Ni mwaka wa tatu
sasa toka Soko la Mwanjelwa lianze kujengwa upya baada ya ajali ya moto iliyowapatia
hasara kubwa wafanyabiashara wa Mbeya kwa kuunguliwa bidhaa na mazao mbalimbali
ya biashara, yaliyokuwemo katika soko hilo.
Wengi wao walitarajiwa
kuwa ujenzi wa soko ungeenda haraka kutokana na umuhimu na mahitaji makubwa ya soko
hili kwa wakazi wa Mbeya, mikoa ya karibu na nchi jirani za Zambia na Malawi.
Hali imekuwa tofauti
kwa sababu sasa ni mwaka wa tatu tangu ujenzi uanze huku shauku kubwa kwa wafanyabiashara
ikilitaka liishe mapema na waingie kuendeleza biashara zao.
Mkoa wa Mbeya ni Jiji
linalokua kwa kasi na matarajio wengi kuboreka kwa miundo mbinu na masoko ya biashara
kama kichocheo cha uchumi.
Je, pamoja na jitihada
mpya ya kulijenga soko hili, je litaweza kumudu majanga ya moto ambayo yamekuwa
yakilikumba soko hilo mara kwa mara. Hili ndilo swali kubwa ambalo linapaswa kuulizwa
na kila mmoja wetu mpenda maendeleo. Tusubili tuone mara baada ya kukamilika na
kuanza kutumika.
Zifuatazo ni baadhi
ya picha zilizopigwa kuonesha ujenzi wa Soko la Mwanjelwa ukiendelea....
No comments:
Post a Comment