Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Monday, 18 March 2013

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA TISA WA KAUKI



TANGAZO

MKUTANO WA TISA WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE-KAUKI

Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), kwa heshima na taadhima, unachukua fursa hii kuwatangazia Wana-KAUKI wote, Ndugu, Jamaa na Marafiki, wanaoishi mijini na vijijini kutoka katika Mikoa yote ya Tanzania Bara; Mkutano wa Mkuu wa Tisa (9) wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), utakaofanyika katika Kijijini Kidamali, Wilayani ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa; kuanzia tarehe 29 - 30 Juni, 2013.

Wana-KAUKI Wote na Wapenda Maendeleo kwa Ujumla, na wale wote wanaoguswa na harakati zetu, wanaombwa kusaidia maandalizi ya Mkutano huo kwa kuchangia fedha, nafaka na raslimali nyingine, ambazo zitasaidia kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo, pamoja na huduma muhimu kama chakula, kabla, wakati na baada ya Mkutano huo, kwa wageni wote.

Kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI, inakuomba/inawaomba

Pia nachukua fursa hii kuwakaribisha jamaa na marafiki ambao wanapenda kujifunza namna KAUKI inavyofanya kazi kwa kipindi cha miaka 8, toka umoja huu ulipoanzishwa rasmi mwaka 2005.

Kwa taarifa mbalimbali kuhusiana na shughuli za KAUKI na matukio mbalimbali katika mikutano yetu, matatizo ya kijamii mfano misiba na mengine mengi fungua http://www.tagumtwa.blogoak.com pia tunapatikana kupitia http://www.facebook.com/tagumtwa na www.twitter.com/tagumtwa 

Natanguliza shukrani zangu za dhati,


Wako katika kazi,

Adam Kivenule
KATIBU MKUU-KAUKI

No comments:

Post a Comment