Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Friday, 20 January 2017

Historia ya Mkwawa (Mkwavinyika)


Wahehe mnamo 1906

Mkwawa au kwa jina refu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855 – 19 Julai 18981) alikuwa chifu na kiongozi mkuu wa kabila la Wahehe katika Tanzania ya leo wakati wa upanuzi wa ukoloni wa Ujerumani mwishoni mwa karne ya 19.

Mkwawa ni maarufu hasa kwa kuongoza vita vya Wahehe dhidi ya Wajerumani.

Upanuzi wa Wahehe

Jina la Mkwawa ni kifupisho cha Mukwava ambalo tena ni kifupisho cha Mukwavinyika, lililokuwa jina lake la heshima likimaanisha "kiongozi aliyetwaa nchi nyingi".

Mkwawa alizaliwa mnamo mwaka 1855 mahali palipoitwa Luhota karibu na Iringa mjini. Alikuwa mtoto wa chifu Munyigumba aliyeaga dunia mwaka 1879.

Babake Munyingumba aliwahi kuunganisha temi ndogo za Wahehe na makabila ya majirani kuwa dola moja. Aliiga mfumo wa kijeshi wa Wasangu waliowahi kuwa kabila lenye nguvu kwa kujifunza mfumo huu kutoka kwa Wangoni na impi za Shaka Zulu.

Hadi miaka ya 1870 eneo la Wahehe lilipanuliwa mbali kuanzia kusini hadi katikati ya Tanzania ya leo.

Baada ya kifo cha chifu mzee watoto wake walishindania urithi wake, na Mkwawa alishinda akawa kiongozi mpya.

Aliendelea kupanua utawala wake. Hadi mwisho wa miaka ya 1880 alitawala sehemu muhimu za njia ya misafara kati ya pwani na Ziwa Tanganyika. Misafara hiyo ambayo ilikuwa ikibeba bidhaa za nje kama vitambaa, visu na silaha kutoka pwani, ikirudi na watumwa na pembe za ndovu, ilipaswa kumlipia hongo ikanunua pia wafungwa wa vita vyake. Hapo athiri na uwezo wake wa kulipa jeshi kubwa ikaongezeka.

Mkwawa na upanuzi wa Wajerumani

Tangu mwaka 1885 hivi Wajerumani walianza kuunda koloni lao katika afrika ya Mashariki ya Kijerumani (Tanganyika pamoja na Rwanda na Burundi) za leo).

Mwaka 1888/1889 utawala wao ulitikiswa na vita ya Abushiri lakini baada ya kushinda upinzani wa Waafrika wa pwani Wajerumani walilenga kuimarisha utawala wao juu ya sehemu za bara.

Mkwawa aliwahi kusikia mapema habari za Wajerumani akajaribu kuwasiliana nao lakini bila kuelewana. Hapo aliamua kujenga boma imara lenye kuta za mawe kwenye makao makuu yake huko Kalenga karibu na Iringa.

Katika mwezi Februari 1891 alituma wajumbe kwa kambi la Wajerumani huko Mpwawa wakapokewa na gavana Mjerumani. Wakati huohuo Mkwawa aliendelea kutuma askari zake hadi Usagara iliyotazamwa na Wajerumani kama eneo lao. [1]

Katika kipindi hicho gavana mpya Julius von Soden alifika Dar es Salaam. Hakuwa na mamlaka juu ya mkuu mpya wa jeshi Emil von Zelewski aliyepokea amri zake kutoka Berlin moja kwa moja. Baada ya kusikia habari za mashambulio ya Mkwawa katika Usangara aliomba na kupata kibali cha "kuwaadhibu Wahehe".

Mapigano ya Lugalo

Katika mwezi Julai 1891 von Zelewski aliongoza kikosi cha maafisa Wajerumani 13 na askari Waafrika hasa kutoka Sudan 320, pamoja na wapagazi 113. Walikuwa na bunduki za kisasa, bunduki za mtombo na mizinga midogo. Zelewski aliwadharau Wahehe kama washenzi ambao walikuwa na mikuki na pinde tu. Kwa hiyo hakuona haja ya kutuma wapelelezi wa awali.

