Toleo la
Kwanza - 2013
UKOO NI NINI?
Ukoo
ni muungano wa familia kadhaa zenye utambulisho fulani. Unaweza kuwa
utambulisho wa jina, alama au mwelekeo mmoja. Utambulisho wowote kati ya hizo
nilizotaja, unaufanya ukoo utambulike miongoni mwa jamii mbalimbali. Mara
nyingi utambulisho ambao huufanya ukoo utambulike baina ya jamii za Kiafrika ni
Jina. Pamoja na jina, halikadhalika kuna tunu (values) mbalimbali ambazo
huheshimiwa na ukoo husika na jamii kwa ujumla.
Tunu
hubeba mambo mengi, ikiwa ni pamoja na miiko, maadili, heshima, vyakula na
tamaduni. Sambamba na tunu, pia kuna Mila na Desturi, ambazo huzingatiwa sana
katika masuala ya kijamii, mfano wakati wa kuoa au kuoza, misiba, sherehe za
jadi mfano matambiko na masuala ya kimila.
Ukoo
wa Kivenule ni mmojawapo wa koo nyingi kubwa zilizopo katika Himaya ya Uhehe
katika Mkoa wa Iringa. Ukoo wa Kivenule ulianza kutambulika toka Karne ya 18.
Historia inaonesha kuwa Ukoo huu asili yake ni kutoka kwa Wabena-Manga, waliopo
Kusini mwa Mji wa Iringa; yaani maeneo ya Mufindi na Njombe. Ni mchanganyiko wa
Wahehe na Wabena wanaojulikana kama Wabena-Manga.
Wahehe
ni moja kati ya makabila makubwa hapa Tanzania ambalo kiasili linaishi katika Wilaya
za Kaskazini mwa Mkoa wa Iringa, yaani Iringa Vijijini, Iringa Mjini, Kilolo na
Mufindi. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinazopatikana na kutafitiwa,
inasemekana kuwa ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto
Rufiji; yaani Wahehe wenye Asili ya Ungazija. Pengine hata ile sababu ya kuzika
wafu wao wakielekea mashariki inapewa uzito.
Lugha
ya Kabila hili ni Kihehe na limegawanyika kiasi fulani katika lahaja (matamshi)
tofauti tofauti kutokana na maeneo ambayo huzungumzwa. Inafanana kimatamshi na
kimaana na lugha ya Kibena iliyopo wilayani Njombe. Pamoja na Wabena wanaohesabika
kuwa zaidi ya watu milioni moja. Wengi wao ni wafuasi wa Ukristo, hasa wa
Kanisa Katoliki (Jimbo Katoliki la Iringa). Kihistoria Wahehe ni maarufu kwa
jinsi walivyopambana na Wajerumani walioteka maeneo yao, kama katika mapigano ya
Lugalo mwaka 1891. Kiongozi wao alikuwa Chifu Mkwawa.
Katika
kuenzi na kutunza tunu za asili za Uhehe, Ukoo wa Kivenule hauli nyama ya
Mbawala (kwa lugha ya Kihehe Mato/Imato). Imani kubwa imejengeka miongoni mwa
jamii ya Ukoo wa Kivenule kuwa kula Mbawala ni kuvunja miiko ya Ukoo ambayo
iliyowekwa na Waasisi wetu (Babu zetu). Mara mwanaukoo anapokiuka miiko hii na
kula nyuma ya Mbawala (Imato) basi huweza kufikwa na matatizo mbalimbali, mfano
kudhurika afya yake. Mara nyingi huwapata matatizo kama ya kuvimba miguu na
pengine kuoza kabisa.
Tunu
nyingine ambazo Ukoo wa Kivenule unazienzi kama zilivyo koo nyingine katika
Uhehe ni Miitikio (Midikiso). Tunu hii huutambulisha
Ukoo wa Kivenule miongoni mwa Koo za Wahehe. Mwitikio (Mwidikiso) wa Ukoo wa
Kivenule ni 'MLIGO'. Mwitikio huu hutumika
katika maeneo mbalimbali mfano katika salamu, kuapa (kufanya viapo) na pia kujitofautisha
na koo nyingine. Miitikio (Midikiso) huutambulisha Ukoo wa
Kivenule katika koo nyingine katika ardhi ya Uhehe.
