Adam Kivenule, Katibu Mkuu-KAUKI |
Umoja
wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa kushirikiana na Kanda ya Nduli, kwa heshima kubwa unapenda kuwajulisha ndugu,
jamaa, marafiki na Wana Ukoo wote, umeanza maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika Kijijini Nduli, Mkoani
Iringa, tarehe 2 had 3 Julai, 2016.
Kwa
taarifa hii, tunaomba Viongozi wote wa KAUKI na Viongozi wa Kanda, kuanza
kujiandaa kwa Mkutano huo muhimu. Sambamba na hilo, Viongozi wa KAUKI waendelee
kuratibu maandalizi ya Mkutano kwa kusambaza taarifa na kuweka mikakati imara
ya kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI unafanikiwa. Wadau wakuu wa
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI ni Viongozi wa Kanda kwa kushirikiana
na ndugu wote.
Ikumbukwe
kuwa, mwaka huu (2015), Mkutano wa Mkuu wa KAUKI uliopangwa ufanyika Kijijini
Irore, Mkoano Iringa, umeshindwa kufanyika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo
wetu. Maana nyingine Kanda ya Irore bado inayo nafasi nyingine ya kuandaa
Mkutano Mkuu wa 12 wa KAUKI, 2017. Kwa hiyo wana Irore na sehemu zote za
Igominyi mnaombwa kuanza kufanya maandalizi ya mkutano wenu, sambamba na
maandalizi ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Nduli mwakani.
Kuna
mambo mengi muhimu yanaweza kufanyika kama sehemu muhimu ya maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika Kijijini Nduli:
1.
Kila ndugu
kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI na
kuhakikisha kuwa unafanikiwa. Kila mwana ukoo anaweza kujitoa kwa chochote kile
ambacho kitasaidia kufanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI.
2.
Ndugu wenye uwezo
kujitolea ili kufanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI. Kuna wana Ukoo ambao
wamejiajili na wana vipato vya uhakika. Tunaomba kwa moyo wa upendo wasaidie
kuandaa mkutano huu. Pia kuna ndugu ambao wameajiliwa na wana vipato vizuri. Tunaomba
wachukue jukumu la kusaidia kugharama za maandalizi ya Mkutano huo.
3.
Wana Ukoo wa Kanda
ya Nduli na Kanda nyingine ambazo zina fursa ya ardhi, wanaweza kulima angalau
nusu ekari kwa lengo la kupanda mazao ambayo yatatumika kwa ajili ya
kufanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI. Mazao ambayo yanaweza kupandwa ni
pamoja na Mahindi, Maharage, Viazi na mazao mengine ya nafaka.
4.
Kuhamasishana na
kuhimizana ndugu na wana ukoo miongoni mwetu ili kuendelea kuwa na moyo wa
kupendana, kushirikiana na kusaidiana; na pia kuwa pamoja katika masuala yote
yanayohusu ndugu na ukoo kwa ujumla kwa faida yetu wote.
Matarajio ya Mkutano Mkuu wa 11 wa
KAUKI, utakaofanyika tarehe 2 – 3 Julai, 2016, Kijijini Nduli.
Mkutano
Mkuu wa 11 wa KAUKI unatarajia yafuatayo:
1.
Kuendelea kuboresha
Kitabu cha Wana Ukoo kwa kujaza taarifa mbalimbali za ndugu (Clan Organization
Tree).
2.
Kuwafahamisha wana
ukoo, Historia na Chimbuko la Ukoo. Hususani Ukoo wa Kivenule.
3.
Mwingiliano wa Ukoo
wa Kivenule na Koo nyingine uliopelekea kuwepo kwa Ukoo wa Kivenule.
4.
Kufanya tathmini ya
mipango mbalimbali ya KAUKI tuliyojiwekea kwa miaka kadhaa.
5.
Kutathmini
changamoto na vikwazo mbalimbali vinavyoukabili Umoja wetu.
6.
Yatakayojiri katika
Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI, utakaofanyika tarehe 2 – 3 Julai,
Imeandaliwa
na kusambazwa na:
Katibu Mkuu (Adam Alphonce
Kivenule)
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
Mobile: 0713 270364
E-mail: tagumtwa@gmail.com
Facebook: https://www.facebook.com/kivenule
No comments:
Post a Comment