Njiani aliangamiza vijiji alivyokuta na katika mwezi Agosti alipoona Wahehe 3 waliomkaribia aliagiza kuwaua bila kuongea nao. Kumbe walikuwa mabalozi wa Mkwawa aliyetaka kujadiliana na Wajerumani.
Emil von Zelewski, kiongozi Mjerumani wa Lugalo
 

Tarehe 17 Agosti 1891 Zelewski na jeshi lake walipita kwenye manyasi marefu karibu na Lugalo. Mkwawa alikuwa alimsubiri na Wahehe 3,000 walionyamaza hadi Wajerumani waliotembea kwa umbo la safu ndefu walipokuwa karibu kabisa wakawashambulia.

Wajerumani walikosa muda wa kuandaa silaha zao wakashtushwa kabisa. Sehemu kubwa ya askari waliuawa katika muda wa dakika chache pamoja na jemadari von Zelewski. Sehemu ya kombania ya nyuma ilirudi nyuma na kusimama kwenye kilima kidogo walipoweza kutumia bunduki la mtombo wakajitetea na kuua Wahehe wengi. Sehemu hii ilijumlisha maafisa 2 na maafande 2 Wajerumani waliweza kukimbia na kujiokoa pamoja na askari 62 na wapagazi 74.

Kipindi cha vita

Baada ya mapigano Mkwawa alihesabu wafu wake waliokuwa wengi. Alikataza mila za kilio kwa sababu alitaka kuficha idadi ya askari waliokufa. Akielewa sasa kwamba silaha za Wazungu zilikuwa hatari alituma tena mabalozi kwa gavana von Soden walioeleza ya kwamba Wahehe walikuwa walijihami tu dhidi ya shambulio na walitaka amani.

Lakini madai ya Wajerumani yalikuwa magumu, eti kuwaruhusu wafanyabiashara kupita bila matata na kutoshambulia majirani tena.

Mkwawa hakuwa tayari kuahidi yote akachelewesha mikutano. Wakati huo kamanda mpya Mjerumani Tom von Prince alijenga boma jipya la Wajerumani katika Uhehe na Mkwawa alijibu kwa kusambulia vikosi vidogo vya jeshi la kikoloni. Gavana Soden alidai kutoendelea na mapigano. [2], lakini mwaka 1893 aliondoka Afrika, na gavana mpya von Schele alitaka kulipiza kisasi akaamuru mashambulio dhidi ya Mkwawa.

Anguko la Kalenga

Mwezi Oktoba 1894 von Schele aliongoza kikosi cha maafisa Wajerumani 33 na askari Waafrika pamoja na wagajai zaidi ya 1000 kuelekea Kalenga. Walikuwa na mizinga 4 na bunduki bombomu.

Walipofika mbele ya Kalenga Wahehe walijisikia salama kutokana na kuta imara lakini Wajerumani walijipanga kilomita kadhaa nje ya mji wakaanza kufyatulia mizinga yao na kuua watu ndani ya mji.

Wakati wa giza kwenye asubuhi wa tarehre 30 Oktoba 1894 askari wa jeshi la Schutztruppe walipanda ukuta katika sehemu uliyodhoofishwa tayari na kuingia mjini. Hadi jioni walikuwa wameteka mji wote.

Gombora na mikuki ya Wahehe hazikuweza kushindana na bombomu za Wajerumani. Mkwawa mwenyewe aliamua kukimbia pamoja na askari 2000 - 3000, lakini kabla ya kukimbia alimwua mganga mzee aliyewahi kutabiri ya kwamba atawashinda Wajerumani waliokuja.

Gavana von Schele aliandika taarifa kwa serikali ya Ujerumani "tulizika maadui 250, wengine walichomwa katika nyumba zao, wanawake na watoto 1500 kutekwa nyara" [3].

