Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa13 wa KAUKI

Wednesday, 9 January 2013

RASLIMALI YA GESI MTWARA

MKANGANYIKO NAMNA YA KUNUFAIKA NA RASLIMALI WALIGUBIKA TAIFA

§   Wazawa zinakotoka Raslimali hizo wanufaike kwanza, kisha baadaye maeneo mengine 

Taifa limekumbwa na mgawanyiko mkubwa wa namna ya kunufaika na raslimali zinazopatikana hapa nchini. Uzoefu unaonesha kuwa, watanzania wengi bado hawajanufaika kikamilifu na raslimali za asili zinazopatikana kutoka katika maeneo yao. Maandamano yaliyofanywa na wananchi kutoka Mkoa wa Mtwara, ni mfano tosha kuonesha kilio chao cha muda mrefu cha kushindwa kunufaika na raslimali, hali ambayo wenye mamlaka na watunga sera inabidi wajifunze. 

Mkoa wa Mtwara, Lindi na Pwani imekuwa ni maarufu kwa kilimo cha Korosho, zao la biashara ambalo limechangia kwa kiwango kikubwa mapato ya kigeni. Korosho yenyewe haijawanufaisha kabisa wakazi wa mikoa hiyo na hususani Mtwara ambayo ilikuwa bado iko nyuma kielimu, kimiundombinu na kimaendeleo. Watunga sera na serikali kwa ujumla waliingilia kwa kiasi kikubwa kupitia Bodi ya Korosho kusimamia soko na uuzaji wa zao la Korosho. Matokeo ya udhibiti wa soko uliofanywa na serikali umeendelea kuwadidimiza wakulima hao na pia kudidimiza zao la biashara la Korosho na hivyo kuwasabishia machungu makubwa na umaskini. 

Waswahili wana msemo huu, "Uking'atwa na Nyoka, hata ukiguswa na ujani unashtuka". Wananchi wa Mtwara tayari wameng'atwa na nyoka kupitia zao la biashara la Korosho. Kwa sasa hawana imani tena na watunga sera na wasimamizi wa sera hizo. Wananchi hawa wana kilio cha kushindwa kunufaika na zao la Korosho na matokeo yake kuendelea kuwa masikini. 

Tofauti na ilivyotegemewa wengi, kuwa kwa sababu zao la Korosho bado lipo kwenye soko tofauti na zao la Kahawa na Pamba katika Mikoa ya Kilimanjaro, Kagera na Mwanza ambalo limekufa kabisa; ilibidi hali yao ya kiuchumi iwe juu.  Umasikini ni somo kwao. Wamelitambua tatizo walilonalo na pia wamejitambua. Ndiyo maana kwa sasa wameshikamana kuhusiana na mustakabali wa Gesi na Mafuta ambayo yamegundulika katika pwani ya Mnazi Bay, katika Mkoa wa Mtwara. 

Kwa nini wananchi hawa wanadai kuwa wa kwanza kunufaika na raslimali hii? Hii inatokana na mifano mbalimbali ambayo wanayo kutoka mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Arusha, Kagera na Mara ambapo mikoa hii ilikuwa maarufu kwa uchimbaji wa Dhahabu, Almasi na Tanzanite. Je ni kwa kiwango gani mikoa hii imenufaika na raslimali hizo? 

Kwa upande wa Arusha huko Mererani Wilaya ya Simanjiro ambayo ni mtoaji wa Tanzanite pekee duniani, bado kabisa haijanufaika kikamilifu na raslimali hiyo. Wananchi wake bado ni maskini wa kupindukia. Madini ya Tanzanite yanapoteza umiliki wake halali kiasi cha nchi ya Kenya na Afrika Kusini kutawala soko la Tanzanite. Wananchi wa Mtwara wameyaona haya na ndiyo maana waliandamana kudai kunufaika na Gesi.  

