Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Friday, 3 May 2013

GIDAGUMHINDI CECILIA SIGATAMBULE KIVENULE WA MAGUBIKE-IRINGA AFARIKI



TANZIA
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa masikitiko makubwa unawatangazia Wana-KAUKI, ndugu, jamaa, marafiki na wanaukoo kwa ujumla, kifo cha Bi. Gidagumhindi Cecilia Sigatambule Kivenule, kilichotokea tarehe usiku wa kuamukia tarehe 18 Aprili 2013, huko Magubike, Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.

Marehemu Gidagumhinda Kivenule alikuwa akiumwa kwa muda mrefu na hasa akisumbuliwa na tatizo la upofu wa macho, homa, miguu na uzee. Kabla ya mauti kumkuta, Marehemu alilazwa kwa muda wa wiki mbili katika hospitali ya Ipamba, na hali yake kupata auheni lakini siku ya Jumatano tarehe 17 Aprili 2013 akiwa nyumbani hali ilibadilika na hatimaye kumpelekea mauti kumfika usiku wa tarehe 18 Aprili 2013.

Bi Gidagumhindi ni Mtoto wa Kwanza kwa Bibi Siwangumhavi Singaile, ambaye alikuwa Mke Mkubwa wa Sigatambule Tavimyenda Tagumtwa Kivenule. Bibi Siwangumhavi alikuwa na watoto 7 ambapo mpaka sasa wamebaki watoto 3 tu. Wengine waliomfuata Bi Gidagumhindi ni Semyamba Khadija Kivenule, Sivinitu Alphonce Kivenule, Kadungu William Kivenule, Fibumo Xavery Kivenule, Mlagile Anyesi Kivenule na John Kivenule.

Mazishi yake yalifanyika tarehe 18 Aprili 2013, eneo la Magubike katika Makaburi ya Ukoo wa akina Nyangalima. Bi Gidagumhindi ataendelea kukumbukwa kwa upendo, mshikamano na hamasa yake katika kuhakikisha kuwa KAUKI inaendelea kuwa imara hususani katika eneo la Magubike.

Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.

Imeandaliwa na:


Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu - KAUKI

Friday, 12 April 2013

MKUTANO MKUU WA TISA WA KAUKI NA MATARAJIO MAPYA


Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) uliofanyika kwa siku mbili Kijijini Kidamali, Mkoani Iringa mwaka 2006

Thursday, 11 April 2013

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’ NA STASHAHADA KWA MWAKA 2013/2014

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’ NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anatangaza nafasi za Mafunzo ya Ualimu ngazi yaCheti na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2013/2014
http://www.moe.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=1670:tangazo-la-nafasi-za-mafunzo-ya-ualimu-ngazi-ya-cheti-daraja-a-na-stashahada-kwa-mwaka-20132014&catid=1:latest-news
icon TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’ NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014 (44.43 kB)
 

TANGAZO LA UALIMU



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 022-2110146/2110150/2211679, Faksi: 022-2113271 Tovuti: www.moe.go.tz
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’ NA
STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anatangaza nafasi za Mafunzo ya Ualimu ngazi yaCheti na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2013/2014 kama ifuatavyo:

A: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’: MUDA MIAKA 2
UALIMU: KAWAIDA
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2008 na 2012 na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua daraja la IV alama 27 katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja Au
-Awe na ufaulu kwa kiwango cha alama C katika masomo manne tofauti katika Mtihani wa Kidato cha IV ulioyofanyika katika vikao zaidi ya kimoja.
-Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics, Biology, Physics, Chemistry, Englishna Kiswahili;
-Mwombaji aliyehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2012 hiyo ni sifa ya nyongeza.

UALIMU: MICHEZO
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2008 na 2012 na kufaulu Kidato cha IV kwa kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.
-Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics, Biology, Physics, Chemistry’, ‘Englishna Kiswahili;
-Mwombaji aliyehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2012 na mwenye uzoefu katika kufundisha michezo (uthibitisho uambatishwe) ni sifa ya nyongeza.

UALIMU: ELIMU YA AWALI
-Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2008 na 2012 na kufaulu Kidato cha IV kwa
kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja; na
-Mwombaji aliyehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2012 ni sifa ya nyongeza.