Mkwawa alijificha msituni pamoja na askari zake akasubiri. Gavana von Schele alishindwa kuendelea na mashambulio kwa sababu gharama za vita zilishinda makisio yake na wabunge wa upinzani katika Reichstag huko Berlin walipinga vita vya kikoloni; walikataa kuongeza makisio na kiongozi wa wasoshalisti Agosti Bebel aliita mtindo wa kuchoma mji na kuteka nyara watoto na wanawake "ushenzi mkuu".

Amani fupi

Baada ya kuondoka kwa Wajerumani, Mkwawa aliweza kurudi na kujenga tena nyumba mahali pa Kalenga.

Mnamo Septemba 1895 Mkwawa alikuwa tayari kujadiliana na Wajerumani na tarehe 12 Oktoba walipatana amani. Wajerumani walimkubali Mkwawa kama chifu wa Wahehe, Wahehe waliahidi kukabidhi gobori zote, kupandisha bendera ya Ujerumani na kuwaruhusu wafanyabiashara na wasafiri kupitia Uhehe. Mkwawa alimwagiza mjomba wake kutia sahihi akakataa mwenyewe akisema hii ingemwua.

Hata hivyo miezi kadhaa baadaye alitafuta msaada wa Wajerumani kwa shambulio dhidi ya Wabena.

Afisa mmoja Mjerumani aliyefika Kalenga mpya alizuiliwa kuingia na kumwona chifu akaambiwa alipe hongo ya bunduki 5 ili kuingia katika eneo la Mkwawa. Hapo maafisa wa jeshi la Wajerumani waliolinda mpaka, ambao bado walikuwa wakitafuta nafasi ya kulipiza kisasi cha Lugalo, walidai kuwa chifu amevunja mkataba.

Kapteni Tom von Prince alijenga boma jipya karibu na Kalenga alianza kuwasiliana na machifu wadogo wa Wahehe. Mkwawa alijaribu kujenga mapatano na majirani lakini Wabena na makabila mengine walikumbuka vita na mashambulio ya awali kutoka Uhehe walipendelea kushikamana na Wajerumani.

Mkwawa aliwaua machifu wawili Wahehe waliowahi kukaa na von Prince, lakini aliona hawakuwa peke yao kusita kumtii tena. Alipata habari ya kwamba hata mdogo wake Mpangile alishikamana na Wajerumani.

Wakati wa Septemba 1896 Wahehe waligawanyika na sehemu kubwa ya viongozi waliochoka vita ilikuwa tayari kuwakubali Wajerumani.[4]. Wajerumani waligawa eneo lao. Wasangu walirudishwa katika eneo lao la awali wakarudi kutoka Usafwa katika mji mkuu wa Utengule Usangu. Mpangile alisimikwa kama kiongozi mpya wa Uhehe penyewe, lakini baaa ya siku 50 alisimamishwa na kuuwa na Wajerumani waliomshtaki, eti anamsaidia kaka yake kisiri.

Katika maficho na kifo

Mkwawa alikuwa ameondoka sehemu za Iringa mwezi Agosti 1896 alipoona mgawanyiko. Alifuata mwendo wa mto Ruaha akilindwa na wenyeji waliokuwa tayari kumficha na kumlinda dhidi ya vikosi vya Wajerumani waliomtafuta.

Mnamo Desemba 1896 alihamia milima ya Uzungwa alipojificha. Kutoka huko alitelemka mara kwa mara kwenye mabonde alipopata vyakula na kushambulia vikosi vidogo vya askari vya Kijerumani.

Katika Julai 1897 kikosi kikubwa cha Wasangu pamoja na Wahehe chini ya uongozi wa Wajerumani walikuta kambi la Mkwawa mlimani wakalishambulia lakini Mkwawa aliweza kukimbia.

Mwaka 1898 Mkwawa aliendelea kujificha kwenye misitu akiongozana na watu wachache sana. Aliishi hasa kwa njia ya kuvinda.

Wakati wa Julai 1898 aliongozana na wavulana 4 pekee, halafu Wazungwa 2, mume na mke. Tarehe 16 Julai Wajeumani waliowahi kusikia habari zake walimkuta huyu mama Mzungwa alipotafuta chakula wakamkamata hata akawaambia Mkwawa alielekea kusini. Wakamfuata na tarehe 18 Julai Mkwawa alimwua mume Mzungwa kwa hofu ya kusalitiwa.

