KAUKI KUFANYA JUBILEI YA KUTIMIZA MIAKA 10, KUELEKEA MKUTANO MKUU WA
KUMI WA KAUKI-KIDAMALI, IRINGA
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) unatarajia kufanya Jubilee ya Miaka
10 wakati wa Mkutano Mkuu wa Kumi wa KAUKI utakaofanyika Kidamali,
Iringa mnamo tarehe 28-29, 2014.
Jubilei ya Miaka Kumi inafanyika kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa
kwa umoja huu mwaka 2005, Kidamali, Iringa. Sambamba na kufanyika kwa
Jubilei hiyo, pia KAUKI itakuwa inafanya Mkutano Mkuu wa 10 tangu
kuanzishwa kwake.
Akizungumza na mwandishi wa Blogu hii, Katibu Mkuu wa KAUKI Ndugu Adam
Alphonce Sigatambule Kivenule, alibainisha kuwa, ni kweli tumefikisha
miaka kumi na tarehe hiyo ya Mkutano Mkuu itakuwa pia siku ya Jubilei
yetu.
HISTORIA YA KAUKI
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), ulianzishwa tarehe 18 Desemba 2005
wakati wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa KAUKI uliofanyika Kijijini
Kidamali. KAUKI ilianzishwa kutokana na mashauriano ya Ndugu watatu,
yaani Faustino Sigatambule Kivenule, Christian John Kivenule na Adam
Alphonce Kivenule.
Ndugu hawa watatu baada ya kubaini mapungufu yaliyokuwapo ndani ya
Ukoo wa Kivenule, waliamua kuungusha nguvu zao na kisha kuushirikisha
ukoo kuhusiana na adhima yao ya kutaka kuirudisha jamii ya ukoo wa
Kivenule kuwa pamoja.
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mashauriano ulifanyika Jijini Dar es Salaam,
mnamo tarehe 06 Februari 2005 katika Ukumbi wa Riverside uliopo eneo
la Ubungo, ambapo ndugu zaidi ya 15 walihudhuria.
Matokeo ya Kikao hiki yaliazimia kwa kauli moja, kulishirikisha wazo
la kuandaliwa kwa MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO, kwa ndugu zao
wanaoishi maeneo ya Magubike, Kidamali, Nyamihuu, Ilalasimba, Idete,
Ibogo, Nzihi na Iringa Mjini.
Kukubalika kwa wazo hili ndiko kulikopelekea kufanyika kwa Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, mnamo tarehe 17 -18 Desemba 2005,
Kijijini Kidamali, Mkoani Iringa.
Tokea wakati huo, Mikutano ya KAUKI imekuwa ikifanyika kila mwaka.
Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa, Mikutano 9 ya KAUKI imefanyika
maeneo mbalimbali ya Kanda za KAUKI kama inaoneshwa hapa chini:
Kanda ya Kidamali – Mikutano ya KAUKI 3
Kanda ya Magubike – Mikutano 2
Kanda ya Irore – Mkutano 1
Kanda ya Nduli – Mkutano 1
Kanda ya Mufindi – Mkutano 1
Kanda ya Dar es Salaam – Mkutano 1
Kwa KAUKI haya ni matokeo ya Kujivunia kwa sababu siyo rahisi
kufanyika kwa mikutano ya namna kutokana na kuwa na gharama kubwa.
MAFANIKIO YA KAUKI
KAUKI imefanikiwa kufanya yafuatayo kwa maendeleo ya wana-ukoo. Kwa mfano,
Imeanzisha Blogu zake kwa ajili ya upashanaji habari. Anuani za blogu hizo ni:
http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.kauki-kauki.blogspot.com
http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com
Hali kadhalika, blogu inayomilikiwa na ndugu Adam Kivenule, ambaye pia
ni Katibu Mkuu wa KAUKI imekuwa ikisaidia katika suala nzima
usambazaji na upashanaji wa habari za KAUKI. Anuani ya blogu hiyo ni:
http://www.adamkivenule.blogspot.com
KAUKI pia imefanikiwa kufungua Ukurasa wa Facebook wenye anuani ifuatayo:
http://www.facebook.com/kivenule
KAUKI pia imefungua ukurasa wa TWITTER http://www.twitter.com/kivenule
Sambamba na mafanikio hayo, kwa sasa KAUKI ipo katika mchakato wa
kufungua ofisi yake KAUKI huko Kidamali, Iringa.
Hali kadhalika, unaweza kuwasiliana na viongozi wa KAUKI au ofisi ya
KAUKI kwa kutumia anuani zifuatazo:
kauki2006@gmail.com
tagumtwa@gmail.com
tagumtwa.kauki@gmail.com
kivenule@gmail.com
kivenule@live.com
Kuna masuala mengi ambayo bado yanaendelea kushuhudiwa na wana-KAUKI,
pamoja na jamii kwa ujumla. Mafanikio ya Ujumla ni kuendelea kufanyika
kwa mikutano mikuu ya KAUKI katika kanda zake. Hali kadhalika mwitikio
na ushiriki wa Wana-KAUKI katika mikutano hiyo ni mafanikio tosha.
Kuelekea kufanyika kwa Jubilei ya KAUKI, mambo mengi yanatarajiwa
kufanyika kwa lengo la kuhakikisha kuwa, Mkutano Mkuu wa KAUKI unafana
na kufanikiwa.
ADAM KIVENULE BLOG: For information call +255 713 270364 E-mail: kivenule@gmail.com Blog: http://www.adamkivenule.blogspot.com Twitter: http://www.twitter.com/kivenule Youtube: http://www.youtube.com/tagumtwa KIVENULE CLAN BLOGS: http://www.tagumtwa.blogoak.com http://www.kauki-kauki.blogspot.com E-mail: KAUKI2006@gmail.com or tagumtwa@gmail.com
Friday, 20 September 2013
Sunday, 15 September 2013
KAUKI KUFUNGUA OFISI YAKE KIDAMALI
KAUKI KUFUNGUA OFISI YAKE KIDAMALI
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) upo katika mchakato wa kufungua
ofisi yake katika Kijiji cha Kidamali, Mkoani Iringa. Mpango wa
kufungua ofisi ni wa muda mrefu na ulikuwa bado kukamilika kutokana na
matatizo mbalimbali ya kifedha yanayoukabili umoja huo.
Akizungumza na mwandishi wa blogu ya KAUKI, Mwenyekiti wa KAUKI Ndugu
Faustino Sigatambule Kivenule, alisema kuwa, baada ya kuchaguliwa
kuongoza umoja huo kwa kipindi cha miaka mitatu (2013-20160,
atahakikisha ofisi inafunguliwa, inakuwa na vifaa na inafanya kazi,
kama mipango ya KAUKI inavyojieleza.
Mwenyekiti wa KAUKI aliongeza kuwa, kwa muda mrefu suala la ofisi
limekuwa likizungumzwa bila kutekeleza. Sasa imefika hatua ya
kuhakikisha kuwa ofisi hiyo inafunguliwa na kuendelea kufanya kazi
kikamilifu.
Akiongezea, Katibu Mkuu wa KAUKI, Ndugu Adam Alphonce Kivenule,
alimweleza mwandishi kuwa hatua zilizochukuliwa na uongozi mpya
uliochaguliwa mwaka 2013 katika Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI,
uliofanyika katika Kijiji cha Magubike, Mkoani Iringa, ni kuhakikisha
kuwa, chumba/nyumba ya ofisi inapatikana mapema iwezekanavyo.
