WIKI YA NENDA KWA USALAMA, CHANGAMOTO INAYOKUA KWA KWA KASI KWA WAENDESHAJI NA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA USAFIRI, MIUNDOMBINU NA WADAU WA USIMAMIZI
Akiongea wakati wa hafla hiyo mgeni rasmi , Naibu Waziri wa mambo ya
ndani Mheshimiwa Pereira Ame Silima alisema” nachukua fulsa hii kuwashukuru
wadhamini wa kampeni ya usalama barabarani kwa mwaka huu kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel na Kampuni ya Mafuta ya PUMA kwa kutoa mchango wao wa pamoja
na kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani kufikia malengo kwa
kuhakikisha usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani ”
Ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa nguvu
kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila mtanzania kuwa
sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za barabarini huku tukiishi na
kutimiza kauli mbiu ya mwaka huu “Pambana na Ajali za barabarani kwa vitendo,
Zingatia Sheria”.
Nachukua fulsa hii kuwaaasa watumiaji wa vyombo vya moto kupeleka magari yao
kukaguliwa na kuthibitishwa ubora wa kutembea barabarani ili kuhakikisha vyombo
vinavyotumika kubeba abiria viko salama na vinakidhi viwango vilivyowekwa
kuhakikisha usalama barabarani.” aliongeza Silima.
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Beatrice Singano
Mallya alisema “Airtel tunajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya
watanzania na mali zao na tunayo dhamira ya kuhakikisha tunashirikiana na wadau
wote wenye wito wa kusaidia usalama barabarani na jeshi la polisi usalama
barabarani kupunguza ajali za barabarini kwani ushika hiuu wa Airtel leo ni
moja kati ya shughuli za kijamii tunazozifanya nchini.
Nia na madhumuni yetu makubwa ni kusaidia shughuli zinazofanywa na jeshi la
polisi kusimamia na kupunguza maokeo ya ajali za barabarani, kila mwaka kuna
kunakua na matukio ya ajali za barabarani ambazo zingeweza kuepukika kama
wahusika wangekua na elimu ya kutosha. Hii ndio sababu kubwa na madhumini ya
Airtel kuwa mmoja ya washiriki wakuu katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu
itakayofanikisha upungufu wa ajali barabarani kwa wa tano sasa.”.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ya PUMA ENERGY Mkurugenzi Mkuu wa
PUMA ENERGY ndugu MAREGESI BEN MANYAMA… alisema “tuna malengo makuu matatu
kuhusu usalama kazini nayo ni kutokua/kutosababisha ajali,
kutoumiza mtu yeyote na kutoharibu mazingira. Sisi tunaamini
kuwa Baraza la Usalama Barabarani lina jukumu kubwa na muhimu sana la kupunguza
ajali za barabarani.
Hivyo mchango wetu kusaidia juhudi za Baraza, zinaendana sawasawa na malengo
yetu ya usalama. Kama huu msaada wetu mdogo utafanikisha kuepusha hata kifo
kimoja, sisi tutaona kuwa malengo ya msaada yatakuwa yamefikiwa. PUMA ENERGY
wamakuwa wabia wa muda mrefu (kabla ya hapo BP Tanzania) wa masuala ya Usalama
Barabarani. Ni nia yetu kwamba tutaendelea kushirikiana na jeshi la Polisi
pamoja na wadau wengine kuendelea na mapapambano ya kupunguza ajali nyingi
ambazo tunaamini nyingi zinaweza kuzuilika”
Nae kamanda mkuu wa jeshi la usalama Tanzania afande Mohamed Mpinga alisema.”Tunatoa
wito kwa watu wote kushirikiana nasi kufanikisha zoezi hili na nimatumaini yetu
elimu tutakayoendelea kuitoa kwa wananchi itasaidia katika kupunguza na
kudhibiti ajali zinazotoka barabarini nakusababisha maafa makubwa kwa taifa na
jamii kwa ujumla. Tunawaomba watanzania wote wahakikishe magari yao yamefanyiwa
ukaguzi katika kipindi hiki cha usalama barabarani na rai yetu sio tu kwa
wakazi wa Iringa ila pia ni kwa watanzania wote katika mikoa yote nchini.
Airtel kwa mwaka huu imechangia kuchapisha stika, kutoa elimu kwa kupitia
vyombo za habari nchini pamoja na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 800
zenye ujumbe wa mwaka huu “Pambana na Ajali za barabarani kwa vitendo, Zingatia
Sheria”. Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja
atafanya sehemu yake Mallya aliongeza.
Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli za usalama barabarani
nchini , kwa miaka 4 mfululizo sasa Airtel kwa kushirikiana na Baraza la
Usalama Barabarani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ajali zinadhibitiwa.
No comments:
Post a Comment