Aliendelea na wavulana 2 tu walioitwa Musigombo na Lifumika. Watoto waliogopa angeweza kuwaua pia. Hapo Lifumika aliamua kukimbia asubuhi ya tarehe 19 Julai. Lakini siku ileile alipotelemka kutoka mlimani alikutana na kikosi cha Wajerumani akakimbia lakini wakamshika wakamlazimisha kuwaambia habari za Mkwawa. Kijana alimwambia sajenti Mjerumani kuwa chifu alikaa mgonjwa mahali kwa umbali wa masaa 3. Walimlazimisha kuwaongoza. Njiani walisikia kwa mbali sauti ya bunduki, risasi 1. Wakaendelea na baada ya masaa mawili walikuta maiti za Mkwawa na yule kijana mwingine. Inaonekana waliwahi kujiua na sauti ya bunduki ilikuwa Mkwawa aliyejipigia risasi.[5].

Fuvu la Mkwawa

Fuvu la Mkwawa katika Makumbusho ya Kalenga karibu na Iringa, Tanzania.

Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen.

Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema. Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthibitishwa kwa mkataba huu ... Ujerumani utakabidhi fuvu la Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza."
Fuvu la Mkwawa katika Makumbusho ya Kalenga karibu na Iringa, Tanzania.
 
Wajerumani walikataa habari za fuvu hili na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kulipata.

Lakini baada ya Vita vikuu vya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Katika mkusanyiko wa mafuvu 2000, 84 yalikuwa na namba zilizoonyesha yalitokea Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapo aliyapanga kufuatana na ukubwa na kutazama yale yaliyokuwa na vipimo vya karibu na ndugu wa Mkwawa aliowahi kuwapima kabla ya safari yake. Hapo aliteua fuvu lenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipiga risasi kichwani.

Fuvu hilo lilipelekwa Tanganyika tarehe 9 Julai 1954 na kuhifadhiwa katika jengo la makumbusho ya Mkwawa kwenye kijiji cha Kalenga.

Athari yake upande wa dini

Mkwawa alifuata dini za jadi, na alikataa ombi la Walutheri la kuanzisha misheni Uhehe, lakini baadaye alikubali wamisionari Wabenedikto wa Kanisa Katoliki wahamie Tosamaganga na kuanza kazi yao kati ya Wahehe.

Hata wakati wa vita vyake dhidi ya Wajerumani, Mkwawa aliwaheshimu wageni wake hawa.

Matokeo yake Wahehe wengi waliingia taratibu Ukristo kupitia madhehebu ya Kikatoliki hadi leo.

Saturday, 3 September 2016

AJIRA ZA WALIMU MWAKA HUU

TAARIFA MUHIMU KUHUSU AJIRA ZA WALIMU MWAKA HUU,

Naibu Waziri ofisi ya Nchini,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)Suleiman Jaffo (kulia)akizungumza na Mwandishi wa Fullhabari.blogs Karoli Vinsent (Kushoto) leo Jijini dar es SalaamNaibu waziri ofisi ya Nchi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleiman Jaffo amewatoa hofu wahitimu wote nchini waliosomea ualimu ambaowamekuwa wakisubili ajira kutoka serikalini kwa muda mrefu,Hivyo amewataka walimu hao kuwa na subira kwani ajira hizo zitatangazwa mda wowote kutoka sasa.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.Jaffo ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na Mtandao huu ambapo amesema wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya Elimu wameshamaliza hatua ya kwanza ya kuhakiki idadi haswa ya walimu wanaohitajika pamoja na ile idadi ya wahitimu  wa masuala hayo .Amesema zoezi lilobakia kwa sasani kumalizia takwimu za walimu waliostaafu kazi pamoja na waliohama kutoka serikali kwenda kwenye shule binafsi ili serikali iweze kujua idadi harisi ya pengo la walimu nchini.Hata hivyo,Jaffo amesema katika mwaka huu serikali inampango wakuongeza idadi ya ajira za walimu hadi kufikia walimu elfu 40000 katika ngazi za shule za msingi na sekondari.Jaffo pia amesema kwa sasa ajira hizo zitapewa kipaumbele katika maeneo ya pembezoni mwa nchi ambayo amedai kuwa kuna uhaba sana wa walimu .Ameitaja mikoa hiyo ni Mkoa wa Kigoma,Mara,Tabora,Rukwa,kwa mujibu wa Jaffo amewataka wahitimu hao kujiandaa kufundisha katika maeneo hayo nakutoa dhana ya kufundisha kwenye shule za mijini.

