CHADEMA
YAZINDUA MISINGI KATA YA MAKUBURI KAMA SEHEMU YAKE YA OPERESHENI YA M4C
Na mwandishi wetu,
Mheshimiwa John Mnyika, Jumamosi ya tarehe 15
mwezi Septemba 2012, alikuwa na kazi nzito ya kufungua misingi katika Jimbo la
Ubungo, hususani katika kata ya Makuburi. Akihitimisha ziara yake ya ufunguzi
wa misingi, pamoja na kuhutubia mikutano mbalimbali ya hadhara, huku akijibu
hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wananchi.
Mheshimiwa Mnyika aliwaeleza wakazi wa Jimbo la
Ubungo kuhusiana na shughuli ambazo wamezifanya toka walipochaguliwa.
Akiongozana na Madiwani wa Kata ya Ubungo na Kata ya Makuburi, alitoa fursa kwa
wananchi kuuliza maswali mbalimbali ambayo baadaye aliyajibu kikamilifu.
Mojawapo ya maswali yaliyoulizwa ni pamoja na
tatizo la matapeli ambao wapo eneo la daraja la Ubungo, kwenye mitambo ya
TANESCO, na jinsi polisi wa wa kituo cha Kata cha Ubungo RiverSide
wanavyofumbia macho uhalifu huo na kuwakumbatia wahalifu, na namna watu
wanavyotapeliwa na mateli hao.
Akijibu hoji hiyo, Mhe. Mnyika aliwapa jukumu
Madawani kulifuatilia kwa karibu suala hilo na kisha kumfahamisha hatua ambazo
zimekwisha chukulia. Akiongezea, alisema, yeye kama Mbunge, anapambana na mtu
kama Mkuu wa Jeshi la Polisi, Polisi wa Operesheni Mbalimbali na si polisi wa
kituo cha polisi cha Kata.
Kuhusu ujenzi wa daraja na barabara ya Mabibo
External na Ubungo Maziwa, alisema, tayari mipango yote kuhusiana na kuanza
ujenzi huo imekwisha kamilika. Kinachosubiliwa ni kuona kama kutakuwa na fungu
la kuwalipa fidia watu waliofuatwa na barabara.
Mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika eneo la
Riverside kwenye Kijiwe cha Taksi, Mhe. Mbunge alihitimisha ziara yake kwa
kufungua msingi na kupandisha Bendera Mbili.
No comments:
Post a Comment