Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Sunday, 24 January 2016

JINSI YA KUMUUA MAMA-MKWE

Miaka kadhaa huko Uchina, Binti aitwaye Li-Li aliolewa na akaenda kuishi kwao mumewe na mama wa mumewe.Ndani ya muda mfupi Li-Li alijikuta hana maelewano kabisa na mama Mkwe wake.

Tabia zao zilikuwa tofauti kabisa, walipishana kauli kila mara na Li-Li alichukizwa sana na tabia nyingi za mama mkwe wake.

Mbaya zaidi, mama-mkwe alimlaumu na kumsema vibaya Li-Li mara zote.Kadri ya siku na wiki zilivyopita, Li-Li na mamamkwe wake walizidi kubishana na kugombana. Kilichofanya hali kuwa ngumu sana nimila kuwa Li-Li alitakiwa kumnyenyekea na kutimiza kila alichohitaji.

Ugomvi na kukosekana amani ndani ya nyumba vilimsababishiamfadhaiko na kumyima amani mume wa Li-Li kwani aliwapenda wrote.

Baada ya kushindwa kumvumilia mama Mkwe wake ambaye alinung'unika kila mara na kutaka kuwa ndiye anayefanya maamuzi yote ndani ya nyumba, Li-Li aliamua kwenda kwa rafiki wa baba yake,Huang, ambaye alikuwa anauza Dawa za mitishamba.Alimuelezea hali ilivyo na akamuomba kama anaweza kumpa Dawa yenye sumu ili aweze kutatua tatizo mara moja na lisijirudie tena.Huang, alifikiria kwa muda na mwishowe akamwambia, "Li-Li, nitakusaidia kutatua tatizo lako. Lakini lazima unisikilize na utekeleze masharti nitakayokuambia"Li-Li akasema, "Ndiyo, Huang, nitafanya chochote utakachoniambia'. Huang akazunguka nyuma ya chumba na akarejea dakika chache baadae akiwa na kifurushi cha mitishamba.

Akamwambia Li-Li,"Huwezi kutumia sumu itakayo muua haraka mamamkwe wako kwa maana itasababisha watu wakuhise kuwa wewe ndiyo umemuua.Hivyo nakupa sumu itakayojengeka mwilini mwake taratibu na kumuua baada ya muda mrefu. Sharti ni kuwa kila siku muandalie chakula kitamu anachokipenda na changanya kiasi kidogo cha Dawa hii. Ili kuhakikisha hakuna anayekuhisi atakapokufa, lazima uwe makini na kuwa naye karibu na kuwa rafiki yake kuanzia sasa. Usibishane wala kugombana naye, kila anachoomba mtekeleze na mjali na kumthamini kama malkia.

Li-Li alfurahi sana maana sasa alijua tatizo lake limekwisha.Alimshukuru Huang na akaenda mbio nyumbani na kuanza mkakati wake wa kumuua mama mkwe wake.

Wiki na miezi ilipita na kila siku Li-Li alimpikia mama Mkwe wake chakula maalumu anachokipenda. Alikumbuka masharti ya Huang kuwa aepuke kugombana naye au kumsema vibaya, hivyo akajifunza kuzuia hasira zake, akatii maagizo na kumjali mama mkwe wake kama mama yake wa kumzaa.Baada ya miezi sita, maisha ndani ya nyumba yalibadilika sana.Li-Li alikuwa amemudu kudhibiti hasira zake kiasi kwamba hakuna siku aliyokasirikawala kujisikia vibaya.

Hakuwa amegombana na mama mkwe wake kwa miezi 6 maana mama Mkwe wake sasa alionekana mpole, mwenye moyosafi na rahisi kuelewana naye.

Tabia ya manunguniko na lawama za mama Mkwe kwa Li-Li pia ziliisha, na mama huyu alianza kumpenda Li-Li kama mwanaye wa kumzaa. Mamahuyu alianza kuwaeleza ndugu na marafiki zake jinsi ambavyo Li-Li ni mkamwana bora ambaye siyo rahisi kupata mkamwana kama huyu.

Li-Li na mamamkwe wake wakaanza kuishi kama Binti na mama yake halisi wa kumzaa.Mume Wa Li-Li alijawa na furaha kuona kinachoendelea.Siku moja Li-Li akarudi kwa Huang kuomba msaada wake tena. Akasema, "Huang,tafadhali naomba unisaidie sumu isimuue mama yangu. Amebadilika sana na sasa ni mama mzuri sana, nampenda kama mama yangu wa kunizaa. Sitaki afe kwa sababu kwamba nimempa sumu"Huang alitabasamu na kutikisa kichwa.

