GHARAMA YA DHULUMA NI HOFU
Spika yapaswa utende haki kwa kuzingatia sheria na kanuni za Bunge
Katika
hali ya kuwa na hofu kutokana na yaliyojitokeza katika Bunge la hivi karibuni,
Spika wa Bunge, Anne Makinda ameongezewa ulinzi pamoja na kubadilishiwa namba
za gari analotumia kutokana na vitisho anavyovipata kutoka kwa wananchi ambao
wamekuwa wakimtumia ujumbe wa simu.
Ni vyema
ndugu Makinda akajiuliza hii hofu ya kuongezewa ulinzi inatokana nini, kwa
sababu hali haikuwa hivi siku za nyuma. Kuna msemo wa kidini ambao unasema
kuwa, "Gharama ya Dhambi ni Mauti". Lazima ndugu Makinda atambue kuwa
anachowafanyia Wabunge wa upinzani Bungeni, pia anawafanyia wananchi
waliowatuma wabunge hao.
Kwa hiyo,
kama wawakilishi wa wananchi hawa maskini wanakwazwa na mtu mmoja au wawili
kuwasilishwa kilio cha wananchi walio wengi kwa sababu zisizo za msingi, na atambue
kuwa anatenda dhambi ya dhuluma. Na mara nyingi dhuluma ya wengi ni msiba na
pia ni hatari sana.
Kitendo
cha Wabunge wa Upinzani kuamua kutoa namba za simu za Spika na Naibu wake kwa
wananchi, ilikuwa ni kuwashtaki na wategemee kupokea simu au ujumbe ambao
hautakuwa na lugha njema kwao kwa sababu wamedhulumiwa sehemu ya haki zao.
Tatizo la
elimu na maji si geni kwa Watanzania walio wengi maskini. Maji yamekuwa
yakitoka sehemu ambako wakubwa na watu wenye hadhi na uwezo wanakoishi. Sehemu
ambazo wanaishi walalahoi ambao Mhe. Mnyika alikuwa anawasemea, hamna maboma na
pengine hayapo kabisa. Kwa kifupi, matatizo ya elimu na maji yanawagusa moja
kwa moja wananchi wa kawaida.
Kuendelea
kuporoka kwa kiwango cha elimu ni kikwazo kikubwa kwa watanzania walio wengi
kwa sababu kunawanyima fursa watoto wao kuendelea mbele kielimu na kuishia
mitaani na kuharibikiwa. Endapo mfumo wa elimu ungekuwa ni mzuri, wananchi
walio wengi maisha yao yangekuwa yameboreka kwa sababu kuongezeka kwa fursa kwa
watoto waliosomo.
Watoto wa
hao viongozi ambao wanapinga hoja za msingi za matatizo yanayowakabili
wananchi, wanasomo nje ya nchi au kwenye shule zenye hadhi ya juu hapa
Tanzania. Wao wana uwezo wa kulipa mamilioni ya pesa ili watoto wao wafanikiwe
kielimu. Lakini kwa mtoto wa Maskini hali ni tofauti kwa sababu yeye anaendelea
kusota kwenye shule za Kayumba ambazo hazina walimu, vifaa wala tija kwa maisha
ya sasa ya kidijitali.
Kwa hiyo,
ulinzi wa Spika upo kwa wananchi wenyewe na siyo polisi. Ni vyema Mhe. Makinda
akaondoa tofauti na upendeleo ambao amekuwa akiuelekeza kwa upande wa serikali
na kurudi kwa wananchi. Natumaini mahusiano mazuri baina ya makundi haya mawili
yatarudi na kuwa kama zamani. Kumbuka siku zote kuwa, "Mshahara wa Dhambi ni Mauti".
No comments:
Post a Comment