KAUKI ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005,
kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii
inayounda umoja huu na jamii nyingine kwa ujumla; hususani katika
kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana ili
kukabiliana na kuondokana na changamoto mbalimbali, likiwemo wimbi la
umaskini, ujinga, maradhi, migogoro ya ardhi, uongozi na utegemezi.
Ilibainika kuwa, ukoo unapokuwa mkubwa sana, basi huwepo na mahusiano
baina ya mtu mmoja na mwingine katika eneo husika mfano Kijiji, Kata
na Wilaya. Hali kadhalika, ilibainika kuwa, zaidi ya koo 40
zimechangamana na Ukoo wa Kivenule. Hivyo mwishowe hujikuta katika
Kijijini kizima, watu wanahusiana japo si moja kwa moja, bali kwa
kupitia mtu mmoja hadi mwingine.
Dira ya KAUKI inajizatiti kuwa na jamii elewa, angavu na inayowajibika
kwa kujitegemea; hali kadhalika Maono yake ikiwa ni kujengeana uwezo
kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia
mafunzo, kongamano, mijadala na mikutano kama hii, ili kuboresha
maisha.
Lengo kuu la KAUKI ni kuinua na kuboresha maisha ya Wana-KAUKI,
kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa kutumia ujuzi, maarifa na raslimali
zinazotuzunguka. Mipango ya KAUKI inajikita katika kujiimarisha katika
ngazi zote za kiutendaji, kiuendeshaji na kuleta mabadiliko ya
kiuchumi, kielimu, kisiasa, kimaendeleo na kimapinduzi.
Kwa muktadha huo, malengo mengine ya KAUKI ni pamoja na:
1.Kuchapisha Kitabu cha Historia ya Wahehe Toleo la Kwanza: Ndani ya
kitabu kutakuwa na sehemu zifuatazo: Historia ya Wahehe na Kuibuka kwa
Tawala na Koo mbalimbali ndani ya Uhehe (Wanitole, Wahabeshi,
Wangazija); Harakati za Mapambano ya Kikabila na Himaya mbalimbali
(Vita za Luhota; Mkwawa na Wajerumani; Mkwawa na Mnyigumba; Mkwawa na
Wabena, Wasangu na Himaya Mbalimbali; Sehemu ya Pili: Historia ya Koo
za Wahehe: Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule [Mtengelingoma
Balama na akina Tagumtwa Kivenule], Vita za Vatawangu na Ushujaa wa
Tagumtwa katika Vita; Sehemu ya Tatu: Umoja wa Ukoo wa Kivenule
(KAUKI); Mipango na Harakati zake katika kuwakwamua Wanaukoo katika
lindi la umaskini, ujinga na maradhi, kutoka zaidi ya Vijiji 25 vya
Wilaya ya Iringa Vijijini;
2.Kuanzisha kitengo cha Utaalam wa Kitaaluma (weledi) na Ujuzi ambacho
kitafanya shughuli mbalimbali za kuiletea jamii maendeleo, kupitia
maandiko ya miradi (project proposal and appraisal), pamoja na
kuanzisha miradi mbalimbali ya ujasiamali.
3.Kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ambayo itawasadia wanajamii
kupunguza umaskini, utegemezi, kuboresha maisha na kuwasomesha watoto
ambao wazazi wao hawana uwezo na wana nia ya dhati ya kusoma. Kwa
mfano, eneo la Irore, Iringa Vijijini wamebuni na kuanzisha mradi wa
kilimo cha Alizeti.
4.Kutoa elimu mbalimbali kwa jamii inayounda KAUKI na jamii yote
inayoizunguka kupitia mikutano mikuu kama itakavyofanyika katika
Mkutano wa Tina wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, utakaofanyika Kijijini
Kidamali-Iringa, Juni 29 - 30, 2013;
5.Kununua vitendea kazi mfano Kompyuta, Printa, Simu, Meza na Viti
ambavyo vitaisaidia KAUKI na jamii yote inayoizunguka katika
kutekeleza majukumu mbalimbali ya maendeleo, pamoja na wanafunzi kwa
ujumla;
6.Kuanzisha Mfuko wa KAUKI ambao jukumu lake ni kusaidia jamii
kupunguza umaskini kupitia elimu ya ujasiliamali, kusaidia kusomesha
watoto wanaofaulu na wazazi wao hawana uwezo, na pia kusaidia
kugharamia Tiba kwa wagonjwa ambao hawajimudu. Akaunti ya Mfuko wa
KAUKI tayari imekwisha funguliwa; na inajulikana kwa jina la: KAUKI,
imefunguliwa katika Benki ya NMB, Akaunti Namba 6052301709, Tawi la
Mkwawa, Iringa Mjini; "Tunawaomba Watu Wote wenye nia ya Kutusaidia
Kutumia namba hii ya Akaunti na kisha kututumia taarifa kupitia
tagumtwa@gmail.com na simu namba +255 0713 270364".