Akasema,"Li-Li, usihofu chochote. Dawa niliyokupa haikuwa sumu. Ilikuwa ni vitamini za kuboresha Afya.Sumu pekee ya kuharibu uhusiano wenu ilikuwa ndani ya fikra zako kwa jinsi uliyokuwa unamtendea mama Mkwe wako vibaya, lakini sasa sumu hiyo imesafishwa kwa upendo mkubwa uliomwonyeshamama huyu"CHA KUJIFUNZA:

Umewahi kufikiria kwamba jinsi unavyowatendea wenzako ndivyo hivyo hivyo wanavyokutendea? Ukiwasengenya watakusengenya pia, ukiwasema vibaya watakusema vibaya pia, ukiwachukia wanakuchukia pia.Pana Msemo wa Kichina unasema, "MTU yeyote anayewapenda wengine, naye atapendwa pia" Mungu anaweza kuwa anatenda katika maisha ya wengine kwa kukutumia wewe.Tuma ujumbe huu kwa wengine na usambaze nguvu ya upendo katika maisha ya watu.

Thursday, 14 January 2016

MAAJABU YA NJOZI

MAAJABU YA NJOZI

Ilikuwa ni muda wa saa 7 usiku nashukuru Mungu niliweza kutembea mpaka posta kutokea Gymkana na hakukuwa na basi ilinilazimu niende ATM kutoa pesa ili nipande taksi nikiwa naenda nilipishana nadada mmoja akiwa anakimbia sikumjali ila nilpoingia ATM sikuamini macho yangu nikuta pesanyiiiingii zimemwagka na mkoba wakike uliojaa pesa na smart phone 2 za bei kali sikupoteza muda nilivua shati na kukusanya ela zote nikazfunga vizuri nikaubeba na ule mkoba na simuniliita taksi ikanipeleka hom fasta nikiwa na waswas nilifika hom salama nikaanza kuhesabu pesa mara simu ikaita kati ya zile nilizochukuwa nikapuuzia zikaita kwa zamu kwa fujo nikapokea sauti ya kike ikasikika samahani sana naomba uniambie uko wapi nikufate please nionee hurumanilipgwabutwaa kwanza nilijikuta naropoka niko mbagala kizuiani ukishuka hapo ulizia mahakama ya chapati alijibu asante nashukuru sana kaka Mungu akulinde baadae nikajilaumu dahh! nimefanya nini sasa ?? nikaamua kulala saa 12:00 asbh simu ikaita tena nikapokea sauti iliskka nimefika naomba unifate kakaangu please nilimjibu nakuja nilitoka nje mita chache niliona prado mpyaa imesmama then kuna bint kasmamamlangoni akipgasimu simu ikaita tena nikajibu nimekuona . nilimkarbisha geto akasogeza gari hom aliniomba nimpe zilipesa na vitu vyote ni vyakwake huku machozi yakimtoka niliingiwa na huruma nikampa huku nikisema kisichorzki hakilikiakniambia usiseme hivyo yalinikuta makubwa paleATM aliondoka lakini kesho yake akaja mchana aliniomba tutoke tukatembee kidogo alinipeleka mbezi beach na kunikabidh funguo ya nyumba kubwa ya kifahari akisema zawadi yako kwa wema wako nilizimia kwa furaha nilipozinduka aliniambiaturudi hom tulifika akanimbia kafungue but ya garinilikuta pesa nyingi mmmnooo nilipanda tena gari nikaropoka nakupenda saaana alinikumbatia moyoni niksema umaskini byeeeee gafla nilshtuka baada ya kupigwapigwa bega amka amka mjomba mama kasema usipochota maji leo huli we unalala tuuuu.!!..dahhh!! dogo amekatsha ndota yangu shenz kabsaa narudia umaskini