Hadi muda huu ninapozungumza na wewe mwandishi, Chumba cha ofisi kipo
tayari. Kuhusiana na vifaa vya ofisi, Ndugu Adam amesisitiza kuwa
jitihada za makusudi zimekuwa zikifanyika toka mwezi wa Julai 2013
hadi sasa, za kuhakikisha kuwa vifaa vya ofisi vinapatikana.
Vifaa ambavyo vipo na ahadi kwa mujibu wa takwimu zilizopo katika
ofisi ya KAUKI ni kama ifuatavyo:
Kochi la watu watatu (lipo Dar es Salaam)
Mafaili ya ofisi
Machapisho
Mapazia ya ofisi
Stepla mashine na pini zake
Punchi mashine
Meza
Stuli
Hali kadhalika kuna ahadi na fedha taslimu kwa ajili ya ununuzi wa
Kompyuta ya ofisi. Fedha taslimu ambayo tayari imepokelewa ni shilingi
15,000/=. Pia uongozi wa KAUKI kanda ya Dar es Salaam ulipokea ahadi
ya shilingi 50,000/= kutoka kwa mwana-KAUKI.
Jitihadi za ukusanyaji michango mbalimbali kwa ajili ya ofisi na
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI bado zinaendelea katika
Kanda mbalimbali. Taarifa zilizopatikana kutoka kwa Makamu Katibu
anayetoka kanda ya Magubike, Iringa, anasema kuwa wapo katika mchakato
wa kukusanya michango ya ofisi pamoja na ununizi wa kompyuta ya ofisi.
Hali kadhalika, Kanda ya Kidamali nayo haipo nyuma katika
kulishughulikia suala hili. Mipango kabambe bado inaendelea ili
kuhakikisha kuwa vifaa vya ofisi vinapatikana kwa wakati.
Kwa mujibu wa takwimu za kiofisi kutoka kwa Katibu Mkuu wa KAUKI,
Ndugu Adam Kivenule, ilipangwa kila Kanda ichangie shilingi 35,000/-
kwa ajili ya ununuzi. Pamoja na kuwepo kwa mkakati huu, pia wana-KAUKI
kutoka katika kanda zao waliombwa kuchangia vifaa mbalimbali vya ofisi
kwa maana ya kusaidia kupunguza gharama ya ununuzi wa vifaa hivyo.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, mwitikio umekuwa siyo mzuri sana japo bado
tunaendelea kuhimiza wana-KAUKI kuendelea kuchangia vifaa vya ofisi,
hata vya gharama ndogo.
Uongozi wa KAUKI unaamini kuwa hadi mwezi Desemba mwaka huu, ofisi
itakuwa imekamilika, huku ikiwa na vifaa muhimu vya kiofisi.
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) upo katika mchakato wa kufungua
ofisi yake katika Kijiji cha Kidamali, Mkoani Iringa. Mpango wa
kufungua ofisi ni wa muda mrefu na ulikuwa bado kukamilika kutokana na
matatizo mbalimbali ya kifedha yanayoukabili umoja huo.
Akizungumza na mwandishi wa blogu ya KAUKI, Mwenyekiti wa KAUKI Ndugu
Faustino Sigatambule Kivenule, alisema kuwa, baada ya kuchaguliwa
kuongoza umoja huo kwa kipindi cha miaka mitatu (2013-20160,
atahakikisha ofisi inafunguliwa, inakuwa na vifaa na inafanya kazi,
kama mipango ya KAUKI inavyojieleza.
Mwenyekiti wa KAUKI aliongeza kuwa, kwa muda mrefu suala la ofisi
limekuwa likizungumzwa bila kutekeleza. Sasa imefika hatua ya
kuhakikisha kuwa ofisi hiyo inafunguliwa na kuendelea kufanya kazi
kikamilifu.
Akiongezea, Katibu Mkuu wa KAUKI, Ndugu Adam Alphonce Kivenule,
alimweleza mwandishi kuwa hatua zilizochukuliwa na uongozi mpya
uliochaguliwa mwaka 2013 katika Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI,
uliofanyika katika Kijiji cha Magubike, Mkoani Iringa, ni kuhakikisha
kuwa, chumba/nyumba ya ofisi inapatikana mapema iwezekanavyo.
Hadi muda huu ninapozungumza na wewe mwandishi, Chumba cha ofisi kipo
tayari. Kuhusiana na vifaa vya ofisi, Ndugu Adam amesisitiza kuwa
jitihada za makusudi zimekuwa zikifanyika toka mwezi wa Julai 2013
hadi sasa, za kuhakikisha kuwa vifaa vya ofisi vinapatikana.
Vifaa ambavyo vipo na ahadi kwa mujibu wa takwimu zilizopo katika
ofisi ya KAUKI ni kama ifuatavyo:
Kochi la watu watatu (lipo Dar es Salaam)
Mafaili ya ofisi
Machapisho
Mapazia ya ofisi
Stepla mashine na pini zake
Punchi mashine
Meza
Stuli
Hali kadhalika kuna ahadi na fedha taslimu kwa ajili ya ununuzi wa
Kompyuta ya ofisi. Fedha taslimu ambayo tayari imepokelewa ni shilingi
15,000/=. Pia uongozi wa KAUKI kanda ya Dar es Salaam ulipokea ahadi
ya shilingi 50,000/= kutoka kwa mwana-KAUKI.
Jitihadi za ukusanyaji michango mbalimbali kwa ajili ya ofisi na
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI bado zinaendelea katika
Kanda mbalimbali. Taarifa zilizopatikana kutoka kwa Makamu Katibu
anayetoka kanda ya Magubike, Iringa, anasema kuwa wapo katika mchakato
wa kukusanya michango ya ofisi pamoja na ununizi wa kompyuta ya ofisi.
Hali kadhalika, Kanda ya Kidamali nayo haipo nyuma katika
kulishughulikia suala hili. Mipango kabambe bado inaendelea ili
kuhakikisha kuwa vifaa vya ofisi vinapatikana kwa wakati.
Kwa mujibu wa takwimu za kiofisi kutoka kwa Katibu Mkuu wa KAUKI,
Ndugu Adam Kivenule, ilipangwa kila Kanda ichangie shilingi 35,000/-
kwa ajili ya ununuzi. Pamoja na kuwepo kwa mkakati huu, pia wana-KAUKI
kutoka katika kanda zao waliombwa kuchangia vifaa mbalimbali vya ofisi
kwa maana ya kusaidia kupunguza gharama ya ununuzi wa vifaa hivyo.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, mwitikio umekuwa siyo mzuri sana japo bado
tunaendelea kuhimiza wana-KAUKI kuendelea kuchangia vifaa vya ofisi,
hata vya gharama ndogo.
Uongozi wa KAUKI unaamini kuwa hadi mwezi Desemba mwaka huu, ofisi
itakuwa imekamilika, huku ikiwa na vifaa muhimu vya kiofisi.
