula kikuu na lafudhi ya lugha. Majina ya ukoo ya Cigogo

majina hayo ni kama Mazengo, Cidosa, Cilongani, Malecela, Mwaluko, Mavunde, Ndejembi, Manyesela, Mbogambi, Mdachi, Kapaya,Matonya, Mtunya, Kusila, Nhonya,Mhalanyuka, Mbenaa, Chibile, Mdoli, Lusinde,Njamasi,Majenda,Chiwamba,Mazoya,Ufinyu,Chilyawanhu,Magaya, Ngoli,Chiwanga,Lubeleje,Makupila,Fukunyi

Waha ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kigoma, pia mpakani na Burundi. Lugha yao ni Kiha.

Wahaya ni Kabila linalopatikana katika Mkoa wa Kagera, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, kandokando mwa Ziwa Victoria. Lugha yao ni Kihaya

Wahehe ni kabila la Tanzania ambalo kiasili linaishi katika wilaya za kaskazini za Mkoa wa Iringa, yaani Iringa, Kilolo na Mafinga.

Ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji. Ndiyo sababu wanazika wafu wao wakielekea mashariki.

Lugha yao (Kihehe) imegawanyika kiasi fulani katika lahaja (matamshi) tofautitofauti kutokana na maeneo ambayo huzungumzwa. Inafanana kimatamshi na kimaana na lugha ya Kibena iliyopo wilayani Njombe.

Wajita ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni Kijita.

Wakaguru ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilosa. Lugha yao ni Kikaguru.

Wakinga ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Makete. Lugha yao ni Kikinga

Wakuria ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara, pia wako Kenya. Lugha yao ni Kikuria
Waluguru ni kabila la Tanzania wanaoishi katika mikoa ya Morogoro na Pwani, hasa kwenye Milima ya Uluguru. Lugha yao ni Kiluguru.
Waluo (pia Wajaluo) ni kabila hasa la Kenya. Wako pia Uganda ya msahriki na wachache wanaishi nchini Tanzania katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni Kiluo. Wenyewe hujiita Jaluo na lugha yao Dhulou.na mengi kuhusu waluo.tembelea websitehii;www.jaluo.com utacheka mpaka ujambe puuu.ongito nyamwanda 0784334032 en an jakiseru jakanyango

Waluo ni mkusanyiko wa kabila la kinilotiki ambalo lilisafiri kutoka Afrika ya Kaskazini kufuata mto Nile kuja Kusini. Waluo wengi wameenea kandokando ya Ziwa Viktoria kutokana na utamaduni wao wa uvuvi. Kwa Afrika mashariki utawakuta nchini Sudan, Kenya, Uganda na Tanzania.Waluo mashuhuri

• Gidi Gidi Maji Maji - Waimbaji wa hiphop

• Tom Mboya - mwanasiasa aliyeuawa 1969

• Barack Obama - mwanasiasa na seneta wa Marekani ni mwana wa baba Mluo

• Jaramogi Oginga Odinga - kiongozi wa Waluo wakati wa uhuru, mwanzilishaji wa chama cha KANU na makamu wa rais wa kwanza

• Raila Amolo Odinga - mwana wa Jaramogi na mwanasiasa muhimu wa kitaifa

• Robert Ouko - waziri wa mambo ya nje aliyeuawa 1990

Wamasai ni kabila wazawa wa Afrika la watu wahamaji katika wanaopatikana Kenya kaskazini Tanzania.
Wamachinga ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, wilaya za Kilwa na Lindi. Lugha yao ni Kimachinga.

Kwa kipindi cha karne ya 21 wamekuwa maarufu katika miji kwa kuuza bidhaa wakiwa wameshika mkononi wakisaka wateja.

Wamakonde ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mtwara. Pia wako Msumbiji. Lugha yao ni Kimakonde.

Wamwera ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, hasa kwenye Wilaya ya Nachingwea. Lugha yao ni Kimwera.

Wandengereko ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Rufiji. Lugha yao ni Kindengereko.Hapana, Wandengereko hawaishi Mkoa wa Ruvuma bali mkoa wa Pwani kusini ya Dar es salaam katika Wilaya za Mkuranga na Rufiji.

Wangindo ni kabila la Tanzania wanaoishi upande wa Kusini wa Tanzania. Lugha yao ni Kingindo,

Wanyakyusa (pia huitwa Wangonde au Wasochile) ni jina kwa ajili ya watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania) upande wa kaskazini ya Ziwa Nyasa. Lugha yao ni Kinyakyusa. Mara nyingi Wagonde upande wa kusini ya mto Songwe nchini Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.