Sunday, 10 January 2016

MAAJABU YA MUNGU

Ilikuwa ni mwaka 1979, nikiwa nasafiri kutoka Dares salaam kwenda Arusha. Sijui ilikuwaje, lakiniilitokea. Tuliondoka Dar es salaam saa 12:30jioni. Wakati ule mabasi yalikuwa yakisafiri jionina usiku, siyo kama siku hizi.Nilikuwa nakwenda Arusha kwenye usaili kwa ajiliya ajira, nikiwa ndo kwanza nimemaliza kidatocha nne. Niliajiriwa moja kwa moja serikalini,kwani siku zile ajira zilikuwa ni za kumwaga.Hata hivyo, sikulizishwa na kazi niliyokuwanafanya, hivyo niliomba kazi kwenye kampunimoja kule Arusha na niliitwa kwa usaili.Tulifika mji unaoitwa Korogwe, ambao wakati uleulikuwa ndiyo mji maarufu kwa hoteli zake katikabarabara yote ya Segera hadi Moshi na Arusha.Tulipofika Korogwe, basi lilisimama kwa ajili yaabiria kupata chakula. Niliingia kwenye hotelimoja ambayo nakumbuka hadi leo kwamba,ilikuwa ikiitwa Bamboo. Niliagiza chakula na kulaharaka kutokana na muda mfupi wa kulauliotolewa na wenye basi la TTBS ambalo ndilonililosafiri nalo.Wakati wa kulipa ndipo niliposhangaa nakuogopa. Niliingiza mkono mifukoni na kukutakwamba, sikuwa na hela. Nilianza kubabaika namwenye hoteli alisema hawezi kukubali ujingahuo. "Abiria wengine wahuni bwana, anakula nakujifanya kaibiwa, ukikubaliana nao kla sikuhasara tu." Mwenye hoteli alisema kwakudhamilia hasa.Kulizuka zogo kubwa, huku mwenye hotelakisema ni lazima anipeleke polisi. Ni kweli,alimtuma mmoja wa watumishi wake kwendakituo cha polisi ili nishughulikiwe.Hapo hotelinikulikuwa na bwana mmoja aliyekuwa amekaapembeni na mkewe na mtoto wao wakila. Yulebwana alipoona vile, alimtuma mhudumu mmojaaniiite. Niliondoka pale kaunta nilipokuwanabembeleza na kuja kwa yule bwana.Alikuwa ni kijana mtu mzima kidogo, mwenyemiaka kama 50 hivi. Nilimsalimia na aliniitikia.Nilimsalimia mkewe pia. Yule mtu aliniuliza kisacha vurugu ile na nilimsimulia. Aliniuliza sasahuko Arusha ningeishi vipi wakati wa usaili kamanilikuwa nimeibiwa fedha zote, na ningerudi vipiDar es salaam. Nilimwambia nilikuwa napangakuangalia namna ya kurudi Dar es salaam, kamahuko polisi ningeaminika.Kama mzaha, bwana yule aliniambia angenipafedha za kutumia huko Arusha na nikirudi Dar essalaam, nimrudishie fedha zake. Nakumbukaalinipa shilingi 90 kwa ahadi kwamba nikirudi Dares salaam, nimpelekee pesa zake ofisini kwake.Alinielekeza ofisini kwake, mtaa wa Nkurumah nakuniambia kwamba, ameamua kunisaidia kwasababu, kila binadamu anahitaji msaada wamwingine na maisha haya ni mzunguko.Nilishukuru na kuondoka kukimbilia basini. Basililikuwa linanisubiri mimi tu. Nilipanda ndani yabasi na abiria wengine walinipa pole. TuliondokaKorogwe, lakini haikuchukuwa muda kabla basiletu halijapata tatizo la pancha ya gurudumumoja la mbele. Ilibidi tuegeshe pembeni ililitengenezwe. Baada ya matengenezo, tuliondokakuendelea na safari yetu.Karibu na mji wa Same kwenye saa saba usiku,basi letu lilisimama ghafla. Abiria walisimamandani ya basi na kulizuka aina ya kusukumana.Huko nje kulikuwa na ajali. Abiria tulishukaharaka na wengine huko chini walishaanza kupigamayowe, hasa wanawake. Niliposhuka niliona garindogo nyeusi ikiwa imebondeka sana na hapokando kulikuwa na maiti wawili.Nilijua ni maiti kwa sababu, walikuwawamefunikwa gubigubi. Halafu kulikuwa nakatoto kalikokuwa kanalia sana, kakiwakamefugwa kanga kichwani. "Tumwahishe huyumtoto hapo Same hospitalini, ameumia, ingawasiyo sana". Nilikatazama kale katoto ka kiumekenye umri wa miaka