CHIMBUKO LA UKOO WA KIVENULE
Historia ya Chimbuko la Ukoo wa Kivenule limetoka mbali zaidi hata
kabla ya Jina la sasa la KIVENULE kupatikana. Utafiti unaonesha kuwa BABU NYAKUDIRA BALAMA ndiye aliyemzaa
(Baba yake) BABU KANOLO BALAMA. Hapa
tunauangalia Ukoo wa Balama. Hali
kadhalika, BABU KANOLO BALAMA,
akamzaa BABU MTENGELINGOMA BALAMA. Maelezo
haya yote tunayoyazungumzia ni katika Karne ya 17 kabla ya kuja kwa BABU TAGUMTWA BALAMA, ambaye aliuleta
Jina la KIVENULE.
BABU
MTENGELINGOMA BALAMA ndiye Baba Mzazi wa TAGUMTWA BALAMA. Wakati huu Babu
Tagumtwa Balama alikuwa hajaenda kwenye Vita za LIGALU.
Kwa
Asili, Ukoo wa Balama na baadaye Kivenule ni maarufu kama Wapiganaji wa Vita.
Ukoo wa Balama (Kivenule) ulikuwa hodari sana katika vita vya msituni ambavyo
viliwahusisha Babu zetu akina TAGUMTWA.
Enzi hizo za Mababu zetu vita za Koo na Kabila zilipiganwa maeneo mengi ya
himaya ya Uhehe kwa lengo la kupata mali, mifugo na heshima.
Babu TAGUMTWA BALAMA (KIVENULE) ndiye
aliyewazaa Babu TAVIMYENDA KIVENULE na Babu KALASI KIVENULE. Ikumbukwe kuwa, jina halisi la ukoo wa
Kivenule ni BALAMA. Kama
ilivyokwisha julikana katika mada zilizowasilishwa katika Mikutano Mikuu Tisa
ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), ambapo ilielezwa kuwa, neno KIVENULE linamaanisha sifa ya kuwa jasiri Vitani na hasa katika kutumia
silaha za Mishale na Mikuki yaani kwa Lugha Asilia ya Kihehe
“KUMIGOHA”. Yaani kwa maana nyingine LIGALU yenye maana ya Kwihoma
Imigoha – Kuhoma Vatavangu au Kuvenula
Avatavangu. LIGALU maana yake Vita. Kuhoma maana yake Kuchoma na Migoha maana
yake Mikuki. Venula maana yake ua, fyeka
maadui.
LIGALU ndiyo iliyochangia
kuzaliwa kwa jina la Ukoo la KIVENULE.
KIVENULE maana yake ni Ushujaa kutokana na Shabaha ya Mikuki.
KUVENULA likiwa na maana halisi
ya kuwa na shabaha ya kuwaangamiza maadui kwa kutumia silaha ya Mishale na
Mikuki. Babu zetu akina TAGUMTWA BALAMA
walilidhihirisha hili katika Vita na Watavangu na hivyo kusababisha kuzawadiwa
kwa jina la KIVENULE kama jina la sifa kutokana na ushujaa katika Vita.
Tagumtwa Balama asili yake ni kutoka katika Ukoo
wa Balama. Sifa kubwa ya Tabu Tagumtwa, alikuwa ana Shabaha sana ya Mikuki
katika uwanja wa Vita. Alikuwa hakosei shabaha
(target) na hivyo hupelekea
kuwaangamiza na kuwaua sana maadui. Wakati akiwamaliza/fyeka/kuwaua adui zake
kwa Mikuki, Wakuu wa Vita (Vatavangu) walikiita kitendo hicho 'KUVENULA'. Taarifa za Tagumtwa kuua
(Kuvenula) adui zake katika uwanja wa vita, zilizagaa kila mahali na hivyo
kupelekea Wakuu (Viongozi) wa Vita (Vatavangu) kumzawadia Jina la KIVENULE, kama jina la sifa na heshima kwa kuwa shujaa wa Vita.
Ikumbukwa
kuwa asili ya Ukoo wa Kivenule ni kutoka katika ukoo wa BALAMA (MWIBALAMA). Hawa ni ndugu wa karibu wa Kivenule kabisa na
hawapaswi kuoana. Koo za Mwibalama zinapatikana maeneo mengi katika Mkoa wa
Iringa hususani katika Wilaya za
Mufindi, Iringa Vijijini, Iringa Mjini na Kilolo; hali kadhalika kama ilivyo
ukoo wa kina Mwakivenule.
