Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Monday, 10 September 2012

Usafiri wa Baiskeli Tegemeo Kubwa Afrika

Adha ya Usafiri katika nchi za Kiafrika
Usafiri wa baiskeli umekuwa ni wa kutegemea kwa kiwango cha juu katika bara la Afrika na mabara mengine duniani. Toka baiskeli ilipogunduliwa mwanzoni mwa miaka ya 1900, familia nyingi za kiafrika ziliutegemea sana usafiri huu. Familia ilionekana yenye maendeleo pale tu ilipoweza kupata baiskeli. Lakini kutokana na kuendelea kudidimia kwa maendeleo hususani katika maeneo ya vijijini, tofauti na na miaka ya nyuma ambapo uzalishaji wa mazao mbalimbali ya nafaka na mifugo ilikuwa juu, familia ziliweza kupata ziada na baadaye kuuza na kununua baiskeli.
 
Baada ya Azimio la Arusha kufa, maendeleo ya vijiji vingi yamekuwa yakididimia kila siku na hivyo kupelekea maradhi wakuu wa watatu waliokuwa wanaikabili Tanganyika na Tanzania baadaye baada ya uhuru, kuendelea kuwanyanyasa wananchi. Suala la kupata baiskeli au usafiri mbadala katika baadhi ya vijiji, imekuwa ni ndoto tofauti na hali halisi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia inavyoendelea kukua.
 
Kama mwananchi akifanikiwa kuipata baiskeli huiboresha ili ifanye kazi zaidi na kumudu mahitaji mengine ya kifamilia mfano kutoa huduma ya usafiri. Mfano mdogo tu, angalia picha hii hapa ambapo baiskeli ina uwezo wa kubeba idadi kubwa ya abiria. Shuhudia mwenyewe... Haya ndiyo maisha ya dunia ya tatu.

No comments:

Post a Comment