kama mitatu. Kalikuwakameumia kwenye paji la uso, lakini kalikuwa hai.Bila shaka, wale walikuwa ni wazazi wake,kalikuwa yatima tayari. Machozi yalinitoka.Baada ya kutoa msaada na askari wa usalamabarabarani kuchukua maiti wale, tulipanda basinikuanza safari yetu. Kale katoto kalichukuliwa najamaa fulani waliokuwa na Landrover ya serikalikukimbizwa hospitalini. Ndani ya basimazungumzo yalikuwa ni kuhusu ajali ile tu, haditunafika Arusha. Tulichelewa sana kufika Arushakwani tulifika kwenye saa tano asubuhi, badalaya saa mbili.Nililala kwenye hoteli rahisi na kufanya usailikesho yake. Ni hiyo kesho, baada ya usaili,niliponunua gazeti ndipo nilipata mshtukomkubwa ajabu. Kumbe wale watu wawiliwaliokufa kwenye ajali ile ya Same walikuwa niYule bwana aliyenisaidia hela na mkewe. Yulemtoto wao ndiye aliyeokoka. Niligundua hilobaada ya kusoma jina lake na jina la Kampunialiponiambia nimpelekee fedha zake nikirudi Dar,pamoja na picha yake, mke na mtoto. Nililia sanakama mtoto.Nilishindwa kujua ni kwa nini ilikuwa afe.Nilijiuliza ni nani sasa ambaye angemlea mtotoyule? Yalikuwa ni maswali yasiyo na majibu napengine ya kijinga pia. Nilijua kwamba, nilikuwa nadeni, deni la shilingi tisini zilikuwa ni sawa nashilingi laki moja za sasa. Kwa mara ya kwanzasasa nilijiuliza ni kwa nini marehemu Yulealiniamini na kuamua kunipa fedha zile. Sikupatajibu.Nilikata kipande kile cha gazeti la kiingerezakilichokuwa na habari ile. Nilichukua kipandehicho na kukiweka kwenye diary yangu. Deni,ningelipa vipi deni la watu? Nilijikuta nkipigamagoti na kuomba. Niliomba Mungu anipe uwezowa kuja kulilipa deni la mtu yule mwema. "Kwanjia yoyote Mungu naomba uje uniwezeshekulilipa kwa sura na namna ujuavyo wewe.Nataka kulilipa ili nami niwe nimemfanyia jambomarehemu." Niliomba. Nilirejea Dar es salaamsiku hiyohiyo.Kwa sababu ya mambo mengi na hasa baada yamatokeo ya usaili ule kuwa mabaya kwangu,nilijikuta nimekuwa na mambo mengi na kusahauharaka sana kuhusu mtu yule aliyenisaidia.Nilifanikiwa hata hivyo kupata nafasi ya kwendakusoma Chuo cha Saruji na baadaye chuo chaUfundi na hatimaye nilibahatika kwendaUingereza. Mwaka 1991, nilianza shughuli zangu.Ilikuwa ni mwaka 1995, nikiwa ofisini kwangupale jengo la Nasaco, ambalo liliungua mwaka1996. Nikiwa nafanya kazi zangu niliambiwa naseketari wangu kwamba kulikuwa na kijanaaliyekuwa anatalkka kuniona. Nilimuuliza ni kijanagani, akasema hamjui. Nilimwambia amruhusuaingie. Kijana huyo aliingia ofisini. Alikuwa kijanamdogo wa miaka 17 au 18 hivi, mweupe mrefukidogo. Alikuwa amevaa bora liende, yaanihovyohovyo huku afya yake ikiwa hairidhishisana.Nilimkaribisha ili mradi basi tu, kwani nilionaatanipotezea bure muda wangu. Ni lazima niwemkweli kwamba, sikuwa mtu mwenye hurumasana na nilikuwa naamini sana katika watuwenye pesa au majina. Nilimuuliza, "nikusaidienini kijana na ukifanya haraka nitashukuru maananina kikao baada ya muda mfupi." Nilisema nasikuwa na kikao chochote, lakini nilitaka tuaondoke haraka."Samahani mzee, nilikuwa na shida.Nina..nimefukuzwa shule na sina tena mtu wakunisaidia kwa sababu…Nime…nkokidato cha pilina hivyo natafuta tu kama atatokea mtu…"Nilimkatisha, "sikiliza kijana. Kama huna jambolingine la kusema, ni bora ukaniacha nifanye kazi.Hivi unafikiri kama nikiamua kumsaidia kila mtualiyefukuzwa shule, si nitarudi kwetu kwa mguu!Nenda Wizara ya Elimu waambie…Kwanzawazazi wako wanafanya kitu gani, kwa niniwashindwe…Kwa nini