Utangulizi
Wairaqw ni miongoni
mwa rnakabila yanayoishi katika Mkoa wa Manyara Wilaya za Mbulu, Babati, Hanang
na Mkoa wa Arusha Wiiaya ya Karatu.
Kwa asili Wairaqw
walitokea Mesopotamia Iraq. Uhamiaji wao ulianza katika karne ya 4 - 6 baada ya
kuzaliwa kwa Kristo. Wairaqw ni jamii ya Wakushi ambao Walivuka bahari ya Sham
kwa mashua na kutua Ethiopia, waliishi hapo kwa muda kutokana na vita vya mara
kwa mara, waiiendelea kuhama kuelekea kusini magharibi waiipitia bonde la ufa
kando ya ziwa Victoria. Katika kuhama hama huko na kukaa mahali kwa muda vita vikaanza
wakakimbilia na waiiendelea hivyo hivyo kupitia njia ya kati kupitia Singida
Iramba hadi mpakani mwa Dodoma na Iringa. Kwa upande wa kusini kuiikuwa na mapambano
ya Wahehe, Wangoni na Wazimba wakarejea kuelekea kaskazini hadi sehemu ya
Kondoa mahali panapoitwa Guser Tuwalay. Waliishi hapo wakiwa wafugaji na kilimo
kidogo. Ndipo walipoanza mapambano kati yao na Wabarbaig. Waliposhindwa vita
walikirnbilia karibu na mlima Hanang. Wakagawanyika wengine wakaelekea,Gallapo (Tsea Daaw).
Hawa waliitwa Wagorowa na Wairaqw walipandisha mlima Dabil hadi Guser, Gangaru
ambapo walifanya maskani.
Baada ya muda Kiongozi wao aiiyeitwa Haymu Now wa ukoo wa Haytipe aliwaongoza hadi Nou na walifanya rnaskani yao katika maeneo ya Mama Isara. Aidha inasemakana kuwa eneo lote la Mama Isara lilikuwa ni ziwa wakati ule, hivyo Haymu na watu wake walifanya maskani katika maeneo ya milima.
Baadaye Wairaqw wakatawanyika
taratibu sehemu za Karatu, Babati na Hanang kama makao makuu yao mpaka leo.
Baadhi ya miia na desturi za Wairaqw zinafanana na za Wayahudi kama matumizi ya
kondoo katika jamii.
Chakula cha asili cha WAIRAQW
Chakula chao kikuu
kilikuwa nyama ya wanyamapori na ya mifugo waliyofuga. Walichuna nyama kwa
kutumia mawe yenye ncha kali mithili ya kisu. Mapishi yao yalitokana na moto unaopatikana
kwa njia ya kupekecha mti hadi moto unatokea, chombo hicho kiliitwa (Bui na Daha).
Baadaye waligundua mazao aina ya mtama, ulezi, uwele na mboga yao ilikuwa
kunde.
Wairaqw walikuwa na
ngoma aina mbili:-
1. Ngoma ya ndani
yaani ya harusi. Ngoma hii huchezwa siku mtoto wa
kike anapoolewa au
wa kiume anapooa.
2. ngoma ya nje ya
mwaka wakati wa mavuno huitwa "Gilo". Ngoma hii huchezwa wakati wa mavuno
kama ishara ya furaha na shukrani kwa Mungu.
Nyimbo ya
"Mudeli" huimbwa wakati wa harusi kwa kumpongeza bwana harusi na bibi
harusi, na nyimbo hizp huimbwa na akina mama. Wakati wa kuweka sherehe ya
shukrani kwa mwaka, Wairaqw wana utaratibu wa maombi
yaani inaitwa
"slufay" pamoja na "Giriyda". Giriyda hi nyimbo maalum ya
kuomba mambo rnazuri na kuepusha mambo mabaya.
Nyimbo maarufu kwa
akina mama inaitwa "sibeli" ni nyimbo ya shukrani kwa
Mungu.
Mavazi ya asili ya
Wairaqw ni ngozi. Ngozi hizo zililainishwa vizuri na kushonwa mithili ya shuka,
sketi au kanga. Vazi la kiume lilikuwa moja ambalo lilifunikwa kama shuka. Vazi
la kike lilikuwa sketi na shuka ndogo iliyofanana na kanga. Pia wanaume na
wanawake walivaa viatu vilivyotengenezwa na ngozi.
