JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 022-2110146/2110150/2211679, Faksi: 022-2113271
Tovuti: www.moe.go.tz
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI DARAJA
‘A’ NA
STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
anatangaza nafasi za Mafunzo ya Ualimu ngazi yaCheti na Stashahada kwa mwaka wa
masomo 2013/2014 kama ifuatavyo:
A: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA
‘A’: MUDA MIAKA 2
UALIMU: KAWAIDA
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka
2008 na 2012 na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua daraja la IV alama 27 katika Mtihani
uliofanyika katika kikao kimoja Au
-Awe na ufaulu kwa kiwango cha alama C katika masomo
manne tofauti katika Mtihani wa Kidato cha IV ulioyofanyika katika vikao zaidi
ya kimoja.
-Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics’,
‘Biology’, ‘Physics’, ‘Chemistry’, ‘English’
na Kiswahili;
-Mwombaji aliyehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008
na 2012 hiyo ni sifa ya nyongeza.
UALIMU: MICHEZO
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka
2008 na 2012 na kufaulu Kidato cha IV kwa kiwango kisichopungua daraja la IV alama
27 kwa Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.
-Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics’,
‘Biology’, ‘Physics’, ‘Chemistry’, ‘English’
na Kiswahili;
-Mwombaji aliyehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008
na 2012 na mwenye uzoefu katika kufundisha michezo (uthibitisho uambatishwe) ni
sifa ya nyongeza.
UALIMU: ELIMU YA AWALI
-Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka
2008 na 2012 na kufaulu Kidato cha IV kwa
kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa
Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja; na
-Mwombaji aliyehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008
na 2012 ni sifa ya nyongeza.
B: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA:- MUDA
MIAKA 2
UALIMU:- MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII, BIASHARA
NA LUGHA.
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka
2008 na 2013 na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’
moja.
- Awe mhitimu wa mafunzo mbalimbali katika ngazi ya NTA
level 5 kutoka katika chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
1.
Tanbihi: Masomo ya ‘Economics’, ‘Basic
Applied Mathematics’, ‘General Studies’, ‘Islamic
Knowledge’ na ‘Divinity’ hayatatumika
kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji.
UALIMU: MICHEZO, MUZIKI, SANAA ZA UFUNDI NA SANAA ZA
MAONESHO.
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka
2008 na 2013 kwa kiwango kisichopungua
‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja kwa kuzingatia masomo yafuatayo kwa kila kozi:-
Sanaa za Ufundi: masomo ya ‘Fine Art’ pamoja na
ufaulu wa Kidato cha IV masomo ya ‘Biology,
History,
Physics, English, na Civil Engineering’
Sanaa za Maonesho: masomo ya ‘Thearte Arts’ pamoja
na ufaulu wa Kidato cha IV masomo ya ‘Literature in English, Kiswahili, Geography na History;
Muziki: masomo ya ‘Music’ pamoja na ufaulu wa Kidato
cha IV masomo ya ‘English, Kiswahili,
Music, Physics, Geography na History’; na
Elimu kwa Michezo: masomo ya ‘Physical Education’
pamoja na ufaulu wa Kidato cha IV masomo
ya Biology, Chemistry, Physics, English’ na Kiswahili.
UALIMU: UFUNDI
- Mwombaji awe amehitimu mafunzo ya FTC kati ya mwaka
2008 na 2013 kutoka vyuo vya Ufundi
Au awe amehitimu mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA
level 6 kutoka chuo chochote cha Ufundi
kinachotambulika na Serikali.
UALIMU: KILIMO
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka
2008 na 2013 kwa kiwango kisichopungua
“Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja katika
somo la ‘Agricultural Science’ na ‘Biology’
Au ‘Chemistry’.
UALIMU: SAYANSI KIMU
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka
2008 na 2013 na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’
moja katika masomo ya ‘Biology’,
‘Chemistry’ na ‘Nutrition’.
C: MAFUNZO YA
UALIMU KAZINI NGAZI YA STASHAHADA: MUDA MIAKA 2
UALIMU: MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII, BIASHARA
NA LUGHA.