walikupeleka shule yakulipia kama hawana uwezio, wanataka sifa?""Hapana wazazi wangu walikufa na ninasomashule ya serikali. Nimekosa mahitaji ya msingi nanauli ya kwendea shuleni. Nasoma shule yaKwiro, Morogoro. Shangazi ndiyeanayenisomesha,naye ana kansa hivi sasa hatakazi hafanyi…" Alianza kulia.Huruma fulani ilinijia na nilijiambia, kama ni naulitu na matumizi ni kwa nini nisiwe mwema,angalau kwa mara moja tu. "Baba na mamawamekufa lini?" Niliuliza nikijua kwambawatakuwa wamekufa kwa ukimwi, maana kipindikile ndipo fasheni ya ukimwi ilipoanza, ambapokila anayekufa alihesabiwa kwamba kafa kwaukimwi."Walikufa kwa ajali nilipokuwa mdogo sana,nilipokuwa na miaka mitatu. Ndiyo shangaziyangu alinichukua na kunilea hadi sasa anakufakwa kansa." Yule kijana alilia zaidi. Naombaniwaambie wasomaji kwamba, kuna nguvu fulanina sasa naamini kwamba, ziko nguvu nyingiambazo huwa zinaongoza maisha yetu bila sisikujua.Kitu Fulani kilinipiga akilini paa! Nilijikutanamuuliza yule kijana. "Kwa nini umeamua kujakwangu, ni nani alikuelekeza hapa na wazaziwako walikufa mwaka gani na wapi?" Yule kijanaalisema "nimeona nijaribu tu kwa mtu yeyoteambaye anaweza kunisaidia, ndiyo nimejikutanikiingia hapa, sijui…sikutumwana mtu. Wazaziwangu walikufa mwaka 1979 huko Same na mimiwanasema nilikuwa kwenye ajali, nikaokoka.Niliumia tu hapa," alishika kwenye kovu juu yapaji lake la uso.Nilihisi kitu fulani kikipanda tumboni na kujakifuani, halafu niliona kama vile nimebanwa nakushindwa kupumua. "Baba yako alikuwa anaitwanani?" "Alikuwa anaitwa Siame…Cosmas Siame…"Niliinuka ghafla hadi yule kijana alishtuka.Nilikwenda kwenye kabati langu mle ofisini nakuchakura kwenye droo moja na kutoka na diary.Mikono ikitetemeka, nilitoa kipande cha gazetikutoka ndani ya diary hiyo, nilichokuwanimekihifadhi."Ndiyo, alikuwa anaitwa Cosmas Siame. Huyu nimtoto wake, ni yule mtoto aliyenusurika."Nilinong'ona. Nilijikuta nikipiga magoti na kusali."Mungu wewe ni mweza na hakunakinachokushinda. Nimeamini baba kwamba, kilajema tunalofanya ni akiba yetu ya kesho nakesho hiyo huanzia hapa duniani." Halafunilinyamaza na kulia sana. Nililia kwa furaha naugunduzi wa nguvu zinazomgusa binadamu kwaanalofanya.Nilisimama nikiwa nimesawajika kabisa. Nilijihisikuwa mtu mwingne kabisa. Nilimfuata yule kijanana kumkumbatia huku bado nikiwa ninalia. "Mimini baba yako mdogo, ndiye nitakayekulea sasa.Ni zamu yangu sasa kukulea hadi mwisho." Nayealilia bila kujua sababu na alikuwaamechanganyikiwa kabisa. Nilirudi kwenye kiti nakumsimulia kilichotokea miaka 17 iliyopita.Tuliondoka hapo na kwenda kumwona shangaziyake Ubungo, eneo la Maziwa ambako alikuwaamepanga chumba. Kutokana na hali yakenilimhamishia kwangu, baada ya kumsimuliakilichotokea. Huyu dada yake Cosmas alifurahihadi akashindwa kuzungumza kwa saa nzima.Hata hivyo alifariki mwaka mmoja baadaye, lakiniakiwa ameridhika sana.Kijana Siame alisoma na kumaliza Chuo Kikuu nakwenda Australia kufanya kazi. Ukweli nikwamba, ni mwanangu kabisa sasa. Naaminihuko waliko Mbinguni wazazi wake wanafurahiakile walichokipanda miaka mingi sana nyuma.Lakini nami najiuliza bado, ilikuwaje Cosmasakanipa msaada ule? Halafu najiuliza, ni kitu ganikilimvuta mwanaye Siame hadi ofisini kwanguakizipita ofisi nyingine zote? Nataka nikuambie,usiwe mbishi sana bila sababu, kuna nguvu zaziada zinazoongoza matokeo maishani mwetu.***************************kama umeguswa jaribu kuishare na rafiki zakowaisome

