Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Friday, 21 September 2012

PICHA ZA MATUKIO KATIKA MIKUTANO YA MHE. MBUNGE KATA YA MAKUBURI

CHADEMA YAZINDUA MISINGI KATA YA MAKUBURI KAMA SEHEMU YAKE YA OPERESHENI YA M4C

Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika ufunguaji wa misingi ya CHADEMA kata ya Makuburi, Jimbo la Ubungo, kama ilivyopigwa picha na mwandishi wetu.


Hapa eneo la River Side ambapo Msingi wa CHADEMA katika Kata ya Makuburi, ulihitimisha ziara ya Mhe. Mbunge Mnyika


Hapa eneo la Ubungo Kibangu Transforma karibu kabisa na Kibangu Medium School and Kanisa la Mzee wa Upako, Anthony Lusekelo, muda mfupi baada ya Mheshimiwa Mbungu kufungua msingi wa CHADEMA

Hapa ni Ubungo Kibangu, Tranforma

Mhe. Mbunge akiwasili katika viwanja vya River Side

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wa Kata ya Makuburi pamoja na Mhe. Mbunge

Alama ya Chama cha CHADEMA ya Vuguvugu la Mabadiliko (Movement for Change)

Mhe. Diwani wa Kata ya Ubungo akiwasalimu wananchi na wanachama wa CHADEMA

Mhe. Mbunge, John Mnyika akiwahutubia wananchi wa eneo la Kata ya Makaburi hasa wakazi wa River Side

Mhe. Mbunge, John Mnyika akiwahutubia wananchi wa eneo la Kata ya Makaburi hasa wakazi wa River Side

Mhe. Mbunge, John Mnyika akiwahutubia wananchi wa eneo la Kata ya Makaburi hasa wakazi wa River Side

Wananchi toka sehemu mbalimbali katika Kata ya Makuburi walijitokeza kumwuliza maswali Mhe. Mbunge, ambapo baadaye aliweza kuyajibu maswali yao.


Carolyn Kivenule hakuwa mbali katika kumsikiliza Mhe. Mbunge, John Mnyika akiwahutubia wananchi wa eneo la Kata ya Makaburi hasa wakazi wa River Side

Mandhari ya eneo la Ubungo RiverSide, mara baada ya kukamilika kwa ukumbi wa kisasa wa Sherehe mbalimbali

Mhe. Mbunge, John Mnyika akiwahutubia wananchi wa eneo la Kata ya Makaburi hasa wakazi wa River Side

M4C JIMBO LA UBUNGO


CHADEMA YAZINDUA MISINGI KATA YA MAKUBURI KAMA SEHEMU YAKE YA OPERESHENI YA M4C

Na mwandishi wetu,

Mheshimiwa John Mnyika, Jumamosi ya tarehe 15 mwezi Septemba 2012, alikuwa na kazi nzito ya kufungua misingi katika Jimbo la Ubungo, hususani katika kata ya Makuburi. Akihitimisha ziara yake ya ufunguzi wa misingi, pamoja na kuhutubia mikutano mbalimbali ya hadhara, huku akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wananchi. 

Mheshimiwa Mnyika aliwaeleza wakazi wa Jimbo la Ubungo kuhusiana na shughuli ambazo wamezifanya toka walipochaguliwa. Akiongozana na Madiwani wa Kata ya Ubungo na Kata ya Makuburi, alitoa fursa kwa wananchi kuuliza maswali mbalimbali ambayo baadaye aliyajibu kikamilifu.  

Mojawapo ya maswali yaliyoulizwa ni pamoja na tatizo la matapeli ambao wapo eneo la daraja la Ubungo, kwenye mitambo ya TANESCO, na jinsi polisi wa wa kituo cha Kata cha Ubungo RiverSide wanavyofumbia macho uhalifu huo na kuwakumbatia wahalifu, na namna watu wanavyotapeliwa na mateli hao.  

Akijibu hoji hiyo, Mhe. Mnyika aliwapa jukumu Madawani kulifuatilia kwa karibu suala hilo na kisha kumfahamisha hatua ambazo zimekwisha chukulia. Akiongezea, alisema, yeye kama Mbunge, anapambana na mtu kama Mkuu wa Jeshi la Polisi, Polisi wa Operesheni Mbalimbali na si polisi wa kituo cha polisi cha Kata.  

Kuhusu ujenzi wa daraja na barabara ya Mabibo External na Ubungo Maziwa, alisema, tayari mipango yote kuhusiana na kuanza ujenzi huo imekwisha kamilika. Kinachosubiliwa ni kuona kama kutakuwa na fungu la kuwalipa fidia watu waliofuatwa na barabara.  

Mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika eneo la Riverside kwenye Kijiwe cha Taksi, Mhe. Mbunge alihitimisha ziara yake kwa kufungua msingi na kupandisha Bendera Mbili.

 

 

 

 

WIKI NENDA KWA USALAMA, CHANGAMOTO INAYOKUA KWA KWA KASI KWA WAENDESHAJI NA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA USAFIRI

Wimbi la ongezeko la ajali za barabarani ni changamoto hususani kwa wadau na vyombo vinavyosimamia usalama barabarani na Wiki ya Nenda kwa Usalama. Kuthibitisha hili, shuhudi baadhi ya matukio ya ajali yaliyotokea sehemu mbalimbali hapa Tanzania.







 

WIKI NENDA KWA USALAMA, CHANGAMOTO INAYOKUA KWA KWA KASI KWA WAENDESHAJI NA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA USAFIRI, MIUNDOMBINU NA WADAU WA USIMAMIZI
 
Angalia mlolongo wa picha zifuatazo kuthibitisha makala

WIKI NENDA KWA USALAMA, CHANGAMOTO INAYOKUA KWA KWA KASI KWA WAENDESHAJI NA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA USAFIRI, MIUNDOMBINU NA WADAU WA USIMAMIZI

WIKI YA NENDA KWA USALAMA HAINA TIJA


WIKI YA NENDA KWA USALAMA HAINA TIJA KATIKA KUPUNGUZA AJALI NA KUONGEZA WELEDI NA UMAHIRI KATIKA KUTUMIA NA KUHUDUMIA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA USAFIRI 

Imekuwa ni kasumba kwa Jeshi la Polisi hususani kitengo cha Usalama Barabarani kuonekana wakiwa barabarani wakiwadhibiti madereva kuhusu zoezi la ukaguzi wa magari na leseni za udereva. Na kwa bahati mbaya ukaguzi wa magari umekuwa ukiegemea zaidi kwenye magari ya abiria na kuacha magari mengine watu binafsi yakiendelea kutembea mitaani.  
Kamanda mkuu kikosi cha usalama barabarani Mohamedi Mpinga akionyesha (waandishi wa habari hawapo pichani) jinsi ya kufungua na kubandika stika maaalum kwaajili ya kampeni ya kudhibiti Usalama barabarani mara baada ya kukabidhiwa stika hizo na wadhamini wao kampuni ya simu za mkononi Airtel na Puma, wanashudia pichani toka kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa airtel Bi Beatrice Singano na Mkurugenzi wa kampuni ya Mafuta Puma bw, Maregesi Manyama, na kushoto ni Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mh, Pereira Ame Silima, wiki ya Nenda kwa usalama mwaka huu kitaifa itafanyika mkoani iringa ikiwa imebeba ujumbe usemao “ Pambana na ajiali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria
Ukaguzi wa vyombo vya usafiri kama magari ni muhimu kwa sababu kuna wamiliki wengine hujisahau na hivyo kushindwa kuchukua hatua za makusudi kuangalia na kuhudumia magari yao. Lakini pia katika ajali za barabarani magari yote huusika, yawe na binafsi au ya usafiri na kwa maana hiyo, sheria lazima izingatiwe sawe kwa vyombo vyote vya usafiri. 

Lakini kwa nini serikali haiweki nguvu yake katika kushughulikia kwa mapana yake Wiki ya Nenda kwa Usalama Tanzania? Ni dhahiri, viongozi hawana mwito au nia ya dhati katika kuhakikisha kuwa roho za watanzania zinalindwa kutokana na wimbi kubwa la ajali za barabarani. Mara nyingi najiuliza ni kwa nini hakuna bajeti maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa watumiaji wote wa barabara na waendesha vyombo vya usafiri na watumiaji wake. Sijawahi kusikia kutengwa kwa bajeti au fungu fulani kwa ajili ya kutoa elimu ya msingi/mahususi kwa watumiaji wa magari, abiria na pia watumia barabara zetu. 

Makampuni baki kwa maslahi yao, ndiyo yameonekana kujitokeza kutoa fedha kiasi na nguo au baadhi ya vifaa kiduchu ambavyo vinatumika wakati wa wiki hiyo moja tu ya nenda kwa usalama. Hii ni kijeli na dharau kwa Watanzania ambao wengi wao wanaendelea kuumia kutokana na lindi kubwa la ajili za barabarani zinazoendelea kutokea kila siku. 

