Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Thursday, 2 February 2017

NECTA CSEE 2016 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES

http://41.188.172.30/matokeo/index.htm

NECTA PSLE-2016 EXAMINATION RESULTS

http://necta.go.tz/matokeo/2016/psle/psle.htm

Website ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Tambelea hii website upate taarifa mbalimbali

http://www.moe.go.tz/index.php/sw/

TANGAZO KWA UMMA:

 NAFASI ZA KAZI KWA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA ZA SHULE (SCHOOL LABORATORY TECHNICIANS)
Serikali inatarajia kuajiri Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule Daraja la II. Ajira hii ni kwa Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule waliohitimu kati ya mwaka 2013 - 2015.
 Hivyo, wenye sifa stahiki na wanaotaka kuajiriwa Serikalini, wanatangaziwa kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya:
  • Elimu ya Sekondari (Kidato cha nne na / au Sita);
  • Taaluma ya Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule na
  • Cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya uhakiki.
Aidha, mwombaji aambatishe nakala ya wasifu binafsi (CV) ya Elimu, Taaluma na Uzoefu.  Mwombaji aainishe majina yake matatu kwa kirefu na usahihi.
Mwombaji ambaye katika vyeti vyake vya Elimu na Taaluma havina jina la tatu, akamilishe taratibu za kisheria kuongeza jina la tatu na kuwasilisha kiapo stahiki pamoja na maombi yake.
Nyaraka zote ziwasilishwe kwa barua pepe ifuatayo: apa@moe.go.tz
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na cheti cha Kidato cha IV au Kidato cha VI katika masomo ya Sayansi na waliofuzu Mafunzo ya Laboratory Technology au Laboratory Science and Technology katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na kupata Stashahada (National Technical Awards [NTA] Level VI) au Full Technician Certificate.
KAZI ZA KUFANYA
  1. Kutayarisha vitendea kazi vya maabara ya somo la Sayansi kwa vitendo.
  2. Kusaidiana na mwalimu wa somo katika kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo.
  3. Kupokea na kutunza vifaa na madawa kwa ajili ya maabara ya shule.
  4. Kubaini mahitaji ya vifaa na madawa kwa ajili ya maabara ya shule.
  5. Kufanya majaribio ya awali (Pre-Test) kabla ya majaribio (Practical) kufanyika na wanafunzi kwa mazoezi na mitihani ya ndani.
  6. Kutunza vitendea kazi na kuhakikisha usafi wa maabara kabla na baada ya mazoezi ya mitihani na majaribio ya ndani.
  7. Kusimamia usalama wa maabara na waliomo wakati wa mazoezi ya vitendo (Practicals) kwa kuhakikisha kuwepo vizimamoto (Fire Extinguisher).
  8. Kutunza vifaa vya usalama na huduma ya kwanza kwenye vyumba vya maabara.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. Mwombaji anatakiwa ‘ku-scan’ vyeti / nyaraka halisi na siyo kivuli (photocopy) na kuhifadhi katika ‘file’ moja la ‘pdf’.  ‘File’ lipewe majina matatu ya mwombaji kuanzia la kwanza, kati na la mwisho ndipo litumwe.
  2. Mwombaji atumie anuani ya barua pepe yake mwenyewe na siyo ya mtu mwingine kutuma nyaraka zake.
TANBIHI:
  1. Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 20 Februari, 2017.
  2. Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika ajira
  3. Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji zitumwe mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu.
IMETOLEWA NA
Tarishi M.K.
KATIBU MKUU
30 Januari 2017



http://www.moe.go.tz/index.php/sw/component/k2/item/652-tangazo-kwa-umma-nafasi-za-kazi-kwa-mafundi-sanifu-wa-maabara-za-shule-school-laboratory-technicians

TANGAZO KWA UMMA: NAFASI ZA KAZI KWA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA ZA SHULE (SCHOOL LABORATORY TECHNICIANS)

  NAFASI ZA KAZI KWA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA ZA SHULE (SCHOOL LABORATORY TECHNICIANS)

Serikali inatarajia kuajiri Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule Daraja la II. Ajira hii ni kwa Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule waliohitimu kati ya mwaka 2013 - 2015.
 Hivyo, wenye sifa stahiki na wanaotaka kuajiriwa Serikalini, wanatangaziwa kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya:
  • Elimu ya Sekondari (Kidato cha nne na / au Sita);
  • Taaluma ya Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule na
  • Cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya uhakiki.
Aidha, mwombaji aambatishe nakala ya wasifu binafsi (CV) ya Elimu, Taaluma na Uzoefu.  Mwombaji aainishe majina yake matatu kwa kirefu na usahihi.
Mwombaji ambaye katika vyeti vyake vya Elimu na Taaluma havina jina la tatu, akamilishe taratibu za kisheria kuongeza jina la tatu na kuwasilisha kiapo stahiki pamoja na maombi yake.
Nyaraka zote ziwasilishwe kwa barua pepe ifuatayo: apa@moe.go.tz
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na cheti cha Kidato cha IV au Kidato cha VI katika masomo ya Sayansi na waliofuzu Mafunzo ya Laboratory Technology au Laboratory Science and Technology katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na kupata Stashahada (National Technical Awards [NTA] Level VI) au Full Technician Certificate.
KAZI ZA KUFANYA
  1. Kutayarisha vitendea kazi vya maabara ya somo la Sayansi kwa vitendo.
  2. Kusaidiana na mwalimu wa somo katika kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo.
  3. Kupokea na kutunza vifaa na madawa kwa ajili ya maabara ya shule.
  4. Kubaini mahitaji ya vifaa na madawa kwa ajili ya maabara ya shule.
  5. Kufanya majaribio ya awali (Pre-Test) kabla ya majaribio (Practical) kufanyika na wanafunzi kwa mazoezi na mitihani ya ndani.
  6. Kutunza vitendea kazi na kuhakikisha usafi wa maabara kabla na baada ya mazoezi ya mitihani na majaribio ya ndani.
  7. Kusimamia usalama wa maabara na waliomo wakati wa mazoezi ya vitendo (Practicals) kwa kuhakikisha kuwepo vizimamoto (Fire Extinguisher).
  8. Kutunza vifaa vya usalama na huduma ya kwanza kwenye vyumba vya maabara.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. Mwombaji anatakiwa ‘ku-scan’ vyeti / nyaraka halisi na siyo kivuli (photocopy) na kuhifadhi katika ‘file’ moja la ‘pdf’.  ‘File’ lipewe majina matatu ya mwombaji kuanzia la kwanza, kati na la mwisho ndipo litumwe.
  2. Mwombaji atumie anuani ya barua pepe yake mwenyewe na siyo ya mtu mwingine kutuma nyaraka zake.
TANBIHI:
  1. Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 20 Februari, 2017.
  2. Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika ajira
  3. Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji zitumwe mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu.
IMETOLEWA NA
Tarishi M.K.
KATIBU MKUU
30 Januari 2017