TAGUMTWA KIVENULE alifia
katika uwanja wa mapambano (vita) na mwili wake haukuweza kupatikana. Kama
zilivyo koo za machifu au watu maarufu miili yao ilikuwa haizikwi. Baada ya
kufa iliegemezwa kwenye miti mikubwa na kuliwa na wanyama. Wakija watu
wasiukute mwili basi huamini kuwa mwili umechukuliwa na Mungu.
KUKUA NA KUZAGAA KWA UKOO
WA KIVENULE
Kwa
mujibu wa taarifa mbalimblai za kitafiti ambazo zimekuwa zikifanyika toka mwaka
2005 hadi sasa 2013; kupitia mikutano mbalimbali ya KAUKI; zinabainisha kuwa,
BABU NYAKUDIRA BALAMA alimzaa BABU KANOLO BALAMA. Hali kadhalika
BABU KANOLO BALAMA alimzaa MTENGELINGOMA BALAMA. BABU MTENGELINGOMA BALAMA
ndiye aliyemzaa Tagumtwa Balama (Kivenule).
Baada
ya hapo, tunaona sasa Kizazi cha TAGUMTWA
KIVENULE kinaanza kujitokeza. Hii ilikuwa ni Karne ya 18. TAGUMTWA KIVENULE
alizaa watoto wawili (2). Bado utafiti
unafanyika kumfahamu Mama wa watoto hawa. Watoto wa Tagumtwa Kivenule walikuwa ni
TAVIMYENDA KIVENULE na KALASI KIVENULE.
Kwa mujibu wa taarifa kadhaa tulizonazo kwa sasa; hawa ni vinara wa Ukoo wa
Kivenule ulioenea maeneo mbalimbali hapa Tanzania.
Tavimyenda
Kivenule na Kalasi Kivenule katika harakati za kutafuta maisha walifika katika
eneo la Kalenga, mahali alipoishi Mkwawa na kukutana na na Mwamyinga, aliyekuwa
mfugaji maarufu katika eneo la Ulefi huko Magubike, Iringa Vijijini. Tavimyenda
Kivenule alibahatika kupata kazi kwa Mwa-Myinga baada ya kuombwa kwenda
kumwangalizia mifugo yake huko Magubike, huku akimwacha mwenzake Kalasi pale
Kalenga.
Kalasi
Kivenule yeye hakupata fursa hiyo ya kazi na hivyo akaamua kuelekea eneo Irore
katika Wilaya Iringa Vijijini (kwa sasa Kilolo) kutafuta maisha. Huu ukawa ni
mwanzo wa kugawanyika kwa watoto hawa wawili wa Tagumtwa Kivenule.
Tavimyenda
Kivenule akielekea upande wa Magharibi mwa Mji wa Iringa na Kalasi alielekea
upande wa Mashariki mwa Mji wa Iringa.
Historia
inabainisha kuwa pamoja na Babu hawa kugawanyika kutokana na utafutaji wa
maisha, mahusiano na ushirikiano baina yao haukuvunjika. Babu zetu waliendelea
kushirikiana na kutembelea licha ya ukoo kukua na kuwa mkubwa sana.
KIZAZI CHA TAVIMYENDA
KIVENULE
Katika
Karne ya 19 hadi 20, Kizazi cha Tavimyenda Kivenule kilizaliwa na kuzagaa
katika maeneo ya Ulefi, Magubike na Mlafu, Wilaya ya Iringa Vijijini, Iringa
Mjini na maeneo mengine mkoani Iringa.
Taarifa
tulizonazo kupitia tafiti tunazofanya, hali inaonesha kuwa, Babu Tavimyenda
alikuwa na wake watatu (3), ambao ni:
1.
Bibi Mkami Sekabogo
2.
Bibi Senosa
3.
Bibi Pili
Mvemba
Mke
wa kwanza wa Tavimyenda Kivenule aliolewa akiwa na mtoto; aliyejulikana kama
Bibi Sikimbilavi Semabiki. Kwa mke huyu wa Kwanza Sekabogo, Tavimyenda alizaa
nae watoto wanne (4); ambao ni:
1.
