HISTORIA FUPI YA KAUKI
KAUKI ni Umoja
wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na changamoto
mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii inayounda umoja huu; hususani
katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana ili
kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga, maradhi na utegemezi. Kuanzishwa kwa KAUKI
kuliambatana na maandalizi yaliyojumuisha mikutano zaidi ya 10 ya mashauriano
iliyofanyika sehemu mbalimbali Jijini Dar es Salaam na Kidamali, Iringa.
Dira
ya KAUKI
Kuwa na
jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa kujitegemea.
Maono
ya KAUKI
Kujengeana
uwezo kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia mafunzo,
kongamano, mijadala na mikutano ili kuboresha maisha.
Malengo
ya KAUKI
Lengo
Kuu
Kuinua na
kuboresha maisha ya wanaukoo wa Kivenule, kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa
kutumia ujuzi, maarifa na raslimali zinazotunguka.
Malengo
mengine mahsusi
§
Kuujua na kuelewa kwa kina Chimbuko na Historia ya Ukoo wa
Kivenule;
§
Kuzikusanya, kuziratibu na kuzihifadhi kumbukumbu
mbalimbali za Ukoo wa Kivenule.
§
Wanaukoo kupata fursa ya kufahamiana na kutambuana;
§
Kufanya senza ya ndugu/wanaukoo wanaounda Ukoo wa Kivenule
kila inapobidi kufanya hivyo na Senza hiyo itajumuisha watu waliohai na wafu;
§
Kuanzisha Mfuko wa Ukoo wa Kivenule utakaosaidia kuinua
kiwango cha Elimu na pia kusomesha wanaukoo wasio na uwezo wa kumudu kulipa ada
za shule au vyuo;
§
Kuboresha Elimu ndani ya Ukoo wa Kivenule ili
ndugu/wanaukoo wawe na uelewa wa hali juu na kumudu mabadiliko ya Sayansi na
Teknolojia katika Dunia ya Utandawazi;
§
Kusuluhisha na kutatua matatizo yanayojitokeza katika Ukoo
wa Kivenule kwa kupitia vikao vinavyokubalika;
§
Kuelimisha Wanaukoo/ndugu kuhusiana na madhara ya ugonjwa
wa UKIMWI, matumizi ya Madawa ya Kulevya na Ulevi wa kupindukia;
§
Kuinua viwango vya maisha vya wanaukoo wa Kivenule na
kuishi maisha mbadala yenye milo kamili, furaha na nyumba bora na nadhifu;
§
Kuongeza na kuimarisha mahusiano mazuri ndani na nje ya
ukoo kwa kushirikiana katika matatizo mfano raha, ugonjwa, misiba pamoja na
majanga makubwa;
§
Kuwa na nguvu ya kurekebisha tabia zisizostahili kwa
wanaukoo/ndugu ndani ya Ukoo na kutafuta suluhu ya migogoro/migongano baina ya
mtu au jamii inayotuzunguka;
§
Wanaukoo kuutambua na kuuelewa mtawanyiko/mgawanyiko wa
Ukoo wa Kivenule;
§
Wanaukoo/ndugu kushirikiana katika shughuli za uzalishaji
mali pamoja na utendaji kazi wa kila siku;
§
Kushirikiana na umoja au vikundi vingine vilivyoungana ili
kuuletea Ukoo wa Kivenule maendeleo endelevu;
§
Kuanzisha Mfuko wa kukopeshana (SACOSS); na
§
Kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya uvivu na uzembe ndani
ya Ukoo wa Kivenule.
