WAZIRI
NCHIMBI HAKUVAMIA KWA BAHATI MBAYA MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI LEO
JANGWANI
Mwandishi wa Kujitegemea
Nawapongeza sana waandishi wa habari kwa
kumtimua waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi nawapongeza sana kwa
kuonyesha hisia zenu kwa kitendo kiovu kabisa ambacho kila mpenda demokrasia na
haki katika ulimwengu huu ambacho amefanyiwa mbali ya kuwa mwandishi wa habari
ni Mtanzania mwenzetu huyu marehemu Daudi Mwangosi.
Haina ubishi polisi ndio wameua kinachopiganiwa hapa wahusika wote ambao wako nyuma ya mauji haya washughulikiwe zaidi wale ambao wanatoa amri dhalimu kwa polisi,lakini nataka niwaambie waandishi wa habari Emanuel Nchimbi waziri wa mambo ya ndani, kuvamia maandamano yenu ya wanahabari na kutaka kuhutubia bila kualikwa sio bahati mbaya anajua mtaandika zaidi kuhusu yeye kutimuliwa kwake kwenye maandamano na kuacha kuandika maaovu na ujumbe mliokusudia kuupeleka kwa serikali na polisi wao,haingii akilini kwa mtu mwenye ngazi ya waziri kuvamia kwa mfano sherehe ambayo hana kadi ya mwaliko?
Kwa hiyo rai yangu kwa wanahabari ni kuandika kile ambacho mlikusudia kukiwakilisha leo kwa watanzania na dunia nzima !!Hawa ndio mawaziri wa tanzania huwezi kujua wakati gani yuko serious!!
Je mnakumbuka mjadala wa dowans ulivyopamba
moto wakatuletea kikombe cha babu loliondo?? Na viongozi wote waserikali wakawa
wa kwanza kupata kikombe na kusifia kikombe?? Kwa hiyo nchimbi asiwatoe kwenye
lengo lenu. Kama hamfahamu vizuri Nchimbi ni zao la wanamtandao waliomweka
Kikwete madarakani na ndio mwenyekiti aliyevuruga uvccm, na kama mnataka ukweli
zaidi nendeni mkamhoji Sumaye Fredrick waziri mkuu mstaafu alikua anamaanisha
nini alivyosema "anayefagia njia ya kwenda ikulu kwa karatasi basi akifika
huko atatumia risasi ili aweze kutawala"mwaka 2005 kwenye kinyang'anyilo
cha urais alipokuwa amechafuliwa sana na wanamtandao kwenye kampeni za kuwania
urais kwa tiketi ya CCM.
kwa hiyo waandishi mshikamane mno kipindi
hiki kwani serikali inajaribu kutumia kila aina ya hila kuwagawa na kuwatoa
kwenye mjadala wa msingi kuwa waliomuua Daudi Mwangosi wachukuliwe hatua na
wengine wawajibishwe kutokana na nyadhfa zao.
No comments:
Post a Comment