Babu Kavilimembe Kivenule
2.
Babu Mgaifaida Kivenule
3.
Babu Sigatambule Kivenule
4.
Babu Hussein Kivenule (Bado yupo hai)
Kwa
Mke wa Pili Bibi Senosa, Babu Tavimyenda akizaa nae watoto watatu (3); ambao
ni:
1.
Babu Abdallah Kivenule
2.
Bibi Sigungilimembe Kivenule
3.
Bibi Malibora Kivenule
Watoto
hawa wa Bibi Senosa waliishi maeneo ya Kihesa katika Mji wa Iringa.
Kwa
upande wa mke wa Tatu wa Bibi Pili Mvemba; Babu Tavimyenda alizaa mtoto mmoja
aliyejulikana kwa jina la BIBI MGASI KIVENULE aliishi eneo la Ulefi. Baada ya
kufariki amezikwa Mlafu. Babu Tavimyenda Kivenule amezikwa katika eneo la
Ulefi.
Bibi SIKIMBILAVI alikuwa
mtoto wa kufikia wa Bibi MKAMI SEKABOGO. Bibi
SIKIMBILAVI aliolewa na Ukoo wa
Mgoda na kubahatika kupata watoto wanne (4) ambao ni:
1.
Mama wa Kitatambe
2.
Salia Maneno
Mgoda
3.
Galamale Mgoda
4.
William Mgoda
Baada
ya hapo kizazi hiki kimeendelea kukua hadi hivi sasa Karne ya 21. **Angalia Chati kuonesha Muundo wa Ukoo wa KIVENULE**
KIZAZI CHA KALASI
KIVENULE
Kwa
upande wa Kalasi Tagumtwa Kivenule, kizazi hiki kilienea maeneo ya Nduli,
Mgongo, Itagutwa, Kigonzile, Igominyi na Irore. Taarifa zinaonesha kuwa, Babu
Kalsi Kivenule alikuwa na wake wawili (2); yaani:
1.
Bibi Semsakwa
Mnonikilwa
2.
Bibi Mnyamtage
Sekindole
Bibi
Semsakwa Mnoni Kirwa kwa Babu Kalasi Kivenule alizaa watoto wawili (2) ambao
ni:
1.
Bibi Cheilaje Nginasambula Kivenule
2.
Gingilemesa Kivenule
Kwa
bahati mbaya hakuna taarifa zozote za hawa watoto wawili wa Kalasi.
Kwa
upande wa Bibi Mnyamtage Sekindole, Babu Kalasi Kivenule alizaa mtoto mmoja
ambaye ni Salamalenga Kahengula Kivenule. Bibi Mnyatage Sekindole awali alikuwa
ameolewa kwa Mwa-Mhumba na kuzaa nae mtoto mmoja aliyeitwa Bibi Mganga Semhumba
na baadaye kufariki. Baada ya hapo aliolewa na Kalasi ambapo pia alizaa mtoto
mmoja tu anayefahamika kwa jina la Salamalenga Kahengula Kivenule. * Angalia
watoto wa Kahengula katika Chati ya Muundo wa Ukoo wa Kivenule*
Kuna
taarifa nyingi kutoka kwa Babu Tavimyenda Kivenule na Kalasi Kivenule.
Mwingiliano wa koo nao unaonesha simulizi hizi. Kwa upande wa Tavimyenda mke wa
Kwanza Bibi Mkami Sekabogo alikuwa na mtoto wa kufikia, aliyejulikana kwa jina
la Bi Sikimbilavi Semabiki. Hatujapata taarifa rasmi kuhusiana na kizazi cha
Bibi huyu, kama ilivyotokea kuwa Sipanganakumtwa Mwilongo Regina Sematagi
aliyekuwa mtoto wa kufikia Bibi Semkonda mke wa Salamalenga Kahengula Kivenule.
Sipanganakumtwa
Mwilongo Regiona Sematagi amesaidia kueneza kizazi cha Ukoo wa Mnyavanu. Taarifa
zaidi na ukoo wa Mnyavanu upo katika Chati ya Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa
Kivenule.**
TABIA YA KIZAZI CHA
TAVIMYENDA NA KALASI KIVENULE KUOA WAKE WENGI
Tabia
nyingine ya kizazi hiki cha Tavimyenda na Kalasi ilikuwa ni kuoa wake wengi.