Binafsi naamini kabisa, kama serikali kupitia jeshi la polisi, kitengo cha usalama barabarani wangeelekeza nguvu zake katika kutoa elimu badala ya kujipanga barabarani kula rushwa, ajili nyingi zinazoendelea kutokea, zingekoma kabisa. Madereva na watumia barabara wangepata umahiri katika bahari hii ya usalama barabarani. Elimu pekee ndiyo njia mahsusi ya kujikwamua na taifa hili na vifo na majanga ya ajali. 

Pia, kuendelea kushamiri kwa matatu katika barabara zote za Tanzania ni chanzo kikuu cha ajali. Na hii ni ishara ya kushindwa kwa jeshi la polisi na mamlaka nyingine husika katika kusimamia matumizi bora ya barabara na watumiaji wake. Matuta barabarani yanaendelea kudidimiza uchumi wa Tanzania kutokana na wananchi kulipa fedha nyingi za kigeni kuagiza spea/vipuri vya magari yao. Mtikisiko mkubwa ambao unalipata gari dogo, gari kubwa la mizigo na basi la abiria katika umbali wa kilometa 1000, ni ishara kwamba, katika kipindi cha mwaka mmoja, gari litakuwa limepunguza zaidi ya miaka miwili ya muda wake wa kufanya kazi kwa ufanisi.  

Matuta barabarani si suluhi ya matatizo ya ajali yanayoendelea kutokea katika nchi ya Tanzania. Serikali, polisi na mamlaka nyingine husika, zimeshindwa kabisa kutafuta suluhi ya kuboresha usalama barabara na kuishia kuweka matuta. Hapa ndipo akili za wadau wa usafiri zilipoishia. Hii ni aibu kwa taifa hili, hususani kwa wageni mbalimbali wanaondelea kumiminika Tanzania.

Ukitembelea nchi za wenzetu kuna mambo mengi ya kujifunza, mfano alama za barabarani huweka kwa kutumia mabanga makubwa ambayo hayahitaji mtu kuvaa miyani kuyaona. Na pia huwekwa kila baada ya umbali wa kilometa 1 au 2 huku humu katikati kukiwa na punguza la umbali wa mita mia 200 hadi mia 300 kabla ya tukio halisi ambalo lilikuwa limelengwa. Mfano kupinda kushoto kwenda mji mwingine, ambapo aina ya barabara na idadi ya barabara huashiriwa katika mapango hayo elekezi ya usalafiri.

Tofauti na hapa kwetu, kibao cha kuonesha kuwa unapaswa kutembelea kilometa 50 kwa saa huonekana ghafla tena kwa maandishi madogo sana. Na pengine, unamkuta askari wa tochi amekaa hapo hapo na kusema, umeovaspidi. Hii ni fedheha na ni aibu kwa taifa letu.

Naamini viongozi na watendaji mbalimbali ambao ni wadau wa usafiri na usalama barabarani wanatembea mara kwa mara katika nchi za wenzetu kwa nini hawaji na somo jipya.

Kauli mbinu na fulani hazina tija kwa taifa letu katika tasnia ya usalama barabarani kama kutakuwa hakuna sera na msingi mahsusi katika utoaji elimu na pia kuwaelimisha watumiaji wa barabara, vyombo vya usafiri na vyombo vyenyewe.

WIKI YA NENDA KWA USALAMA


Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mh, Pereira Ame Silima akipokea sehemu ya ya stika maaalum kwa ajili ya kampeni ya Usalama barabarani toka kwa wadhamini wa stika hizo kwa mwaka huu Airtel na Puma, wnaokabidhi toka kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa airtel Bi Beatrice Singano na Mkurugenzi wa kampuni ya Mafuta Puma bw, Maregesi Manyama. Anaeshudia makabidhiano ni kamanda mkuu kikosi cha usalama barabarani Mohamedi Mpinga. Airtel Tanzania na Puma ni wadhamini wakuu wa wiki ya uhameasisaji wa wiki ya Nenda kwa usalama ambapo mwaka huu kitaifa itafanyika mkoani iringa ikiwa imebeba ujumbe usemao “ Pambana na ajiali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria
 
WIKI YA NENDA KWA USALAMA, CHANGAMOTO INAYOKUA KWA KWA KASI KWA WAENDESHAJI NA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA USAFIRI, MIUNDOMBINU NA WADAU WA USIMAMIZI
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta PUMA kwa pamoja wameungana na serikali ya jamuhuri ya Tanzania kwa kupitia baraza la taifa la usalama barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti idadi ya ajali za barabarani nchini.


