Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Friday, 20 January 2017

Historia ya chimbuko, mila na desturi za kabila la WAIRAQW


Utangulizi


Wairaqw ni miongoni mwa rnakabila yanayoishi katika Mkoa wa Manyara Wilaya za Mbulu, Babati, Hanang na Mkoa wa Arusha Wiiaya ya Karatu.


 
Asili ya kabila la WAIRAQW

Kwa asili Wairaqw walitokea Mesopotamia Iraq. Uhamiaji wao ulianza katika karne ya 4 - 6 baada ya kuzaliwa kwa Kristo. Wairaqw ni jamii ya Wakushi ambao Walivuka bahari ya Sham kwa mashua na kutua Ethiopia, waliishi hapo kwa muda kutokana na vita vya mara kwa mara, waiiendelea kuhama kuelekea kusini magharibi waiipitia bonde la ufa kando ya ziwa Victoria. Katika kuhama hama huko na kukaa mahali kwa muda vita vikaanza wakakimbilia na waiiendelea hivyo hivyo kupitia njia ya kati kupitia Singida Iramba hadi mpakani mwa Dodoma na Iringa. Kwa upande wa kusini kuiikuwa na mapambano ya Wahehe, Wangoni na Wazimba wakarejea kuelekea kaskazini hadi sehemu ya Kondoa mahali panapoitwa Guser Tuwalay. Waliishi hapo wakiwa wafugaji na kilimo kidogo. Ndipo walipoanza mapambano kati yao na Wabarbaig. Waliposhindwa vita walikirnbilia karibu na mlima Hanang. Wakagawanyika wengine wakaelekea,Gallapo (Tsea Daaw). Hawa waliitwa Wagorowa na Wairaqw walipandisha mlima Dabil hadi Guser, Gangaru ambapo walifanya maskani.

 
Mji wa Babati
Baada ya muda Kiongozi wao aiiyeitwa Haymu Now wa ukoo wa Haytipe aliwaongoza hadi Nou na walifanya rnaskani yao katika maeneo ya Mama Isara. Aidha inasemakana kuwa eneo lote la Mama Isara lilikuwa ni ziwa wakati ule, hivyo Haymu na watu wake walifanya maskani katika maeneo ya milima.

 
Kiongozi huyo alikuwa na mtumishi wake aiiyeitwa MOYA. Hi kuongeza maeneo ya kilimo kiongozi huyo alitumia uganga wake kuhamisha ziwa katika eneo la Mama Isara kwa kumwagiza mtumishi wake kurusha mshale katikati ya ziwa hilo. mtumishi alipofanya hivyo ziwa lilihama pamoja naye hadi katika bonde la ufa ambalo linajulikana kwa jina la ziwa manyara kwa sasa na Kiiraqw hujulikana kama "Tlawta Moya".

 
Baada ya ziwa kuhama kiongozi huyo aliendelea kuishi hapo na watu wake na kuendelea kutawanyika katika maeneo ya Muray, Kuta, Amoa, Kainam, Suum, Datlaa, Tsaayo Wilaya ya Mbulu.

 

Baadaye Wairaqw wakatawanyika taratibu sehemu za Karatu, Babati na Hanang kama makao makuu yao mpaka leo. Baadhi ya miia na desturi za Wairaqw zinafanana na za Wayahudi kama matumizi ya kondoo katika jamii.

Chakula cha asili cha WAIRAQW

Chakula chao kikuu kilikuwa nyama ya wanyamapori na ya mifugo waliyofuga. Walichuna nyama kwa kutumia mawe yenye ncha kali mithili ya kisu. Mapishi yao yalitokana na moto unaopatikana kwa njia ya kupekecha mti hadi moto unatokea, chombo hicho kiliitwa (Bui na Daha). Baadaye waligundua mazao aina ya mtama, ulezi, uwele na mboga yao ilikuwa kunde.

 
Nafaka hiyo ilisagwa kwa kutumia jiwe la mkono na unga uliopatikana ulitumika kupikia ugali mlaini (Xwante) unaofanana na uji uliopoa. Nafaka hiyo pia hutumika kutengenezea pombe ya asili ambayo ilinyweka kama viburudisho wakati wa sherehe mbalimbali za kimila.

 
Michezo ya asili

Wairaqw walikuwa na ngoma aina mbili:-

1. Ngoma ya ndani yaani ya harusi. Ngoma hii huchezwa siku mtoto wa

kike anapoolewa au wa kiume anapooa.

2. ngoma ya nje ya mwaka wakati wa mavuno huitwa "Gilo". Ngoma hii huchezwa wakati wa mavuno kama ishara ya furaha na shukrani kwa Mungu.

 

Nyimbo ya "Mudeli" huimbwa wakati wa harusi kwa kumpongeza bwana harusi na bibi harusi, na nyimbo hizp huimbwa na akina mama. Wakati wa kuweka sherehe ya shukrani kwa mwaka, Wairaqw wana utaratibu wa maombi

yaani inaitwa "slufay" pamoja na "Giriyda". Giriyda hi nyimbo maalum ya kuomba mambo rnazuri na kuepusha mambo mabaya.

 

Nyimbo maarufu kwa akina mama inaitwa "sibeli" ni nyimbo ya shukrani kwa

Mungu.

