Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Wednesday, 19 September 2012

Nguvu umma yamtesa pinda mwanza, azomewa, awa mbogo


Vijana Mwanza Waimba ‘People’s Power, Hatuitaki CCM’

Na mwandishi wetu
 
Mizengo Pinda, Waziri Mkuu
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kuhutubia maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza kwa muda kutokana na wananchi wengi kumzomea.

Kiongozi huyo alikumbana na kisanga hicho cha aina yake akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Welle Ndikilo.

Pinda na viongozi hao, walikumbana na zomeazomea hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Sahara jijini hapa, ikiwa ni hitimisho la ziara ya Waziri Mkuu huyo ya siku saba mkoani Mwanza.


Chanzo cha Pinda na viongozi hao kuzomewa mkutanoni hapo, ilitokana na kile kilichoonekana kuwepo kwa kero nyingi zilizodaiwa kushindwa kupatiwa ufumbuzi na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete.


Kitendo hicho cha wananchi kilimlazimisha Pinda kushindwa kuhutubia kwa muda, huku akionekana kujawa jazba.


Sababu nyingine ya wananchi kuzomea, ni hatua ya Pinda kuwaambia wananchi hao watoke mjini waende vijijini wakalime waachane na mambo ya upinzani wa kisiasa.


Pinda alitoa kauli hiyo baada ya kundi la vijana mkutanoni hapo kuonesha alama ya V, bendera ya CHADEMA na nyimbo za Peoples, Power.


Kwa mazingira hayo, askari wa polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), waliokuwa na silaha nzito za kivita aina ya SMG, mabomu na marungu waliokuwepo mkutanoni hapo, walianza kuwatishia kuwapiga wananchi hao kwa lengo la kumlinda kiongozi huyo.


Baada ya kuzidi zomeazomea hiyo, Waziri Mkuu, Pinda alilazimika kumuita mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), aliyekuwa meza kuu, kisha kusema: "Nyamazeni basi!. Wenje...hii ndiyo serikali ya siku chache zijazo. Kwa namna hii naona hamuwezi, maana itakuwa ni vurugu asubuhi hadi jioni". Akazomewa kisha wakaimba hatutaki CCM, hatutaki CCM. .


Baada ya kuona hivyo, Pinda akacheka na kusema: "Hahahaaaaa, hata mkiimba peoples power, CCM ndiyo inayowaongoza". Akazomewa tena kisha Pinda akashindwa kuendelea kuzungumza jukwaani.


Akahutubia mkutanoni hapo, Pinda aliwataka wananchi hao waache ushabiki wa kisiasa, na kwamba halmashauri ya jiji la Mwanza inayoongozwa na CHADEMA, ndiyo itapaswa kulaumiwa kama itashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.


"Hapa jiji la Mwanza linaongozwa na CHADEMA. Meya wa CHADEMA, mwenyekiti wa Mipango miji wa CHADEMA, Naibu Meya ni wa CHADEMA. Lakini kama wameshindwa kuweka mipango mikakati ya kuwasaidia tutasema hawafai," alisema kisha akazomewa kwa mara nyingine.

Baada ya zomeazomea hiyo kuonekana kumwelemea Waziri Mkuu huyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Ndikilo alilazimika kuingilia kati kwa kusema: "Wanaozomea tunawafahamu, na tunawafahamu waliowaleta hapa ili mje kufanya nini". Akazomewa.

Hata hivyo, baada ya hali kutulia kidogo, Pinda aliendelea kuhutubia huku akiwataka wananchi wa jiji la Mwanza waondoke mjini waende vijijini wakalime, jambo lililoonekana pia kuwakasirisha wananchi wengi kisha kumzomea tena.


Ingawa Pinda alilazimika kutumia muda mfupi kutoa hotuba yake, aliwaomba wana Mwanza washirikiane kuleta maendeleo yao, na kwamba iwapo tatizo ni Mkurugenzi wa jiji suala hilo litaangaliwa.


