Historia ya Kabila la Wahehe na Wangoni katika mapambano ya kivita ni inajumuisha sehemu muhimu ya historia ya Tanzania. Makabila haya mawili yalijulikana kwa ustadi wa kijeshi, uongozi imara, na uwezo wa kupigana dhidi ya maadui wa ndani na wale wa kikoloni.
Historia ya Wahehe
Wahehe ni moja ya Kabila maarufu katika Mkoa wa Iringa. Wahehe wanaishi katika Wilaya zote za Mkoa wa Iringa na mikoa mengine hapa Tanzania. Umaarufu wao unatoka katika karne ya 19 chini ya uongozi madhubuti wa Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga, maarufu kama Mkwawa. Mkwawa alikuwa miongoni mwa Watoto 5 wa Munyigumba Mwamuyinga.
| Makumbusho ya Mkwawa - Kalenga, Iringa |
Mbinu za kivita za Wahehe
Wahehe chini ya Amiri Jeshi Mkuu wao Mkwawa
(Mkwavinyika) walikuwa na jeshi imara lenye mfumo mzuri wa kiulinzi na viongozi
wa kijeshi.
Silaha kubwa walizotumia katika vita vya makabila na vita
dhidi ya wakokoni ilikuwa ni mikuki, ngao, pinde na mishale, na baadaye
walipata baadhi ya bunduki.
Mbuzi ya mashambulizi ya kushtukiza (guerrilla
tactics) ilitumika zaidi na Jeshi la Mkwawa, huku wakitumia milima na misitu
kuwazingira maadui.
Uhodari wa jeshi la Mkwawa lilitokana na
kuwashirikisha vijana katika umri mdogo kushiriki katika vita. Vijana walipata
mafunzo ya kijeshi tangu wakiwa wadogo.
Vita dhidi ya Wajerumani
Hii ni vita iliyotingisha Ujerumani. Vita vinavyokumbukwa
zaidi ni vile vya Mnamo mwaka 1891, Wahehe walilishinda jeshi la Kijerumani
katika Vita vya Lugalo, ambapo askari wengi wa Kijerumani waliuawa. Ushindi huu
uliifanya jamii ya Wahehe ijulikane kama moja ya wapinzani wakubwa wa utawala
wa Kijerumani katika Afrika Mashariki.
Baada ya miaka kadhaa ya mapigano, Wajerumani waliteka
makao makuu ya Mkwawa huko Kalenga. Mwaka 1898, Mkwawa alikataa kukamatwa akiwa
hai na alifariki baada ya kujitoa uhai, jambo lililomfanya kuwa ishara ya
ujasiri na upinzani dhidi ya ukoloni.
Wahehe ni akina nani?
Wahehe ni moja ya kabila linalopatikana mkoani Iringa.
Ni moja ya kabila ambalo limejiwekea historia kubwa hapa Tanzania.
Inafafanuliwa kuwa kabila la Wahehe ni muunganiko wa makabila madogomadogo kama
kabila la Wadongwe, na koo zingine
kutoka Ng’uluhe na Lugemba, ambayo yalipata kukaa maeneo ya Iringa. Sababu ya
muungaiko huo ni vita vilivyokuwa vikipigana kati ya Wahehe na Wasangu.
Kabla ya miaka ya 1860, hakukuwa na kabila
lililofahamika kwa jina la Wahehe, lakini
mpaka kufikia miaka ya 1860, kipindi ambacho wageni wanafika na kuandika
habari za makabila ya Tanzania, walipolipa jina kabila hili kuitwa Wahehe. Na
asili ya jina hili linatokana na namna ya makelele( Heee….heeee….heee…)
waliokuwa wakiyapiga wakati wa kwenda kwenye vita au hata wakati wa kupambana
vitani.
Vita za Wahehe na Makabila
Ufalme wa kihehe ambao uliopata kukua karne ya 19,
ulitokana na uongozi wa chifu Munyigumba (Bunini au Mugohang’amwa) na mtoto
wake Mkwawa. Inasimuliwa kuwa mnamo miaka ya 1850, ufalme wa wahehe au kabila
hili la wahehe lilikuwa likiogopeka sana na makabila mengine kama Wasengo hata
Wasangu pia.