KISA MKASA

Ilikuwa siku iliyochosha sana, mvua kubwa ilikua ikinyesha ikiambatana na radi, ngurumo na miale isiyokwisha. Niliingia nyumbani mishale ya saa tano na nusu usiku. Nilikuwa nimechoka mno!! Nyumbani nilikuta ukimya usio wa kawaida huku nikipokelewa na kiza tororo "Maria! Maria!" niliita jina la mke wangu lakini sikupata muitikio wowote.Nikiwasha taa na kumkuta akiwa amelala ktk kochisebuleni.Kwa vile nilikua na njaa nilienda kula chakula alichoniandaliakilichokuwa mezani, sikutaka kumsumbua kumuamsha. Baada ya kula nilienda kuoga na nikaenda kulala. Kwa vile nilikuwa nimechoka nilipitiwa na usingizi mzito mno! Niliamshwa asubuhi na miale ya mwanga wa jua laasubuhi. Niliangalia muda na kukuta nikiwa nimechelewa kwenda kazini. Lakini kwa vile nilikua nimejiajiri sikuona kama itakuwa shida.Niliamka kivivu na kuanza kumuita maria lakini sikupata muitikio wowote pia, nilitoka nje na kumuangalia ila sikumkuta, nikajua atakuwa ashawahi kwenda kazini na hakutaka kunisumbua kuniamsha. Nilioga na nikala kifungua kinywa alichokua ameniandalia. Nilihisi hali ya tofauti kuhusu Maria. Miaka yetu mitano ya ndoa siku zote tumekuwa tukiongea wote kabla ya kwenda kazini. Na leo imekuwaje hali hii!? Nilipata wasiwasi sana.Baada ya kumaliza kifungua kinywa nilimpigia simulakini hakupokei nilifanya hivyo mara kadhaa lakinihakupokea hata mara moja. Niliumia mno moyoni.Nikaamua kwenda kazini. Huko kazi hazikwenda muda wote nilikuwa nikimkumbuka mke wangu. Watu wanasema ukimkumbuka mtu sekunde huwa kama mwaka. Niliamini huo msemo. Kila muda nilikuwa nikiangalia muda na simu yangu labda nitapata simu ya mke wangu lakini haikuwa kama nilivyotarajia.Niliumia sana. Nilikuwa nampenda sana mke wangu na sikujua kwanini amebadilika ghafla namna hiyo!Nilimaliza kazi zangu na kuondoka ofisini straight to home huku nikiwa na hamu ya kumuona mke wangu. Nikifika home na kupokelewa na binti yangu wa miaka mitatu. Alifurahi kuniona nikampachocolate na kumuuliza wapi mama. Alinionesha kuwa yuko jikoni. Nilikimbia haraka kuelekea jikonikama fisi aliyeuona mfupa. Nilimuona akiwa anaandaa chakula cha jioni. Nilinyata taratibu na kumkumbatia kwa nyuma. Ajabu hakuonesha kustuka wala kufurahia jambo lile. Alinisukuma nyuma na kuondoka jikoni. Sikumuelewa kwa kweli. Nilichanganyikiwa!!Siku zilisonga akizidi kujiweka mbali na mimi. Nikimuuliza kwanini sikupata jibu lolote la maana. Mapenzi yanauma sana. Hauwezi amini jinsi nilivyokonda kwa hizo siki chache. Nilimmiss mke wangu sio kidogo. Ufanisi wa kazi ulipungua sana. Alianza tabia ya kuwahi kwenda kazini na kuchelewa sana kurudi! Sikuweza kupata sababu yoyote ya maana!!Nilirudi nyumbani kama siku zingine za kawaida, nikijua nitamkuta Maria amelala kama kawaida, ila bahati nzuri nilimkuta akiwa macho sebuleni akionekana kunisubiri mimi. Nilifurahi walau sasa naweza pata wasaa wa kuzungumza nae. Aliinuka na kuja kunipokea begi langu la kompyuta pakato. Niliiona huzuni kubwa machoni mwake. Nilitaka kumkumbatia lakini alinikwepa na kwenda kukaa ktk kochi.Nilikaa karibu yake! "Nafikiri sikupendi tena David, nahitaji taraka yangu" moyo wangu ulinipasuka kupita maelezo ni kama fundi wa tanesco au kishoka anapopigwa na shoti ya umeme wa gridi ya taifa. Nilihisi sikusikia vizuri analosema. Nilimuuliza kama anajua analoongea. Akashikilia msimamo wake kwamba anataka taraka kwa kuwahanipendi tena. Niliinuka bila kumsemesha chochote nikaelekea chumbani kwangu. Mwanaume Nililia sana, niliumia moyoni, nilimpenda mke wangu mno!! Yeye ndiye aliyekuwa furaha yangu. Sasa bila sababu yoyote ya msingi anataka taraka yake. Niliangalia ni wapi nimemkosea sikuona kosa lolote! Au amepata mchepuko? Kwa kweli sikujua ni nin kimempata....nikazama ktk mawazo mazito.Nilikumbuka jinsi tulivyoonana kwa mara ya kwanza chuo kikuu cha Dar es salaam wote tukiwa wanafunzi mwaka wa kwanza, nikakumbuka jinsi mapenz yetu yalivyopitia vikwazo vingi ikiwemo wazazi wake kunikataa kabisa pale nilipoenda kumchumbia. Nikakumbuka jinsi alivyotoroka