 
Mavazi

Mavazi ya asili ya Wairaqw ni ngozi. Ngozi hizo zililainishwa vizuri na kushonwa mithili ya shuka, sketi au kanga. Vazi la kiume lilikuwa moja ambalo lilifunikwa kama shuka. Vazi la kike lilikuwa sketi na shuka ndogo iliyofanana na kanga. Pia wanaume na wanawake walivaa viatu vilivyotengenezwa na ngozi.

 
Uchumi wa jadi ya WAIRAQW

Uchurni wa jadi wa Wairaqw ulikuwa ufugaji, kilimo, na utengenezaji wa zana mbalimbali za kilimo na ulinzi. Hapakuwa na biashara ya fedha taslimu ila ilikuwa kubadilishana mali au mifugo kwa vifaa au zana.
Moja ya barabara katika Mkoa wa Manyara
 
Ziwa Manyara

 
Zana za kilimo

Majembe ya asili yalitengenezwa kwa kutumia miti iliyochongwa kama mithili ya jembe. Majembe hayo yalitumika kulimia na kushindilia udongo juu ya nyumba ya Tembe. Jembe hilo liliitwa "Taqhwani", pia kwa ajili ya kutindua shamba jipya walitumia chimbuo lililotengenezwa na miti migumu na ilichongwa upande mmoja mithili ya chimbuo. Jembe hilo liliitwa 'Dughsay". Baadaye waligundua zana zilizotengenezwa kwa udongo wa mfmyanzi uliotoka Mbugwe. Zana hizo zilitumika hadi majembe ya mkono yalipopatikana kutoka kwa wataalam wa nje.

 
Zana za vita na uwindaji

Mikuki na mishale ya asili ilitengenezwa na miti iliyochongwa mfano wa mkuki wa chuma unaotumika sasa. Pia walitumia mawe yenye ncha kali na baadaye waligundua zana zinazotengenezwa kwa kuturnia udongo wa mfinyanzi ambazo zilikaushwa kwa moto mkali kama tofali.

 
Hifadhi ya nafaka

Walipovuna walikuwa na utaratibu wa kuweka mazao yao kwenye ghala zao za asili (kuntay) zilizotengenezwa kwa vinyesi vya ng'ombe. Pia aina ya majani ya miti ya asili na majivu ya vinyesi vya ng'ombe vilitumika katika kuhifadhi nafaka kutokana na kushambuliwa na wadudu. Majivu ya majani hayo yalichanganywa na nafaka mithili ya dawa zinazotumika sasa.

 
Utawala/uongozi

Walikuwa na uongozi toka ngazi ya familia, ukoo, jamii ya kabila zima la Wairaqw

waliotawaliwa na Kahamusmo ambaye ni kiongozi mkuu wao. Kiongozi msaidizi anaitwa Yaabusmo. Kila mmoja anafanya kazi kwa nafasi yake. Kwa ujumla ni kabila linalopenda kushirikiana katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa; "Walikuwa na waganga wa kiasili waliojulikana kwa majina kwa jamii nzima.

 
Malezi ya mtoto wa kike na kiume wa KIIRAQW

Mtoto wa kike na wa kiume wa Kiiraqw anapozaliwa na kukua hufundishwa maadili mema ya kuishi na jamii. Mtoto wa kike hufundishwa na akina mama maadili mema ya kuishi na nume na namna ya kutunza familia anapoolewa na kuzaa. Mtoto wa kiume hufundishwa na akina baba maadili ya kuishi na jamii, mbinu za kujitegemea katika kutunza familia anapokuwa ameoa.

 
Elimu

Wairaqw wa asili hawakupenda kuwasomesha watoto wao wakidai kuwa wakipata elimu watapotoka au mila zao zingepotea. Pia waliwazuja watoto kwenda shule kwa ajili ya kufanya kazi za nyumbani kama vile kucunga mifugo hasa kwa watoto wa kiume. Kwa watoto wa kike waliwazuia kwenda shule ili waolewe na wapate mali (mahari).

 
Mahakama ya jadi za WAIRAQW

Adhabu zilitolewa kwa taratibu za mila kwa kuzingatia kosa alilotenda mhalifu. Masuala ya makosa yote yaliyotoka katika jamii hujadiliwa na wazee wa jinsia tofauti yaani wanaume na wanawake na kutolewa uamuzi. Pia fursa Hitolewa kwa masuala yaliyohusu kesi ya jinsia moja kujadiiiwa na wazee wa jinsia hiyo kwanza ili hatimaye adhabu itolewe na jamii nzima.

 
Watuhumiwa waliopatikana na makosa yaliyothibitika walitozwa faini ya kimila iliyoitwa "Dohho" au waliagizwa kulipa fidia kwa mlalamikaji. Watuhumiwa waliokana mashtaka hata kama kuna ushahidi walipewa adhabu ya kutengea na jamii nzima. Pia kwa kesi ambazo hazina ushahidi mlalamikaji na mlalamikiwa waliapishwa kwa yote aliyoeleza ni sahihi na laana ilitolewa kwa aliyesema uongo fotauti na hali halisi.

 
Tiba za asili

Wairaqw walitumia mizizi na majani ya miti kama tiba ya magonjwa mbalimbali. Mizizi hiyo ilichemshwa au kusagwa na kuchanganywa na maji na kupewa wagonjwa.

No comments:

Post a Comment