NECTA RESULTS

http://matokeoyamitihani.blogspot.com/p/blog-page_849.html

Friday, 20 January 2017

Historia ya chimbuko, mila na desturi za kabila la WAIRAQW


Utangulizi


Wairaqw ni miongoni mwa rnakabila yanayoishi katika Mkoa wa Manyara Wilaya za Mbulu, Babati, Hanang na Mkoa wa Arusha Wiiaya ya Karatu.


 
Asili ya kabila la WAIRAQW

Kwa asili Wairaqw walitokea Mesopotamia Iraq. Uhamiaji wao ulianza katika karne ya 4 - 6 baada ya kuzaliwa kwa Kristo. Wairaqw ni jamii ya Wakushi ambao Walivuka bahari ya Sham kwa mashua na kutua Ethiopia, waliishi hapo kwa muda kutokana na vita vya mara kwa mara, waiiendelea kuhama kuelekea kusini magharibi waiipitia bonde la ufa kando ya ziwa Victoria. Katika kuhama hama huko na kukaa mahali kwa muda vita vikaanza wakakimbilia na waiiendelea hivyo hivyo kupitia njia ya kati kupitia Singida Iramba hadi mpakani mwa Dodoma na Iringa. Kwa upande wa kusini kuiikuwa na mapambano ya Wahehe, Wangoni na Wazimba wakarejea kuelekea kaskazini hadi sehemu ya Kondoa mahali panapoitwa Guser Tuwalay. Waliishi hapo wakiwa wafugaji na kilimo kidogo. Ndipo walipoanza mapambano kati yao na Wabarbaig. Waliposhindwa vita walikirnbilia karibu na mlima Hanang. Wakagawanyika wengine wakaelekea,Gallapo (Tsea Daaw). Hawa waliitwa Wagorowa na Wairaqw walipandisha mlima Dabil hadi Guser, Gangaru ambapo walifanya maskani.

 
Mji wa Babati
Baada ya muda Kiongozi wao aiiyeitwa Haymu Now wa ukoo wa Haytipe aliwaongoza hadi Nou na walifanya rnaskani yao katika maeneo ya Mama Isara. Aidha inasemakana kuwa eneo lote la Mama Isara lilikuwa ni ziwa wakati ule, hivyo Haymu na watu wake walifanya maskani katika maeneo ya milima.

 
Kiongozi huyo alikuwa na mtumishi wake aiiyeitwa MOYA. Hi kuongeza maeneo ya kilimo kiongozi huyo alitumia uganga wake kuhamisha ziwa katika eneo la Mama Isara kwa kumwagiza mtumishi wake kurusha mshale katikati ya ziwa hilo. mtumishi alipofanya hivyo ziwa lilihama pamoja naye hadi katika bonde la ufa ambalo linajulikana kwa jina la ziwa manyara kwa sasa na Kiiraqw hujulikana kama "Tlawta Moya".

 
Baada ya ziwa kuhama kiongozi huyo aliendelea kuishi hapo na watu wake na kuendelea kutawanyika katika maeneo ya Muray, Kuta, Amoa, Kainam, Suum, Datlaa, Tsaayo Wilaya ya Mbulu.

 

Baadaye Wairaqw wakatawanyika taratibu sehemu za Karatu, Babati na Hanang kama makao makuu yao mpaka leo. Baadhi ya miia na desturi za Wairaqw zinafanana na za Wayahudi kama matumizi ya kondoo katika jamii.

Chakula cha asili cha WAIRAQW

Chakula chao kikuu kilikuwa nyama ya wanyamapori na ya mifugo waliyofuga. Walichuna nyama kwa kutumia mawe yenye ncha kali mithili ya kisu. Mapishi yao yalitokana na moto unaopatikana kwa njia ya kupekecha mti hadi moto unatokea, chombo hicho kiliitwa (Bui na Daha). Baadaye waligundua mazao aina ya mtama, ulezi, uwele na mboga yao ilikuwa kunde.

 
Nafaka hiyo ilisagwa kwa kutumia jiwe la mkono na unga uliopatikana ulitumika kupikia ugali mlaini (Xwante) unaofanana na uji uliopoa. Nafaka hiyo pia hutumika kutengenezea pombe ya asili ambayo ilinyweka kama viburudisho wakati wa sherehe mbalimbali za kimila.

 
Michezo ya asili

Wairaqw walikuwa na ngoma aina mbili:-

1. Ngoma ya ndani yaani ya harusi. Ngoma hii huchezwa siku mtoto wa

kike anapoolewa au wa kiume anapooa.

2. ngoma ya nje ya mwaka wakati wa mavuno huitwa "Gilo". Ngoma hii huchezwa wakati wa mavuno kama ishara ya furaha na shukrani kwa Mungu.

 

Nyimbo ya "Mudeli" huimbwa wakati wa harusi kwa kumpongeza bwana harusi na bibi harusi, na nyimbo hizp huimbwa na akina mama. Wakati wa kuweka sherehe ya shukrani kwa mwaka, Wairaqw wana utaratibu wa maombi

yaani inaitwa "slufay" pamoja na "Giriyda". Giriyda hi nyimbo maalum ya kuomba mambo rnazuri na kuepusha mambo mabaya.

