Kweli Naibu Spika ameshindwa kabisa kulimudu Bunge letu. Angalia video hii
Bunge lachafuka
*Wabunge wapiga kelele, wamzomea Naibu Spika
*Bunge lalazimika kuahirishwa kabla ya wakati
NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai, jana alilazimika kuahirisha Bunge kabla ya wakati. Tukio hilo la aina yake, lilitokea jioni, baada ya kutokea hali ya kutoelewana kati ya wabunge wa upinzani na wapande wa CCM.
Dalili za Bunge kuvunjika zilianza mapema, baada ya wabunge kuingia bungeni katika kipindi cha jioni wakati Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, alipowasilisha hoja yake kwa dakika 25 badala ya 15 zinazoruhusiwa kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.
Kutokana na Profesa Maghembe kutumia muda mwingi unaodaiwa kwenda kinyume cha kanuni za Bunge, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) alisimama na kuomba Mwongozo wa Spika, akionyesha kutoridhishwa na muda aliotumia Profesa Maghembe.
Katika maelezo yake, mbunge huyo alisema Profesa Maghembe alitakiwa kutumia dakika 15 na siyo zaidi ya hapo.
Baada ya Lissu kujenga hoja hiyo, Naibu Spika, alikiri Profesa Maghembe kutumia muda mwingi, lakini akajitetea kwamba kosa hilo limesababishwa na makatibu wa Bunge na kwamba waliteleza katika hilo.
Pamoja na kukiri kosa hilo, alimruhusu Profesa Maghembe aendelee kuwasilisha hoja yake kwa dakika tatu zaidi ili amalizie alichokuwa akikiwasilisha.
Baada ya Naibu Spika kusema hayo, wabunge wa upinzani waliokuwa wakiongozwa na Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, walisimama na kuanza kuzomea wakionyesha kutoridhishwa na uamuzi wa Naibu Spika.
Hali ilipokuwa hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, alisimama kutoa mwongozo, lakini hakusikilizwa, kwa kuwa wakati huo Bunge lilikuwa limetawaliwa na kelele. Kutokana na hali hiyo, aliamua kukaa kwa kuwa hakukuwa na hali ya utulivu.
Wakati wabunge wakipiga kelele, Naibu Spika alikuwa amekaa kimya kwa muda wa dakika zipatazo mbili, kisha akasimama na kuahirisha Bunge.
Hata hivyo, wakati kelele hazijazidi bungeni, Naibu Spika kabla hajaahirisha Bunge, alisikika akiwataka wabunge wanaotaka kujadili hoja ya Waziri wajiorodheshe.
Baada ya Bunge kuahirishwa, Naibu Spika pamoja na Lissu alikutana nje ya Ukumbi wa Bunge na kuanza kunyoosheana vidole, wakitoleana maneno yasiyofaa.
Naibu Spika azungumza
Naibu Spika, Job Ndugai, alipozungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Bunge, alitetea uamuzi wa kumzidishia muda Profesa Maghembe, kwa kuwa hoja yake ndiyo iliyokuwa ikitakiwa kujadiliwa.
Jaji Werema anena
Naye Jaji Werema aliwaambia waandishi wa habari, kwamba kilichotokea bungeni siyo jambo la ajabu kwa mabunge yenye mfumo wa vyama vingi.
“Alichofanya Naibu Spika kilikuwa sahihi kwa sababu kanuni zinasema kama kuna hoja mbili zinazohitaji kujadiliwa, ile ya Serikali ndiyo inapewa umuhimu wa kwanza.
“Kanuni ziko wazi, kwamba Mbunge yeyote anaweza kusimama na kutoa hoja, lakini ile ya Serikali lazima ipewe kipaumbele kwanza, lakini hilo halikukubaliwa ndiyo maana ya songombingo mliyoona pale.
“Katika hili, hatuwezi kukwepa, kwani hii siyo mara ya kwanza jambo kama hili kutokea. Mimi nilisimama ili nitoe angalizo, kwamba hoja zote mbili, ile ya Mnyika na ya Waziri Maghembe, zote zinaweza kujadiliwa kwa pamoja, lakini hawakukubali, waliendelea na vurugu.
Mnyika anasemaje?
Kwa upande wake, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, aliwaambia waandishi wa habari, kwamba, hoja yake ilikataliwa na Naibu Spika tangu awali.
“Utaratibu haukufuatwa tangu mwanzo, mliona nilikatazwa kuingiza marekebisho ya hoja zangu, ingawa walizipokea tangu jana na lengo lao lilikuwa kuzuia hoja iondolewe,” alisema Mnyika.
Awali Mnyika aliwasilisha hoja binafsi akitaka upatikanaji wa maji uwe sehemu ya hitaji muhimu la binadamu.
Kwa mujibu wa Mnyika, kama maji salama yakipatikana, umasikini utapungua kwa kuwa ukosefu wa maji salama nsiyo unaochangia umasikini huo.
Kuhusu Jiji la Dar es Salaam, alisema hadi kufikia mwaka 2011, lilikuwa likikadiriwa kuwa na watu wapatao milioni nne hadi tano, lakini halina maji ya uhakika.
Akijenga hoja yake, alisema upatikanaji huo wa maji baada ya uhuru mwaka 1968 ulikuwa asilimia 68, lakini miaka 50 baadaye upatikanaji huo umekuwa asilimia 55 tu tena ya mgawo.
Kutokana na hali hiyo, aliitaka Serikali ishughulikie mpango wa dharura wa kupunguza kero ya maji uliowekwa na Wizara ya Maji, kwa kushirikiana na DAWASA tangu Juni 2010.
Pamoja na hayo, aliahidi kukata rufaa dhidi ya kiti cha Spika, baada kuzuiwa kuingiza maneno mengine katika hoja yake aliyokuwa akiiwasilisha.

No comments:
Post a Comment