Kwa mfano Tavimyenda pekee alikuwa na wake watatu. Hali kadhalika Kalasi naye
alikuwa na wake wawili.
Hali
hii ya kuwa na mke zaidi ya mmoja walirithi watoto wao. Kwa mfano watoto watatu
wa kiume wa Tavimyenda waliozaliwa kwa Bibi Mkami Sekabogo walioa wake wawili
hadi watatu. Mtoto wa kwanza wa Babu Tavimyenda Kivenule aliyejulikana kama
Kavilimembe Kivenule alikuwa na wake wawili (2). Mtoto wa tatu wa Bibi Mkamai
Sekabogo, aliyejulikana kwa jina la Sigatambule Matesa Kivenule, alikwa na wake
watatu. Hali kadhalika mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo anayejulikana kama
Hussein Kivenule alikuwa na wake wawili. Mtoto pekee wa Pili wa Bibi Mkami
hakubahatika kuwa na familia; na alijiita jina la kujinyanyapaa "Mgaifaida"
Kivenule.
Sambamba
na tabia ya Ukomo wa Kivenule kuoa mke zaidi ya moja; pia kuna utamaduni
uliojitokeza kwa baadhi ya watoto wa Bibi Mkami Sekabogo kuoa dada na mdogo
wake. Hili linajidhihirisha kwa wake wawili wa Babu Kavilimembe Kivenule ambao
walikuwa ni Bibi Sikumwendinguluvi Sekusiga (Bi Mkubwa) na Bibi Gakumwalia
Sekusiga (Bi Mdogo).
Hali
kadhalika kwa mtoto wa tatu wa Bibi Mkami Sekabogo; Babu Sigatambule Matesa
Kivenule alioa wake watatu, ambapo wake wawili wakubwa, 'Bibi Sikumwendinguluvi
Singaile (Bi Mkubwa) na Bibi Nyanyilemale Singaile (Bi Mdogo wa Pili); na wa
tatu aliitwa Bibi Pangulimale Setwanga.
Mtoto
wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo Hussein Kivenule, yeye alioa wake wawili kutoka
familia tofauti. Wake zake waliitwa Bibi Yimilengeresa Semsisi (Bi Mkubwa) na
Bibi Dalika Setala (Bi Mdogo). Kwa upande wa watoto Kalasi Kivenule, mtoto wake
Salamalenga Kahengula Kivenule naye alioa wake watatu; ambao ni Bibi Semkonda,
Bibi Semfilinge na Bibi Nyangali.
Hatujapata
taarifa rasmi za watoto wa Kalasi kutoka kwa mke wake Bibi Semsakwa Mnonikilwa
ambao ni Cheilaje Nginasambula Kivenule na Gingilemesa Kivenule. Kwa upande wa
Kahengula yeye alioa kutoka katika familia tofauti.
UZAO WA BABU
KAVILIMEMBE, MGAIFAIDA, SIGATAMBULE NA HUSSEIN KIVENULE
Babu
Kavilimembe Kivenule aliishi eneo la Magubike, Wilaya ya Iringa Vijijini, huku
akipakana na Ulefi upande wa Kaskazini, Idete na Ibogo upande wa Magharibi.
Akiwa ameoa wake wawili wa familia moja, Babu Kavilimembe alibahatika kupata
watoto sita (6).
Kwa
upande wa mke wa kwanza Bibi Sikumwendinguluvi Sekusiga; Mzee Kavilimembe
Kivenule alipata watoto wafuatao:
1.
Elizabert Kivenule
2.
Dalikimale Kivenule
3.
Sandra Kivenule
4.
Pangalasi Kivenule
Na
kwa mke mdogo Bibi Gakumwalia Sekusiga, Mzee Kavilimembe alipata watoto wawili
ambao ni:
1.
Salikuvaganga Kivenule
2.
Francis Kivenule
Watoto
hao wa Babu Kavilimembe wengi wao waliishi maeneo ya Ulefu na Magubike. Baadhi
yao walihamia maeneo mengine kama Nzihi, ukiacha wale waliokuwa watumishi wa
serikali wakaenda kuishi maeneo mbalimbali. Babu Kavilimembe amezikwa eneo la
Magubike, Iringa Vijijini.