 

Nyimbo maarufu kwa akina mama inaitwa "sibeli" ni nyimbo ya shukrani kwa

Mungu.

 
Mavazi

Mavazi ya asili ya Wairaqw ni ngozi. Ngozi hizo zililainishwa vizuri na kushonwa mithili ya shuka, sketi au kanga. Vazi la kiume lilikuwa moja ambalo lilifunikwa kama shuka. Vazi la kike lilikuwa sketi na shuka ndogo iliyofanana na kanga. Pia wanaume na wanawake walivaa viatu vilivyotengenezwa na ngozi.

 
Uchumi wa jadi ya WAIRAQW

Uchurni wa jadi wa Wairaqw ulikuwa ufugaji, kilimo, na utengenezaji wa zana mbalimbali za kilimo na ulinzi. Hapakuwa na biashara ya fedha taslimu ila ilikuwa kubadilishana mali au mifugo kwa vifaa au zana.
Moja ya barabara katika Mkoa wa Manyara
 
Ziwa Manyara

 
Zana za kilimo

Majembe ya asili yalitengenezwa kwa kutumia miti iliyochongwa kama mithili ya jembe. Majembe hayo yalitumika kulimia na kushindilia udongo juu ya nyumba ya Tembe. Jembe hilo liliitwa "Taqhwani", pia kwa ajili ya kutindua shamba jipya walitumia chimbuo lililotengenezwa na miti migumu na ilichongwa upande mmoja mithili ya chimbuo. Jembe hilo liliitwa 'Dughsay". Baadaye waligundua zana zilizotengenezwa kwa udongo wa mfmyanzi uliotoka Mbugwe. Zana hizo zilitumika hadi majembe ya mkono yalipopatikana kutoka kwa wataalam wa nje.

 
Zana za vita na uwindaji

Mikuki na mishale ya asili ilitengenezwa na miti iliyochongwa mfano wa mkuki wa chuma unaotumika sasa. Pia walitumia mawe yenye ncha kali na baadaye waligundua zana zinazotengenezwa kwa kuturnia udongo wa mfinyanzi ambazo zilikaushwa kwa moto mkali kama tofali.

 
Hifadhi ya nafaka

Walipovuna walikuwa na utaratibu wa kuweka mazao yao kwenye ghala zao za asili (kuntay) zilizotengenezwa kwa vinyesi vya ng'ombe. Pia aina ya majani ya miti ya asili na majivu ya vinyesi vya ng'ombe vilitumika katika kuhifadhi nafaka kutokana na kushambuliwa na wadudu. Majivu ya majani hayo yalichanganywa na nafaka mithili ya dawa zinazotumika sasa.

 
Utawala/uongozi

Walikuwa na uongozi toka ngazi ya familia, ukoo, jamii ya kabila zima la Wairaqw

waliotawaliwa na Kahamusmo ambaye ni kiongozi mkuu wao. Kiongozi msaidizi anaitwa Yaabusmo. Kila mmoja anafanya kazi kwa nafasi yake. Kwa ujumla ni kabila linalopenda kushirikiana katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa; "Walikuwa na waganga wa kiasili waliojulikana kwa majina kwa jamii nzima.

 
Malezi ya mtoto wa kike na kiume wa KIIRAQW

Mtoto wa kike na wa kiume wa Kiiraqw anapozaliwa na kukua hufundishwa maadili mema ya kuishi na jamii. Mtoto wa kike hufundishwa na akina mama maadili mema ya kuishi na nume na namna ya kutunza familia anapoolewa na kuzaa. Mtoto wa kiume hufundishwa na akina baba maadili ya kuishi na jamii, mbinu za kujitegemea katika kutunza familia anapokuwa ameoa.

 
Elimu

Wairaqw wa asili hawakupenda kuwasomesha watoto wao wakidai kuwa wakipata elimu watapotoka au mila zao zingepotea. Pia waliwazuja watoto kwenda shule kwa ajili ya kufanya kazi za nyumbani kama vile kucunga mifugo hasa kwa watoto wa kiume. Kwa watoto wa kike waliwazuia kwenda shule ili waolewe na wapate mali (mahari).

 
Mahakama ya jadi za WAIRAQW

Adhabu zilitolewa kwa taratibu za mila kwa kuzingatia kosa alilotenda mhalifu. Masuala ya makosa yote yaliyotoka katika jamii hujadiliwa na wazee wa jinsia tofauti yaani wanaume na wanawake na kutolewa uamuzi. Pia fursa Hitolewa kwa masuala yaliyohusu kesi ya jinsia moja kujadiiiwa na wazee wa jinsia hiyo kwanza ili hatimaye adhabu itolewe na jamii nzima.

 
Watuhumiwa waliopatikana na makosa yaliyothibitika walitozwa faini ya kimila iliyoitwa "Dohho" au waliagizwa kulipa fidia kwa mlalamikaji. Watuhumiwa waliokana mashtaka hata kama kuna ushahidi walipewa adhabu ya kutengea na jamii nzima. Pia kwa kesi ambazo hazina ushahidi mlalamikaji na mlalamikiwa waliapishwa kwa yote aliyoeleza ni sahihi na laana ilitolewa kwa aliyesema uongo fotauti na hali halisi.

 
Tiba za asili

Wairaqw walitumia mizizi na majani ya miti kama tiba ya magonjwa mbalimbali. Mizizi hiyo ilichemshwa au kusagwa na kuchanganywa na maji na kupewa wagonjwa.

Ijue Historia Na Chimbuko La Wahehe na Vita na Wajerumani


MAANDIKO kadhaa yamekuwepo kuhusiana na historia ya Wahehe na hasa ukoo wa Mtwa Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga, maarufu kama Mkwawa, lakini yote hayo hayakunizuia kuisaka historia hiyo.