Uchurni wa jadi wa
Wairaqw ulikuwa ufugaji, kilimo, na utengenezaji wa zana mbalimbali za kilimo
na ulinzi. Hapakuwa na biashara ya fedha taslimu ila ilikuwa kubadilishana mali
au mifugo kwa vifaa au zana.
Moja ya barabara katika Mkoa wa Manyara |
Ziwa Manyara |
Majembe ya asili
yalitengenezwa kwa kutumia miti iliyochongwa kama mithili ya jembe. Majembe
hayo yalitumika kulimia na kushindilia udongo juu ya nyumba ya Tembe. Jembe
hilo liliitwa "Taqhwani", pia kwa ajili ya kutindua shamba jipya
walitumia chimbuo lililotengenezwa na miti migumu na ilichongwa upande mmoja
mithili ya chimbuo. Jembe hilo liliitwa 'Dughsay". Baadaye waligundua zana
zilizotengenezwa kwa udongo wa mfmyanzi uliotoka Mbugwe. Zana hizo zilitumika
hadi majembe ya mkono yalipopatikana kutoka kwa wataalam wa nje.
Mikuki na mishale ya
asili ilitengenezwa na miti iliyochongwa mfano wa mkuki wa chuma unaotumika
sasa. Pia walitumia mawe yenye ncha kali na baadaye waligundua zana zinazotengenezwa
kwa kuturnia udongo wa mfinyanzi ambazo zilikaushwa kwa moto mkali kama tofali.
Walipovuna walikuwa
na utaratibu wa kuweka mazao yao kwenye ghala zao za asili (kuntay) zilizotengenezwa
kwa vinyesi vya ng'ombe. Pia aina ya majani ya miti ya asili na majivu ya vinyesi
vya ng'ombe vilitumika katika kuhifadhi nafaka kutokana na kushambuliwa na wadudu.
Majivu ya majani hayo yalichanganywa na nafaka mithili ya dawa zinazotumika
sasa.
Walikuwa na uongozi
toka ngazi ya familia, ukoo, jamii ya kabila zima la Wairaqw
waliotawaliwa na
Kahamusmo ambaye ni kiongozi mkuu wao. Kiongozi msaidizi anaitwa Yaabusmo. Kila
mmoja anafanya kazi kwa nafasi yake. Kwa ujumla ni kabila linalopenda kushirikiana
katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa; "Walikuwa na waganga wa
kiasili waliojulikana kwa majina kwa jamii nzima.
Mtoto wa kike na wa
kiume wa Kiiraqw anapozaliwa na kukua hufundishwa maadili mema ya kuishi na
jamii. Mtoto wa kike hufundishwa na akina mama maadili mema ya kuishi na nume na
namna ya kutunza familia anapoolewa na kuzaa. Mtoto wa kiume hufundishwa na
akina baba maadili ya kuishi na jamii, mbinu za kujitegemea katika kutunza
familia anapokuwa ameoa.
Wairaqw wa asili
hawakupenda kuwasomesha watoto wao wakidai kuwa wakipata elimu watapotoka au
mila zao zingepotea. Pia waliwazuja watoto kwenda shule kwa ajili ya kufanya kazi
za nyumbani kama vile kucunga mifugo hasa kwa watoto wa kiume. Kwa watoto wa
kike waliwazuia kwenda shule ili waolewe na wapate mali (mahari).
Adhabu zilitolewa
kwa taratibu za mila kwa kuzingatia kosa alilotenda mhalifu. Masuala ya makosa
yote yaliyotoka katika jamii hujadiliwa na wazee wa jinsia tofauti yaani
wanaume na wanawake na kutolewa uamuzi. Pia fursa Hitolewa kwa masuala
yaliyohusu kesi ya jinsia moja kujadiiiwa na wazee wa jinsia hiyo kwanza ili
hatimaye adhabu itolewe na jamii nzima.
Wairaqw walitumia
mizizi na majani ya miti kama tiba ya magonjwa mbalimbali. Mizizi hiyo ilichemshwa
au kusagwa na kuchanganywa na maji na kupewa wagonjwa.