Tanzanite imekuwa na mchango mdogo sana katika pato la Taifa licha ya kuwa ni madini pekee duniani yanayopatikana katika nchi ya Tanzania pekee. Hakuna usimamizi wa kina na mapato au bidhaa zinazotokana na raslimali hii. Mwekezaji mgodini hapo yaani Tanzanite One mkataba wake umeisha, lakini akapewa tena mkataba tata ambao wawakilishi wa wananchi wamepiga kelele sana huko bungeni lakini hawakusikilizwa. Wananchi wanaoishi kuzunguka katika migodi hii ni maskini wa kutupwa na wameangukia katika lindi la migogoro isiyoisha na hata wakati mwingine kupoteza maisha yao. Hili ni somo kwa wana Mtwara. 

Mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Mara ilijaliwa kuwa na raslimali ya Dhahabu na Almasi. Matokeo ya kuwepo kwa raslimali hizo imesababisha mfarakano na vifo kwa wakazi wa mikoa hiyo. Kwa mfano katika Mgodi wa North Mara, wananchi wengi wamepoteza maisha kutokana na kuchafuliwa kwa mazingira na sumu, kuuawa na askari (kupigwa risasi) wakati wanapoenda kuokota mabaki ya mawe yaitwayo Magwangwala ambayo wanafikiria wakiyasaga wanaweza kupata kiasi kidogo cha madini ambayo wakiuza wanakidhi mahitaji yao; kuachiwa mashimo yasiyo na kitu, kupoteza mifugo kutokana na sumu; kuchafuliwa maji kutokana na kemikali zinazozagaa ovyo kwa sababu ya kushindwa kudhibiti uharibifu wa mazingara na pia kuangukia katika wimbi la umaskini. Wananchi hawa pia walizuiwa kushiriki katika uchimbaji mdogo mdogo wa madini ambao ungewasaidia kupata kipato na kuweza kupunguza umaskini, kusomesha watoto na pia kuzihudumia familia zao.  

Kama ilivyo kwa mgodi wa North Mara, huko Geita hali haikuwa tofauti  kwa sababu wananchi walihamishwa katika maeneo yao na kuachwa bila makazi. Baadhi ya vijana walifukiwa mashimoni katika maeneo ambayo walikuwa wanachimba dhahabu. Wachimbaji wadogo waliondolewa na kukosa kabisa eneo la kutafuta riziki yao. 

Kwa taarifa za sasa Ndugu Abrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM alitumia madaraka yake vibaya alipowapelekea wananchi wanaoishi karibu na mgodi wa GGM leseni tano za uchimbaji mdogo, badala ya shughuli hiyo kufanywa na wizara husika. Kitendo hiki kinatafsiriwa kuwa CCM inawajali wakaazi hao kuliko wizara husika yenye dhamana hiyo. 

 Hali kama hii pia iliukumba mgodi wa Bulyahulu ambapo kuna vijana wengi walifukiwa ndani ya migodi kwa kuelekezewa maji ya mvua. Uhamishwaji usiofuata taratibu na ukatili wa kila aina ulifanyika kwao. Matokeo yake wamebaki na wanaendelea kuwa masikini katika nchi yao yenye neema.  

Katika mkoa wa Kagera, Mwanza na Mara hali imendelea kuwa hivyo hivyo kama ilivyo mikoa mingine yenye raslimali. Kwa mfano wakazi wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria wameendelea kukosa kabisa haki ya kupata kitoweo cha samaki. Wameendelea kula mikia na vichwa maarufu kama mapanki huku minofu ikisafirishwa nje ya nchi. Bei ya samaki ni kubwa mno kiasi kwamba mwanachi maskini wa kawaida hawezi kumudu kumnunua samaki mmoja.  

Wananchi wa mikoa hiyo walikuwa na uvuvi wao wa asili huku wakilinda na kutunza mazingira ya ziwa hilo, lakini wawekezaji walikuja na jina lao, wanaitwa wavuvi haramu. Humo ziwani kuna aina nyingi ya samaki ambao wote waliliwa na Sangara aliyepandikizwa humo na kuua vizazi vya samaki asili wa ziwa hilo; lakini serikali inasimamia Sangara tu aina nyingine haitambuliwi kabisa. Ikumbukwe kuwa humo ziwani kuna aina ya samaki ambao hata wakiwa na miaka kumi hawakui kufikia inchi mbili. 

