Maoni ya Wananchi
Nchimbi
angekatwa shingo!!!
Kama mtanzania niliyeumizwa na mauaji ya
makusudi aliyofanyiwa Mwangosi na Jeshi la Polisi, nimesikitishwa sana na
uamuzi wa Nchimbi kwenda kuingilia kati Maandamano halali ya wanahabari pale
Jangwani yaliolenga kuonyesha hisia zao na kulaani. Nchimbi hakualikwa kuwepo
mahala hapo kwa wakati huo, baada ya kumuomba aondoke, nilimsikia kwa kauli
yake anasema wao (kama Serikali) wanachochukia sana ni Mtu kufanya maandamano
bila kibali, je yeye alipata wapi kibali cha kuingilia kati maandamano ya
waandishi wa habari?
Jeshi la Polisi lililo chini ya mamlaka ya
Nchimbi limekuwa likijichukulia sheria mkononi ikiwemo kuhukumu vifo kama
lilivyofanya kwa Mwangosi kwa watu wa aina ya Nchimbi ambao kwa maelezo yao
linadai wanakuwa wanasabibisha fujo, je hizi sheria za kudhibiti fujo
hazi-apply kwa Nchimbi? Kwa polisi walio makini nilitegemea Nchimbi angekamatwa
mara moja na kuhojiwa kwa kosa la kuingilia maandamano halali ya waandishi wa
habari na hivyo kuhatarisha amani.
Nijuavyo mimi kwa maandamano ya majonzi
kama yale yakifanywa na watu wasio wastahimilivu iwapo atatokea mtu asiyealikwa
na kuyaingilia kati anaweza akauawa, hiki ndicho kilichonilazimu niandike
thread hii kuwapongeza wanahabari kwa kuwa na mioyo ya ustahimirivu.
Ninawapongeza sana Waandishi wa habari kwa
kumuonyesha Nchimbi kwamba wao ni wakomavu kuliko yeye kwasababu waandishi wa
habari wameingiliwa katika maandamano yao lakini hawakuchukua sheria mkononi
kama wanavyofanya Polisi mbali na ukweli kwamba waandishi wa habari hawajapata
mafunzo maalumu kama Jeshi la Polisi jinsi ya kumshughulikia mharifu.
Nawapongeza sana waandishi wa habari
msingekuwa wakomavu na wastahimirivu jana Nchimbi angekatwa Shingo.
Ushauri wangu kwa Waandishi wa Habari.
Nawaombeni mumsamehe bure Nchimbi huenda hajui alifanyalo.
Ushauri wangu kwa Polisi. Nawaombeni mumkamate Nchimbi na kumhoji ili muweze kujua alikuwa
amekusudia nini kwenda mahala ambapo hajaalikwa? je alitaka waandishi wa habari
wamfanyie fujo ili wapigwe risasi na baadhi ya Polisi wasiojua kazi yao hasa ni
nini? ikiwezekana mumshitaki Nchimbi kwa kuingilia kati maandamano yasiyo
muhusu ili iwe onyo kwa wananchi wengine wasio staarabika kwani kitendo
alichofanya jana Nchimbi kikiendelea kuchukuliwa kama ni cha kawaida ipo siku
amani yaweza kuvunjika. kwa mfano Waislam waweza kuwa na maandamano yao
akatokea Mchungaji mbele yao kwa nia ya kuwapokea, hopefully wasipokuwa
wastahimilivu amani yaweza kutoweka.
Ushauri wangu kwa Nchimbi. Nakuomba uwatake radhi waandishi wa habari kwa fujo ulizozifanya
jana, pia uwatake radhi wananchi maana wengi wetu hatukutegemea kama ipo siku
kiongozi kama wewe unaweza kukosa busara kiasi hicho kwa kwenda mahala bila
mualiko kwasababu uzijuazo wewe mwenyewe.
No comments:
Post a Comment