TANZIA
MZEE HUSSEIN TAVIMYENDA TAGUMTWA KIVENULE AFARIKI DUNIA
BABU HUSSEIN
TAVIMYENDA TAGUMTWA KIVENULE AMEFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 115, KATIKA
HOSPITALI YA IPAMBA IRINGA. MIPANGO YA MAZISHI BADO INAENDELEA KUFANYIKA NA
UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI). MZEE HUYU ALIZALIWA ENEO LA ULEFI, MAGUBIKE,
MKOANI IRINGA KUNAKO MIAKA YA 1890. KWA TAARIFA ZAIDI: http://www.kauki-kauki.blogspot.com
/http://www.tagumtwa.blogoak.com au simu 0713270364
E-mail:
kauki2006@gmail.com / kivenue@gmail.com
HISTORIA YA BABU HUSSEIN TAVIMYENDA TAGUMTWA
KIVENULE
Mzee Hussein Tavimyenda
Kivenule alikuwa ni mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo. Yeye aliishi eneo la
Ulefi na baadaye Mlafu. Kwa sasa alikuwa anaishi eneo la Magubike. Mpaka leo
hii anafariki, Babu Hussein Kivenule anakadiriwa kuwa na umri wa miaka zaidi ya
115 kwa mujibu wa taarifa na tafiti ambazo tunazo.
Babu Hussein Tavimyenda
Kivenule ameshiriki kikamilifu katika Vita vya Pili ya Dunia. Wakati anashiriki
vita hiyo alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 44. Amepigana vita maeneo
mbalimbali mfano Burma, India, Ulaya na Makoloni mbalimbali ya Waingereza. Alikuwa
anakabiliwa na upofu wa macho ambao anasema ulisababishwa na Baruti. Hali
kadhalika anakiri kuwa kuendelea kuwa hai ni kwa sababu alipigana upande wa
Mwingereza. Anakiri vita ndiyo iliyomsababishia upofu pengine asingekuwa na hali
aliyonayo kwa sasa.
Mzee Hussein Kivenule alioa
wake wawili na kubahatika kupata watoto kumi na tatu (13). Kwa mke wake wa
kwanza Bibi Yimilengeresa Semsisi. Babu Hussein alipata watoto wafuatao:
1. Nyakudila Benjemin Kivenule
2. Sekiyavile Modesta Kivenule
3. Dominicus Kivenule
4. Emmanuel Kivenule
5. Luciana Kivenule
6. Ajendina Kivenule
Kwa upande wa mke wa pili wa
Bibi Dalika Setala, Mzee Hussein Kivenule alipata watoto wafuatao:
1. Kabogo Bernadi Kivenule
2. Sembata Josephine Kivenule
3. Necia Kivenule
4. Batromeo Kivenule
5. Brandino Kivenule
6. Tavina Kivenule
7. Masikitiko Kivenule
Asilimia kubwa ya familia ya
Babu Hussein Kivenule inaishi maeneo ya Magubike, Idete na Ibogo. Pia wapenda
historia mnakaribishwa kwenda kumtembelea Babu Hussein Kivenule.
No comments:
Post a Comment