Wednesday, 28 August 2013
CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE
CHIMBUKO NA HISTORIA YA
UKOO WA KIVENULE
Toleo la Kwanza - 2013
Kwa mawasiliano:
Umoja wa
Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
Kando ya Barabara ya Hifadhi ya
Ruaha
Sanduku la Posta 193
Kidamali, Iringa
Simu: +255 713 270364 (Katibu
Mkuu-KAUKI)
Barua-pepe: kauki2006@gmail.com
kivenule@gmail.com
tagumtwa.kauki@gmail.com
Blogu: http://www.kauki-kauki.blogspot.com
UTANGULIZI
UKOO NI NINI?
Ukoo ni muungano wa familia kadhaa zenye utambulisho
fulani. Unaweza kuwa utambulisho wa jina, alama au mwelekeo mmoja. Utambulisho
wowote kati ya hizo nilizotaja, unaufanya ukoo utambulike miongoni mwa jamii
mbalimbali. Mara nyingi utambulisho ambao huufanya ukoo utambulike baina ya
jamii za Kiafrika ni Jina. Pamoja na jina, halikadhalika kuna tunu (values) mbalimbali ambazo huheshimiwa na ukoo husika
na jamii kwa ujumla.
Tunu hubeba mambo mengi, ikiwa ni pamoja na miiko,
maadili, heshima, vyakula na tamaduni. Sambamba na tunu, pia kuna Mila na
Desturi, ambazo huzingatiwa sana katika masuala ya kijamii, mfano wakati wa
kuoa au kuoza, misiba, sherehe za jadi mfano matambiko na masuala ya kimila.
Ukoo wa Kivenule ni mmojawapo wa koo nyingi kubwa
zilizopo katika Himaya ya Uhehe katika Mkoa wa Iringa. Ukoo wa Kivenule ulianza
kutambulika toka Karne ya 18. Historia inaonesha kuwa Ukoo huu asili yake ni
kutoka kwa Wabena-Manga, waliopo Kusini mwa Mji wa Iringa; yaani maeneo ya
Mufindi na Njombe. Ni mchanganyiko wa Wahehe na Wabena wanaojulikana kama
Wabena-Manga.
Wahehe ni moja kati ya makabila makubwa hapa
Tanzania ambalo kiasili linaishi katika Wilaya za Kaskazini mwa Mkoa wa Iringa,
yaani Iringa Vijijini, Iringa Mjini, Kilolo na Mufindi. Kwa mujibu wa taarifa
mbalimbali zinazopatikana na kutafitiwa, inasemekana kuwa ni moja kati ya
makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji; yaani Wahehe wenye Asili ya
Ungazija. Pengine hata ile sababu ya kuzika wafu wao wakielekea mashariki
inapewa uzito.
Lugha ya Kabila hili ni Kihehe na limegawanyika
kiasi fulani katika lahaja (matamshi) tofauti tofauti kutokana na maeneo ambayo
huzungumzwa. Inafanana kimatamshi na kimaana na lugha ya Kibena iliyopo
wilayani Njombe. Pamoja na Wabena wanaohesabika kuwa zaidi ya watu milioni
moja. Wengi wao ni wafuasi wa Ukristo, hasa wa Kanisa Katoliki (Jimbo Katoliki
la Iringa). Kihistoria Wahehe ni maarufu kwa jinsi walivyopambana na Wajerumani
walioteka maeneo yao, kama katika mapigano ya Lugalo mwaka 1891. Kiongozi wao
alikuwa Chifu Mkwawa.
Katika kuenzi na kutunza tunu za asili za Uhehe,
Ukoo wa Kivenule hauli nyama ya Mbawala (kwa lugha ya
Kihehe Mato/Imato).
Imani kubwa imejengeka miongoni mwa jamii ya Ukoo wa Kivenule kuwa kula Mbawala
ni kuvunja miiko ya Ukoo ambayo iliyowekwa na Waasisi wetu (Babu zetu). Mara
mwanaukoo anapokiuka miiko hii na kula nyuma ya Mbawala (Imato) basi huweza
kufikwa na matatizo mbalimbali, mfano kudhurika afya yake. Mara nyingi huwapata
matatizo kama ya kuvimba miguu na pengine kuoza kabisa.
Tunu nyingine ambazo Ukoo wa Kivenule unazienzi kama
zilivyo koo nyingine katika Uhehe ni Miitikio (Midikiso). Tunu hii huutambulisha Ukoo wa Kivenule
miongoni mwa Koo za Wahehe. Mwitikio (Mwidikiso) wa Ukoo wa Kivenule ni 'MLIGO'. Mwitikio huu hutumika katika maeneo
mbalimbali mfano katika salamu, kuapa (kufanya viapo) na pia kujitofautisha na
koo nyingine. Miitikio (Midikiso) huutambulisha Ukoo wa Kivenule katika koo
nyingine katika ardhi ya Uhehe.
CHIMBUKO LA UKOO WA
KIVENULE
Historia ya Chimbuko la Ukoo wa Kivenule limetoka
mbali zaidi hata kabla ya Jina la sasa la KIVENULE
kupatikana. Utafiti
unaonesha kuwa BABU NYAKUDIRA BALAMA
ndiye aliyemzaa BABU KANOLO BALAMA.
Hapa tunauangalia Ukoo wa Balama.
Hali kadhalika, BABU KANOLO BALAMA,
akamzaa BABU MTENGELINGOMA BALAMA. Maelezo
haya yote tunayoyazungumzia ni katika Karne ya 17 kabla ya kuja kwa BABU TAGUMTWA BALAMA, ambaye aliuleta
Jina la KIVENULE.
BABU MTENGELINGOMA BALAMA ndiye Baba Mzazi wa TAGUMTWA
BALAMA. Wakati huu Babu Tagumtwa Balama alikuwa hajaenda kwenye Vita za LIGALU.
Kwa
Asili, Ukoo wa Balama na baadaye Kivenule ni maarufu kama Wapiganaji wa
Vita. Ukoo wa Balama (Kivenule) ulikuwa hodari sana katika vita vya msituni
ambavyo viliwahusisha Babu zetu akina TAGUMTWA.
Enzi hizo za Mababu zetu vita za Koo na Kabila zilipiganwa maeneo mengi ya
himaya ya Uhehe kwa lengo la kupata mali, mifugo na heshima.
Babu TAGUMTWA BALAMA (KIVENULE) ndiye
aliyewazaa Babu TAVIMYENDA KIVENULE na Babu KALASI KIVENULE. Ikumbukwe kuwa, jina halisi la ukoo wa
Kivenule ni BALAMA. Kama
ilivyokwisha julikana katika mada zilizowasilishwa katika Mikutano Mikuu Tisa
ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), ambapo ilielezwa kuwa, neno KIVENULE linamaanisha sifa ya kuwa jasiri Vitani na hasa katika kutumia
silaha za Mishale na Mikuki yaani kwa Lugha Asilia ya Kihehe
“KUMIGOHA”. Yaani kwa maana nyingine LIGALU yenye maana ya Kwihoma
Imigoha – Kuhoma Vatavangu au Kuvenula
Avatavangu. LIGALU maana yake Vita. Kuhoma maana yake Kuchoma na Migoha maana
yake Mikuki. Venula maana yake ua, fyeka
maadui.
LIGALU ndiyo iliyochangia kuzaliwa kwa jina la Ukoo la KIVENULE. KIVENULE maana
yake ni Ushujaa kutokana na Shabaha ya Mikuki.
