TANZIA
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa masikitiko makubwa
unawatangazia Wana-KAUKI, ndugu, jamaa, marafiki na wanaukoo kwa ujumla, kifo cha
Bi. Gidagumhindi Cecilia Sigatambule Kivenule, kilichotokea tarehe usiku wa
kuamukia tarehe 18 Aprili 2013, huko Magubike, Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.
Marehemu Gidagumhinda Kivenule alikuwa akiumwa kwa
muda mrefu na hasa akisumbuliwa na tatizo la upofu wa macho, homa, miguu na
uzee. Kabla ya mauti kumkuta, Marehemu alilazwa kwa muda wa wiki mbili katika
hospitali ya Ipamba, na hali yake kupata auheni lakini siku ya Jumatano tarehe
17 Aprili 2013 akiwa nyumbani hali ilibadilika na hatimaye kumpelekea mauti
kumfika usiku wa tarehe 18 Aprili 2013.
Bi Gidagumhindi ni Mtoto wa Kwanza kwa Bibi
Siwangumhavi Singaile, ambaye alikuwa Mke Mkubwa wa Sigatambule Tavimyenda Tagumtwa
Kivenule. Bibi Siwangumhavi alikuwa na watoto 7 ambapo mpaka sasa wamebaki
watoto 3 tu. Wengine waliomfuata Bi Gidagumhindi ni Semyamba Khadija Kivenule,
Sivinitu Alphonce Kivenule, Kadungu William Kivenule, Fibumo Xavery Kivenule,
Mlagile Anyesi Kivenule na John Kivenule.
Mazishi yake yalifanyika tarehe 18 Aprili 2013, eneo
la Magubike katika Makaburi ya Ukoo wa akina Nyangalima. Bi Gidagumhindi ataendelea
kukumbukwa kwa upendo, mshikamano na hamasa yake katika kuhakikisha kuwa KAUKI
inaendelea kuwa imara hususani katika eneo la Magubike.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi,
Amina.
Imeandaliwa na:
Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu - KAUKI
No comments:
Post a Comment