‘Jicho halishibi kuona na Sikio halikinai kusikia!’ hivyo nikaamua kufunga safari hadi Lungemba, yaliko makaburi ya Mtwa Munyigumba na ndugu wengine wa ukoo huo, yapata kilometa 62 kutoka Iringa Mjini.

Wapo walioandika kwamba chimbuko la Mtwa Mkwawa ni Ungazija, lakini simulizi ninazokutana nazo hapa ni tofauti, maana zinatoka katika vinywa vya wanaukoo wa Muyinga, ambao nao wameipata ama kurithishwa kutoka kizazi na kizazi kutokana na simulizi za mababu zao.

Wale waliopata kuandika kwamba asili ya akina Mkwawa ni Ungazija wanaeleza kuwa mtawala wa Ngazija aliyeitwa Yusuf Hassan ambaye alikuwa Mwarabu, alizaa watoto wawili wa kiume, Hassan ‘Mbunsungulu’ na Ahmad. Wanasema kwamba Mufwimi alikuwa mmoja wa watoto watatu wa Mbunsungulu aliozaa na mwanamke wa Kikaguru. Ndugu zake wengine walikuwa Ngulusavangi na Ngwila, kwa maelezo yaliyo kwenye baadhi ya maandishi ambayo inatoweka kutokana na Watanzania kukosa utamaduni wa kutembea, kujifunza na kudadisi.

Rungemba ni kijiji ambacho hakijasikika sana katika historia kama lilivyo jina la Mkwawa, lakini hapa ndipo kwa kiasi kikubwa lilipo chimbuko la Chifu huyo wa kabila la Wahehe na ndipo lilipo kaburi la Mtwa Munyigumba.

Ignas Pangiligosi Muyinga, maarufu kama Malugila Mwamuyinga (61), ambaye ni kitukuu wa Msengele Kilekamagana, anaona fahari kuisimulia historia ya ukoo huo maarufu.

“Shina la ukoo wetu linaanzia kwa mtu aliyeitwa Mufwimi (yaani Mwindaji), ambaye mababu zetu walitusimulia kwamba alitokea Ethiopia,” Malugala anaanza kueleza. “Mufwimi alipita akiwinda kutoka Ethiopia, Kenya kabla ya kuingia Tanganyika na kujikuta yupo Usagara na hatimaye eneo la Nguluhe-Dabaga akipitia Ikombagulu, himaya ya Chifu Mwamududa. Wengi walimfananisha na mtu wa kabila la Wakamba kutoka Kenya kutokana na umbile lake kubwa.”

Wakati huo eneo ambalo sasa linaitwa Iringa lilikuwa na makabila mbalimbali. Walikuwepo ‘Wahafiwa’ katika Bonde la Milima Welu, Luvango, Wutinde, Lugulu, Makongati, Kalenga, Kipagala, Kihesa, Tambalang’ombe, Ibanagosi, Tipingi, Ikolofya, Nyambila, Kibebe na Isanzala.

‘Vanyategeta’ wao walioishi Udzungwa, Kitelewasi na Lundamatwe, ambao walikuwa wahunzi hodari. ‘Vanyakilwa’ walilowea Mufindi wakitokea Kilwa; ‘Vasavila’ waliishi milima ya Welu huko Makungu (Kihanga ya sasa),Magubike na Malangali; na ‘Vadongwe’ waliishi kando ya milima ya Uhambingeto, Ipogolo, Nyabula na Luhota.



HADI wakati huo, tayari von Heydebreck – mmoja wa manusura katika vita hivyo – alikuwa amekwishajeruhiwa na kuanguka akiwa amepoteza fahamu, lakini baadaye aliandika kwenye ripoti yake: “…Mfululizo wa matukio hadi wakati huu ulikuwa umetumia dakika mbili au tatu tu. Nilitambua hilo kabla ya kujeruhiwa, Wasudani tayari walikuwa wamekimbia kurudi nyuma vichakani baada ya kufyatua risasi mara mbili hivi. Mimi na askari wa Kikosi cha Tano tulilazimika kujilinda na kujitetea baada ya kuona Wahehe wakija katika umbali wa hatua 30. Kama sikosei, nilimsikia Sajini Tiedemann akisema alikuwa ameumia kabla hajafyatua risasi. Haikuwa rahisi kuona zaidi ya umbali wa hatua tano msituni kutoka pale njiani. Pia hakuna ambaye aliweza kunusurika kwa sababu Wahehe walikuja kwa kasi… Ni wazi walipanga kutushambulia baada ya kufika katikati msitu. Kuvurugika kwa mipango yao kulichangiwa hasa na kitendo cha Luteni von Zitewitz kufyatua risasi…”

Muanzilishi wa Himaya ya Ujerumani Afrika Mashariki, Carl Peters, baadaye Novemba 23, 1891 alimwandikia Gavana von Soden akisema kwamba, katika mapambano mengine na makabila mbalimbali ya Tanganyika, ilikuwa ni bahati tu kwao kutoweza kupata madhara kama waliyopata Wajerumani pale Lugalo, kwani mafunzo yao ya vita yalikuwa yanalenga zaidi kupigana wakiwa wamejipanga pamoja kwa mbinu maalum. Hawakuwa wamejifunza kupigana kila mtu kwa uwezo wake, bali walitegemea zaidi kushambulia kwa pamoja.

Iliwachukua Wahehe dakika 15 tu (kuanzia saa 1:15 hadi 1:30 asubuhi) kuwafyeka Wajerumani na majeshi yao. Von Zelewiski aliuawa kwa kupigwa nyundo kichwani akiwa amepanda punda wake wakati akijiandaa kuwafyatulia risasi wapiganaji wa Mkwawa. Kabla hajadondoka akachomwa mkuki ubavuni.

Hii ndiyo asili hasa ya jina la ‘Nyundo’ kutokana na kamanda huyo wa Wajerumani kuuawa kwa nyundo!

