MAANDIKO kadhaa yamekuwepo kuhusiana na
historia ya Wahehe na hasa ukoo wa Mtwa Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga,
maarufu kama Mkwawa, lakini yote hayo hayakunizuia kuisaka historia hiyo.
‘Jicho halishibi kuona na Sikio halikinai kusikia!’ hivyo nikaamua kufunga
safari hadi Lungemba, yaliko makaburi ya Mtwa Munyigumba na ndugu wengine wa
ukoo huo, yapata kilometa 62 kutoka Iringa Mjini.
Wapo walioandika kwamba chimbuko la Mtwa Mkwawa ni Ungazija, lakini simulizi
ninazokutana nazo hapa ni tofauti, maana zinatoka katika vinywa vya wanaukoo wa
Muyinga, ambao nao wameipata ama kurithishwa kutoka kizazi na kizazi kutokana
na simulizi za mababu zao.
Wale waliopata kuandika kwamba asili ya akina Mkwawa ni Ungazija wanaeleza kuwa
mtawala wa Ngazija aliyeitwa Yusuf Hassan ambaye alikuwa Mwarabu, alizaa watoto
wawili wa kiume, Hassan ‘Mbunsungulu’ na Ahmad. Wanasema kwamba Mufwimi alikuwa
mmoja wa watoto watatu wa Mbunsungulu aliozaa na mwanamke wa Kikaguru. Ndugu
zake wengine walikuwa Ngulusavangi na Ngwila, kwa maelezo yaliyo kwenye baadhi
ya maandishi ambayo inatoweka kutokana na Watanzania kukosa utamaduni wa
kutembea, kujifunza na kudadisi.
Rungemba ni kijiji ambacho hakijasikika sana katika historia kama lilivyo jina
la Mkwawa, lakini hapa ndipo kwa kiasi kikubwa lilipo chimbuko la Chifu huyo wa
kabila la Wahehe na ndipo lilipo kaburi la Mtwa Munyigumba.
Ignas Pangiligosi Muyinga, maarufu kama Malugila Mwamuyinga (61), ambaye ni
kitukuu wa Msengele Kilekamagana, anaona fahari kuisimulia historia ya ukoo huo
maarufu.
“Shina la ukoo wetu linaanzia kwa mtu aliyeitwa Mufwimi (yaani Mwindaji),
ambaye mababu zetu walitusimulia kwamba alitokea Ethiopia,” Malugala anaanza
kueleza. “Mufwimi alipita akiwinda kutoka Ethiopia, Kenya kabla ya kuingia
Tanganyika na kujikuta yupo Usagara na hatimaye eneo la Nguluhe-Dabaga akipitia
Ikombagulu, himaya ya Chifu Mwamududa. Wengi walimfananisha na mtu wa kabila la
Wakamba kutoka Kenya kutokana na umbile lake kubwa.”
Wakati huo eneo ambalo sasa linaitwa Iringa lilikuwa na makabila mbalimbali.
Walikuwepo ‘Wahafiwa’ katika Bonde la Milima Welu, Luvango, Wutinde, Lugulu,
Makongati, Kalenga, Kipagala, Kihesa, Tambalang’ombe, Ibanagosi, Tipingi, Ikolofya,
Nyambila, Kibebe na Isanzala.
‘Vanyategeta’ wao walioishi Udzungwa, Kitelewasi na Lundamatwe, ambao walikuwa
wahunzi hodari. ‘Vanyakilwa’ walilowea Mufindi wakitokea Kilwa; ‘Vasavila’
waliishi milima ya Welu huko Makungu (Kihanga ya sasa),Magubike na Malangali;
na ‘Vadongwe’ waliishi kando ya milima ya Uhambingeto, Ipogolo, Nyabula na
Luhota.
