TAARIFA MUHIMU KUHUSU AJIRA ZA WALIMU MWAKA HUU,
Naibu Waziri ofisi ya Nchini,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)Suleiman Jaffo (kulia)akizungumza na Mwandishi wa Fullhabari.blogs Karoli Vinsent (Kushoto) leo Jijini dar es SalaamNaibu waziri ofisi ya Nchi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleiman Jaffo amewatoa hofu wahitimu wote nchini waliosomea ualimu ambaowamekuwa wakisubili ajira kutoka serikalini kwa muda mrefu,Hivyo amewataka walimu hao kuwa na subira kwani ajira hizo zitatangazwa mda wowote kutoka sasa.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.Jaffo ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na Mtandao huu ambapo amesema wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya Elimu wameshamaliza hatua ya kwanza ya kuhakiki idadi haswa ya walimu wanaohitajika pamoja na ile idadi ya wahitimu wa masuala hayo .Amesema zoezi lilobakia kwa sasani kumalizia takwimu za walimu waliostaafu kazi pamoja na waliohama kutoka serikali kwenda kwenye shule binafsi ili serikali iweze kujua idadi harisi ya pengo la walimu nchini.Hata hivyo,Jaffo amesema katika mwaka huu serikali inampango wakuongeza idadi ya ajira za walimu hadi kufikia walimu elfu 40000 katika ngazi za shule za msingi na sekondari.Jaffo pia amesema kwa sasa ajira hizo zitapewa kipaumbele katika maeneo ya pembezoni mwa nchi ambayo amedai kuwa kuna uhaba sana wa walimu .Ameitaja mikoa hiyo ni Mkoa wa Kigoma,Mara,Tabora,Rukwa,kwa mujibu wa Jaffo amewataka wahitimu hao kujiandaa kufundisha katika maeneo hayo nakutoa dhana ya kufundisha kwenye shule za mijini.
No comments:
Post a Comment