KUVENULA likiwa na maana halisi ya kuwa na shabaha ya
kuwaangamiza maadui kwa kutumia silaha ya Mishale na Mikuki. Babu zetu akina TAGUMTWA BALAMA walilidhihirisha hili
katika Vita na Watavangu na hivyo kusababisha kuzawadiwa kwa jina la KIVENULE kama jina la sifa kutokana na ushujaa katika Vita.
Tagumtwa Balama
asili yake ni kutoka katika Ukoo wa Balama. Sifa kubwa ya Tabu Tagumtwa, alikuwa
ana Shabaha sana ya Mikuki katika uwanja wa Vita. Alikuwa hakosei shabaha (target) na hivyo hupelekea kuwaangamiza na kuwaua sana maadui.
Wakati akiwamaliza/fyeka/kuwaua adui zake kwa Mikuki, Wakuu wa Vita (Vatavangu)
walikiita kitendo hicho 'KUVENULA'.
Taarifa za Tagumtwa kuua (Kuvenula) adui zake katika uwanja wa vita, zilizagaa
kila mahali na hivyo kupelekea Wakuu (Viongozi) wa Vita (Vatavangu) kumzawadia
Jina la KIVENULE, kama jina la sifa na heshima kwa kuwa
shujaa wa Vita.
Ikumbukwa
kuwa asili ya Ukoo wa Kivenule ni kutoka katika ukoo wa BALAMA (MWIBALAMA). Hawa ni ndugu wa karibu wa Kivenule kabisa na
hawapaswi kuoana. Koo za Mwibalama zinapatikana maeneo mengi katika Mkoa wa
Iringa hususani katika Wilaya za
Mufindi, Iringa Vijijini, Iringa Mjini na Kilolo; hali kadhalika kama ilivyo
ukoo wa kina Mwakivenule.
TAGUMTWA KIVENULE alifia katika uwanja wa mapambano (vita)
na mwili wake haukuweza kupatikana. Kama zilivyo koo za machifu au watu maarufu
miili yao ilikuwa haizikwi. Baada ya kufa iliegemezwa kwenye miti mikubwa na
kuliwa na wanyama. Wakija watu wasiukute mwili basi huamini kuwa mwili
umechukuliwa na Mungu.
KUKUA NA KUZAGAA KWA UKOO WA KIVENULE
Kwa
mujibu wa taarifa mbalimblai za kitafiti ambazo zimekuwa zikifanyika toka mwaka
2005 hadi sasa 2013; kupitia mikutano mbalimbali ya KAUKI; zinabainisha kuwa, BABU NYAKUDIRA
BALAMA alimzaa BABU KANOLO BALAMA. Hali kadhalika BABU KANOLO BALAMA alimzaa MTENGELINGOMA
BALAMA. BABU MTENGELINGOMA BALAMA ndiye aliyemzaa Tagumtwa Balama
(Kivenule).
Baada
ya hapo, tunaona sasa Kizazi cha TAGUMTWA
KIVENULE kinaanza kujitokeza. Hii ilikuwa ni Karne ya 18. TAGUMTWA KIVENULE alizaa watoto wawili
(2). Bado utafiti unafanyika kumfahamu
Mama wa watoto hawa. Watoto wa Tagumtwa Kivenule walikuwa ni TAVIMYENDA KIVENULE na KALASI KIVENULE.
Kwa mujibu wa taarifa kadhaa tulizonazo kwa sasa; hawa ni vinara wa Ukoo wa
Kivenule ulioenea maeneo mbalimbali hapa Tanzania.
Tavimyenda Kivenule na Kalasi Kivenule katika harakati za kutafuta maisha
walifika katika eneo la Kalenga, mahali alipoishi Mkwawa na kukutana na na
Mwamyinga, aliyekuwa mfugaji maarufu katika eneo la Ulefi huko Magubike, Iringa
Vijijini. Tavimyenda Kivenule alibahatika kupata kazi kwa Mwa-Myinga baada ya
kuombwa kwenda kumwangalizia mifugo yake huko Magubike, huku akimwacha mwenzake
Kalasi pale Kalenga.
Kalasi Kivenule yeye hakupata fursa hiyo ya kazi na
hivyo akaamua kuelekea eneo Irore katika Wilaya Iringa Vijijini (kwa sasa
Kilolo) kutafuta maisha. Huu ukawa ni mwanzo wa kugawanyika kwa watoto hawa
wawili wa Tagumtwa Kivenule.
Tavimyenda Kivenule akielekea upande wa Magharibi mwa Mji wa
Iringa na Kalasi alielekea upande wa Mashariki mwa Mji wa Iringa.
Historia
inabainisha kuwa pamoja na Babu hawa kugawanyika kutokana na utafutaji wa
maisha, mahusiano na ushirikiano baina yao haukuvunjika. Babu zetu waliendelea
kushirikiana na kutembelea licha ya ukoo kukua na kuwa mkubwa sana.
KIZAZI CHA TAVIMYENDA KIVENULE
Katika
Karne ya 19 hadi 20, Kizazi cha Tavimyenda Kivenule kilizaliwa na kuzagaa
katika maeneo ya Ulefi, Magubike na Mlafu, Wilaya ya Iringa Vijijini, Iringa
Mjini na maeneo mengine mkoani Iringa.
Taarifa
tulizonazo kupitia tafiti tunazofanya, hali inaonesha kuwa, Babu Tavimyenda
alikuwa na wake watatu (3), ambao ni:
1.
Bibi Mkami Sekabogo
2.
Bibi
Senosa
3.
Bibi
Pili Mvemba
Mke
wa kwanza wa Tavimyenda Kivenule
aliolewa akiwa na mtoto; aliyejulikana kama Bibi Sikimbilavi Semabiki. Kwa mke huyu wa Kwanza Sekabogo,
Tavimyenda alizaa nae watoto wanne (4); ambao ni:
1.
Babu
Kavilimembe Kivenule
2.
Babu
Mgaifaida Kivenule
3.
Babu
Sigatambule Kivenule
4.
Babu
Hussein Kivenule (Bado yupo hai)
Kwa
Mke wa Pili Bibi Senosa, Babu Tavimyenda
akizaa nae watoto watatu (3); ambao ni:
1.
Babu
Abdallah Kivenule
2.
Bibi
Sigungilimembe Kivenule
3.
Bibi
Malibora Kivenule
Watoto
hawa wa Bibi Senosa waliishi maeneo ya Kihesa katika Mji wa Iringa.
Kwa
upande wa mke wa Tatu wa Bibi Pili Mvemba; Babu Tavimyenda alizaa mtoto mmoja
aliyejulikana kwa jina la BIBI MGASI
KIVENULE aliishi eneo la Ulefi. Baada ya kufariki amezikwa Mlafu. Babu
Tavimyenda Kivenule amezikwa katika eneo la Ulefi.
Bibi SIKIMBILAVI alikuwa mtoto wa kufikia wa Bibi MKAMI
SEKABOGO. Bibi SIKIMBILAVI aliolewa na Ukoo wa Mgoda na kubahatika kupata watoto
wanne (4) ambao ni:
1.
Mama
wa Kitatambe
2.
Salia
Maneno Mgoda
3.
Galamale
Mgoda
4.