kwao na kuja kuishi na mimi ktk chumba changu kimoja huko kigogo sambusa.Nikakumbuka jinsi alivyozozana na wazazi wake mpaka akawaambia kama laana wampe tu, kwani ashakuwa kichaa juu ya kunipenda mimi. Leo hii tumeishi wote ktk shida mpaka mwenyezi Mungu ametujalia utajiri ambao tumeusotea wote. Hanitaki tena!!Sikumuelewa!Nililia mno!! Wala hakuja kunifuta machozi. Nikajua kweli amemaanisha na hanipendi tena. Nilipitiwa na usingizi.!Asubuhi niliamka na kumkuta akiwa pembeni yangu, safari hii akiwa na karatasi za kutia sahihi ya taraka. Sikumuelewa kwa kweli. Sikukubali kumpa taraka.Nilijiandaa nikaenda kazini! Kazi hazikuwa rafiki kwangu hata kidogo nilikuwa ktk mtihani mzito sanaa! Niluamua nirudi tu nyumbani nikaongee nae labda atanielewa.Nilipokelewa na ukimya usio wa kawaida. Nilimuitamke wangu lakini sikupata muitikio wowote. Nilienda chumbani moja kwa moja na kumkuta akiwa amelala huku uzuri wake ukijionesha dhahiri, nilijiambia kuwa nitajilaumu kama nikikubali kumpa taraka mke wangu mzuri aliyenivutia miaka yote kiasi hiki. Alikuwa amelala huku amekumbatia fremu kubwa yenye picha yangu. Nikahisi kuwa kumbe bado ananipenda.! Nilimshtua lakini hakuamka nilimtikisa lakini hakuonekana kushtuka. Nilimgusa ktk shingo na kumuona akiwa wa baridi mno. Sikutaka kuamini ninachokiona!Niliinua ile picha na mara ikaanguaka karatasi, ulikuwa ni ujumbe alioundika mke wangu na ulisomeka hivi.Mpendwa mme wangu David.Naandika kwa masikitiko makubwa waraka huu. Sijawahi kuona upendo wa dhati kama ulionao mume wangu. Nimekuwa nikikupenda sana ulikamilisha asilimia zote za maisha yangu. Kuwa na wewe nilijihisi ni mwanamke mwenye bahati sana ambaye amepata kuishi ktk ulimwengu huu. Hata hvyo nasikitika sana kwa kukatisha furaha hii kubwa tuliyokuwa nayo. Vituko vyote nilivyokuwa nikikufanyia ilikuwa na katika harakati za kukuwezesha kuishi bila mimi tena. Kwani nahisi ingekuwa tabu sana kwako kama ningeondoka ghafla!Ukweli ni kwamba siku ile uliponituma kusimamia mradi wetu wa kule morogoro wewe ukiwa nje ya nchi, wakati nikirudi Dar es salaam gari liliniharibikia. Kwa vike nilichelewa kuondoka Morogoro kiza kilikuwa kimeshaingia. Na kulikuwa kukitisha mno! Ghafla nilivamiwa na vijana wanne ambao mpaka sasa siamini kama walikuwa ni vibaka kwani hawakuniibia chochote. Walichofanya ni kwamba walinibaka kwa zamu na kwa vile walikuwa na mapanga sikuweza kupiga kelele kwa kuhofia kuchalazwa mapanga. Nilijihisi kutendewa unyama mkubwa!!Walivyomaliza walitokomea wakiniacha nikiwa na maumivu makali mno. Bahati nzuri niliomba msaada wa dereva wa lorry ambaye pia alikuwa naujuzi wa utengenezaj wa magari gari likatengamaa na nikarudi Dsm. Tukio lile halikukaa kufutika kichwani mwangu na kwa bahati mbaya nilivoendakupima nikakukutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi. Ndio maana kwa miezi mitano nimekuwa nikikukwepa bika ya kushirikiana na wewe.Sijaona sababu ya mimi kuendelea kuishi, sina furaha tena. Nimejiona sina thamani tena ktk ulimwengu huu. Wewe bado ni kijana siwezi kukuua na kukatisha zile ndoto zetu tulizokuwa tukizipanga pamoja.Jambo moja tu. Naomba umtunze binti yetu kama ulivokua ukiniambia kuwa utakuwa baba bora kwake basi endelea kuwa hivyo hvyo! Akiniulizia mwambie mama ametangulia kwa Mungu tutaenda kumuona huko siku ikifika.Nakupenda David!Wasaalam Maria!Nililia! nililia! Sikuamini maisha yalivyonibadilikia kwa kasi mno, niliwalaani wabakaji wote duniani! Niliwachukia mno.Mpaka leo naandika haya binti yangu ana miaka 20, akiwa mwaka wa pili chuo kikuu cha Dar es salaam akisomea shahada ya sayansi ya uhandisi. Sijawahi kifikiria suala la kuoa tena. Nimekuwa nikimlea binti yangu mwenyewe. Yeye ndio zawadi pekee ambayo mke wangu Maria ameniachia na furaha yangu iliyobaki duniani.Napenda kuwaambia ubakaji bado umeshamiri Hapa Tanzania na duniani kote. Ni vema tukajikita katika kupambana na hali hii. Wahanga bado ni wengi, muda mwingine wanawajua waliowafanyia unyama lakini kwa vile wanapokea vitisho wamekuwa kimya tu.