7.Kumiliki tovuti. Blog tayari imefunguliwa na inapatikana kupitia
anuani za: http://www.tagumtwa.blogoak.com /
http://www.kauki-kauki.blogspot.com na
http://www.tagumwafoundation.wetpaint.com
8.Kuisajili KAUKI ili iwe Mfuko (Foundation) rasmi ambapo hadi sasa
tunapendeza kuitwa TAGUMTWA FOUNDATION, ambapo tayari tumetumia jina
hili katika kusajili BLOG na pia tunakusudia kusajili jina (domain) ya
website. Lengo la hii Tagumtwa Foundation itakuwa ni kusaidia jamii
kwa ujumla na wanaukoo wanaunda KAUKI, katika nyanja za elimu, afya,
uchumi na matatizo mengine ya kijamii na kimaendeleo. Tayari mfuko
umeanzishwa na wanaukoo wanaombwa waendelee kuuchangia;
9.Kuanzisha Ofisi za Kuratibu shughuli mbalimbali za kiutendaji,
Kijijini Kidamali na pia sehemu nyingine za Kanda zake zilizopo Dar es
Salaam, Irore (Iringa), Magubike (Iringa), Mufindi (Iringa) na Nduli
(Iringa).
Toka mwaka 2005 Mikutano ya KAUKI ilipoanza kufanyika, pamekuwepo na
mwamko wa hali ya juu, ambapo wanaukoo wengi kutoka maeneo ya Iringa
Vijijini na kwingineko, na jamii kwa ujumla inayoizunguka, wamekuwa
wakihudhuria na kujifunza mambo mengi na muhimu ya kimaendeleo.
Wastani wa washiriki 200 toka zaidi ya vijiji 25, pamoja na mikoa
mingine (Dar es Salaam Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma na Mbeya),
wamekuwa wakihudhuria katika siku mbili za Mkutano na kupata mafunzo
mbalimbali kutokana na mada ambazo zimekuwa zikifundishwa. Elimu hizo
zimekuwa zikigusa Ujasiliamali (Entrepreneurship), Afya, Elimu,
kupeana uzoefu wa shughuli za maendeleo. Hadi leo hii, tayari Mikutano
Nane ya KAUKI tayari imekwisha fanyika. Takwimu zinaonesha kuwa
Mikutano Mitatu imefanyika Kijijini Kidamali, na Mkutano moja moja
Kijijini Irore, Nduli, Magubike-Iringa Vijijini, Igowole-Mufindi,
mkoani Iringa na Dar es Salaam. Mwaka 2013 Kanda ya Kidamali, jamii
inayounda KAUKI pamoja na jamii nyingine yenye nia ya kujifunza
itashiriki katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI, utakaofanyika tarehe
Juni 29 -30, 2013. Kwa kutambua nafasi na wadhifa wa asasi yako
katika nchi, kwa heshima na taadhima ninawasilisha rasmi barua katika
meza yako kukufahamisha harakati mbalimbali zinazofanywa na KAUKI
katika katika kukabiliana na changamoto za maendelo kwa watu wake
wanaotoka maeneo ya Nduli, Ismani, Mgongo, Itagutwa, Irore, Igominyi,
Kidamali, Nzihi, Magubike, Kalenga, Idodi, Kipera, Pawaga, Idete,
Ibogo, Iringa Mjini na kwengineko.
Hali kadhalika, KAUKI inafanya utafiti wa kina kuhusu chimbuko na
historia ya Ukoo wa Kivenule na Koo mbalimbali katika Mkoa wa Iringa;
na namna mwilingiliano wa koo hizi unavyoweza kuwa kiunganishi katika
kujiletea maendeleo.
Pamoja na barua hii, naambatanisha ratiba ya mkutano mkuu w 9 wa KAUKI.