HADI wakati huo, tayari von Heydebreck – mmoja wa
manusura katika vita hivyo – alikuwa amekwishajeruhiwa na kuanguka akiwa
amepoteza fahamu, lakini baadaye aliandika kwenye ripoti yake: “…Mfululizo wa
matukio hadi wakati huu ulikuwa umetumia dakika mbili au tatu tu. Nilitambua
hilo kabla ya kujeruhiwa, Wasudani tayari walikuwa wamekimbia kurudi nyuma
vichakani baada ya kufyatua risasi mara mbili hivi. Mimi na askari wa Kikosi
cha Tano tulilazimika kujilinda na kujitetea baada ya kuona Wahehe wakija
katika umbali wa hatua 30. Kama sikosei, nilimsikia Sajini Tiedemann akisema
alikuwa ameumia kabla hajafyatua risasi. Haikuwa rahisi kuona zaidi ya umbali
wa hatua tano msituni kutoka pale njiani. Pia hakuna ambaye aliweza kunusurika
kwa sababu Wahehe walikuja kwa kasi… Ni wazi walipanga kutushambulia baada ya
kufika katikati msitu. Kuvurugika kwa mipango yao kulichangiwa hasa na kitendo
cha Luteni von Zitewitz kufyatua risasi…”
Muanzilishi wa Himaya ya Ujerumani Afrika Mashariki, Carl Peters, baadaye Novemba 23, 1891 alimwandikia Gavana von Soden akisema kwamba, katika mapambano mengine na makabila mbalimbali ya Tanganyika, ilikuwa ni bahati tu kwao kutoweza kupata madhara kama waliyopata Wajerumani pale Lugalo, kwani mafunzo yao ya vita yalikuwa yanalenga zaidi kupigana wakiwa wamejipanga pamoja kwa mbinu maalum. Hawakuwa wamejifunza kupigana kila mtu kwa uwezo wake, bali walitegemea zaidi kushambulia kwa pamoja.
Iliwachukua Wahehe dakika 15 tu (kuanzia saa 1:15 hadi 1:30 asubuhi) kuwafyeka Wajerumani na majeshi yao. Von Zelewiski aliuawa kwa kupigwa nyundo kichwani akiwa amepanda punda wake wakati akijiandaa kuwafyatulia risasi wapiganaji wa Mkwawa. Kabla hajadondoka akachomwa mkuki ubavuni.
Hii ndiyo asili hasa ya jina la ‘Nyundo’ kutokana na kamanda huyo wa Wajerumani kuuawa kwa nyundo!
Kuhusiana na kifo cha Kamanda von Zelewiski, kama Mjerumani Tom von Prince alivyoandika baadaye, “Kama nilivyosimuliwa baadaye… na Wahehe walioshuhudia, alijitetea mwenyewe kwa kutumia bastola yake kubwa na kuwapiga risasi watu watatu, wakati kijana mmoja wa Kkihehe alipomchoma na mkuki ubavuni. Kijana huyo alikuwa na umri wa miaka 16 tu na alizawadiwa ng’ombe watatu na Mkwawa kwa kitendo hicho.”
Luteni von Pirch na Dk. Buschow pia waliuawa wakiwa juu wa punda wao ambapo majeraha yao yalikuwa makubwa mno. Karibu askari wote wa Kikosi cha 7, Kikosi cha Silaha, Kikosi cha 5 na baadhi ya askari wa Kikosi cha 6 waliuawa kabla hata hawajajua wafanye nini.
Luteni von Heydebreck, Luteni Usu Wutzer na Murgan Effendi pamoja na askari 20 hivi ndio waliofanikiwa kukimbia kutoka eneo hilo la mapigano na kukimbilia upande mwingine wa mlima na kuweka ngome wakijilinda dhidi ya mashambulizi ya Wahehe. Wapiganaji hao wa wajerumani walijificha kwenye pagala moja la tembe lililokuwa limetelekezwa mlimani. Askari mmoja Msudani ndiye aliyekiona kibanda hicho.