William
Mgoda
Baada
ya hapo kizazi hiki kimeendelea kukua hadi hivi sasa Karne ya 21. **Angalia Chati kuonesha Muundo wa Ukoo wa
KIVENULE**
KIZAZI CHA KALASI KIVENULE
Kwa
upande wa Kalasi Tagumtwa Kivenule, kizazi hiki kilienea maeneo ya Nduli,
Mgongo, Itagutwa, Kigonzile, Igominyi na Irore. Taarifa zinaonesha kuwa, Babu
Kalsi Kivenule alikuwa na wake wawili (2); yaani:
1.
Bibi
Semsakwa Mnonikilwa
2.
Bibi
Mnyamtage Sekindole
Bibi
Semsakwa Mnoni Kirwa kwa Babu Kalasi Kivenule alizaa watoto wawili (2) ambao
ni:
1.
Bibi
Cheilaje Nginasambula Kivenule
2.
Gingilemesa
Kivenule
Kwa
bahati mbaya hakuna taarifa zozote za hawa watoto wawili wa Kalasi.
Kwa
upande wa Bibi Mnyamtage Sekindole, Babu Kalasi Kivenule alizaa mtoto mmoja
ambaye ni Salamalenga Kahengula Kivenule. Bibi Mnyatage Sekindole awali alikuwa
ameolewa kwa Mwa-Mhumba na kuzaa nae mtoto mmoja aliyeitwa Bibi Mganga Semhumba
na baadaye kufariki. Baada ya hapo aliolewa na Kalasi ambapo pia alizaa mtoto
mmoja tu anayefahamika kwa jina la Salamalenga Kahengula Kivenule. * Angalia
watoto wa Kahengula katika Chati ya Muundo wa Ukoo wa Kivenule*
Kuna
taarifa nyingi kutoka kwa Babu Tavimyenda Kivenule na Kalasi Kivenule.
Mwingiliano wa koo nao unaonesha simulizi hizi. Kwa upande wa Tavimyenda mke wa
Kwanza Bibi Mkami Sekabogo alikuwa na mtoto wa kufikia, aliyejulikana kwa jina
la Bi Sikimbilavi Semabiki. Hatujapata taarifa rasmi kuhusiana na kizazi cha
Bibi huyu, kama ilivyotokea kuwa Sipanganakumtwa Mwilongo Regina Sematagi
aliyekuwa mtoto wa kufikia Bibi Semkonda mke wa Salamalenga Kahengula Kivenule.
Sipanganakumtwa
Mwilongo Regiona Sematagi amesaidia kueneza kizazi cha Ukoo wa Mnyavanu.
Taarifa zaidi na ukoo wa Mnyavanu upo katika Chati ya Chimbuko na Muundo wa
Ukoo wa Kivenule.**
TABIA YA KIZAZI CHA TAVIMYENDA NA KALASI
KIVENULE KUOA WAKE WENGI
Ukoo
wa KIVENULE hususani kizazi cha Babu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule ulikuwa na tabia
tofauti pengine na vizazi vya sasa. Tabia ya kizazi hiki cha Tavimyenda na
Kalasi ilikuwa ni kuoa wake wengi. Kwa mfano Babu Tavimyenda pekee alikuwa na
wake watatu. Hali kadhalika Babu Kalasi naye alioa wake wawili.
Hali
hii ya kuwa na mke zaidi ya mmoja walirithi watoto wao. Kwa mfano watoto watatu
wa kiume wa Babu Tavimyenda waliozaliwa kwa Bibi Mkami Se-Kabogo walioa wake
wawili hadi watatu. Mtoto wa kwanza wa Babu Tavimyenda Kivenule aliyejulikana
kama Kavilimembe Kivenule alikuwa na wake wawili (2). Mtoto wa tatu wa Bibi
Mkamai Sekabogo, aliyejulikana kwa jina la Sigatambule Matesa Kivenule, alikwa
na wake watatu. Hali kadhalika mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo
anayejulikana kama Hussein Kivenule alikuwa na wake wawili. Mtoto pekee wa Pili
wa Bibi Mkami hakubahatika kuwa na familia; na alijiita jina la kujinyanyapaa
"Mgaifaida" Kivenule.
Sambamba
na tabia ya Ukomo wa Kivenule kuoa mke zaidi ya moja; pia kuna utamaduni
uliojitokeza kwa baadhi ya watoto wa Bibi Mkami Sekabogo kuoa dada na mdogo
wake. Hili linajidhihirisha kwa wake wawili wa Babu Kavilimembe Kivenule ambao
walikuwa ni Bibi Sikumwendinguluvi Sekusiga (Bi Mkubwa) na Bibi Gakumwalia
Sekusiga (Bi Mdogo).
Hali
kadhalika kwa mtoto wa tatu wa Bibi Mkami Sekabogo; Babu Sigatambule Matesa
Kivenule alioa wake watatu, ambapo wake wawili wakubwa, 'Bibi Sikumwendinguluvi
Singaile (Bi Mkubwa) na Bibi Nyanyilemale Singaile (Bi Mdogo wa Pili); na wa
tatu aliitwa Bibi Pangulimale Setwanga.
Mtoto
wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo Hussein Kivenule, yeye alioa wake wawili kutoka
familia tofauti. Wake zake waliitwa Bibi Yimilengeresa Semsisi (Bi Mkubwa) na
Bibi Dalika Setala (Bi Mdogo). Kwa upande wa watoto Kalasi Kivenule, mtoto wake
Salamalenga Kahengula Kivenule naye alioa wake watatu; ambao ni Bibi Semkonda,
Bibi Semfilinge na Bibi Nyangali.
Hatujapata
taarifa rasmi za watoto wa Kalasi kutoka kwa mke wake Bibi Semsakwa Mnonikilwa
ambao ni Cheilaje Nginasambula Kivenule na Gingilemesa Kivenule. Kwa upande wa
Kahengula yeye alioa kutoka katika familia tofauti.
UZAO WA BABU KAVILIMEMBE, MGAIFAIDA,
SIGATAMBULE NA HUSSEIN KIVENULE
Babu
Kavilimembe Kivenule aliishi eneo la Magubike, Wilaya ya Iringa Vijijini, huku
akipakana na Ulefi upande wa Kaskazini, Idete na Ibogo upande wa Magharibi.
Akiwa ameoa wake wawili wa familia moja, Babu Kavilimembe alibahatika kupata
watoto sita (6).
Kwa
upande wa mke wa kwanza Bibi Sikumwendinguluvi Sekusiga; Mzee Kavilimembe
Kivenule alipata watoto wafuatao:
1.
Elizabert Kivenule
2.
Dalikimale Kivenule
3.
Sandra Kivenule
4.
Pangalasi
Kivenule
Na
kwa mke mdogo Bibi Gakumwalia Sekusiga, Mzee Kavilimembe alipata watoto wawili
ambao ni:
1.
Salikuvaganga
Kivenule
2.
Francis
Kivenule
Watoto
hao wa Babu Kavilimembe wengi wao
waliishi maeneo ya Ulefi na Magubike. Baadhi yao walihamia maeneo
mengine kama Nzihi, ukiacha wale
waliokuwa watumishi wa serikali wakaenda kuishi maeneo mbalimbali. Babu Kavilimembe amezikwa eneo la Magubike, Iringa Vijijini.
Kwa
upande wa Babu Mgaifaida (Yakobo) Kivenule,
yeye hakubahatika kupata familia. Mgaifaida
alikuwa na ulemavu ambao ulimfanya ashindwe kutembea katika hali ya kawaida.