Kuhusiana na kifo cha Kamanda von Zelewiski, kama Mjerumani Tom von Prince alivyoandika baadaye, “Kama nilivyosimuliwa baadaye… na Wahehe walioshuhudia, alijitetea mwenyewe kwa kutumia bastola yake kubwa na kuwapiga risasi watu watatu, wakati kijana mmoja wa Kkihehe alipomchoma na mkuki ubavuni. Kijana huyo alikuwa na umri wa miaka 16 tu na alizawadiwa ng’ombe watatu na Mkwawa kwa kitendo hicho.”

Luteni von Pirch na Dk. Buschow pia waliuawa wakiwa juu wa punda wao ambapo majeraha yao yalikuwa makubwa mno. Karibu askari wote wa Kikosi cha 7, Kikosi cha Silaha, Kikosi cha 5 na baadhi ya askari wa Kikosi cha 6 waliuawa kabla hata hawajajua wafanye nini.

Luteni von Heydebreck, Luteni Usu Wutzer na Murgan Effendi pamoja na askari 20 hivi ndio waliofanikiwa kukimbia kutoka eneo hilo la mapigano na kukimbilia upande mwingine wa mlima na kuweka ngome wakijilinda dhidi ya mashambulizi ya Wahehe. Wapiganaji hao wa wajerumani walijificha kwenye pagala moja la tembe lililokuwa limetelekezwa mlimani. Askari mmoja Msudani ndiye aliyekiona kibanda hicho.
Lakini von Heydebreck aliishuhudia vita hiyo katika kipindi cha dakika mbili au tatu tu kabla ya kupoteza fahamu. “Kulingana na ushuhuda wa Wahehe walioshiriki mapigano yale, vita hivyo havikumalizika mapema kama ambavyo Wazungu wa mstari wa nyuma walivyotegemea, badala yake askari walionusurika waliendelea kupambana hadi saa 4:30 asubuhi na kuwaua maadui wengi (Wahehe).”

Askari wa mwisho wa kikosi cha Luteni von Tettenborn ndio hawakupata madhara makubwa ya mashambulizi ya Wahehe, washukuru kutokana na makosa ya ishara, vinginevyo wote wangeangamia katika kipindi hicho cha dakika 15 tu. Von Tettenborn, Feldwebel Kay na askari kama 20 hivi Wasudani wakahamia upande wa kushoto wa eneo la mapigano na kutengeneza nusu duara kwa ajili ya mashambulizi huku wakiwa wameumia. Wakiwa hapo walipandisha bendera ya Ujerumani juu ya mti na kupiga mbinja ili kuwaita manusura wengine.

Wakati huo Wahehe waliendelea kuwakimbiza manusura na kushambulia kila waliyemuona mbele yao. Mkanganyiko ukaongezeka baada ya kuwasha nyasi.

Mnamo saa 2:30 asubuhi hiyo, Luteni von Heydebreck, Luteni Usu Wutzer na Murgan Effendi wakiwa na askari wao 12 walipenya na kuungana na kikosi cha von Tettenborn. Von Heydebreck alikuwa anavuja sana damu kutokana na majeraha mawili makubwa ya mikuki. Kwa kuwatazama tu watu hao, von Tettenborn akatambua kwamba vikosi vyao vyote vilikuwa vimesambaratishwa na kikosi cha silaha kutekwa, ambapo Mkwawa aliteka bunduki 300. Askari wa jeshi la Wajerumani waliouawa siku hiyo walikuwa zaidi ya 500.

Ilipofika saa 3:00 Luteni Usu Thiedemann, akiwa na majeraha makubwa ya moto aliingizwa kwenye kikosi cha Luteni von Tettenborn akiwa amebebwa na askari waliokuwa wanafanya doria. Nyasi zilizokuwa zinaungua sasa zilimtisha von Tettenborn na manusura wengine.

Hadi kufikia saa 10:00 jioni Luteni von Tettenborn alikuwa amewakusanya majeruhi wengi na kuokota baadhi ya mizigo yao. Wahehe waliokuwa wamepagawa kwa hasira pamoja na moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuteketeza msitu viliifanya kazi ya kuwatafuta majeruhi wengine kuwa ngumu, hivyo wengi waliteketea kwa moto. Von Tettenborn akaamua kuanza kurudi nyuma kabla hajazuiwa na Wahehe.

Wakati wa usiku wa manane kikosi kilichokuwa na Luteni von Tettenborn kikapiga kambi ng’ambo ya pili ya mto tofauti na mahali walipolala kabla ya kuanza mapambano. Kikosi chake sasa kilikuwa na yeye mwenyewe na Luteni von Heydebreck, ma-NCO watatu wa Kijerumani (ingawa Luteni Usu Thiedemann alikufa baadaye njiani), maofisa wawili wa Kiafrika, ma-NCO 62 wa Kiafrika, wapagazi 74 na punda 7. Kutoka hapo wakaanza kutembea hasa nyakati za usiku kurudi nyuma ambapo walifika Myombo Agosti 29.

BAADA ya ushindi wa Lugalo, Chifu Mkwawa hakutulia, bali aliendelea kuimarisha himaya yake pamoja na jeshi lake. Lakini pia kipindi hicho Wajerumani nao walikuwa wakipanga mikakati ya namna ya kuisambaratisha himaya hiyo.

Kitendo cha kupigwa kwa jeshi lao imara lenye silaha kali, tena na wapiganaji wenye mikuki na mishale tu, kiliichanganya Berlin kwa sababu hakikuwahi kutokea hapo kabla. Hivyo Gavana Julius Freiherr von Soden aliyekuwa anaongoza koloni hilo la Afrika Mashariki alikuwa katika presha kubwa kutoka kwa wakubwa wake kuhusiana na namna atakavyomshinda Mkwawa.

Gavana huyo alijitahidi kukabiliana na presha ya Wahehe waliokuwa wakkivamia misafara yake hadi miaka miwili baadaye alipoondoka nchini. Wajerumani walikuwa na mbinu ya kuidhoofisha himaya ya Wahehe kwa mazungumzo, siyo kwa vita, kwa sababu walitambua kwamba hiyo ingeweza kuwagharimu tena.