Lakini von Heydebreck aliishuhudia vita hiyo katika kipindi cha dakika mbili au tatu tu kabla ya kupoteza fahamu. “Kulingana na ushuhuda wa Wahehe walioshiriki mapigano yale, vita hivyo havikumalizika mapema kama ambavyo Wazungu wa mstari wa nyuma walivyotegemea, badala yake askari walionusurika waliendelea kupambana hadi saa 4:30 asubuhi na kuwaua maadui wengi (Wahehe).”
Askari wa mwisho wa kikosi cha Luteni von Tettenborn ndio hawakupata madhara makubwa ya mashambulizi ya Wahehe, washukuru kutokana na makosa ya ishara, vinginevyo wote wangeangamia katika kipindi hicho cha dakika 15 tu. Von Tettenborn, Feldwebel Kay na askari kama 20 hivi Wasudani wakahamia upande wa kushoto wa eneo la mapigano na kutengeneza nusu duara kwa ajili ya mashambulizi huku wakiwa wameumia. Wakiwa hapo walipandisha bendera ya Ujerumani juu ya mti na kupiga mbinja ili kuwaita manusura wengine.
Wakati huo Wahehe waliendelea kuwakimbiza manusura na kushambulia kila waliyemuona mbele yao. Mkanganyiko ukaongezeka baada ya kuwasha nyasi.
Mnamo saa 2:30 asubuhi hiyo, Luteni von Heydebreck, Luteni Usu Wutzer na Murgan Effendi wakiwa na askari wao 12 walipenya na kuungana na kikosi cha von Tettenborn. Von Heydebreck alikuwa anavuja sana damu kutokana na majeraha mawili makubwa ya mikuki. Kwa kuwatazama tu watu hao, von Tettenborn akatambua kwamba vikosi vyao vyote vilikuwa vimesambaratishwa na kikosi cha silaha kutekwa, ambapo Mkwawa aliteka bunduki 300. Askari wa jeshi la Wajerumani waliouawa siku hiyo walikuwa zaidi ya 500.
Ilipofika saa 3:00 Luteni Usu Thiedemann, akiwa na majeraha makubwa ya moto aliingizwa kwenye kikosi cha Luteni von Tettenborn akiwa amebebwa na askari waliokuwa wanafanya doria. Nyasi zilizokuwa zinaungua sasa zilimtisha von Tettenborn na manusura wengine.
Hadi kufikia saa 10:00 jioni Luteni von Tettenborn alikuwa amewakusanya majeruhi wengi na kuokota baadhi ya mizigo yao. Wahehe waliokuwa wamepagawa kwa hasira pamoja na moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuteketeza msitu viliifanya kazi ya kuwatafuta majeruhi wengine kuwa ngumu, hivyo wengi waliteketea kwa moto. Von Tettenborn akaamua kuanza kurudi nyuma kabla hajazuiwa na Wahehe.
Wakati wa usiku wa manane kikosi kilichokuwa na Luteni von Tettenborn kikapiga kambi ng’ambo ya pili ya mto tofauti na mahali walipolala kabla ya kuanza mapambano. Kikosi chake sasa kilikuwa na yeye mwenyewe na Luteni von Heydebreck, ma-NCO watatu wa Kijerumani (ingawa Luteni Usu Thiedemann alikufa baadaye njiani), maofisa wawili wa Kiafrika, ma-NCO 62 wa Kiafrika, wapagazi 74 na punda 7. Kutoka hapo wakaanza kutembea hasa nyakati za usiku kurudi nyuma ambapo walifika Myombo Agosti 29.
BAADA ya ushindi wa Lugalo, Chifu Mkwawa hakutulia, bali aliendelea kuimarisha himaya yake pamoja na jeshi lake. Lakini pia kipindi hicho Wajerumani nao walikuwa wakipanga mikakati ya namna ya kuisambaratisha himaya hiyo.