Hali kadhalika katika mgodi wa Almasi huko Shinyanga hali ya umaskini kwa wakazi wanaoendelea kuzunguka machimbo hayo ni kubwa na ya kutisha licha ya uchimbaji kuendelea kufanyika kwa takribani miaka 32. 

Wana Mtwara wasibezwe, waungwe mkono kwa sababu wamejitambua na huu ndiyo wajibu wao. Kisingizio cha kusema kuwa raslimali ziwanufaishe wananchi wote hii ni sawa lakini wenye nacho wapewe kipaumbele, kwa sababu hata maendeleo baina ya mikoa yametofautiana na hii ni sababu tosha.  

Pamekuwepo na kujipendelea kwa baadhi ya viongozi wanaopata fursa katika Baraza la Mawaziri kuelekeza uwingi wa raslimali katika mikoa, wilaya na kata zao. Mfano pekee ambao ninaoukumbuka ni kipindi ambapo Ndugu Basil Mrambo alipokuwa Waziri wa Fedha ambapoweza kutenga kiasi cha shilingi bilioni 9 katika barabara ya hadhi ya kata, kipindi hicho mikoa mingine ikishindwa kuunganishwa na barabara ya lami. Huu ni mfano mdogo lakini kuna mifano mingi.

Wana Mtwara pengine wameangalia asilimia ya fursa ambazo wamezipata wananchi kutoka katika mkoa huo katika vikao vya kufanya maamuzi pamoja na kutunga sera. Kunyimwa kwa fursa hizo za kufanya maamuzi pengine zimechangia kuifanya iendelee kuwa nyuma kimaendeleo.  

Uamuzi wa sasa wa kung'ang'ania kujenga bomba la gesi kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuzalisha umeme si la busara kabisa na ndiyo maana wakazi wa Mtwara wamelipinga. Kiasi cha Trilioni Moja kilichobajetiwa kujenga bomba, ni vyema kingetumika kununua mitambo ya kuzalisha umeme na kujengwa mkoani Mtwara. Hii itasaidia kuleta maendeleo katika mkoa wa Mtwara huku ikitoa changamoto ya kuwa na Kiwanda Kikubwa (Big Power Plant) ambazo itazalisha umeme ambao utaunganishwa kwenye gridi ya Taifa toka huko huko Mtwara. 

Pia siyo vyema na salama kila kitu kujengwa Dar es Salaam maana yanaweza kutokea maafa kama vita au mafuriko ya bahari ikizingatiwa kuwa Dar es Salaam ipo pembezoni mwa bahari. Ni vyema tukawa na maeneo mengi ambayo yana mitambo ya umeme tukaepuka nchi kuwa gizani kwa kuwa na chanzo kimoja kwenye umeme. Angalia hata viwanja vya ndege mbona vimejengwa maeneo mengi nchini siyo tu Dar, hii inasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu. 

Mwisho wa maoni yangu. 

 

Imeandaliwa na:

Adam Kivenule

0713270364

kivenule@gmail.com

Tanzia

TANZIA

Enzi za uhai wakeUmoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) Kanda ya Dar es Salaam, kwa masikitiko makubwa, unawatangazia ndugu, jamaa na marafiki, Kifo cha Flomina Pangalasi Kivenule, kilichotokea siku ya Ijumaa ya tarehe 28 Desemba 2012, saa tano asubuhi katika hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa Marehemu Flomina amefariki kutokana na tatizo la upungufu wa damu ambapo kwa tarehe 24 Desemba tatizo lake lilipogundulika.

Mipango ya mazishi inafanywa na ndugu wa marehemu nyumbani kwake, Mbezi Inn.
 

Mwenyezi Mungu Ametoa, Pia Ametwaa, Jina la Mungu lihimidiwe, Amina.


Imeandaliwa na Kutolewa na:



Adam Kivenule
Katibu - KAUKI

SAFARI YA MWISHO YA FLOMINA KIVENULE

MAZISHI YA MAREH FLOMINA KIVENULE

 enzi ya uhai wakeHuko nyumbani kwa marehemu, Ibada fupi ya kumwombea ilifanyika, pamoja na kutoa heshima za mwisho kwa ndugu, jamaa na marafiki waliojumuika nyumbani hapo. 