B: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA:- MUDA MIAKA 2
UALIMU:- MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII, BIASHARA NA LUGHA.
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2013 na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja.
- Awe mhitimu wa mafunzo mbalimbali katika ngazi ya NTA level 5 kutoka katika chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
1.
Tanbihi: Masomo ya ‘Economics, Basic Applied Mathematics, General Studies, Islamic
Knowledgena Divinityhayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji.

UALIMU: MICHEZO, MUZIKI, SANAA ZA UFUNDI NA SANAA ZA MAONESHO.
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2013 kwa kiwango kisichopungua
‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja kwa kuzingatia masomo yafuatayo kwa kila kozi:-
 Sanaa za Ufundi: masomo ya ‘Fine Art’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha IV masomo ya ‘Biology,
History,  Physics, English, na Civil Engineering’
 Sanaa za Maonesho: masomo ya ‘Thearte Arts’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha IV masomo ya ‘Literature in  English, Kiswahili, Geography na History;
 Muziki: masomo ya ‘Music’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha IV masomo ya ‘English, Kiswahili,
Music, Physics, Geography na History’; na
 Elimu kwa Michezo: masomo ya ‘Physical Education’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha IV masomo
ya Biology, Chemistry, Physics, English’ na Kiswahili.
UALIMU: UFUNDI
- Mwombaji awe amehitimu mafunzo ya FTC kati ya mwaka 2008 na 2013 kutoka vyuo vya Ufundi
Au awe amehitimu mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA level 6 kutoka chuo chochote cha Ufundi
kinachotambulika na Serikali.

UALIMU: KILIMO
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2013 kwa kiwango kisichopungua
Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja katika somo la ‘Agricultural Science’ na ‘Biology’
Au ‘Chemistry’.

UALIMU: SAYANSI KIMU
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2013 na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika masomo ya ‘Biology’,
‘Chemistry’ na ‘Nutrition’.

C:  MAFUNZO YA UALIMU KAZINI NGAZI YA STASHAHADA: MUDA MIAKA 2
UALIMU: MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII, BIASHARA NA LUGHA.
- Mwombaji awe mwalimu wa Daraja A aliyethitimu Kidato cha VI na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua “Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja; na awe na uzoefu wa kufanya kazi
kwa muda wa usiopungua miaka miwili
( 02) Tanbihi: Masomo ya ‘Economics, Basic Applied Mathematics, General Studies, Islamic Knowledgena Divinityhayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji, na
UALIMU: ELIMU MAALUM

(i) Mwombaji awe mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na
uzoefu kazini usiopungua miaka miwili
(02) ; na

(ii) Awe mwalimu wa Daraja A aliyethitimu Kidato cha VI na kufaulu kwa kiwango kisichopungua
“Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja; na awe na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili
(02)
Tanbihi: Masomo ya ‘Economics, Basic Applied Mathematics, General Studies, Islamic
Knowledgena Divinityhayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumudahili mwombaji, na
Mwalimu anayefundisha watoto wenye mahitaji maalum [wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili n.k.

(vithibitisho viambatishwe)
], ni sifa ya nyongeza.
2
D: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI NGAZI YA CHETI: MUDA MWAKA 1
UALIMU: SAYANSI KIMU
- Mwombaji awe mwalimu wa Daraja A na awe na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili
(02) .UALIMU: ELIMU MAALUM
- Mwombaji awe mwalimu wa Daraja A na awe na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili
(02)
- Awe amefaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi: Mwalimu anayefundisha Elimu Maalum hata kama hana mafunzo rasmi ni sifa ya nyongeza

(uthibitisho uambatishwe) .
A)
VIAMBATISHO
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu watume barua za maombi yao kwa njia ya posta. Barua hiyo iwe na
anuani sahihi ya mwombaji
(ya posta, au anuani ya barua pepe) , pamoja na viambatisho vifuatavyo kulingana na aina ya mafunzo:

(i)Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV ,VI na ufundi;

(ii)Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada
(kwa waombaji walioajiriwa)
; na

(iii) Barua zilizopitishwa na waajiri
(kwa waombaji walioajiriwa)
.B)
MAELEZO MUHIMU

(i) Sifa zilizoelekezwa kwa mafunzo ya ualimu ngazi Cheti Daraja ‘A’ni kwa ajili ya waombaji wa
mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali.