Muda mwingi aliishi eneo la Ulefu kabla ya sehemu kubwa ya Ukoo wa Kivenule
kuhamia sehemu ya Mlafu. Baada ya
kufariki, alizikwa Mlafu.
Babu
Sigatambule Matesa Kivenule alikuwa ni mtoto wa tatu wa Tavimyenda Kivenule kwa
Bibi Mkami Sekabogo. Babu Sigatambule
aliishi Ulefi, akahamia Mlafu na
baadaye Kidamali. Babu Sigatambule ndiye aliyehakikisha Ukoo
wa Kivenule unapata eneo la Mlafu huku akipambana na Wagiriki. Walowezi na
wawekezaji katika zao la Tumbaku.
Babu Sigatambule Kivenule katika uhai wake alibahatika kuoa wake
watatu (3); huku wake zake wawili wakitoka katika familia moja ya ukoo wa
Singaile. Wake zake hawa wakubwa waliitwa Bibi Sivangumhavi Singaile na Bibi
Nyanyilimale Singaile. Mke wa Tatu wa Babu Sigatambule aliitwa Bibi Pangulimale
Setwanga. Wote waliishi Mlafu na baadaye wake zake kuhamia eneo Kidamali baada
yeye kufariki.
Wake
zake wawili Bibi Nyanyilimale Singaile
na Bibi Pangulimale Setwanga bado wapo hai na wanaishi Kidamali mpaka leo.
Watoto
wa Babu Sigatambule Kivenule ni hawa wafuatao:
Kwa
Bibi Sivangumhavi Singaile (Mke
Mkubwa):
1.
Gidagumhindi
Cecilia Kivenule
2.
Semyamba
Khadija Kivenule
3.
Sivinitu Alphonce Kivenule
4.
Kadungu
William Kivenule
5.
Fibumo
Xavery Kivenule
6.
Mlagile
Anyesi Kivenule
7.
John
Kivenule
Bibi
Nyanyilimale Singaile (Mke wa Pili)
1.
Mgulwa
Agnes Kivenule
2.
Luhanage
Ponsiano Kivenule
3.
Mgendwa
Eusebio Kivenule
4.
Msinziwa
Daniel
Kivenule
5.
Kanolo
Edward Kivenule
Mke
wa Tatu wa Bibi Pangulimale Setwanga
1.
Conjeta
Kivenule
2.
Pyela
Kivenule
3.
Faustino Kivenule
4.
George Kivenule
5.
Carolina Kivenule
Babu Sigatambule Kivenule alifariki mwaka 1995 na kuzikwa eneo la Mlafu,
Kidamali - Iringa. Hali kadhalika mke wake Mkubwa
Bibi Siwangumhavi Singaile Mwilumbwa
alifariki dunia mwaka 1999 na kuzikwa eneo hilo hilo la Mlafu.
Mzee Hussein Tavimyenda Kivenule alikuwa ni mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo. Yeye aliishi eneo
la Ulefi na baadaye Mlafu. Hatimaye alihamia tena Magubike. Babu Hussein Kivenule hadi anafariki dunia
Juni 26, 2013 anakadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 113 kwa mujibu wa taarifa na tafiti ambazo tunazo.
Babu Hussein Tavimyenda Kivenule ameshiriki kikamilifu katika Vita vya Pili ya Dunia. Wakati
anashiriki vita hiyo alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 44. Amepigana vita
maeneo mbalimbali mfano Burma, India na Ulaya. Kwa sasa ana upofu wa macho
ambao anasema ulisababishwa na Baruti. Hali kadhalika anakiri kuwa kuendelea
kuwa hai ni kwa sababu alipigana upande wa Mwingereza. Anakiri vita ndiyo
iliyomsababishia upofu pengine asingekuwa na hali aliyonayo kwa sasa.
Mzee Hussein Kivenule alioa wake wawili na kubahatika kupata
watoto kumi na tatu (13). Kwa mke wake wa kwanza Bibi Yimilengeresa Semsisi. Babu
Hussein alipata watoto wafuatao:
1.
Nyakudila
Benjamin Kivenule
2.
Sekiyavile
Modesta Kivenule
3.
Dominicus
Kivenule
4.
Emmanuel
Kivenule
5.
Luciana
Kivenule
6.
Ajendina
Kivenule
Kwa
upande wa mke wa pili wa Bibi Dalika
Setala, Mzee Hussein Kivenule alipata watoto wafuatao:
1.
Kabogo
Bernadi Kivenule
2.
Sembata
Josephine Kivenule
3.
Necia
Kivenule
4.
Batromeo
Kivenule
5.
Brandino
Kivenule
6.
Tavina
Kivenule
7.
Masikitiko
Kivenule
Asilimia
kubwa ya familia ya Babu Hussein Kivenule inaishi maeneo ya Vijiji vya Magubike,
Idete na Ibogo ambavyo vipo jirani kabisa na barabara ya kwenda Hifadhi ya
Wanyama ya Ruaha, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.
Mke
wa pili wa Babu Tavimyenda Tagumtwa
Kivenule, alijulikana kwa jina la BIBI
SENOSA. Bibi huyu alibahatika kupata watoto watatu (3) waliojulikana kwa
majina yafuatayo:
1.
Babu
Abdallah Kivenule
2.
Bibi
Sigungilimembe Se-Kivenule
3.
Bibi
Malibora Se-Kivenule
Tafiti
za awali zinazofanywa na KAUKI zinaonesha kuwa kizazi cha Bibi SENOSA kiliishi maeneo ya Mkimbizi eneo la Kihesa, Wilaya ya
Iringa Mjini, Mkoani Iringa. Tafiti zinaendelea kubainisha kuwa Babu Abdallah
Tavimyenda Kivenule hakubahatika kupata familia. Na baada ya kufariki alizikwa
katika makaburi ya Mlafu, Kidamali - Iringa Vijijini.
KAUKI
bado inaendelea na jitihadi za kutafiti kuhusiana na Bibi Sigungilimembe na
Bibi Malibora, ambazo zinaonesha kuwa wao waliishi maeneo ya Mkimbizi Kihesa,
na hata baada ya kufariki walizikwa huko huko. Hapajakuwepo na taarifa rasmi
kuhusiana na uzao wao, pamoja na vifo vyao. KAUKI inaandaa mpango wa kutuma
ujumbe kwenda kufuatilia taarifa za ndugu hawa.
Mke
wa Tatu wa Babu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule alijulikana kwa jina la BIBI PILI SE-MVEMBA. Bibi huyu aliishi eneo la Ulefi, Magubike, Wilaya
ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa. Bibi Se-Mvemba alibahatika kupata mtoto moja
tu aliyejulikana kwa jina la BIBI MGASI
SE-KIVENULE.
Bibi Mgasi Tavimyenda Sekivenule alizaliwa akiwa mtoto pekee wa KIKE kwa
Babu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule. Bibi MGASI
KIVENULE aliolewa katika Ukoo wa akina KIGERESO
na kubahatika kupata watoto sita (6). Watoto hao ni:
1.
Gisapa
Kigereso
2.
Sinatoga
Kigereso
3.
Mtogapawene
Kigereso
4.
Chesilemungu
Kigereso
5.
Ronjino
Kigereso
6.