AJIRA ZA WALIMU 2016/17

Angalia link hii

http://fullhabari.blogspot.com/2016/04/taarifa-muhimu-kuhusu-ajira-za-walimu.html?m=1

Monday, 4 July 2016

PO-RALG

PO-RALG http://tamisemi.go.tz/form_five_selection/ -- shared by UC Mini

Friday, 22 April 2016

Billionair (Bill) William Henry Gates

Jina lake halisi anaitwa William Henry Gates, III ingawa wengi wanamjua zaidi kama Bill Gates. Kwa mujibu wa Mtandao wa Forbes na Jarida la Bloomberg Billionaires List, Bill Gates ndiye tajiri namba moja duniani kwa mwaka 2014.

Yafuatayo ni mambo kumi ambayo huyajui (au unayajua lakini nakukumbusha) kuhusu bilionea huyu.

1. Kwa mara ya kwanza, alitangazwa kuwa bilionea mwaka 1987, akiwa na umri wa miaka 32 tu, akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.25.

2. Bill Gates alianza utundu wa kuchezea vifaa vya kielektroniki akiwa na umri wa miaka 13. Amewahi kusimamishwa masomo kwa kuharibu kompyuta shuleni.

3. Licha ya kufaulu kwa kiwango kikubwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Havard, Bill Gates alisoma kwa kipindi kifupi tu, akaacha chuo na kuelekeza nguvu kwenye kubuni programu za kompyuta.

4. Kabla hajaoa, Bill Gates amewahi kuingia kwenye orodha ya mabachela wasafi zaidi na wanaojua kutunza nyumba zao.

5. Amelelewa katika maadili ya kidini, alianza kupelekwa kanisani na wazazi wake tangu akiwa mdogo na anaendelea kufanya hivyo mpaka sasa. Ni Mkatoliki.

6. Watu wake wa karibu huwa wanamlalamikia mara kwa mara kutokana na tabia yake ya kutopokea simu akipigiwa au kutumiwa meseji. Hata mkewe huJmlaumu kwa tabia hii.

7. Amewahi kukamatwa na kutupwa selo kutokana na kukutwa na hatia ya kuendesha gari kwa spidi kubwa.

8. Ni shabiki mkubwa wa wasanii Bruno Mars na Lady Gaga. Anaweza kuuimba wimbo wote wa I Wanna be a Billionaire wa Bruno Mars.

9. Amepanga kwamba akifa, wanaye watatu wasirithi hata senti tano yake, badala yake utajiri wote ugawiwe kwa watu maskini. Anasisitiza kuwa lazima wanaye wajitafutie fedha zao.

10. Eti anachukia kuwa tajiri kwa sababu anashindwa kuishi maisha yake halisi. Anatamani kuwa mtu wa kawaida.

Saturday, 2 April 2016

FAIDA 17 ZA KUTUMIA MAJANI YA MPERA(GUAVA LEAVES).

Habari yako rafiki yangu mpendwa ambae unendelea kufuatilia Makala za afya kwenye page hii iitwayo Koroti Product Supply Tanzania na kama hujalike bofya like sasa uendelee kupata  Makala zinazohusu afya yako. Siku ya leo ningependa kueleza kuhusu faida za kutumia mmea ambao umeonekana ni mmea wa kawaida ila unafaida nyingi katika afya yetu
Mapera ni matunda ya msimu yenye wingi wa vitamini A na C, madini ya potasiam, nyuzi nyuzi nzuri yani fiber na 'lycopene' vyote hivi ni muhimu kwa afya.
Watu wengi hutumia tunda tu pasipokujua si tunda pekee lenye manufaa kwa afya zao. Majani ya mpera ni mazuri sana kwa ajili ya kisukari,ngozi, nywele na afya yako kwa ujumla.

