UTANGULIZI
KAUKI
ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na
changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii inayounda umoja huu;
hususani katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana
ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga, maradhi na
utegemezi. Kuanzishwa
kwa KAUKI kuliambatana na maandalizi yaliyojumuisha mikutano zaidi ya 10 ya
mashauriano iliyofanyika sehemu mbalimbali Jijini Dar es Salaam na Kidamali, Iringa.
Dira ya KAUKI
Kuwa na jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa
kujitegemea.
Maono ya KAUKI
Kujengeana uwezo kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi,
maarifa na weledi, kupitia mafunzo, kongamano, mijadala na mikutano ili
kuboresha maisha.
Malengo ya KAUKI
Lengo Kuu
Kuinua na kuboresha maisha ya wanaukoo wa Kivenule,
kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa kutumia ujuzi, maarifa na raslimali
zinazotunguka.
Malengo mengine mahsusi
§
Kuujua na kuelewa kwa kina Chimbuko na Historia ya Ukoo wa
Kivenule;
§
Kuzikusanya, kuziratibu na kuzihifadhi kumbukumbu
mbalimbali za Ukoo wa Kivenule.
§
Wanaukoo kupata fursa ya kufahamiana na kutambuana;
§
Kufanya senza ya ndugu/wanaukoo wanaounda Ukoo wa Kivenule
kila inapobidi kufanya hivyo na Senza hiyo itajumuisha watu waliohai na wafu;
§
Kuanzisha Mfuko wa Ukoo wa Kivenule utakaosaidia kuinua
kiwango cha Elimu na pia kusomesha wanaukoo wasio na uwezo wa kumudu kulipa ada
za shule au vyuo;
§
Kuboresha Elimu ndani ya Ukoo wa Kivenule ili
ndugu/wanaukoo wawe na uelewa wa hali juu na kumudu mabadiliko ya Sayansi na
Teknolojia katika Dunia ya Utandawazi;
§
Kusuluhisha na kutatua matatizo yanayojitokeza katika Ukoo
wa Kivenule kwa kupitia vikao vinavyokubalika;
§
Kuelimisha Wanaukoo/ndugu kuhusiana na madhara ya ugonjwa
wa UKIMWI, matumizi ya Madawa ya Kulevya na Ulevi wa kupindukia;
§
Kuinua viwango vya maisha vya wanaukoo wa Kivenule na
kuishi maisha mbadala yenye milo kamili, furaha na nyumba bora na nadhifu;
§
Kuongeza na kuimarisha mahusiano mazuri ndani na nje ya
ukoo kwa kushirikiana katika matatizo mfano raha, ugonjwa, misiba pamoja na
majanga makubwa;
§
Kuwa na nguvu ya kurekebisha tabia zisizostahili kwa
wanaukoo/ndugu ndani ya Ukoo na kutafuta suluhu ya migogoro/migongano baina ya
mtu au jamii inayotuzunguka;
§
Wanaukoo kuutambua na kuuelewa mtawanyiko/mgawanyiko wa
Ukoo wa Kivenule;
§
Wanaukoo/ndugu kushirikiana katika shughuli za uzalishaji
mali pamoja na utendaji kazi wa kila siku;
§
Kushirikiana na umoja au vikundi vingine vilivyoungana ili
kuuletea Ukoo wa Kivenule maendeleo endelevu;
§
Kuanzisha Mfuko wa kukopeshana (SACOSS); na
§
Kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya uvivu na uzembe ndani
ya Ukoo wa Kivenule.
Muundo wa KAUKI
KAUKI inaundwa na Kanda sita ambazo ni Kidamali, Irole,
Nduli, Magubike, Mufindi na Dar eS Salaam. Kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI, kuna
Mkutano Mkuu ambao ndio mkutano mkubwa kuliko yote. Hufanyika mara moja kwa
mwaka. Pia KAUKI ina mikutano ya Kamati ya Utendaji ambayo hufanyika mara nne
kwa mwaka kwa vipindi vya miezi mitatu mitatu. Katika Kanda pia kuna mikutano midogo
midogo ambayo jukumu lake ni kujadili masuala yanayohusiana na maendeleo ya
kanda. Muundo wa Uongozi wa KAUKI upo kama ifuatavyo:
Nafasi
za Uongozi Mkuu wa KAUKI
§
Mwenyekiti: Donath
P. Mhapa 0658 843 565
§
Makamu Mwenyekiti: Christian
J. Kivenule 0714 146 382
§
Katibu Mkuu: Adam
A. Kivenule 0713 270 364
§
Mweka Hazina Justin
D. Kivenule 0784 855 739
Nafasi za Uongozi wa Kanda
Kila kanda ina kiongozi wake ambaye ni Mwenyekiti, ambaye
naye husaidiana na Katibu. Pia ndani ya Kanda kuna viongozi wa Kamati
mbalimbali ambazo zipo kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI.
Katiba ya KAUKI ndiyo mwongozi mkuu wa shughuli zote
zinazofanywa na umoja huu. Katiba ya KAUKI ilipitishwa rasmi katika Mkutano
MKuu wa Pili wa KAUKI uliofanyika Kidamali, Iringa.