Hatimaye, mwili wa Marehemu Flomina Kivenule ulisafirisha siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Desemba 2012 kwenda Kijijini kwa Mumewe Mbuta huko Igula Mkoani Iringa. Awali kabla ya mwili huo kusafirishwa, kulikuwa na mipango ya ama kumzika Ilula au hapa Jijini Dar es Salaam.

Mume wa Marehemu aliiomba familia ya upande wa marehemu kumruhusu kwenda kumzika mpendwa wake huko kwao Kijijini Igula. Ombi la Mume wa marehemu lilikubaliwa na hivyo safari kuelekea Iringa kuanza mnamo wa saa moja kasoro jioni.

Huko Iringa, mwili wa marehemu uliwasili majira ya saa moja asubuhi ambapo ndugu mbalimbali wa marehemu kutoka Ilula, Magubike na Kidamali walipata fursa ya kushirikiana na ndugu wengine waliotoka Dar es Salaam katika kumsindikiza Flomina Kivenule katika safari yake ya milele.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.

Imeandaliwa na:


Adam Kivenule

Katibu - KAUKI


PICHA ZA KUMBUKUMBU ZA MAREHEMU FLOMINA KIVENULE

Hizi ni baadhi ya kumbukumbu za Mareh Flomina Kivenule katika uhai wake. Matukio mengine ya picha yataletwa.



Marehemu Flomina Kulia ambaye ni shangazi yake na Lemija Mkini Kushoto wakati wa vikao vya harusi vya ndugu Adam Alphonce Sigatambule Kivenule, Chonya Inn, Ubungo Riverside Jijini Dar es Salaam


Marehemu Flomina Kulia ambaye ni shangazi yake na Lemija Mkini Kushoto wakati wa vikao vya harusi vya ndugu Adam Alphonce Sigatambule Kivenule, Chonya Inn, Ubungo Riverside Jijini Dar es Salaam

SHUKRANI KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI

SHUKRANI KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KATIKA MSIBA WA MAREH. FLOMINA PANGALASI KIVENULE
Katibu Mkuu - KAUKI
Kwa niaba ya Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) na wanaukoo kwa ujumla, naomba kutumia fursa hii kuwashukuru wote walishiriki kikamilifu katika kumwuguza na hatimaye kufanikisha mazishi ya Marehemu Flomina Pangalasi Kivenule, aliyefariki siku ya Ijumaa ya tarehe 28 Desemba 2012 katika Hospitali ya Ocean Road iliyopo Jijini Dar es Salaam. 
Uongozi unaamini kuwa jitihada kubwa zilizofanyika kwa pande zote katika kuhakikisha kuwa, mgonjwa anapata huduma kama inavyopaswa na pia kuhakikisha kuwa anafanyiwa mazishi yenye heshima baada ya kifo chake. 
Kuna changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika msiba huu na pia ni funzo kwa wengine. Kama Mola anavyowaasa binadamu kuwa hawajui saa wala siku Bwana Mungu atakapokuita. Ni vyema tukandaa nafsi zetu katika matendo mema ya kumpendeza kila mmoja wetu. 
Mazishi yalifanyika vizuri huko Igula-Iringa kama ilivyopangwa (yaani Jumapili ya tarehe 30 Desemba 2012) na pia baada ya mazishi, wazazi wa marehemu walipeleka msiba kwao Ilula, Iringa ili pia jamii ambayo haikupata fursa ya kushiriki Dar es Salaam na Igula ipate nafasi ya kuwafariji wafiwa. 
KAUKI inawashukuru wanakikundi cha Umoja wa Watu wa Igula ambao walifanikisha upatikanaji wa huduma ya gari la kusafirisha mwili pamoja na sanduku la kuhifadhi mwili wa marehemu. 
KAUKI pia inawashukuru majirani wa Mbezi Inn nyumbani kwa marehemu kwa moyo wao mwema na wa ukarimu waliouonesha katika kuwahudumia wageni mbalimbali pamoja na wafiwa. Bila kuwasahau ndugu, jamaa na marafiki kwa uvumilivu wao hadi hatua ya mwisho ya kuuaga mwili kabla ya kusafirisha Iringa.
Kwetu hili ni somo kubwa na kuhaadi kuyachukua mazuri yote kwa faida ya kizazi kijacho.
Mwenyezi Mungu Awalinde, Amina. 
Imeandaliwa na:
 
