SHUKRANI KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KATIKA MSIBA WA MAREH. FLOMINA PANGALASI KIVENULE
Kwa niaba ya Uongozi wa Umoja wa
Ukoo wa Kivenule (KAUKI) na wanaukoo kwa ujumla, naomba kutumia fursa
hii kuwashukuru wote walishiriki kikamilifu katika kumwuguza na hatimaye
kufanikisha mazishi ya Marehemu Flomina Pangalasi Kivenule, aliyefariki
siku ya Ijumaa ya tarehe 28 Desemba 2012 katika Hospitali ya Ocean Road
iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Uongozi unaamini kuwa jitihada kubwa
zilizofanyika kwa pande zote katika kuhakikisha kuwa, mgonjwa anapata
huduma kama inavyopaswa na pia kuhakikisha kuwa anafanyiwa mazishi yenye
heshima baada ya kifo chake.
Kuna changamoto mbalimbali
zilizojitokeza katika msiba huu na pia ni funzo kwa wengine. Kama Mola
anavyowaasa binadamu kuwa hawajui saa wala siku Bwana Mungu
atakapokuita. Ni vyema tukandaa nafsi zetu katika matendo mema ya
kumpendeza kila mmoja wetu.
Mazishi yalifanyika vizuri huko
Igula-Iringa kama ilivyopangwa (yaani Jumapili ya tarehe 30 Desemba
2012) na pia baada ya mazishi, wazazi wa marehemu walipeleka msiba kwao
Ilula, Iringa ili pia jamii ambayo haikupata fursa ya kushiriki Dar es
Salaam na Igula ipate nafasi ya kuwafariji wafiwa.
KAUKI inawashukuru wanakikundi cha
Umoja wa Watu wa Igula ambao walifanikisha upatikanaji wa huduma ya gari
la kusafirisha mwili pamoja na sanduku la kuhifadhi mwili wa marehemu.
KAUKI pia inawashukuru majirani wa
Mbezi Inn nyumbani kwa marehemu kwa moyo wao mwema na wa ukarimu
waliouonesha katika kuwahudumia wageni mbalimbali pamoja na wafiwa. Bila
kuwasahau ndugu, jamaa na marafiki kwa uvumilivu wao hadi hatua ya
mwisho ya kuuaga mwili kabla ya kusafirisha Iringa.
Kwetu hili ni somo kubwa na kuhaadi kuyachukua mazuri yote kwa faida ya kizazi kijacho.
Mwenyezi Mungu Awalinde, Amina.
Imeandaliwa na:
Adam Kivenule
Katibu - KAUKI
Picha za Matukio Siku ya Msiba
Akina mama wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya geneza lenye mwili wa Flomina Kivenule
Akina mama wakiendelea wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya geneza lenye mwili wa Flomina Kivenule
Akina mama wakiendelea wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya geneza lenye mwili wa Flomina Kivenule
No comments:
Post a Comment