He will choose you, disarm you with his words, and control you with his presence. He will delight you with his wit and his plans. He will show you a good time but you will always get the bill. He will smile and deceiveyou, and he will scare you with his eyes. And when he isthrough with you, and he willbe through with you, he will desert you and take with himyour innocence and your pride. You will be left much sadder but not a lot wiser, and for a long time you will wonder what happened and what you did wrong. And if another of his kind comes knocking on your door, will you open it?-From an essay signed "A psychopath in prison
ADAM KIVENULE BLOG: For information call +255 713 270364 E-mail: kivenule@gmail.com Blog: http://www.adamkivenule.blogspot.com Twitter: http://www.twitter.com/kivenule Youtube: http://www.youtube.com/tagumtwa KIVENULE CLAN BLOGS: http://www.tagumtwa.blogoak.com http://www.kauki-kauki.blogspot.com E-mail: KAUKI2006@gmail.com or tagumtwa@gmail.com
Sunday, 29 November 2015
Thursday, 26 November 2015
Dondoo 10 muhimu sana kwa walezi /Wazazi na Wazazi watarajiwa wote
Dondoo 10 muhimu sana kwa walezi /Wazazi na Wazazi watarajiwa wote
1. Mkanye mtoto wako wa kike na hata wa kiume kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.
2. Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.
3. Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao "Mchumba", "Mke wangu" au "Mme wangu".
4. Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu na wengine wana maambukizi....
5. Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwendakwa mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.
6. Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.
7. Mwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za sirimwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo.
8. Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.
9. Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.
10. Usipende kumruhusu mwanao kulala na housegirl au houseboy au mgeni. Huwezi jua tabia za watu na wanayomtendea usiku!!!!
AROBAINI YA MAREH. LILIAN IGNAS KIVENULE
AROBAINI (40) YA MAREHEMU LILIAN IGNAS KIVENULE
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya familia ya Ignas Kivenule na Mme wake Mareh. Lilian Kivenule, inatumia fursa hii kuwafahamisha ndugu, marafiki na jamaa wa karibu, kuwa Arobaini ya ndugu yao mpendwa itakuwa tarehe 05 Desemba 2015.
Arobaini hiyo inatarajiwa kufanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu, Buyuni – Chanika, Mkoani Dar es Salaam. KAUKI na Familia ya Ignas Kivenule kwa pamoja, wanawaomba ndugu, jamaa, marafiki na umma kwa ujumla kujumuika nao siku hiyo.
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe, AMINA.
Imetolewa na kusambaza na:
Adam Kivenule
Katibu Mkuu – Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
--
P.O. Box 3255,
Dar es Salaam
Mob. +255 713 270364
E-mail: kivenule@gmail.com / KAUKI2006@gmail.com
Blog: www.adamkivenule.blogspot.com
Twitter: www.twitter.com/kivenule
Thursday, 5 November 2015
TANZIA
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya wana ukoo wa Ukoo wa Kivenule, inatoa pole na masikitiko kwa msiba wa ndugu yao Lilian Ignas Kivenule, aliyefariki usiku wa tarehe 31 Oktoba 2015 na kuzikwa siku ya tarehe 02 Oktoba katika Makaburi yaliyopo Buyuni Chanika, mkoani Dar es Salaam.
Kuondoka kwa Lilian Kivenule kumeacha pengo kubwa kwa ukoo wa Kivenule, hususani familia yake na wazazi wake. Ni kifo cha ghafla na hakikutegemewa.
Kama Ukoo na KAUKI tunasema hiyo ni mipango ya Mungu. Kilichobaki ni kumwombea ili aweze kupumzika kwa amani.
Rest in Peace Lilian..
Kama wana Ukoo na KAUKI kwa ujumla, ndugu, jamaa na marafiki tutakukumbuka daima.
Asante,
Imetolewa na:
Adam Alphonce
Katibu - Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)