Kwa
upande wa Babu Mgaifaida (Yakobo) Kivenule, yeye hakubahatika kupata familia.
Mgaifaida alikuwa na ulemavu ambao ulimfanya ashindwe kutembea katika hali ya
kawaida. Muda mwingi aliishi eneo la Ulefu kabla ya sehemu kubwa ya Ukoo wa
Kivenule kuhamia sehemu ya Mlafu. Baada ya kufariki, alizikwa Mlafu.
Babu
Sigatambule Matesa Kivenule alikuwa ni mtoto wa tatu wa Tavimyenda Kivenule kwa
Bibi Mkami Sekabogo. Babu Sigatambule aliishi Ulefi, akahamia Mlafu na baadaye
Kidamali. Babu Sigatambule ndiye aliyehakikisha Ukoo wa Kivenule unapata eneo
la Mlafu huku akipambana na Wagiriki. Walowezi na wawekezaji katika zao la
Tumbaku.
Babu
Sigatambule Kivenule katika uhai wake alibahatika kuoa wake watatu (3); huku
wake zake wawili wakitoka katika familia moja ya ukoo wa Singaile. Wake zake
hawa wakubwa waliitwa Bibi Sivangumhavi Singaile na Bibi Nyanyilimale Singaile.
Mke wa Tatu wa Babu Sigatambule aliitwa Bibi Pangulimale Setwanga. Wote
waliishi Mlafu na baadaye kuhamia eneo Kidamali.
Wake
zake wawili Bibi Nyanyilimale Singaile na Bibi Pangulimale Setwanga bado wapo
hai na wanaishi Kidamali mpaka leo.
Watoto
wa Babu Sigatambule Kivenule ni hawa wafuatao:
Kwa
Bibi Sivangumhavi Singaile (Mke Mkubwa):
1.
Gidagumhindi Cecilia
Kivenule
2.
Semyamba Khadija Kivenule
3.
Sivinitu Alphonce
Kivenule
4.
Kadungu William
Kivenule
5.
Fibumo Xavery
Kivenule
6.
Mlagile Anyesi
Kivenule
7.
John Kivenule
Bibi
Nyanyilimale Singaile (Mke wa Pili)
1.
Mgulwa Agnes
Kivenule
2.
Luhanage Ponsiano
Kivenule
3.
Mgendwa Eusebio
Kivenule
4.
Msinziwa Daniel Kivenule
5.
Kanolo Edward
Kivenule
Mke
wa Tatu wa Bibi Pangulimale Setwanga
1.
Conjeta Kivenule
2.
Pyela Kivenule
3.
Faustino Kivenule
4.
George Kivenule
5.
Carolina Kivenule
Babu
Sigatambule Kivenule alifariki mwaka 1995 na kuzikwa eneo la Mlafu, Kidamali -
Iringa. Hali kadhalika mke wake Mkubwa Bibi Siwangumhavi Singaile Mwilumbwa
alifariki dunia mwaka 1999 na kuzikwa eneo hilo hilo la Mlafu.
Mzee
Hussein Tavimyenda Kivenule alikuwa ni mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo.
Yeye aliishi eneo la Ulefi na baadaye Mlafu. Hatimaye alihamia Magubike. Babu
Hussein Kivenule hadi anafariki dunia Juni 26, 2013 anakadiriwa kuwa na miaka
zaidi ya 113 kwa mujibu wa taarifa na tafiti ambazo tunazo.
Babu
Hussein Tavimyenda Kivenule ameshiriki kikamilifu katika Vita vya Pili ya
Dunia. Wakati anashiriki vita hiyo alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 44.
Amepigana vita maeneo mbalimbali mfano Burma, India na Ulaya. Kwa sasa ana
upofu wa macho ambao anasema ulisababishwa na Baruti. Hali kadhalika anakiri
kuwa kuendelea kuwa hai ni kwa sababu alipigana upande wa Mwingereza. Anakiri
vita ndiyo iliyomsababishia upofu pengine asingekuwa na hali aliyonayo kwa
sasa.
Mzee
Hussein Kivenule alioa wake wawili na kubahatika kupata watoto kumi na tatu
(13). Kwa mke wake wa kwanza Bibi Yimilengeresa Semsisi. Babu Hussein alipata
watoto wafuatao:
1.