(ii)Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2012 waliojaza nafasi ya mafunzo ya ualimu ngazi Cheti Daraja ‘A’kwenye “Seforms” wakati wanamalizaelimu ya sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo kwa njia ya barua na watachaguliwa kwa kufuata vigezo vilivyowekwa.

(iii)Sifa zilizoelekezwa kwa mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wote kwavyuo vya ualimu vya Serikali na vyuo vya ualimu visivyo vya Serikali isipokuwa mwombaji kwa vyuovya ualimu visivyo vya Serikali anaweza akawa amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2003 na 2013.

(iv)Waombaji wa mafunzo ya ualimu aliyeajiriwa apitishe barua ya maombi kwa mwajiri wake.

(v)Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara yaElimu na Mafunzo ya Ufundi: www.moe.go.tz, na OWM-TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz;

(vi)Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa Vyuo ambako
watakuwa wamepangwa kupitia anuani zao sahihi.

(vii)Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM-TAMISEMI:
www.pmoralg.go.tz, kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M)
 na vyuo vya ualimu.
Tanbihi: Kwa waombaji walio Dar es Salaam  wanaweza kufika Wizarani na kutumbukiza barua za maombi
kwenye sanduku lililowekwa mapokezi. Tafadhali barua zote za maombi zitumbukizwe kwenye sanduku la
maombi na si vinginevyo.
MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 10 Mei, 2013.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM
(Aione: Mkurugenzi, Idara ya Elimu yaUalimu)

Thursday, 28 March 2013

OMBI LA TAARIFA ZA KABILA LA WAHEHE



Ndugu Mpendwa,

YAH: OMBI LA TAARIFA MBALIMBALI KUHUSU HISTORIA YA KABILA LA WAHEHE NA WABENA

Rejea kichwa cha habari hapo juu.

Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa heshima na taadhima, unakuomba usaidie kutupa taarifa mbalimbali za Historia ya Wahehe na Wabena ili tuweze kuzitumia wakati wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI, utakaofanyika kwa siku mbili, Kijijini Kidamali, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa; tarehe 29 hadi 30 Juni, 2013. Wakati wa mkutano, pia tutajadili hatua tulizofikia ili kuchapisha kitabu cha Historia ya Wahehe ambacho kipo katika mchakato wa ukusanyaji taarifa, na mada yake itawasilishwa katika mkutano huo na Mwalimu Israel Mposiwa. Huu ni mfululizo wa mikutano ya KAUKI ambayo imekuwa ikifanyika maeneo ya Kidamali mara 3, Irole mara 1, Nduli mara 1, Magubike mara 1, Igowole-Mufindi mara 1 na Dar es Salaam mara 1.
 
Uongozi wa KAUKI unaitambua kazi yako muhimu ya upashanaji habari na thamani yake kwa jamii, na pia nafasi yako katika jamii na ushiriki katika harakati mbalimbali za kupunguza umasikini na kuleta maendeleo kwa kuhabarisha jamii ya Watanzania.

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI yanafanyika katika kanda za Irole, Nduli, Itagumtwa, Mgongo, Idete, Nyamihuu, Kalenga, Wasa, Nyamahana, Ilala Simba, Nzihi, Dar es Salaam, Kidamali, Magubike, Mufindi na kwingineko ambako wanaukoo wanatoka. Maandalizi yanajumuisha michango ya fedha, mazao na mifugo kwa wale ambao hawana fedha, yote ikiwa ni kwa ajili ya kutoa huduma za chakula, maji, uchapishaji wa matini na barua, kabla na siku ya mkutano; na usafiri toka Iringa Mjini hadi Kidamali; na Kidamali hadi Magubike kwa wageni na wenyeji.

Kutokana na uzito wa jukumu hili, uongozi wa KAUKI, pia umeamua kuandika barua rasmi ya kukualika katika mkutano huo. Ratiba na ramani vimeambatanishwa pamoja na barua hii kwa taarifa zaidi.

Mipango ya KAUKI inajikita katika kujiimarisha katika ngazi zote za kiutendaji, kiuendeshaji na kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kielimu, kisiasa, kimaendeleo na kimapinduzi.

