Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Thursday 26 November 2015

Dondoo 10 muhimu sana kwa walezi /Wazazi na Wazazi watarajiwa wote

Dondoo 10 muhimu sana kwa walezi /Wazazi na Wazazi watarajiwa wote

1. Mkanye mtoto wako wa kike na hata wa kiume kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.

2. Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.

3. Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao "Mchumba", "Mke wangu" au "Mme wangu".

4. Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu na wengine wana maambukizi....

5. Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwendakwa mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.

6. Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.

7. Mwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za sirimwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo.

8. Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.

9. Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.

10. Usipende kumruhusu mwanao kulala na housegirl au houseboy au mgeni. Huwezi jua tabia za watu na wanayomtendea usiku!!!!

No comments:

Post a Comment