Nyakudila Benjamin
Kivenule
2.
Sekiyavile Modesta
Kivenule
3.
Dominicus Kivenule
4.
Emmanuel Kivenule
5.
Luciana Kivenule
6.
Ajendina Kivenule
Kwa
upande wa mke wa pili wa Bibi Dalika Setala, Mzee Hussein Kivenule alipata
watoto wafuatao:
1.
Kabogo Bernadi Kivenule
2.
Sembata Josephine Kivenule
3.
Necia Kivenule
4.
Batromeo Kivenule
5.
Brandino Kivenule
6.
Tavina Kivenule
7.
Masikitiko Kivenule
Asilimia
kubwa ya familia ya Babu Hussein Kivenule inaishi maeneo ya Magubike, Idete na
Ibogo. Pia wapenda historia mnakaribishwa kwenda kumtembelea Babu Hussein
Kivenule.
UZAO WA SALAMALENGA
KAHENGULA KIVENULE
Babu
Salamalenga Kahengula Kivenule alikuwa ni mtoto pekee wa kiume wa Babu Kalasi
kwa mke wake wa pili Bibi Mnyamtage Sekindole. Kahengula pia ni kaka wa Bibi
Mganga Semhumba, aliyekuwa mtoto pekee kwa Mwamhumba, aliyefariki mara tu baada
ya kumzaa Bibi Mganga kwa Sekindole.
Babu
Salamalenga Kahengula Kivenule alio wake watatu ambao ni:
1.
Bibi Semkonda
2.
Bibi Semfilinge
3.
Bibi Nyangali
Salamalenga
anapomuoa Bibi Semkonda alimkuta na mtoto wa kufikia Sipanganakumtwa Mwilongo
Regina Sematagi. Kwa wake zake hawa watatu, Babu Salamalenga alibahatika kupata
watoto kumi na tatu (13). Kwa Bibi Semkonda alibahatika kupata watoto wafuatao:
1.
Pangayena Kivenule
2.
Jonas Kivenule
3.
Samwel Kivenule
4.
Galasamaneno Kivenule
5.
Daud (William) Kivenule
6.
Barton Kivenule
Kwa
mke wa pili Bibi Semfilinge, Babu Salamalenga alizaa nae watoto watatu ambao
ni:
1.
Chogavanu Kivenule
2.
Munguatosa Kivenule
3.
Mwilimilisa Kivenule
Na
kwa mke wa tatu Bibi Nyangali, Babu Salamalenga alizaa nae watoto wanne (4)
ambao ni:
1.
Tindasulanga Kivenule
2.
Sigongola Kivenule
3.
Shaban Kivenule
4.
Gungamesa Kivenule
MWINGILIANO NA KOO
NYINGINE KATIKA HIMAYA YA UHEHE
Zaidi
ya Koo mbalimbali 50 zinachangamana na Ukoo wa Kivenule. Hii ni kutoka Karne ya
18 ambapo kizazi hiki kilianza kujitambua na kujikusanya. Baadhi ya Koo ambazo
zimechangamana na ukoo huu ni pamoja na koo za:
1.
Kabogo
2.
Kamtawa
3.
Katowo
4.
Kigereso
5.
Kindole
6.
Kisumbe
7.
Kiteve
8.
Kitu
9.
Kusiga
10.
Lawa
11.
Luhwavi
12.
Lupola
13.
Madembwe
14.
Manimu
15.
Matagi
16.
Mdongwe
17.
Mfilinge
18.
Mhapa
19.
Mhumba
20.
Mkeng'e
21.
Mkonda
22.
Mnonikirwa
23.
Mnyavanu
24.
Msisi
25.
Mtono
26.
Mvemba
27.
Myalla
28.
Ngeng'ena
29.
Ngolo
30.
Ngwenga
31.
Ngweta
32.
Nyakunga
33.
Nyangali
34.
Nyangalima
35.
Twanga
36.
Nzala
37.
Sambagi
38.
Senosa
39.
Setala
40.
Singaile
41.
Utenga
42.
Kalinga
43.
Sungu
44.
Mgimwa
45.
Nyamika
46.
Nongele
Kwa
taarifa na mawasiliano na:
Umoja
wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
http://www.kauki-kauki.blogspot.com
http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.
No comments:
Post a Comment