Friday, 8 January 2016

MATOKEO YA VYUO VYA UALIMU 2015

PROFESA NDALICHAKO ALIPA SIKU SABA BARAZA LA MITIHANI http://www.mwananchi.co.tz/habari/Profesa-Ndalichako-alipa-siku-saba--Baraza-la-Mitihani/-/1597578/3025384/-/cl4bur/-/index.html Kwa ufupi • Katibu wake mkuu ajitetea kuwa walifanya mabadiliko ya kupanga madaraja ya kidato cha nne na sita kwa maelekezo kutoka Wizara ya Elimu • 2014: Mwaka ambao Necta ilianza kutumia mfumo wa wastani wa pointi (GPA) • 47,837: Idadi ya watahiniwa binafsi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014 • 196,805:Idadi ya watahiniwa wa shule waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014


PROFESA NDALICHAKO ALIPA SIKU SABA BARAZA LA MITIHANI

 

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Profesa-Ndalichako-alipa-siku-saba--Baraza-la-Mitihani/-/1597578/3025384/-/cl4bur/-/index.html

 

Kwa ufupi

  • Katibu wake mkuu ajitetea kuwa walifanya mabadiliko ya kupanga madaraja ya kidato cha nne na sita kwa maelekezo kutoka Wizara ya Elimu
  • 2014: Mwaka ambao Necta ilianza kutumia mfumo wa wastani wa pointi (GPA)
  • 47,837: Idadi ya watahiniwa binafsi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014
  • 196,805:Idadi ya watahiniwa  wa shule waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014

 


--
Adam Kivenule
P.O. Box 3255,
Dar es Salaam
Mob. +255 713 270364
E-mail: kivenule@gmail.com / KAUKI2006@gmail.com
Blog: www.adamkivenule.blogspot.com
Twitter: www.twitter.com/kivenule