Walikuwa wakiogopeka kutokana na kuwa na jeshi kubwa
na imara kama lile la mtemi Mirambo wa Urambo. Na mpaka wageni wanafika kwenye
miaka ya 1850/1860, Wahehe bado walionekana kuwa imara katika masuala ya
kivita. Kwani mpaka kufikia miaka ya 1870, Wahehe walifanikiwa kupigana na
kabila la Wamasai waliokuwa wametokea kaskazini-mashariki mwa Tanzania, ambao
nao pia walikimbia vita kutoka kwa
Wachaga na Wapare. Na zaidi ya hapo miaka hiyo hiyo ya 1870, wahehe walikuwa
wameshafanikiwa kutawala maeneo ya Dodoma hasa yale ya upande wa kusini na
kusini-magharibi. Hivyo sio tu makabila mengine waliowaogopa Wahehe bali hata
wageni hao waliwahofia sana Wahehe katika masuala ya kivita.
| Askari wa Kingoni |
Lakini mambo yalikuja kubadilika mara baada ya Wangoni
kuingia katika ardhi ya Uhehe wakitokea maeneo ya kusini mwa Afrika(Rejea
historia ya Wangoni ilishaandikwa). Wangoni ambao walionekana nao kuwa imara
katika vita, kwani walisababisha maafa makubwa sana katika ardhi ya uhehe. Ujio
wa Wangoni kwa mara ya kwanza kwenye ardhi ya Uhehe ulikuwa kwenye miaka ya
1870 na ujio wa mara ya pili ulikuwa miaka ya 1882. Hivyo mipango ya kivita ya
Wahehe, ikabadilika kutoka kwa Wasangu na kugeukia kwa Wangoni.
Na kuna uhakika kuwa, Wasangu waliamua kuungana na
Wabena, kwa lengo la kupambana na Wangoni walioonekana wakija kwa kasi kubwa
sana. Na wakati huo Wangoni wanafika katika ardhi ya Uhehe, walikuwa
wameshagawanyika kwenye makundi matano.
Kwa mara ya kwanza Wangoni na wahehe walipigana maeneo
ya Nyamurenge, ambapo Wahehe waliwapiga
Wangoni na kumuua kiongozi shupavu wa wangoni aliyefahamika kama Chipeta.
Kitendo cha Wahehe kumuua Chifu Chipeta ambaye ndie alikuwa kiongozi wa Wangoni
kwa upande ule, kilipelekea Wahehe kushinda vita.
Mbali na hapo mapambano mengine kati ya Wahehe na
Wangoni yalikuwepo maeneo ya Idete mnamo miaka ya 1870 .Inafafanuliwa kuwa
mapambano kwenye hayo Wangoni walipigwa sana na hii ni kutokana na sababu ya
njaa walikuwa nayo . Kwani mtwa Mkwawa
alitoa amri kwa Wahehe wote kuhama na vyakula vyote na kuchoma moto
mazao mengine. Wahehe walifanya hivi kwa sababu walijua kuwa ujio wa Wangoni
maeneo hayo ulikuwa ni kutafuta chakula,, hivyo kitendo cha kuchoma moto mazao
hayo ni moja ya mbinu ya kuwashinda Wangoni.
Mapambano ya awamu hii kati ya Wahehe na Wangoni
yalifika mpaka maeneo ya Ndandu karibu
na bwawa la Itombololo. Mbali na Wangoni kufa kwa njaa, wengi wao walisukumwa
kwenye hilo bwawa na kufia mule. Na mwisho wa siku, mapambano kati ya Wahehe na
Wangoni yalipelekea kugawanyika kwa Ubena, yaani kukawa na Ubena ya kusini
chini ya Wangoni na Ubena ya kaskazini
chini ya Wahehe. Na mwisho wa siku yaani miaka ya1880 muunganiko kati ya
Wangoni na wahehe ukaanzia huko na utani kati ya Wahehe na Wangoni ukaanzia huko
Inafafanuliwa kuwa kwa kipindi chote hiko cha miaka ya
1870, Wahehe walikuwa chini ya uongozi wa Munyigumba.
Na mara baada ya kifo cha Munyigumba, mtoto wake
ambaye ndiye Mkwawa, alichukua madaraka na kuendeleza ufalme wa Wahehe.
Inafafanuliwa kuwa kifo cha Munyigumba kilisababishwa na mapambano kati ya
Wahehe na Wabena walioungana na Wandamba kutoka maeneo ya Kilombero. Vita kati
ya Wabena na Wahehe, Wabena na Wandamba waliongozwa na Mutengela kutoka kwenye
ukoo wa wakina Wakinamanga.
No comments:
Post a Comment