Muundo
wa KAUKI
KAUKI
inaundwa na Kanda sita ambazo ni Kidamali, Irole, Nduli, Magubike, Mufindi na
Dar eS Salaam. Kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI, kuna Mkutano Mkuu ambao ndio
mkutano mkubwa kuliko yote. Hufanyika mara moja kwa mwaka. Pia KAUKI ina
mikutano ya Kamati ya Utendaji ambayo hufanyika mara nne kwa mwaka kwa vipindi
vya miezi mitatu mitatu. Katika Kanda pia kuna mikutano midogo midogo ambayo
jukumu lake ni kujadili masuala yanayohusiana na maendeleo ya kanda. Muundo wa
Uongozi wa KAUKI upo kama ifuatavyo:
Nafasi za Uongozi Mkuu wa KAUKI
§
Mwenyekiti: Donath
P. Mhapa 0658 843 565
§
Makamu Mwenyekiti: Christian
J. Kivenule 0714 146 382
§
Katibu Mkuu: Adam
A. Kivenule 0713 270 364
§
Mweka Hazina Justin
D. Kivenule 0784 855 739
Nafasi
za Uongozi wa Kanda
Kila kanda
ina kiongozi wake ambaye ni Mwenyekiti, ambaye naye husaidiana na Katibu. Pia
ndani ya Kanda kuna viongozi wa Kamati mbalimbali ambazo zipo kwa mujibu wa
Katiba ya KAUKI.
Katiba ya
KAUKI ndiyo mwongozi mkuu wa shughuli zote zinazofanywa na umoja huu. Katiba ya
KAUKI ilipitishwa rasmi katika Mkutano MKuu wa Pili wa KAUKI uliofanyika
Kidamali, Iringa.
Historia
Fupi ya Kuanzishwa kwa KAUKI
Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI
zilianza kwa kuratibu mawazo ya wana-ukoo wawili, yaani Ndugu Faustino Kivenule
na Ndugu Christian Kivenule mwezi Desemba 2004. Mawazo hayo yalifanyiwa kazi
kwa kumshirikisha pia Ndugu Adam Kivenule, ambaye bila kuchelewa, waliweza
kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mashauriano, Jijini Dar es Salaam. Mkutano
huo ulifanyika katika ukumbi wa River Side, tarehe 6 Februari, 2005 – Jijini
Dar es Salaam.
Harakati nyingine za maandalizi
zilielekezwa upande wa Kidamali, Irore na Nduli. Kwa upande wa Kidamali,
Mkutano wa Kwanza wa Mashauriano kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulifanyika mwezi Mei ambapo wajumbe toka
Dar es Salaam walisafiri kwenda huko ili kuwasilisha hoja, kufanya mashauriano
na majadiliano, kuchagua viongozi wa kusimamia uratibu na kuunda kamati ya
maandalizi.
Maeneo mengine kama Nduli na Irore
hazikuweza kufanya maandalizi ya moja kwa moja japo taarifa toka Dar es Salaam
ziliweza kufikishwa na baadhi ya wanaukoo wanaishi huko. Mjumbe mmoja tu ndugu
Augustino Kivenule, toka Mgongo, Iringa ndiye aliyeweza kumudu kushiriki katika
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule.
Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI
Huu ni
Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI ambao unafanyika nyuma ya mikutano mingine Nane
ambayo imekwisha fanyika, mitatu Kijijini Kidamali na Mkutano moja moja
Kijijini Irole, Nduli, Magubike (Iringa Vijijini), Igowole (Mufindi) Mkoani
Iringa, na Mkutano mmoja Jijini Dar es Salaam (Karibu na Tabata Shule). Kwa
mujibu wa makubaliano na utaratibu ambao umewekwa na Wana-KAUKI, mikutano hii
itakuwa inafanyika katika ngazi ya Kanda, ili kuipa fursa jamii inayounda KAUKI
kushiriki moja kwa moja. Lakini pia, vipaumbele huwekwa pale ambapo kuna idadi kubwa
ya wana-KAUKA, lakini huridhiwa wakati wa Mkutano Mkuu. Kwa msingi huo, Mkutano
Mkuu wa Nane wa KAUKI, kwa kauli moja, uliazimia kuwa Mkutano Mkuu wa Tisa
ufanyike katika Kanda ya Kidamali, Iringa Vijijini, tarehe 29– 30 ya Juni,
2013.
Angalia
picha za matukio katika Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI uliofanyika Jijini Dar es
Salaam, Juni 30 - Julai 1, 2012
http://www.facebook.com/photo.php?fbid=497523093617046&set=a.497521733617182.1073741825.100000780786862&type=1&theater
Kwa taarifa
zaidi, angalia http://www.tagumtwa.blogoak.com http://www.facebook.com/tagumtwa na http://www.twitter.com/tagumtwa
No comments:
Post a Comment