Historia inaeleza kwamba, uamuzi wa Von Soden wa kutotumia jeshi kupambana na Mkwawa ulimfanya aonekane gavana bomu kati ya magavana wote walioongoza koloni hilo, lakini hiyo ilitokana na historia yake. Yeye ndiye alikuwa gavana pekee aliyetokea uraiani, kwani aliyemtangulia von Wissmann na wafuasi wake wa baadaye walikuwa makamanda wa jeshi.

Katika kipindi hicho cha Von Soden, Mkwawa naye alifanya majaribio kadhaa ya mazungumzo na Wajerumani akituma ujumbe wake Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalichukua muda wa miezi kadhaa kupitia kwa wawakilishi wake, lakini hayakuwa na mafanikio kwa sababu watawala wa Kijerumani walikuwa na mashaka na msimamo wa Mtawala huyo wa Wahehe kwamba angeweza kuwabadilikia. Kwa kifupi, hawakumwamini.

Pamoja na Von Soden kuwa na nia njema ya kufanya mapatano, maofisa wengine wa Kijerumani walikuwa na mawazo kwamba hakukuwa na haja yoyote ya kufanya mazungumzo na mtawala wa Kiafrika ambaye alikuwa ameidhalilisha Ujerumani kama alivyofanya Mkwawa.

Luteni Tom von Prince (baadaye Kapteni baada ya kuiangusha Kalenga) aliwahi kusema: “Tangu kuangushwa kwa kikosi cha Zelewski, hasa nikiwa askari wa jeshi lile la zamani, haja yangu kubwa ilikuwa kulipa kisasi kwa kudhalilishwa kwa jeshi letu, na tangu hapo nikaweka mkakati, sikuhitaji kuingia kwenye vita yoyote, sikufanya chochote ambacho kingeweza kuingilia kati mpango huu.”

Wajerumani wakati huo walikuwa na mashaka kwamba watawala wa Kiafrika, hususan Mkwawa walikuwa wameanza kuonyesha upinzani wa wazi, hasa Mtemi Isike wa Tabora na Mbunga wa Ungoni ambao himaya zao zilipakana na Uhehe. Chifu mmoja wa Usagara aliwahi kutamka wazi, “Watu hawa (Wahehe) ndio pekee walioweza kuoga mchanga wa damu ya Mzungu ambao ‘bomba zao za moto’ ziliwafanya wengi washindwe kujitetea. Na kweli, vijiji vingi vilivyokuwa jirani na boma la Wajerumani viliendelea kutoa msaada kwa Mkwawa na Himaya yote ya Uhehe mpaka pale Kalenga ilipoangushwa.

Sababu za Mkwawa kutochukua uamuzi wa kuwafukuzia Wajerumani baada ya vita vya Lugalo zinatajwa kuwa nyingi, ingawa kubwa zaidi, kwa mujibu wa waandishi wa zamani wa historia Erick Mann, Alison Redmayne, na wengineo, ilikuwa ni kupoteza askari wake wengi. Vikosi vya Mkwawa havikuwahi kuvamia eneo lililokuwa likikaliwa na Wajerumani. Katika vita vya Lugalo, Mkwawa alipompoteza makamu kiongozi wa Kalenga, Ngosi Ngosi Mwamugumba.

 

Historia ya Mkwawa (Mkwavinyika)


Wahehe mnamo 1906

Mkwawa au kwa jina refu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (185519 Julai 18981) alikuwa chifu na kiongozi mkuu wa kabila la Wahehe katika Tanzania ya leo wakati wa upanuzi wa ukoloni wa Ujerumani mwishoni mwa karne ya 19.

Mkwawa ni maarufu hasa kwa kuongoza vita vya Wahehe dhidi ya Wajerumani.

Upanuzi wa Wahehe

Jina la Mkwawa ni kifupisho cha Mukwava ambalo tena ni kifupisho cha Mukwavinyika, lililokuwa jina lake la heshima likimaanisha "kiongozi aliyetwaa nchi nyingi".

Mkwawa alizaliwa mnamo mwaka 1855 mahali palipoitwa Luhota karibu na Iringa mjini. Alikuwa mtoto wa chifu Munyigumba aliyeaga dunia mwaka 1879.

Babake Munyingumba aliwahi kuunganisha temi ndogo za Wahehe na makabila ya majirani kuwa dola moja. Aliiga mfumo wa kijeshi wa Wasangu waliowahi kuwa kabila lenye nguvu kwa kujifunza mfumo huu kutoka kwa Wangoni na impi za Shaka Zulu.

Hadi miaka ya 1870 eneo la Wahehe lilipanuliwa mbali kuanzia kusini hadi katikati ya Tanzania ya leo.

Baada ya kifo cha chifu mzee watoto wake walishindania urithi wake, na Mkwawa alishinda akawa kiongozi mpya.

Aliendelea kupanua utawala wake. Hadi mwisho wa miaka ya 1880 alitawala sehemu muhimu za njia ya misafara kati ya pwani na Ziwa Tanganyika. Misafara hiyo ambayo ilikuwa ikibeba bidhaa za nje kama vitambaa, visu na silaha kutoka pwani, ikirudi na watumwa na pembe za ndovu, ilipaswa kumlipia hongo ikanunua pia wafungwa wa vita vyake. Hapo athiri na uwezo wake wa kulipa jeshi kubwa ikaongezeka.

Mkwawa na upanuzi wa Wajerumani

Tangu mwaka 1885 hivi Wajerumani walianza kuunda koloni lao katika afrika ya Mashariki ya Kijerumani (Tanganyika pamoja na Rwanda na Burundi) za leo).

Mwaka 1888/1889 utawala wao ulitikiswa na vita ya Abushiri lakini baada ya kushinda upinzani wa Waafrika wa pwani Wajerumani walilenga kuimarisha utawala wao juu ya sehemu za bara.

Mkwawa aliwahi kusikia mapema habari za Wajerumani akajaribu kuwasiliana nao lakini bila kuelewana. Hapo aliamua kujenga boma imara lenye kuta za mawe kwenye makao makuu yake huko Kalenga karibu na Iringa.

