Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Thursday 13 March 2014

MKUTANO MKUU WA KUMI WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

MKUTANO MKUU WA KUMI WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa heshima na taadhima
unapenda kuwakumbusha kuhusiana na Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 10 wa
KAUKI utakaofanyika wiki ya mwisho ya Mwezi Juni 2014.

Ni hali ya kawaida kabisa kwa KAUKI kuwakumbusha Wanaukoo Wote, Ndugu,
Jamaa na Marafiki wa karibu wa KAUKI kusaidia maandalizi ya Mikutano
ya KAUKI.

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI unafanyika huku tayari Mikutano Mikuu 9
ikiwa imefanyika katika Kanda za Magubike, Kidamali, Nduli, Irore,
Mufindi na Dar es Salaam.

Mkutano wa mwisho wa KAUKI ulifanyika Magubike, Iringa. Mengi
yaliazimiwa ambalo ni jambo jema kwa maendeleo ya KAUKI.

Nawaomba Wadau Wote Wapenda Maendeleo wanaotuunga mkono kutusaidia kwa
hali na mali katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI,
utakaofanyika Mwezi Juni 2014, Kijijini Kidamali, katika Mkoa wa
Iringa.

Hali kadhalika Uongozi wa KAUKI kwa niaba ya Wana-KAUKI kuendelea na
mchakato wa Maandalizi ya Mkutano huo.


Imeandaliwa na Kutolewa na:


--
Adam Kivenule
P.O. Box 3255,
Dar es Salaam
Mob. +255 713 270364
E-mail: kivenule@gmail.com / KAUKI2006@gmail.com
Blog: www.adamkivenule.blogspot.com
Twitter: www.twitter.com/kivenule

No comments:

Post a Comment