Toka mwaka 2005 Mikutano ya KAUKI ilipoanza kufanyika, kumekuwa na mwamko wa hali ya juu kabisa na wanaukoo wengi kutoka maeneo ya Iringa Vijijini na kwingineko wamekuwa wakihudhuria na kujifunza mambo muhimu ya kimaendeleo. Kwa wastani washiriki 160 na 180 toka zaidi ya vijiji 20 Wilaya ya Iringa Vijijini, wamekuwa wakihudhuria katika siku mbili za mkutano na kupata mafunzo mbalimbali kutokana na mada ambazo zimekuwa zikifundishwa.
  
   KAUKI ina malengo mengi, lakini baadhi ya hayo ni pamoja na:
·         Kuchapisha kitabu cha Historia ya Wahehe toleo la Kwanza: Ndani ya kitabu kutakuwa na sehemu zifuatazo: Historia ya Wahehe na Kuibuka kwa Tawala na Koo mbalimbali ndani ya Uhehe (Wanitole, Wahabeshi, Wangazija); Harakati za Mapambano ya Kikabila na Himaya mbalimbali (Vita za Luhota; Mkwawa na Wajerumani; Mkwawa na Mnyigumba; Mkwawa na Wabena, Wasangu na Himaya Mbalimbali; Sehemu ya Pili:  Historia ya Koo za Wahehe: Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule [Mtengelingoma Balama na akina Tagumtwa Kivenule], Vita za Vatawangu na Ushujaa wa Tagumtwa katika Vita; Sehemu ya Tatu: Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI); Mipango na Harakati zake katika kuwakwamua Wanaukoo katika lindi la umaskini, ujinga na maradhi, kutoka zaidi ya Vijiji 25 vya Wilaya ya Iringa Vijijini;
·         KAUKI kuwa na ofisi yake Kijijini Kidamali na pia sehemu nyingine za Kanda zake ili kurahisisha mawasiliano na utekelezaji wa mipango yake;
·         Kuisajili KAUKI na kuwa na mfuko wa kusaidia wanaukoo katika elimu, afya, uchumi na matatizo mengine. Pia kuchukua jukumu la utunzaji na uendelezaji wa historia ya Wahehe pamoja na sehemu mbalimbali za kumbukumbu za mashujaa katika Wilaya ya Iringa Vijijini. Tayari mfuko umeanzishwa na wanaukoo wanaombwa kuuchangia;
·         KAUKI kuwa na sanduku la posta na tovuti. Tovuti (blog) yetu ya muda inapatikana kupitia www.tagumwafoundation.wetpaint.com    
·         KAUKI kufungua Akaunti katika Benki. Akaunti tayari imefunguliwa na inajulikana kwa jina la: KAUKI, Benki ya NMB, Akaunti Namba 6052301709, Tawi la Mkwawa, Iringa Mjini;
·         KAUKI kuwa na vitendea kazi mfano Kompyuta, Printa, Simu, Meza na Viti. Hii inatokana na kuongezeka kwa kazi za KAUKI zinazohusisha kuandika na kuprinti sana. Kusudio la kuchapicha kitabu cha historia ya Wahehe, kinahitaji vitendea kazi kama kompyuta, printa, meza na viti;
·         KAUKI kuanza kutoa elimu mbalimbali kwa wadau wake. Inatoa elimu katika mikutano yake. Elimu hiyo inalenga kuifanya jamii kujitambua, uelewa katika masuala ya kiafya, umuhimu wa elimu, ujasiliamali na kujengeana uwezo kwa kupeana uzoefu katika shughuli za uzalishaji mali ili kupunguza umaskini. Uzoefu unatolewa na wajumbe toka sehemu wanakotoka hususani katika nyanja za uchumi, biashara, kilimo, elimu na uzalishaji mali;
·         KAUKI kubuni na kutekeleza miradi ambayo itawasadia wanajamii. Kwa mfano Irole wamebuni na mradi wa kilimo cha Alizeti na wanakusudia kuuanzisha. Taarifa zaidi zitatolewa kwenye mkutano wa sita wa KAUKI. Jamii nzima tunapenda ijitambue na kutafuta namna ya kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi mfano kilimo cha mazao ya biashara na chakula; na
·         KAUKI kuwa na kitengo cha utaalam, taaluma na ujuzi (teknolojia) ambacho kitafanya shughuli za kuwajengea uwezo wana-KAUKI kupitia elimu, ushawishi, utetezi wa kisera na sheria mbovu; kupunguza umaskini, magonjwa, ujinga na pia kuiletea fedha KAUKI kupitia maandiko ya miradi (project proposal and appraisal), pamoja na miradi mbalimbali ya ujasiamali. Suala hili lipo katika mchakato.

