KAUKI KUFUNGUA OFISI YAKE KIDAMALI
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) upo katika mchakato wa kufungua
ofisi yake katika Kijiji cha Kidamali, Mkoani Iringa. Mpango wa
kufungua ofisi ni wa muda mrefu na ulikuwa bado kukamilika kutokana na
matatizo mbalimbali ya kifedha yanayoukabili umoja huo.
Akizungumza na mwandishi wa blogu ya KAUKI, Mwenyekiti wa KAUKI Ndugu
Faustino Sigatambule Kivenule, alisema kuwa, baada ya kuchaguliwa
kuongoza umoja huo kwa kipindi cha miaka mitatu (2013-20160,
atahakikisha ofisi inafunguliwa, inakuwa na vifaa na inafanya kazi,
kama mipango ya KAUKI inavyojieleza.
Mwenyekiti wa KAUKI aliongeza kuwa, kwa muda mrefu suala la ofisi
limekuwa likizungumzwa bila kutekeleza. Sasa imefika hatua ya
kuhakikisha kuwa ofisi hiyo inafunguliwa na kuendelea kufanya kazi
kikamilifu.
Akiongezea, Katibu Mkuu wa KAUKI, Ndugu Adam Alphonce Kivenule,
alimweleza mwandishi kuwa hatua zilizochukuliwa na uongozi mpya
uliochaguliwa mwaka 2013 katika Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI,
uliofanyika katika Kijiji cha Magubike, Mkoani Iringa, ni kuhakikisha
kuwa, chumba/nyumba ya ofisi inapatikana mapema iwezekanavyo.
Hadi muda huu ninapozungumza na wewe mwandishi, Chumba cha ofisi kipo
tayari. Kuhusiana na vifaa vya ofisi, Ndugu Adam amesisitiza kuwa
jitihada za makusudi zimekuwa zikifanyika toka mwezi wa Julai 2013
hadi sasa, za kuhakikisha kuwa vifaa vya ofisi vinapatikana.
Vifaa ambavyo vipo na ahadi kwa mujibu wa takwimu zilizopo katika
ofisi ya KAUKI ni kama ifuatavyo:
Kochi la watu watatu (lipo Dar es Salaam)
Mafaili ya ofisi
Machapisho
Mapazia ya ofisi
Stepla mashine na pini zake
Punchi mashine
Meza
Stuli
Hali kadhalika kuna ahadi na fedha taslimu kwa ajili ya ununuzi wa
Kompyuta ya ofisi. Fedha taslimu ambayo tayari imepokelewa ni shilingi
15,000/=. Pia uongozi wa KAUKI kanda ya Dar es Salaam ulipokea ahadi
ya shilingi 50,000/= kutoka kwa mwana-KAUKI.
Jitihadi za ukusanyaji michango mbalimbali kwa ajili ya ofisi na
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI bado zinaendelea katika
Kanda mbalimbali. Taarifa zilizopatikana kutoka kwa Makamu Katibu
anayetoka kanda ya Magubike, Iringa, anasema kuwa wapo katika mchakato
wa kukusanya michango ya ofisi pamoja na ununizi wa kompyuta ya ofisi.
Hali kadhalika, Kanda ya Kidamali nayo haipo nyuma katika
kulishughulikia suala hili. Mipango kabambe bado inaendelea ili
kuhakikisha kuwa vifaa vya ofisi vinapatikana kwa wakati.
Kwa mujibu wa takwimu za kiofisi kutoka kwa Katibu Mkuu wa KAUKI,
Ndugu Adam Kivenule, ilipangwa kila Kanda ichangie shilingi 35,000/-
kwa ajili ya ununuzi. Pamoja na kuwepo kwa mkakati huu, pia wana-KAUKI
kutoka katika kanda zao waliombwa kuchangia vifaa mbalimbali vya ofisi
kwa maana ya kusaidia kupunguza gharama ya ununuzi wa vifaa hivyo.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, mwitikio umekuwa siyo mzuri sana japo bado
tunaendelea kuhimiza wana-KAUKI kuendelea kuchangia vifaa vya ofisi,
hata vya gharama ndogo.
Uongozi wa KAUKI unaamini kuwa hadi mwezi Desemba mwaka huu, ofisi
itakuwa imekamilika, huku ikiwa na vifaa muhimu vya kiofisi.
ADAM KIVENULE BLOG: For information call +255 713 270364 E-mail: kivenule@gmail.com Blog: http://www.adamkivenule.blogspot.com Twitter: http://www.twitter.com/kivenule Youtube: http://www.youtube.com/tagumtwa KIVENULE CLAN BLOGS: http://www.tagumtwa.blogoak.com http://www.kauki-kauki.blogspot.com E-mail: KAUKI2006@gmail.com or tagumtwa@gmail.com
No comments:
Post a Comment