- Mwombaji awe mwalimu wa Daraja A aliyethitimu Kidato
cha VI na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua “Principal Pass” moja na “Subsidiary”
moja; na awe na uzoefu wa kufanya kazi
kwa muda wa usiopungua miaka miwili
( 02) Tanbihi: Masomo ya ‘Economics’, ‘Basic
Applied Mathematics’, ‘General Studies’, ‘Islamic Knowledge’
na ‘Divinity’ hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au
kumdahili mwombaji, na
UALIMU: ELIMU MAALUM
(i) Mwombaji awe mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu
fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na
uzoefu kazini usiopungua miaka miwili
(02) ; na
(ii) Awe mwalimu wa Daraja A aliyethitimu Kidato cha
VI na kufaulu kwa kiwango kisichopungua
“Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja; na awe na
uzoefu kazini usiopungua miaka miwili
(02)
Tanbihi: Masomo ya ‘Economics’, ‘Basic
Applied Mathematics’, ‘General Studies’, ‘Islamic
Knowledge’ na ‘Divinity’ hayatatumika
kama kigezo cha kumchagua au kumudahili mwombaji, na
Mwalimu anayefundisha watoto wenye mahitaji maalum [wasioona,
viziwi, wenye ulemavu wa akili n.k.
(vithibitisho viambatishwe)
], ni sifa ya nyongeza.
2
D: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI NGAZI YA CHETI: MUDA MWAKA
1
UALIMU: SAYANSI KIMU
- Mwombaji awe mwalimu wa Daraja A na awe na uzoefu
kazini usiopungua miaka miwili
(02) .UALIMU: ELIMU MAALUM
- Mwombaji awe mwalimu wa Daraja A na awe na uzoefu
kazini usiopungua miaka miwili
(02)
- Awe amefaulu angalau somo moja la Sayansi katika
Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi: Mwalimu anayefundisha Elimu Maalum hata kama
hana mafunzo rasmi ni sifa ya nyongeza
(uthibitisho uambatishwe) .
A)
VIAMBATISHO
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu watume barua za maombi
yao kwa njia ya posta. Barua hiyo iwe na
anuani sahihi ya mwombaji
(ya posta, au anuani ya barua pepe) , pamoja na viambatisho
vifuatavyo kulingana na aina ya mafunzo:
(i)Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV ,VI na
ufundi;
(ii)Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu
ngazi ya Cheti na Stashahada
(kwa waombaji walioajiriwa)
; na
(iii) Barua zilizopitishwa na waajiri
(kwa waombaji walioajiriwa)
.B)
MAELEZO MUHIMU
(i) Sifa zilizoelekezwa kwa mafunzo ya ualimu ngazi Cheti
Daraja ‘A’ni kwa ajili ya waombaji wa
mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali
na visivyo vya Serikali.
(ii)Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2012 waliojaza nafasi
ya mafunzo ya ualimu ngazi Cheti Daraja ‘A’kwenye “Seforms” wakati wanamalizaelimu
ya sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo kwa njia ya barua na
watachaguliwa kwa kufuata vigezo vilivyowekwa.
(iii)Sifa zilizoelekezwa kwa mafunzo ya ualimu ngazi
ya Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wote kwavyuo vya ualimu vya Serikali na
vyuo vya ualimu visivyo vya Serikali isipokuwa mwombaji kwa vyuovya ualimu
visivyo vya Serikali anaweza akawa amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2003
na 2013.
(iv)Waombaji wa mafunzo ya ualimu aliyeajiriwa
apitishe barua ya maombi kwa mwajiri wake.
(v)Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya
ualimu yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara yaElimu na Mafunzo ya Ufundi: www.moe.go.tz, na OWM-TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz;
(vi)Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za
kujiunga na mafunzo na Wakuu wa Vyuo ambako
watakuwa wamepangwa kupitia anuani zao sahihi.
(vii)Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM-TAMISEMI:
www.pmoralg.go.tz, kwenye ofisi za
Makatibu Tawala (M)
na vyuo vya
ualimu.
Tanbihi: Kwa waombaji walio Dar es Salaam wanaweza kufika Wizarani na kutumbukiza barua
za maombi
kwenye sanduku lililowekwa mapokezi. Tafadhali barua
zote za maombi zitumbukizwe kwenye sanduku la
maombi na si vinginevyo.
MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 10 Mei,
2013.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM
(Aione: Mkurugenzi, Idara ya Elimu yaUalimu)
No comments:
Post a Comment