 Kutangazwa kwa ushirikiano huo kumefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya PUMA ambapo Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Tanzania Kamanda Mohamed Mpinga ametangaza wiki ya nenda kwa usalama barabarani ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Iringa.

Akiongea wakati wa hafla hiyo mgeni rasmi , Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Pereira Ame Silima alisema” nachukua fulsa hii kuwashukuru wadhamini wa kampeni ya usalama barabarani kwa mwaka huu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na Kampuni ya Mafuta ya PUMA kwa kutoa mchango wao wa pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani ”

Ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa nguvu kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila mtanzania kuwa sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za barabarini huku tukiishi na kutimiza kauli mbiu ya mwaka huu “Pambana na Ajali za barabarani kwa vitendo, Zingatia Sheria”.

Nachukua fulsa hii kuwaaasa watumiaji wa vyombo vya moto kupeleka magari yao kukaguliwa na kuthibitishwa ubora wa kutembea barabarani ili kuhakikisha vyombo vinavyotumika kubeba abiria viko salama na vinakidhi viwango vilivyowekwa kuhakikisha usalama barabarani.” aliongeza Silima.

Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “Airtel tunajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya watanzania na mali zao na tunayo dhamira ya kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote wenye wito wa kusaidia usalama barabarani na jeshi la polisi usalama barabarani kupunguza ajali za barabarini kwani ushika hiuu wa Airtel leo ni moja kati ya shughuli za kijamii tunazozifanya nchini.

Nia na madhumuni yetu makubwa ni kusaidia shughuli zinazofanywa na jeshi la polisi kusimamia na kupunguza maokeo ya ajali za barabarani, kila mwaka kuna kunakua na matukio ya ajali za barabarani ambazo zingeweza kuepukika kama wahusika wangekua na elimu ya kutosha. Hii ndio sababu kubwa na madhumini ya Airtel kuwa mmoja ya washiriki wakuu katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha upungufu wa ajali barabarani kwa wa tano sasa.”.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ya PUMA ENERGY Mkurugenzi Mkuu wa PUMA ENERGY ndugu MAREGESI BEN MANYAMA… alisema “tuna malengo makuu matatu kuhusu usalama kazini nayo ni kutokua/kutosababisha ajali, kutoumiza mtu yeyote na kutoharibu mazingira. Sisi tunaamini kuwa Baraza la Usalama Barabarani lina jukumu kubwa na muhimu sana la kupunguza ajali za barabarani.

Hivyo mchango wetu kusaidia juhudi za Baraza, zinaendana sawasawa na malengo yetu ya usalama. Kama huu msaada wetu mdogo utafanikisha kuepusha hata kifo kimoja, sisi tutaona kuwa malengo ya msaada yatakuwa yamefikiwa. PUMA ENERGY wamakuwa wabia wa muda mrefu (kabla ya hapo BP Tanzania) wa masuala ya Usalama Barabarani. Ni nia yetu kwamba tutaendelea kushirikiana na jeshi la Polisi pamoja na wadau wengine kuendelea na mapapambano ya kupunguza ajali nyingi ambazo tunaamini nyingi zinaweza kuzuilika”
Nae kamanda mkuu wa jeshi la usalama Tanzania afande Mohamed Mpinga alisema.”Tunatoa wito kwa watu wote kushirikiana nasi kufanikisha zoezi hili na nimatumaini yetu elimu tutakayoendelea kuitoa kwa wananchi itasaidia katika kupunguza na kudhibiti ajali zinazotoka barabarini nakusababisha maafa makubwa kwa taifa na jamii kwa ujumla. Tunawaomba watanzania wote wahakikishe magari yao yamefanyiwa ukaguzi katika kipindi hiki cha usalama barabarani na rai yetu sio tu kwa wakazi wa Iringa ila pia ni kwa watanzania wote katika mikoa yote nchini.

Airtel kwa mwaka huu imechangia kuchapisha stika, kutoa elimu kwa kupitia vyombo za habari nchini pamoja na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 800 zenye ujumbe wa mwaka huu “Pambana na Ajali za barabarani kwa vitendo, Zingatia Sheria”. Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mallya aliongeza.

Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli za usalama barabarani nchini , kwa miaka 4 mfululizo sasa Airtel kwa kushirikiana na Baraza la Usalama Barabarani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ajali zinadhibitiwa.