Kitendo cha kupigwa kwa jeshi lao imara lenye silaha kali, tena na wapiganaji wenye mikuki na mishale tu, kiliichanganya Berlin kwa sababu hakikuwahi kutokea hapo kabla. Hivyo Gavana Julius Freiherr von Soden aliyekuwa anaongoza koloni hilo la Afrika Mashariki alikuwa katika presha kubwa kutoka kwa wakubwa wake kuhusiana na namna atakavyomshinda Mkwawa.
Gavana huyo alijitahidi kukabiliana na presha ya Wahehe waliokuwa wakkivamia misafara yake hadi miaka miwili baadaye alipoondoka nchini. Wajerumani walikuwa na mbinu ya kuidhoofisha himaya ya Wahehe kwa mazungumzo, siyo kwa vita, kwa sababu walitambua kwamba hiyo ingeweza kuwagharimu tena.
Historia inaeleza kwamba, uamuzi wa Von Soden wa kutotumia jeshi kupambana na Mkwawa ulimfanya aonekane gavana bomu kati ya magavana wote walioongoza koloni hilo, lakini hiyo ilitokana na historia yake. Yeye ndiye alikuwa gavana pekee aliyetokea uraiani, kwani aliyemtangulia von Wissmann na wafuasi wake wa baadaye walikuwa makamanda wa jeshi.
Katika kipindi hicho cha Von Soden, Mkwawa naye alifanya majaribio kadhaa ya mazungumzo na Wajerumani akituma ujumbe wake Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalichukua muda wa miezi kadhaa kupitia kwa wawakilishi wake, lakini hayakuwa na mafanikio kwa sababu watawala wa Kijerumani walikuwa na mashaka na msimamo wa Mtawala huyo wa Wahehe kwamba angeweza kuwabadilikia. Kwa kifupi, hawakumwamini.
Pamoja na Von Soden kuwa na nia njema ya kufanya mapatano, maofisa wengine wa Kijerumani walikuwa na mawazo kwamba hakukuwa na haja yoyote ya kufanya mazungumzo na mtawala wa Kiafrika ambaye alikuwa ameidhalilisha Ujerumani kama alivyofanya Mkwawa.
Luteni Tom von Prince (baadaye Kapteni baada ya kuiangusha Kalenga) aliwahi kusema: “Tangu kuangushwa kwa kikosi cha Zelewski, hasa nikiwa askari wa jeshi lile la zamani, haja yangu kubwa ilikuwa kulipa kisasi kwa kudhalilishwa kwa jeshi letu, na tangu hapo nikaweka mkakati, sikuhitaji kuingia kwenye vita yoyote, sikufanya chochote ambacho kingeweza kuingilia kati mpango huu.”
Wajerumani wakati huo walikuwa na mashaka kwamba watawala wa Kiafrika, hususan Mkwawa walikuwa wameanza kuonyesha upinzani wa wazi, hasa Mtemi Isike wa Tabora na Mbunga wa Ungoni ambao himaya zao zilipakana na Uhehe. Chifu mmoja wa Usagara aliwahi kutamka wazi, “Watu hawa (Wahehe) ndio pekee walioweza kuoga mchanga wa damu ya Mzungu ambao ‘bomba zao za moto’ ziliwafanya wengi washindwe kujitetea. Na kweli, vijiji vingi vilivyokuwa jirani na boma la Wajerumani viliendelea kutoa msaada kwa Mkwawa na Himaya yote ya Uhehe mpaka pale Kalenga ilipoangushwa.
Sababu za Mkwawa kutochukua uamuzi wa kuwafukuzia Wajerumani baada ya vita vya Lugalo zinatajwa kuwa nyingi, ingawa kubwa zaidi, kwa mujibu wa waandishi wa zamani wa historia Erick Mann, Alison Redmayne, na wengineo, ilikuwa ni kupoteza askari wake wengi. Vikosi vya Mkwawa havikuwahi kuvamia eneo lililokuwa likikaliwa na Wajerumani. Katika vita vya Lugalo, Mkwawa alipompoteza makamu kiongozi wa Kalenga, Ngosi Ngosi Mwamugumba.

No comments:
Post a Comment