Katika mwezi Februari 1891 alituma wajumbe kwa kambi la Wajerumani huko Mpwawa wakapokewa na gavana Mjerumani. Wakati huohuo Mkwawa aliendelea kutuma askari zake hadi Usagara iliyotazamwa na Wajerumani kama eneo lao. [1]

Katika kipindi hicho gavana mpya Julius von Soden alifika Dar es Salaam. Hakuwa na mamlaka juu ya mkuu mpya wa jeshi Emil von Zelewski aliyepokea amri zake kutoka Berlin moja kwa moja. Baada ya kusikia habari za mashambulio ya Mkwawa katika Usangara aliomba na kupata kibali cha "kuwaadhibu Wahehe".

Mapigano ya Lugalo

Katika mwezi Julai 1891 von Zelewski aliongoza kikosi cha maafisa Wajerumani 13 na askari Waafrika hasa kutoka Sudan 320, pamoja na wapagazi 113. Walikuwa na bunduki za kisasa, bunduki za mtombo na mizinga midogo. Zelewski aliwadharau Wahehe kama washenzi ambao walikuwa na mikuki na pinde tu. Kwa hiyo hakuona haja ya kutuma wapelelezi wa awali.

Njiani aliangamiza vijiji alivyokuta na katika mwezi Agosti alipoona Wahehe 3 waliomkaribia aliagiza kuwaua bila kuongea nao. Kumbe walikuwa mabalozi wa Mkwawa aliyetaka kujadiliana na Wajerumani.
Emil von Zelewski, kiongozi Mjerumani wa Lugalo
 

Tarehe 17 Agosti 1891 Zelewski na jeshi lake walipita kwenye manyasi marefu karibu na Lugalo. Mkwawa alikuwa alimsubiri na Wahehe 3,000 walionyamaza hadi Wajerumani waliotembea kwa umbo la safu ndefu walipokuwa karibu kabisa wakawashambulia.

Wajerumani walikosa muda wa kuandaa silaha zao wakashtushwa kabisa. Sehemu kubwa ya askari waliuawa katika muda wa dakika chache pamoja na jemadari von Zelewski. Sehemu ya kombania ya nyuma ilirudi nyuma na kusimama kwenye kilima kidogo walipoweza kutumia bunduki la mtombo wakajitetea na kuua Wahehe wengi. Sehemu hii ilijumlisha maafisa 2 na maafande 2 Wajerumani waliweza kukimbia na kujiokoa pamoja na askari 62 na wapagazi 74.

Kipindi cha vita

Baada ya mapigano Mkwawa alihesabu wafu wake waliokuwa wengi. Alikataza mila za kilio kwa sababu alitaka kuficha idadi ya askari waliokufa. Akielewa sasa kwamba silaha za Wazungu zilikuwa hatari alituma tena mabalozi kwa gavana von Soden walioeleza ya kwamba Wahehe walikuwa walijihami tu dhidi ya shambulio na walitaka amani.

Lakini madai ya Wajerumani yalikuwa magumu, eti kuwaruhusu wafanyabiashara kupita bila matata na kutoshambulia majirani tena.

Mkwawa hakuwa tayari kuahidi yote akachelewesha mikutano. Wakati huo kamanda mpya Mjerumani Tom von Prince alijenga boma jipya la Wajerumani katika Uhehe na Mkwawa alijibu kwa kusambulia vikosi vidogo vya jeshi la kikoloni. Gavana Soden alidai kutoendelea na mapigano. [2], lakini mwaka 1893 aliondoka Afrika, na gavana mpya von Schele alitaka kulipiza kisasi akaamuru mashambulio dhidi ya Mkwawa.

Anguko la Kalenga

Mwezi Oktoba 1894 von Schele aliongoza kikosi cha maafisa Wajerumani 33 na askari Waafrika pamoja na wagajai zaidi ya 1000 kuelekea Kalenga. Walikuwa na mizinga 4 na bunduki bombomu.

Walipofika mbele ya Kalenga Wahehe walijisikia salama kutokana na kuta imara lakini Wajerumani walijipanga kilomita kadhaa nje ya mji wakaanza kufyatulia mizinga yao na kuua watu ndani ya mji.

Wakati wa giza kwenye asubuhi wa tarehre 30 Oktoba 1894 askari wa jeshi la Schutztruppe walipanda ukuta katika sehemu uliyodhoofishwa tayari na kuingia mjini. Hadi jioni walikuwa wameteka mji wote.

Gombora na mikuki ya Wahehe hazikuweza kushindana na bombomu za Wajerumani. Mkwawa mwenyewe aliamua kukimbia pamoja na askari 2000 - 3000, lakini kabla ya kukimbia alimwua mganga mzee aliyewahi kutabiri ya kwamba atawashinda Wajerumani waliokuja.

Gavana von Schele aliandika taarifa kwa serikali ya Ujerumani "tulizika maadui 250, wengine walichomwa katika nyumba zao, wanawake na watoto 1500 kutekwa nyara" [3].

Mkwawa alijificha msituni pamoja na askari zake akasubiri. Gavana von Schele alishindwa kuendelea na mashambulio kwa sababu gharama za vita zilishinda makisio yake na wabunge wa upinzani katika Reichstag huko Berlin walipinga vita vya kikoloni; walikataa kuongeza makisio na kiongozi wa wasoshalisti Agosti Bebel aliita mtindo wa kuchoma mji na kuteka nyara watoto na wanawake "ushenzi mkuu".

Amani fupi

Baada ya kuondoka kwa Wajerumani, Mkwawa aliweza kurudi na kujenga tena nyumba mahali pa Kalenga.

Mnamo Septemba 1895 Mkwawa alikuwa tayari kujadiliana na Wajerumani na tarehe 12 Oktoba walipatana amani. Wajerumani walimkubali Mkwawa kama chifu wa Wahehe, Wahehe waliahidi kukabidhi gobori zote, kupandisha bendera ya Ujerumani na kuwaruhusu wafanyabiashara na wasafiri kupitia Uhehe. Mkwawa alimwagiza mjomba wake kutia sahihi akakataa mwenyewe akisema hii ingemwua.