Aliwaomba wadumishe amani iliyopo hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Serikali kupambana na vitendo vya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, ili kuweza kuzua samaki wadogo wasivuliwe kisha kuharibu mazalia ya rasilimali hiyo.


"Jambo jingine ninalotaka kuwaeleza hapa leo ni hili la uvuvi haramu. Samaki ndani ya Ziwa Victoria wameisha...na hii ni kwa sababu ya uvuvi usiozingatia sheria. Tushirikianeni kupambana na vitendo hivi", alisema Pinda kisha akazomewa tepa.

Tuesday, 18 September 2012

WAZIRI NCHIMBI HAKUVAMIA KWA BAHATI MBAYA MAANDAMANO YA WAANDISHI


WAZIRI NCHIMBI HAKUVAMIA KWA BAHATI MBAYA MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI LEO JANGWANI

Mwandishi wa Kujitegemea
 
Nawapongeza sana waandishi wa habari kwa kumtimua waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi nawapongeza sana kwa kuonyesha hisia zenu kwa kitendo kiovu kabisa ambacho kila mpenda demokrasia na haki katika ulimwengu huu ambacho amefanyiwa mbali ya kuwa mwandishi wa habari ni Mtanzania mwenzetu huyu marehemu Daudi Mwangosi.

Haina ubishi polisi ndio wameua kinachopiganiwa hapa wahusika wote ambao wako nyuma ya mauji haya washughulikiwe zaidi wale ambao wanatoa amri dhalimu kwa polisi,lakini nataka niwaambie waandishi wa habari Emanuel Nchimbi waziri wa mambo ya ndani, kuvamia maandamano yenu ya wanahabari na kutaka kuhutubia bila kualikwa sio bahati mbaya anajua mtaandika zaidi kuhusu yeye kutimuliwa kwake kwenye maandamano na kuacha kuandika maaovu na ujumbe mliokusudia kuupeleka kwa serikali na polisi wao,haingii akilini kwa mtu mwenye ngazi ya waziri kuvamia kwa mfano sherehe ambayo hana kadi ya mwaliko?

Kwa hiyo rai yangu kwa wanahabari ni kuandika kile ambacho mlikusudia kukiwakilisha leo kwa watanzania na dunia nzima !!Hawa ndio mawaziri wa tanzania huwezi kujua wakati gani yuko serious!!

Je mnakumbuka mjadala wa dowans ulivyopamba moto wakatuletea kikombe cha babu loliondo?? Na viongozi wote waserikali wakawa wa kwanza kupata kikombe na kusifia kikombe?? Kwa hiyo nchimbi asiwatoe kwenye lengo lenu. Kama hamfahamu vizuri Nchimbi ni zao la wanamtandao waliomweka Kikwete madarakani na ndio mwenyekiti aliyevuruga uvccm, na kama mnataka ukweli zaidi nendeni mkamhoji Sumaye Fredrick waziri mkuu mstaafu alikua anamaanisha nini alivyosema "anayefagia njia ya kwenda ikulu kwa karatasi basi akifika huko atatumia risasi ili aweze kutawala"mwaka 2005 kwenye kinyang'anyilo cha urais alipokuwa amechafuliwa sana na wanamtandao kwenye kampeni za kuwania urais kwa tiketi ya CCM.
kwa hiyo waandishi mshikamane mno kipindi hiki kwani serikali inajaribu kutumia kila aina ya hila kuwagawa na kuwatoa kwenye mjadala wa msingi kuwa waliomuua Daudi Mwangosi wachukuliwe hatua na wengine wawajibishwe kutokana na nyadhfa zao.