Cecilia
Kigereso
Baadhi
ya ukoo wa akina KIGERESO
wanapatikana katika maeneo ya Nyamihuu, Igangimali na Kinyamlewa, kando ya
barabara ya kwenda Hifadhi ya Wanyama ya Ruaha, Wilaya ya Iringa Vijijini,
Mkoani Iringa. Baada ya kufariki, BIBI
MGASI KIVENULE alizikwa eneo la MLAFU,
Kidamali -Iringa.
UZAO WA SALAMALENGA KAHENGULA KIVENULE
BABU SALAMALENGA KAHENGULA KIVENULE alikuwa
ni mtoto pekee wa kiume wa BABU KALASI TAVIMYENDA KIVENULE kwa Mke wake wa Pili
BIBI MNYAMTAGE SEKINDOLE. BABU KAHENGULA pia ni KAKA wa BIBI MGANGA SEMHUMBA, aliyekuwa mtoto pekee kwa MWAMHUMBA,
aliyefariki mara tu baada ya kumzaa BIBI
MGANGA SE-MHUMBA kwa Sekindole.
BIBI MGANGA aliolewa kwa
MWALAMBA SAMBAGI, ambapo alibahatika
kuzaa nae watoto kadhaa ambao ni:
1.
Lyamturo Sambagi
2.
Mtemelavanu Sambagi
Kuhusiana
na watoto wengine wa Ukoo wa akina SAMBAGI ambapo timu ya Utafiti ya KAUKI bado
inaendelea kutafuta taarifa zao. Ukoo wa akina SAMBAGI unapatikana zaidi katika
maeneo ya WELU, yaliyopo karibu kabisa na KALENGA-Iringa, hali kadhalika
kuzunguka eneo la TOSAMAGANGA na IPAMBA, Iringa.
Taarifa
za awali zinaonesha kuwa baadhi ya Ukoo wa SAMBAGI walilelewa na BABU yao KAHENGULA
SALAMALENGA KIVENULE. KAUKI ipo katika mchakato wa kuendelea kutafiti zaidi
taarifa mbalimbali za ukoo huu kwa kutuma ujumbe wake eneo la WELU - Iringa.
Historia
inaonesha kuwa Babu Salamalenga Kahengula Kivenule alikuwa ameoa wake watatu ambao ni:
1.
Bibi
Semkonda
2.
Bibi
Semfilinge
3.
Bibi
Nyangali
Babu
Salamalenga Kivenule anapomuoa Bibi Semkonda alimkuta na mtoto wa kufikia
Sipanganakumtwa Mwilongo Regina Sematagi. Kwa wake zake hawa watatu, Babu
Salamalenga alibahatika kupata watoto kumi na tatu (13). Kwa Bibi Semkonda
alibahatika kupata watoto wafuatao:
1.
Pangayena
Kivenule
2.
Jonas
Kivenule
3.
Samwel
Kivenule
4.
Galasamaneno
Kivenule
5.
Daud
(William) Kivenule
6.
Barton
Kivenule
Kwa
mke wa pili Bibi Semfilinge, Babu Salamalenga alizaa nae watoto 3 ambao ni:
1.
Chogavanu
Kivenule
2.
Munguatosa
Kivenule
3.
Mwilimilisa
Kivenule
Na
kwa mke wa tatu Bibi Nyangali, Babu Salamalenga alizaa nae watoto wanne (4)
ambao ni:
1.
Tindasulanga
Kivenule
2.
Sigongola
Kivenule
3.
Shaban
Kivenule
4.
Gungamesa
Kivenule
Historia
inaonesha kuwa baadhi ya akina Bibi waliolewa kwa Babu zetu akina Kivenule
walikuja na watoto wa kufikia. Hili tunaliona kwa Bibi Mkami Sekabogo ambapo
wakati anaolewa na Babu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule, alikuja na mtoto
aliyejulikana kama BIBI SIKIMBILAVI
SEMABIKI. Hali kadhalika, ulezi wa watoto wa kufikia katika Ukoo wa
Kivenule, uliendelea kwa upande wa Irore, ambapo tunaona kuwa BIBI SEMKONDA anapoolewa na Babu
Kahengula Salamalenga Kivenule, alikuwa tayari ameshapata mtoto anayejulikana
kama SIPANGANAKUMTWA MWILONGO REGINA SEMATAGI.
Bibi
huyu MWILONGO, aliolewa katika Ukoo
wa Mwa-MNYAVANU na kufanikiwa kupata watoto sita (6) ambao ni:
1.
Albert
Mnyavanu
2.
Teresia
Mnyavanu
3.
Alphonsina
Mnyavanu
4.
Helena Mnyavanu
5.
Simon
Mnyavanu
6.
Michael
Mnyavanu
MWINGILIANO NA KOO NYINGINE KATIKA HIMAYA
YA UHEHE
Zaidi
ya Koo mbalimbali 50 zinachangamana na Ukoo wa Kivenule. Hii ni kutoka Karne ya
18 ambapo kizazi hiki kilianza kujitambua na kujikusanya. Baadhi ya Koo ambazo
zimechangamana na ukoo huu ni pamoja na koo za:
1.
Kabogo
2.
Kamtawa
3.
Katowo
4.
Kigereso
5.
Kindole
6.
Kisumbe
7.
Kiteve
8.
Kitu
9.
Kusiga
10. Lawa
11. Luhwavi
12. Lupola
13. Madembwe
14. Manimu
15. Matagi
16. Mabiki
17. Mdongwe
18. Mfilinge
19. Mgoda
20. Mhapa
21. Mhumba
22. Mkeng'e
23. Mkonda
24. Mnonikirwa
25. Mnyavanu
26. Msisi
27. Mtono
28. Mvemba
29. Myalla
30. Ngeng'ena
31. Ngolo
32. Ngwenga
33. Ngweta
34. Nyakunga
35. Nyangali
36. Nyangalima
37. Twanga
38. Nzala
39. Sambagi
40. Senosa
41. Setala
42. Singaile
43. Utenga
44. Kalinga
45. Sungu
46. Mgimwa
47. Nyamika
48. Nongele
NAMNA YA KUHIFADHI KUMBUKUMBU ZA KAUKI
Mada ya
Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule, ni muhimu sana kwa kizazi cha sasa na
kijacho; na pia ni mwendelezo wa ukusanyaji wa taarifa mbalimbali zinazohusiana
na Ukoo wa KIVENULE; na pia kuzisambaza kwa jamii inayounda KAUKI. Mada hizi
husaidia kuziboresha taarifa za Ukoo wa Kivenule zilizotangulia, kupitia
taarifa mpya ambazo zinakuwa zimekusanywa kupitia mjumbe mmoja moja na Mikutano
Mikuu ya KAUKI inayoendelea kufanyika kila mwaka. Hali kadhalika, mada hii husaidia kurithisha
Historia na Chimbuko la Ukoo wa Kivenule kwa kizazi cha sasa na baadaye; na pia
kuweka mantiki ya dhana nzima kuhusiana na kuwepo kwa tunu zinazoheshimika na
ukoo; na taarifa kadhaa zinazohusiana na Ukoo wa Kivenule na namna ya kuzihifadhi.
Katika mkakati
wa kuhakikisha kuwa Taarifa Muhimu za Ukoo wa Kivenule zinahifadhiwa, Wana-KAUKI
walipendekeza yachongwe Mawe yenye Majina ya Marehemu ambapo tutayaweka katika Makaburi.