Kihistoria watu wanaoitwa leo Wanyakyusa waliitwa Wakonde na Wanyakyusa walikuwa kabila kubwa kati yao. Wakati wa karne ya 20 "Wanyakyusa" imekuwa jina la kundi kwa jumla. Hadi leo kanisa la kilutheri la KKKT linatumia jina "dayosisi ya Konde" kwa eneo lake katika mkoa wa Mbeya.

Wakati Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini ya Ziwa Nyasa mwisho wa karne ya 19 hawakuona tofauti ya kimsingi kati ya watu wa Malawi kaskazini na wale wa sehemu za Rungwe wakawaita wote "Wakonde" kutokana na jina lililokuwa kawaida ziwani.

Leo hii ni watu zaidi ya milioni wanaojumlishwa kwa jina hili, takriban 700,000 wanaokaa upande wa Tanzania na 300,000 wakikaa Malawi.


Wanyamwezi ni kabila la Tanzania wanaoishi katika mikoa ya Tabora na Shinyanga. Lugha yao ni Kinyamwezi.

Wasukuma ni kabila kubwa kutoka eneo la kusini na mashariki ya Ziwa Viktoria, nchini Tanzania. Kabila hili hasa huishi katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Mwaka 2001 idadi ya Wasukuma ilikadiriwa kuwa 3,200,000 [1]. Lugha yao ni Kisukuma. Kisukuma ni miongoni mwa lugha za Kibantu ambazo hubainishwa kama lugha mabishi.

Wayao ni kabila kutoka eneo la kusini ya Ziwa Nyasa. Mwaka 2001 idadi ya Wayao ilikadiriwa kuwa 1,942,000, ambao 1,000,000 wanaishi Malawi, 450,000 ni wakazi wa Msumbiji, na 492,000 wako Tanzania [1]. Lugha yao ni Kiyao.

Wazanaki ni kabila kutoka eneo la kaskazini-magharibi ya nchi ya Tanzaniai,
Wazaramo ni kabila kutoka eneo baina ya Dar es Salaam na Bagamoyo, nchini TanzaniaWazaramo ni sehemu ya Wabantu. Mababu wanaaminika waliingia katika eneo la Tanzania katika milenia ya kwanza. Historia yao ya kimdomo inasema ya kwamba walihamia pwani katika mazingira ya Daressalaam kutoka Uluguru (Morogoro) katika karne ya 18.

Walipokaa kwenye pwani walikuwa karibu na makazi ya Waswahili wakaanza kufaamiana na Uislamu. Taarifa za wakoloni Wajeruami mwanzoni wa karne ya 20 zinaonyesha ya kwamba wakati ule Uislamu ulikuwa umeenea kati ya Wazaramo na waliendelea kujiunga nayo haraka [2]. Siku hizi idadi kubwa wa Wazaramo ni Waislamu.

Makabila Mengine Ni Haya Hapa Chini

Wakabwa,Wazigula,Wazinza,Wazyoba,Wahadzabe (pia wanaitwa Watindiga),Wahangaza, Wakahe,Wakami,Wakara (pia wanaitwa Waregi),Wakerewe,Wakimbu,Wasumbwa,Waswahili,Watemi(piawanaitwaWasonjo),Watongwe,Watumbuka,Wavidunda,Wavinza,Wawanda,Wawanji,Waware(inaaminikalughayaoimekufa),,Wanyanyembe,Wanyaturu(piawanaitwaWarimi),Wanyiha,Wapangwa,Wapare(piawanaitwaWasu),Wapimbwe,Wapogolo,Warangi(auWalangi),Warufiji,Warungi,Warungu(auWalungu),Warungwa,Warwa,Wasafwa,Wasagara,Wasandawe,Wasangu,Wasegeju,Washambaa,Washubi,Wasizaki,Wasuba, Wanyambo,Wanyamwanga, ,Wandonde,Wangasa, ,Wandali,Wandamba,Wandendeule, .Wangindo,Wangoni,Wangulu,Wangurimi (au Wangoreme),Wanilamba (au Wanyiramba),Wanindi,Wamakua (au Wamakhuwa),Wamakwe(piawanaitwaWamaraba),Wamalila,Wamambwe,Wamanda,Wamatengo,Wamatumbi,Wamaviha,Wambugwe,Wambunga,Wamosiro,Wampoto,Wamwanga, ,Wamagoma, ,Wakutu,Wakw'adza,Wakwavi,Wakwaya,Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele),Wakwifa,Walambya, Wakisankasa,Wakisi,Wakonongo, Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome),Wagweno, Waikizu,Waikoma,Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu),Waisanzu,Wajiji