Baadhi ya kueleza hayo machache, napenda kutanguliza shukrani zangu dhati, na natumaini utalikubali ombi letu.
  
   Wako katika kazi,


   Adam Kivenule
   Katibu Mkuu - KAUKI

TANGAZO NA RATIBA YA MKUTANO MKUU WA 9 WA KAUKI






























RATIBA
MKUTANO MKUU WA TISA WA KAUKI

Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu – Kidamali, Iringa: Tarehe 29 Juni 2013

Muda
Shughuli/Jukumu
Wahusika
12.00 – 12.45
Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano

Washiriki Wote

12.45 – 01.15
Kupata Kifungua Kinywa
Washiriki wote
01:15 – 02:00
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili na kupata Vitambulisho
Washiriki wote
02.00 – 02.20
Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI
Mwenyekiti wa KAUKI/Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 9
02.20-02.45
Ufunguzi Rasmi wa Mkutano na Mgeni Rasmi
Mgeni Rasmi
02.45-03.15
Utambulisho baina wa Ndugu na Wageni Waalikuwa
Wote
03.15 - 04.00
Mada I: KAUKI NI NINI? LENGO KUU, MALENGO MAHSUSI, MUUNDO, JUKUMU LA KILA MWANA-KAUKI NA UENDESHAJI WAKE
Washiriki waijadili mada na kutoa mapendekezo
Viongozi wa KAUKI waongoze mjadala wa mada hii.
04.00 – 04:30
Mada II: CHIMBUKO, HISTORIA NA MUUNDO WA UKOO WA KIVENULE
(a). Washiriki wasambaziwe nakala ya muundo wa Ukoo na kisha kuujadili na kutoa mawazo yao katika makundi
(b). Washiriki waijadili mada na kutoa mapendekezo
Mwakilishi toka  Kidamali, Irore, Nduli, DSM na Mtaalam wa Historia na Washiriki
04:30– 05:00

Pumziko la Chai / Kahawa/Maji

Washiriki Wote

05.00-05.45
Mada Inaendelea.
(c). Washiriki waijadili mada na kupendekeza nini kifanyike kutunza kumbukumbu hizo
(d). Washiriki wazijadili njia mbadala za kutunza taarifa zinazohusiana na ukoo
Wawezeshaji na Washiriki wote
04.45-05.05

Kuwasilisha majadiliano katika Makundi

Washiriki wote na Wawezeshaji
05.05-05.30
Majumuisho ya yote yaliyojitokeza katika Mada
Wawezeshaji
05:30 – 06:30
TAARIFA YA UTENDAJI WA KAUKI
1. Mipango na Shughuli zilizokusudiwa kufanywa na KAUKI 2012/2013;
2. Taarifa ya Utendaji kwa Ujumla;
3. Taarifa ya Mahesabu na Fedha; na Mafanikio na Matatizo ya KAUKI
4. Matarajio ya KAUKI 2013/2014
Makamu Katibu Mkuu
Mhasibu
06.30 – 07.00
TAARIFA YA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA KANDA
1. Uhamasishaji
2. Mwitikio wa Jamii inayounda Ukoo
3. Ushirikiano miongoni mwa wanajamii
4. Mafanikio na Matatizo
Viongozi wa Kanda zote
07.00-08.00
CHAKULA CHA MCHANA
Washiriki wote
8:00 – 8:45
KUSOMA RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA SABA WA KAUKI
Kujadili Mapungufu, Kutoa Ushauri, Nyongeza
Kupitisha Ripoti
Katibu Msaidizi
Washiriki wote
08:45 – 09:15
Salaam mbalimbali kutoka kwa Washiriki wa Mkutano Mkuu (Wastani watu 6 na dakika @ 5)
Washiriki wa Mkutano
09:15– 09:45