Sababu ya msingi ya kuchonga mawe ni kuwa siyo rahisi kufutika au kupotea.
Mkakati
mwingine mahsusi wa kuhifadhi Taarifa na Historia ya Ukoo wa KIVENULE ni kuziweka
katika Maandishi hususani Vitabu ambavyo vitasambwa kwa wanaukoo wote na kuweza
kujisomea.
Hali kadhalika,
mkakati maalum wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information
Communication Technology-ICT) imeanza kutumika kwa lengo kuzitunza na kusambaza
taarifa mbalimbali zinazohusiana na KAUKI na Ukoo wa Kivenule kwa ujumla. Kwa
mfano mpaka sasa tuna Blogu zifuatazo ambazo zimesheheni taarifa za KAUKI na
Ukoo wa KIVENULE kwa ujumla:
http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com
http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.kauki-kauki.blogspot.com
Kwa bahati
mbaya Blogu yenye anuani: www.tagumtwa.blogoak.com hatuwezi kuweka tena taarifa
za KAUKI kwa sasa kwa sababu ya matatizo ya kiufundi yaliyo nje ya uwezo wetu.
Ila tunaweza kupata taarifa mbalimbali ambazo zilikuwa tayari zimeshawekwa. Na
kwa taarifa tu za kufurahisha, mpaka mwishoni mwa mwaka jana (2012), tulikuwa
na watu karibu milioni 2 waliokuwa wametembelea/kuzifungua na kusoma taarifa
zilizomo kwenye blogu yetu. Ni masikitiko makubwa kwetu kwa sababu blogu hii ilipata
hitilafu ya kiufundi kutokana na wezi wa mtandao kujaribu kuiiba. Pamoja na
jitihadi za kujaribu kuirudisha bado hazijafanikiwa. Ila binafsi naipigania kwa
kuendelea kuihangaikia ili iweze kurudi tena.
Hali kadhalika
Blogu binafsi ya Ndugu Adam Alphonce Kivenule ambaye pia ni Katibu Mkuu wa
KAUKI, inatunza na kusambaza taarifa mbalimbali za KAUKI. Blogu hiyo inaitwa:
http://www.adamkivenule.blogspot.com
KAUKI pia
katika mkakati wake kuhifadhi taarifa mbalimbali za Ukoo wa Kivenule imefungua
Ukurasa wa Facebook. Anuani yake ni:
http://www.facebook.com/tagumtwa-kauki
Katika ukurasa
wa facebook, taarifa mbalimbali za KAUKI huwekwa, pamoja na taarifa za
mikutano, misiba, sherehe na hata salaam miongoni mwa wana-ukoo na hata watu
wengine ambao ni marafiki zetu.
Au unaweza
kutafuta tagumtwa-kauki katika ukurasa wa Google na kupata taarifa mbalimbali
za KAUKI, Tagumtwa, Magubike, Kivenule, Kidamali na mambo mengine mengi.
Hali kadhalika,
katika Mtandao wa Twitter pia KAUKI inapatikana kupitia jina la Babu yetu
Tagumtwa.
http://www.twitter.com/tagumtwa
Hali kadhali
taarifa za KAUKI zipo katika mfumo wa video na zimewekwa katika mtandao kupitia anuani zifuatazo:
http://www.youtube.com/tagumtwa-kauki
http://www.youtube.com/kivenule
Taarifa
mbalimbali kuhusiana na video zilizochukuliwa katika matukio ya Wana-KAUKI
zitaonekana, japo siyo nyingi. Matumizi ya video ndio kwanza tunajaribu na hata
video zake hazina ubora sana kutokana na kukosekana kwa kamera za kisasa.
Katika suala la
kuwasiliana na KAUKI, kuna anuani nyingi ambazo zimesajiliwa kwenye mtandao
kama mkakati wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano; ambazo unaweza
kuzitumia kutupatia taarifa au kuomba taarifa kutoka kwetu. Nazo ni barua-pepe
(e-mail) zifuatazo:
tagumtwa@gmail.com
kivenule@gmail.com
tagumtwa-kauki@gmail.com
tagumtwa@yahoo.com
kauki2006@gmail.com
TAFSIRI ZA MAJINA
MBALIMBALI YALIYOPO KATIKA UKOO WA KIVENULE
Kidagamhindi Heka
heka za kukimbia kodi wakati wa mkoloni
Tunyahindi Kupigwa
pigwa na wakoloni
Mwanitu Alizaliwa
kweusi (kwa kutumia lung’ali). Kuwasha moto ili kupata mwanga kwa
kutumia kuni au aina fulani ya nyasi. Mara nyingi ving’ali vinakuwa vinazimika.
Kadungu Kuwa
na Dungu kubwa (kuwa na kitovu kikubwa)
Kibumo Mvefi
(Mtu anayelialia)
Mlagile Alizaliwa
wakati Bibi yake hayupo. Wakati anaonyeshwa Bibi yake akisema
Mlagile akaitwa Mlagile.
Fatamali Alifuata
mali
Yamkopita Bibi
alipomzaa mtoto wa kwanza na kisha kufariki, akapata jina la ya Mkopite
Luhanage Wakati
Bibi anazaa watoto wanakufa, alipomzaa mtoto na akaugua
sana basi akaitwa Luhanage. Luhanage maana yake ni kuugua sana.
Mgendwa Alizaliwa
kwa taabu. Alizaliwa kwa waganga wa kienyeji kwa tabu wakiwa safarini
Msinziwa
Kanolo Wakati
ameugua, anapiga ramli huki akitembea kwa waganga.
Yimilengeresa Mzee
Babu Husein alichukuliwa kwenye Vita ya Pili ya Dunia. Wahindi
walikufa sana na Waingereza wakashinda Vita.
Misamiti ya Lugha ya Kihehe
Mhisive Binamu
Nyavana Degedege
Ligalu Vita
Watavangu Wakubwa (Wakuu wa Nchi) kabla ya
Ukoloni
KWA TAARIFA NA MAWASILIANO NA:
Umoja
wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) unatoa wito kwa Wana-ndugu, Wana-Ukoo, Jamii
inayopenda kukuza utamaduni wa mtanzania, mashirika na taasisi mbalimbali za
umma na kijamii, kuziangalia kazi zetu na pia kutupatia msaada pale inabidi.
Hizi ni hatua tu za awali lakini bado tunaendelea na mkakati wa kutafuta
taarifa nyingi zaidi kuhusiana na jamii yetu na Kabila la Wahehe kwa Ujumla.
Mpaka
mwezi Desemba 2013, angalau sura ya Kitabu inaweza kuonekana kama Mwenyezi
Mungu, mwingi wa Rehema atatupatia uhai na afya njema.
Kwa taarifa na mawasiliano unaweza
kutufikia kupitia.
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
Kando ya Barabara ya Hifadhi ya Ruaha
Sanduku la Posta 193
Kidamali, Iringa
Simu: +255 713 270364 (Katibu Mkuu-KAUKI)
Barua-pepe: kauki2006@gmail.com
kivenule@gmail.com
tagumtwa.kauki@gmail.com
Blogu: http://www.kauki-kauki.blogspot.com
http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com
Twitter: https://twitter.com/kivenule
Facebook: https://www.facebook.com/kivenule
Subscribe to:
Posts (Atom)