Kwa taarifa zaidi na mawasiliano yafanyike kupitia anuani hii hapa chini:
Katibu Mkuu (Adam Kivenule)
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
S.L.P. 742, Iringa/Dar es Salaam
Tel: +255 713 270364 E-mail: kauki2006@gmail.com
Kwa taarifa zaidi kuhusiana na KAUKI, pia zinapatikana kupitia
http://www.kauki-kauki.blogspot.com http://www.tagumtwa.blogoak.com
--
Adam Kivenule
P.O. Box 3255,
Dar es Salaam
Mob. +255 713 270364
E-mail: kivenule@gmail.com / KAUKI2006@gmail.com
Blog: www.adamkivenule.blogspot.com
Twitter: www.twitter.com/kivenule
ADAM KIVENULE BLOG: For information call +255 713 270364 E-mail: kivenule@gmail.com Blog: http://www.adamkivenule.blogspot.com Twitter: http://www.twitter.com/kivenule Youtube: http://www.youtube.com/tagumtwa KIVENULE CLAN BLOGS: http://www.tagumtwa.blogoak.com http://www.kauki-kauki.blogspot.com E-mail: KAUKI2006@gmail.com or tagumtwa@gmail.com
Thursday, 13 March 2014
MKUTANO MKUU WA KUMI WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)
MKUTANO MKUU WA KUMI WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)
Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa heshima na taadhima
unapenda kuwakumbusha kuhusiana na Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 10 wa
KAUKI utakaofanyika wiki ya mwisho ya Mwezi Juni 2014.
Ni hali ya kawaida kabisa kwa KAUKI kuwakumbusha Wanaukoo Wote, Ndugu,
Jamaa na Marafiki wa karibu wa KAUKI kusaidia maandalizi ya Mikutano
ya KAUKI.
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI unafanyika huku tayari Mikutano Mikuu 9
ikiwa imefanyika katika Kanda za Magubike, Kidamali, Nduli, Irore,
Mufindi na Dar es Salaam.
Mkutano wa mwisho wa KAUKI ulifanyika Magubike, Iringa. Mengi
yaliazimiwa ambalo ni jambo jema kwa maendeleo ya KAUKI.
Nawaomba Wadau Wote Wapenda Maendeleo wanaotuunga mkono kutusaidia kwa
hali na mali katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI,
utakaofanyika Mwezi Juni 2014, Kijijini Kidamali, katika Mkoa wa
Iringa.
Hali kadhalika Uongozi wa KAUKI kwa niaba ya Wana-KAUKI kuendelea na
mchakato wa Maandalizi ya Mkutano huo.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
--
Adam Kivenule
P.O. Box 3255,
Dar es Salaam
Mob. +255 713 270364
E-mail: kivenule@gmail.com / KAUKI2006@gmail.com
Blog: www.adamkivenule.blogspot.com
Twitter: www.twitter.com/kivenule
Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa heshima na taadhima
unapenda kuwakumbusha kuhusiana na Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 10 wa
KAUKI utakaofanyika wiki ya mwisho ya Mwezi Juni 2014.
Ni hali ya kawaida kabisa kwa KAUKI kuwakumbusha Wanaukoo Wote, Ndugu,
Jamaa na Marafiki wa karibu wa KAUKI kusaidia maandalizi ya Mikutano
ya KAUKI.
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI unafanyika huku tayari Mikutano Mikuu 9
ikiwa imefanyika katika Kanda za Magubike, Kidamali, Nduli, Irore,
Mufindi na Dar es Salaam.
Mkutano wa mwisho wa KAUKI ulifanyika Magubike, Iringa. Mengi
yaliazimiwa ambalo ni jambo jema kwa maendeleo ya KAUKI.
Nawaomba Wadau Wote Wapenda Maendeleo wanaotuunga mkono kutusaidia kwa
hali na mali katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI,
utakaofanyika Mwezi Juni 2014, Kijijini Kidamali, katika Mkoa wa
Iringa.
Hali kadhalika Uongozi wa KAUKI kwa niaba ya Wana-KAUKI kuendelea na
mchakato wa Maandalizi ya Mkutano huo.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
--
Adam Kivenule
P.O. Box 3255,
Dar es Salaam
Mob. +255 713 270364
E-mail: kivenule@gmail.com / KAUKI2006@gmail.com
Blog: www.adamkivenule.blogspot.com
Twitter: www.twitter.com/kivenule
Subscribe to:
Posts (Atom)