Hata hivyo miezi kadhaa baadaye alitafuta msaada wa Wajerumani kwa shambulio dhidi ya Wabena.

Afisa mmoja Mjerumani aliyefika Kalenga mpya alizuiliwa kuingia na kumwona chifu akaambiwa alipe hongo ya bunduki 5 ili kuingia katika eneo la Mkwawa. Hapo maafisa wa jeshi la Wajerumani waliolinda mpaka, ambao bado walikuwa wakitafuta nafasi ya kulipiza kisasi cha Lugalo, walidai kuwa chifu amevunja mkataba.

Kapteni Tom von Prince alijenga boma jipya karibu na Kalenga alianza kuwasiliana na machifu wadogo wa Wahehe. Mkwawa alijaribu kujenga mapatano na majirani lakini Wabena na makabila mengine walikumbuka vita na mashambulio ya awali kutoka Uhehe walipendelea kushikamana na Wajerumani.

Mkwawa aliwaua machifu wawili Wahehe waliowahi kukaa na von Prince, lakini aliona hawakuwa peke yao kusita kumtii tena. Alipata habari ya kwamba hata mdogo wake Mpangile alishikamana na Wajerumani.

Wakati wa Septemba 1896 Wahehe waligawanyika na sehemu kubwa ya viongozi waliochoka vita ilikuwa tayari kuwakubali Wajerumani.[4]. Wajerumani waligawa eneo lao. Wasangu walirudishwa katika eneo lao la awali wakarudi kutoka Usafwa katika mji mkuu wa Utengule Usangu. Mpangile alisimikwa kama kiongozi mpya wa Uhehe penyewe, lakini baaa ya siku 50 alisimamishwa na kuuwa na Wajerumani waliomshtaki, eti anamsaidia kaka yake kisiri.

Katika maficho na kifo

Mkwawa alikuwa ameondoka sehemu za Iringa mwezi Agosti 1896 alipoona mgawanyiko. Alifuata mwendo wa mto Ruaha akilindwa na wenyeji waliokuwa tayari kumficha na kumlinda dhidi ya vikosi vya Wajerumani waliomtafuta.

Mnamo Desemba 1896 alihamia milima ya Uzungwa alipojificha. Kutoka huko alitelemka mara kwa mara kwenye mabonde alipopata vyakula na kushambulia vikosi vidogo vya askari vya Kijerumani.

Katika Julai 1897 kikosi kikubwa cha Wasangu pamoja na Wahehe chini ya uongozi wa Wajerumani walikuta kambi la Mkwawa mlimani wakalishambulia lakini Mkwawa aliweza kukimbia.

Mwaka 1898 Mkwawa aliendelea kujificha kwenye misitu akiongozana na watu wachache sana. Aliishi hasa kwa njia ya kuvinda.

Wakati wa Julai 1898 aliongozana na wavulana 4 pekee, halafu Wazungwa 2, mume na mke. Tarehe 16 Julai Wajeumani waliowahi kusikia habari zake walimkuta huyu mama Mzungwa alipotafuta chakula wakamkamata hata akawaambia Mkwawa alielekea kusini. Wakamfuata na tarehe 18 Julai Mkwawa alimwua mume Mzungwa kwa hofu ya kusalitiwa.

Aliendelea na wavulana 2 tu walioitwa Musigombo na Lifumika. Watoto waliogopa angeweza kuwaua pia. Hapo Lifumika aliamua kukimbia asubuhi ya tarehe 19 Julai. Lakini siku ileile alipotelemka kutoka mlimani alikutana na kikosi cha Wajerumani akakimbia lakini wakamshika wakamlazimisha kuwaambia habari za Mkwawa. Kijana alimwambia sajenti Mjerumani kuwa chifu alikaa mgonjwa mahali kwa umbali wa masaa 3. Walimlazimisha kuwaongoza. Njiani walisikia kwa mbali sauti ya bunduki, risasi 1. Wakaendelea na baada ya masaa mawili walikuta maiti za Mkwawa na yule kijana mwingine. Inaonekana waliwahi kujiua na sauti ya bunduki ilikuwa Mkwawa aliyejipigia risasi.[5].

Fuvu la Mkwawa

Fuvu la Mkwawa katika Makumbusho ya Kalenga karibu na Iringa, Tanzania.

Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen.

Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema. Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthibitishwa kwa mkataba huu ... Ujerumani utakabidhi fuvu la Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza."
Fuvu la Mkwawa katika Makumbusho ya Kalenga karibu na Iringa, Tanzania.
 
Wajerumani walikataa habari za fuvu hili na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kulipata.

Lakini baada ya Vita vikuu vya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Katika mkusanyiko wa mafuvu 2000, 84 yalikuwa na namba zilizoonyesha yalitokea Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapo aliyapanga kufuatana na ukubwa na kutazama yale yaliyokuwa na vipimo vya karibu na ndugu wa Mkwawa aliowahi kuwapima kabla ya safari yake. Hapo aliteua fuvu lenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipiga risasi kichwani.

Fuvu hilo lilipelekwa Tanganyika tarehe 9 Julai 1954 na kuhifadhiwa katika jengo la makumbusho ya Mkwawa kwenye kijiji cha Kalenga.

Athari yake upande wa dini

Mkwawa alifuata dini za jadi, na alikataa ombi la Walutheri la kuanzisha misheni Uhehe, lakini baadaye alikubali wamisionari Wabenedikto wa Kanisa Katoliki wahamie Tosamaganga na kuanza kazi yao kati ya Wahehe.

Hata wakati wa vita vyake dhidi ya Wajerumani, Mkwawa aliwaheshimu wageni wake hawa.

Matokeo yake Wahehe wengi waliingia taratibu Ukristo kupitia madhehebu ya Kikatoliki hadi leo.