FAIDA ZA KUTUMIA MAJANI YA MPERA KWA AJILI YA AFYA YAKO.
1.Chai ya majani ya mpera inasaidia mwili kuwa stadi, inasaidia madini ya carbohydrates yasigeuzwe kuwa sukari ndani ya mwili hivyo kupunguza hamu ya kula.
2.Chai ya majani ya mpera pia inashusha kiwango cha sukari mwilini na kuzuia mwili kuondoa 'insulin'. Kwa sababu hii wagonjwa wa sukari wanashauriwa kuitumia mara kwa mara.
3.Chai ya majani ya mpera pia hupunguza lehemu mbaya(bad cholestrol) bila kudhuru lehemu nzuri.
4.Chai hii ina nguvu za kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini hasa kuzuia magonjwa ya kuharisha na kipindupindu.
5.Chai hii inalinda mchafuko wa tumbo na pia inasaidia kukabili madhara yaletwayo na chakula chenye sumu.
6.Chai hii hutibu kukohoa na kupumua kwa tabu.
7.Upatapo uvimbe wa fizi na maumivu mdomoni kama jino kuuma, tafuna majani ya mpera.
8.Kwa matatizo ya homa ya dengue, chemsha glasi mbili na nusu na majani ya mpera (kadiria majani 9) mpaka maji yabakie nusu ya ujazo wa awali.
9.Chai ya majani ya mpera imefahamika kutibu kansa na 'prostate' kwa wanaume.
10.Chai hii inasaidia kwa wanaume wenye tatizo la kuzalisha (Infertility).
11.Ponda majani ya mpera na kuweka sehemu ya kidonda au iliyokatika kuondoa maambukizi. Kwa maumivu nje ya sikio tumia chai ya majani ya mpera. Tia matone ya chai hii iliyopoa kwenye sehemu iliyoathirika.
13.Majani ya mpera hupondwa na kupakwa eneo lenye muwasho uletwao na allergy.
14.Unapoumwa na wadudu majani yaliyopondwa ni tiba sahihi.
15.Majani ya mpera yana saidia kupigana na mba na chunusi kutokana na wingi wake wa vitamini C.
16.Kuondoa madoa meusi kwenye ngozi ponda majani ya mpera changanya na maji kiasi na upake badala ya dawa za kawaida.
17.Fanya kama namba16. kwa tatizo la ngozi kuzeeka mapema.
18.Majani ya mpera yanaondoa tatizo la kukatika kwa nywele. Chemsha majani kisha wacha yapoe na ukande kwenye paji na eneo la ngozi taratibu kwa dakika 15. Wacha kwa dakika 30 kisha osha na maji safi bila shampoo au sabuni. Fanya hivyo mara 3 kila wiki.
Wengi wananiuliza namna ya kuitengeza chai ya majani ya mpera. Kuna namna mbili. Aidha chemsha maji kama glasi nne mpaka itokote sana, chukua majani kama 10 ya mpera, weka ndani ya yale maji moto kisha funika kwa dakika 10 - 15 koroga, chuja, chai yako tayari. Aina ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani yakiwa ndani. Ikitokota ondoa kwenye moto, wacha kwa dakika 10 -15 chuja, chai tayari. Waweza ukatumia majani yaliyo kauka pia.
Zingatia ukichanganya na asali badala ya sukari ndio bora zaidi.

Najua umepata kujifunza kitu rafiki yangu kama umependezwa na tiba hii ya leo  share na marafiki zako na magroup mbalimbali 
Pia kwa ushauri juu ya afya yako mpendwa wasiliana nami kwa
NAMBA 0656459057
WhatApp 0656459057
Pia unaweza kunifollow instagram KOROTI MWASHUNGU