Adam Kivenule
Katibu - KAUKI
 
Picha za Matukio Siku ya Msiba
Akina mama wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya geneza lenye mwili wa Flomina Kivenule
Akina mama wakiendelea wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya geneza lenye mwili wa Flomina Kivenule
Akina mama wakiendelea wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya geneza lenye mwili wa Flomina Kivenule

LILIAN KIVENULE AAGWA

LILIAN IGNUS KIVENULE AAGWA NA FAMILIA YAKE


Usiku wa tarehe 02 ya mwezi Januari mwaka 2013, ulikuwa wa aina ya pekee kwa Familia ya Lilian Ignus Pangayena Kivenule, pale binti yao mpendwa Lilian alipoagwa na wazazi wake, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika ukumbi wa Kanisa la Yesu Mfalme, lililopo Tabata, Jijini Dar es Salaam.

Lilian Ignus Pangayena Kivenule
Lilian Kivenule akikata keki katika moja ya sherehe zake kabla ya kuagwa siku ya tarehe 02 Januari 2013 katika Ukumbi wa Yesu Kristo Mfalme, Tabata Jijini Dar es Salaam

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa familia yake ambayo imemlea hadi kufikia hatua hiyo muhimu ya kupata mwenzake wa kushirikiana katika shida na raha katika siku zao za maisha hapa duniani.




Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) unawatakia kila la kheri katika maisha yao mapya. Mwenyezi Mungu awazidishie pale panapopungua.

Kwa picha za matukio katika siku hiyo, angalia links hizi hapa kutoka facebook

http://www.facebook.com/photo.php?fbid=520831541294309&set=at.517995654911231.124811.100001024023552.100001498014794&type=1&theater

http://www.facebook.com/photo.php?fbid=454121264647803&set=a.205615882831677.48963.100001498014794&type=1&theater

Lilian Ignus Pangayena Kivenule
Lilian Kivenule akipongezwa na marafiki siku ya Kuagwa kwake katika ukumbi wa Yesu Kristo Mfalme


Lilian Ignus Pangayena Kivenule
Liliani Kivenule akimkaribisha mmewe mtarajiwa kwenda kupata chakula siku ya sherehe ya kuagwa kwake, katika ukumbi wa Kanisa la Yesu Kristo Mfalme, Tabata Jijini Dar es Salaam

Asante,




Imeandaliwa na:




Adam Kivenule

Katibu - KAUKI

Monday, 29 October 2012

Mikasa ya Soko Kuu la Mwanjelwa

Ni mwaka wa tatu sasa toka Soko la Mwanjelwa lianze kujengwa upya baada ya ajali ya moto iliyowapatia hasara kubwa wafanyabiashara wa Mbeya kwa kuunguliwa bidhaa na mazao mbalimbali ya biashara, yaliyokuwemo katika soko hilo.

Wengi wao walitarajiwa kuwa ujenzi wa soko ungeenda haraka kutokana na umuhimu na mahitaji makubwa ya soko hili kwa wakazi wa Mbeya, mikoa ya karibu na nchi jirani za Zambia na Malawi.

Hali imekuwa tofauti kwa sababu sasa ni mwaka wa tatu tangu ujenzi uanze huku shauku kubwa kwa wafanyabiashara ikilitaka liishe mapema na waingie kuendeleza biashara zao.

Mkoa wa Mbeya ni Jiji linalokua kwa kasi na matarajio wengi kuboreka kwa miundo mbinu na masoko ya biashara kama kichocheo cha uchumi.

Je, pamoja na jitihada mpya ya kulijenga soko hili, je litaweza kumudu majanga ya moto ambayo yamekuwa yakilikumba soko hilo mara kwa mara. Hili ndilo swali kubwa ambalo linapaswa kuulizwa na kila mmoja wetu mpenda maendeleo. Tusubili tuone mara baada ya kukamilika na kuanza kutumika.

Zifuatazo ni baadhi ya picha zilizopigwa kuonesha ujenzi wa Soko la Mwanjelwa ukiendelea....