Pumziko la Chai/Kahawa/Maji

Washiriki wote
09.45 -11:00
Mada III: UZOEFU WA WANAUKOO KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
1.Kidamali/Magubike: Kilimo cha Nyanya /Tumbaku na shughuli nyingine za kiuchumi dakika 25
2. Irole/Nduli/Itagutwa/Mgongo: Uzoefu wa Shughuli za Kiuchumi dakika 25
3. Dar/ Morogoro/ Kilombero / Moshi dakika 15
4. Kalenga, Ifunda, Ilala Simba, Wasa, Idodi na Nyamihuu
Washiriki wote; viongozi wa Kanda au wajumbe watakaochaguliwa kutoa uzoefu wa shughuli hizo za kiuchumi
11.00
KUAHIRISHA MKUTANO
Mwenyekiti wa KAUKI
2:30 – 6:30 Usiku
Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili), vinywaji, kufahamiana zaidi na kubadilisha mawazo
Wanaukoo wote


Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu – Kidamali, Iringa: Tarehe 30 Juni 2013

Muda
Shughuli/Jukumu
Wahusika
12.00 – 12.45
Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano

Wote

12.45 – 01.15
Kupata Kifungua Kinywa
Washiriki wote
01:15 – 02:00
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili
Washiriki wote
02.00-02.45
MADA IV: CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI KAUKI KUJILETEA MAENDELEO
1. Nini kifanyike kwa wana-KAUKI kujiletea Maendeleo?
2. Mnadhani ni vitu gani vipewe Kipaumbele kwa wanaukoo kunufaika na KAUKI!
3. Baadhi ya Malengo ya KAUKI ambayo mnayafahamu mnadhani yatasaidia kuleta mabadiliko? Na ni kwa namna gani? Jadili
4. KAUKI ni sehemu tu ya vikundi vingi vinavyofanya jitihada za kujiinua kiuchumi na kimaendeleo, mnadhani ni changamoto gani tunaipata ukilinganisha na mafanikio au matatizo ambayo yamevipata vikundi vingine? Yajadili na kuyatoa mapendekezo hayo
Wawezeshaji na washiriki wote
Mwenyekiti wa KAUKI
02.45-03.15

Majadiliano katika Makundi : Kila mshiriki ajidiliane na wana kundi kikamilifu na kutoa hoja za msingi za kujenga. Kila hoja ya msingi iwasilishwe ila kila mwanaukoo asikie.

Washiriki wote wagawanyike katika makundi

03.15-03.45
Makundi kuwasilisha hoja kutoka katika makundi

Washiriki wote

03.45-04.30

Majumuisho ya yote yaliyojitekeza katika Mada

Wawezeshaji

04:30 – 05:00

Pumziko la Chai / Kahawa/Maji

Washiriki Wote

05.00-06.00
1.       Kuibuka kwa tawala mbalimbali ndani ya Uhehe (Wanitole, Wahabeshi, Wangazija)
2.       Chimbuko la Koo mbalimbali mkoani Iringa
3.       Mahusiano yaliyopo baina ya koo zilizoibuka wakati wa vita za kikabila na wageni
4.       Mgawanyiko wa Koo katika Mkoa wa Iringa

Washiriki wote na Viongozi wa KAUKI
06.00-07.00
MAHITAJI YA KAUKI NA JINSI YA KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA MAHITAJI HAYO: Huu ni mjadala wa jumla na kila mjumbe wa mkutano anashiriki moja kwa moja kutoa mawazo yake. Katibu na watendaji wengine wa KAUKI wana jukumu ya kuyanakili maswali na majibu yote kwa ajili ya kufanyiwa kazi
Washiriki na Viongozi wa KAUKI
07.00-08.00
CHAKULA CHA MCHANA
Washiriki wote
08:00–08.20
MAJADILIANO YA HOJA MBALIMBALI AMBAZO ZIMEWASIISHWA NA WASHIRIKI WA MKUTANONI
1.        Ndg. Adam Kivenule

08:20 - 8:40
1.        MAJUMUISHO NA TATHMINI YA MKUTANO
2.       MIPANGO NA MIKAKATI YA MBELENI
3.       KUTANGAZWA KWA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA TISA
VIONGOZI WA KAUKI
8:40 - 9:00
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA KAUKI
Washiriki Wote
09.00-09:15
SHUKRANI NA KUFUNGA MKUTANO
UONGOZI MPYA WA KAUKI NA MGENI RASMI
09:15–09:30

Pumziko la Chai/Kahawa/Maji

Washiriki wote
09:30
ZIARA YA KUTEMBELEA MAENEO MBALIMBALI KWA WAGENI WOTE. Maeneo ambayo yatatembelwa ni pamoja na:
Mlafu, nk
Washiriki Wote