Maoni ya Wananchi

Maoni ya Wananchi
 
Nchimbi angekatwa shingo!!!
Kama mtanzania niliyeumizwa na mauaji ya makusudi aliyofanyiwa Mwangosi na Jeshi la Polisi, nimesikitishwa sana na uamuzi wa Nchimbi kwenda kuingilia kati Maandamano halali ya wanahabari pale Jangwani yaliolenga kuonyesha hisia zao na kulaani. Nchimbi hakualikwa kuwepo mahala hapo kwa wakati huo, baada ya kumuomba aondoke, nilimsikia kwa kauli yake anasema wao (kama Serikali) wanachochukia sana ni Mtu kufanya maandamano bila kibali, je yeye alipata wapi kibali cha kuingilia kati maandamano ya waandishi wa habari?
Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi akisindikizwa na Polisi kutoka eneo la Viwanja vya Jangwani
Jeshi la Polisi lililo chini ya mamlaka ya Nchimbi limekuwa likijichukulia sheria mkononi ikiwemo kuhukumu vifo kama lilivyofanya kwa Mwangosi kwa watu wa aina ya Nchimbi ambao kwa maelezo yao linadai wanakuwa wanasabibisha fujo, je hizi sheria za kudhibiti fujo hazi-apply kwa Nchimbi? Kwa polisi walio makini nilitegemea Nchimbi angekamatwa mara moja na kuhojiwa kwa kosa la kuingilia maandamano halali ya waandishi wa habari na hivyo kuhatarisha amani.
Nijuavyo mimi kwa maandamano ya majonzi kama yale yakifanywa na watu wasio wastahimilivu iwapo atatokea mtu asiyealikwa na kuyaingilia kati anaweza akauawa, hiki ndicho kilichonilazimu niandike thread hii kuwapongeza wanahabari kwa kuwa na mioyo ya ustahimirivu.
Ninawapongeza sana Waandishi wa habari kwa kumuonyesha Nchimbi kwamba wao ni wakomavu kuliko yeye kwasababu waandishi wa habari wameingiliwa katika maandamano yao lakini hawakuchukua sheria mkononi kama wanavyofanya Polisi mbali na ukweli kwamba waandishi wa habari hawajapata mafunzo maalumu kama Jeshi la Polisi jinsi ya kumshughulikia mharifu.
Nawapongeza sana waandishi wa habari msingekuwa wakomavu na wastahimirivu jana Nchimbi angekatwa Shingo.
Ushauri wangu kwa Waandishi wa Habari. Nawaombeni mumsamehe bure Nchimbi huenda hajui alifanyalo.
Ushauri wangu kwa Polisi. Nawaombeni mumkamate Nchimbi na kumhoji ili muweze kujua alikuwa amekusudia nini kwenda mahala ambapo hajaalikwa? je alitaka waandishi wa habari wamfanyie fujo ili wapigwe risasi na baadhi ya Polisi wasiojua kazi yao hasa ni nini? ikiwezekana mumshitaki Nchimbi kwa kuingilia kati maandamano yasiyo muhusu ili iwe onyo kwa wananchi wengine wasio staarabika kwani kitendo alichofanya jana Nchimbi kikiendelea kuchukuliwa kama ni cha kawaida ipo siku amani yaweza kuvunjika. kwa mfano Waislam waweza kuwa na maandamano yao akatokea Mchungaji mbele yao kwa nia ya kuwapokea, hopefully wasipokuwa wastahimilivu amani yaweza kutoweka.
Ushauri wangu kwa Nchimbi. Nakuomba uwatake radhi waandishi wa habari kwa fujo ulizozifanya jana, pia uwatake radhi wananchi maana wengi wetu hatukutegemea kama ipo siku kiongozi kama wewe unaweza kukosa busara kiasi hicho kwa kwenda mahala bila mualiko kwasababu uzijuazo wewe mwenyewe.

WANAHABARI WAMTIMUA WAZIRI NCHIMBI KATIKA MAANDAMANO YAO

WANAHABARI WAMTIMUA WAZIRI NCHIMBI KATIKA MAANDAMANO YAO

Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel NchimbiKatibu wa Jukwaa la Wahariri Bw. Nevil Meena akiongea kwa uchungu mbele ya wanahabari wenzake ambapo pamoja na maazimio mengine wametangaza kutoandika habari zinazohusiana na jeshi la polisi kwa siku 40.

Wakiwa katika nyuso za huzuni kubwa ya kuondokewa na mwenzao ambaye aliuawa kwa kupigwa na bomu, kundi la Wanahabari wao wamemtimua Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Emmanuel Nchimbi kutokana na kuwaingilia kwenye maandamano yao.

Wanahabari kote nchini leo wamefanya maandamano ya amani kwa lengo la Kulaani mauaji ya mwenzao wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Kufukuzwa na kuzomewa kwa Waziri Nchimbi kumekuja baada ya kugundulika kuwa ameingilia maandamano kwa lengo la kuyapokea bila kupewa mwaliko.

Kutokana na zomea zomea hiyo ya wanahabari hao dhidi ya Waziri Nchimbi hali ilionekana kuwa si shwari na kupelekea waziri huyo kuondolewa na rais wa UTPC Keneth Simbaya na viongozi wengine wakiwemo askari polisi.

Akizungumza na kundi la waandishi Katibu wa Jukwaa la Jukwaa la wahariri (TEF) Neville Meena amesema “Hatuna ugomvi na Waziri Nchimbi kwani ni mwenzetu, rafiki yetu, ila leo hana vazi la msiba”.

Mara baada ya kuondoka bila kupenda Waziri Nchimbi, hali ya utulivu ilikuwa kama kawaida na shughuli zingine ziliendelea kama ilivyopangwa.

Monday, 10 September 2012

Usafiri wa Baiskeli Tegemeo Kubwa Afrika

Adha ya Usafiri katika nchi za Kiafrika
Usafiri wa baiskeli umekuwa ni wa kutegemea kwa kiwango cha juu katika bara la Afrika na mabara mengine duniani. Toka baiskeli ilipogunduliwa mwanzoni mwa miaka ya 1900, familia nyingi za kiafrika ziliutegemea sana usafiri huu. Familia ilionekana yenye maendeleo pale tu ilipoweza kupata baiskeli. Lakini kutokana na kuendelea kudidimia kwa maendeleo hususani katika maeneo ya vijijini, tofauti na na miaka ya nyuma ambapo uzalishaji wa mazao mbalimbali ya nafaka na mifugo ilikuwa juu, familia ziliweza kupata ziada na baadaye kuuza na kununua baiskeli.
 
Baada ya Azimio la Arusha kufa, maendeleo ya vijiji vingi yamekuwa yakididimia kila siku na hivyo kupelekea maradhi wakuu wa watatu waliokuwa wanaikabili Tanganyika na Tanzania baadaye baada ya uhuru, kuendelea kuwanyanyasa wananchi. Suala la kupata baiskeli au usafiri mbadala katika baadhi ya vijiji, imekuwa ni ndoto tofauti na hali halisi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia inavyoendelea kukua.
 
Kama mwananchi akifanikiwa kuipata baiskeli huiboresha ili ifanye kazi zaidi na kumudu mahitaji mengine ya kifamilia mfano kutoa huduma ya usafiri. Mfano mdogo tu, angalia picha hii hapa ambapo baiskeli ina uwezo wa kubeba idadi kubwa ya abiria. Shuhudia mwenyewe... Haya ndiyo maisha ya dunia ya tatu.

Birthday Party for Carolyn Kivenule


Happy birthday Carolyn Adam Kivenule

Carolyn Adam Kivenule PhotoIt was a marvellous Sunday of 9th September 2012, when Carolyn Adam Kivenule celebrated her second birthday at Ubungo Kibangu, Dar es Salaam. The event started at 19:00 hours after a tight schedule which involved  relatives, send off meeting and Sunday prayers. Mr. Adam Kivenule with a companion of many children whom are close relatives and neighbourhood of Carolyn took part in the cherish event. Carolyn who had a lot of expectations and miscellaneous troubled the event, sometimes crying and sometime laughing. She never tried to dance herself rather than seeking company from somebody else.

It was very entertainment night accompanied with different types of local and gospel dances celebrating invitees.

Juices and a special cake which was taken by everybody who participated the event flavoured the occasion. Photos which was  taken by participants will continue to cherish and remain as a great memory to the anniversary of two years of Carolyn Adam Kivenule.


Thanks,