Historia Fupi ya Kuanzishwa kwa KAUKI
Harakati
za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza kwa kuratibu mawazo ya wana-ukoo wawili, yaani
Ndugu Faustino Kivenule na Ndugu Christian Kivenule mwezi Desemba 2004. Mawazo
hayo yalifanyiwa kazi kwa kumshirikisha pia Ndugu Adam Kivenule, ambaye bila
kuchelewa, waliweza kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mashauriano, Jijini Dar
es Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa River Side, tarehe 6
Februari, 2005 – Jijini Dar es Salaam.
Harakati
nyingine za maandalizi zilielekezwa upande wa Kidamali, Irore na Nduli. Kwa
upande wa Kidamali, Mkutano wa Kwanza wa Mashauriano kwa ajili ya maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulifanyika mwezi Mei
ambapo wajumbe toka Dar es Salaam walisafiri kwenda huko ili kuwasilisha hoja,
kufanya mashauriano na majadiliano, kuchagua viongozi wa kusimamia uratibu na
kuunda kamati ya maandalizi.
Maeneo
mengine kama Nduli na Irore hazikuweza kufanya maandalizi ya moja kwa moja japo
taarifa toka Dar es Salaam ziliweza kufikishwa na baadhi ya wanaukoo wanaishi
huko. Mjumbe mmoja tu ndugu Augustino Kivenule, toka Mgongo, Iringa ndiye
aliyeweza kumudu kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa
Kivenule.
Mkutano Mkuu wa Tisa wa
KAUKI
Huu ni Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI ambao unafanyika nyuma
ya mikutano mingine Nane ambayo imekwisha fanyika, mitatu Kijijini Kidamali na
Mkutano moja moja Kijijini Irole, Nduli, Magubike (Iringa Vijijini), Igowole
(Mufindi) Mkoani Iringa, na Mkutano mmoja Jijini Dar es Salaam (Karibu na Tabata
Shule). Kwa mujibu wa makubaliano na utaratibu ambao umewekwa na Wana-KAUKI,
mikutano hii itakuwa inafanyika katika ngazi ya Kanda, ili kuipa fursa jamii
inayounda KAUKI kushiriki moja kwa moja. Lakini pia, vipaumbele huwekwa pale
ambapo kuna idadi kubwa ya wana-KAUKA, lakini huridhiwa wakati wa Mkutano Mkuu.
Kwa msingi huo, Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI, kwa kauli moja, uliazimia kuwa
Mkutano Mkuu wa Tisa ufanyike katika Kanda ya Kidamali, Iringa Vijijini, tarehe
29– 30 ya Juni, 2013.
Angalia picha za matukio katika Mkutano Mkuu wa Nane wa
KAUKI uliofanyika Jijini Dar es Salaam, Juni 30 - Julai 1, 2012
http://www.facebook.com/photo.php?fbid=497523093617046&set=a.497521733617182.1073741825.100000780786862&type=1&theater
Kwa taarifa
zaidi, angalia http://www.tagumtwa.blogoak.com http://www.facebook.com/tagumtwa na http://www.twitter.com/tagumtwa
TANGAZO
MKUTANO WA TISA (9) WA UMOJA WA
UKOO WA KIVENULE-KAUKI
Uongozi wa Umoja wa Ukoo
wa Kivenule (KAUKI), kwa heshima na taadhima, unachukua fursa hii kuwatangazia
Wana-KAUKI wote, Ndugu, Jamaa na Marafiki, wanaoishi mijini na vijijini kutoka
katika Mikoa yote ya Tanzania Bara; Mkutano wa Mkuu wa Tisa (9) wa Umoja wa
Ukoo wa Kivenule (KAUKI), utakaofanyika katika Kijijini Kidamali, Wilayani ya
Iringa Vijijini, Mkoani Iringa; kuanzia tarehe 29 - 30 Juni, 2013.
Wana-KAUKI
Wote na Wapenda Maendeleo kwa Ujumla, na wale wote wanaoguswa na harakati zetu,
wanaombwa kusaidia maandalizi ya Mkutano huo kwa kuchangia fedha, nafaka na
raslimali nyingine, ambazo zitasaidia kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo,
pamoja na huduma muhimu kama chakula, kabla, wakati na baada ya Mkutano huo,
kwa wageni wote.
Kwa
niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI,
inakuomba/inawaomba
Pia
nachukua fursa hii kuwakaribisha jamaa na marafiki ambao wanapenda kujifunza
namna KAUKI inavyofanya kazi kwa kipindi cha miaka 8, toka umoja huu
ulipoanzishwa rasmi mwaka 2005.
Kwa taarifa na mawasiliano unaweza
kutufikia kupitia.
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
Kando ya Barabara ya Hifadhi ya Ruaha
Sanduku la Posta 193
Kidamali, Iringa
Simu: +255 713 270364 (Katibu Mkuu-KAUKI)
Barua-pepe: kauki2006@gmail.com
kivenule@gmail.com
tagumtwa.kauki@gmail.com
Blogu: http://www.kauki-kauki.blogspot.com
http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com
Twitter: https://twitter.com/kivenule
Facebook: https://www.facebook.com/kivenule
Natanguliza
shukrani zangu za dhati,
Wako katika kazi,
Adam
Kivenule
KATIBU MKUU-KAUKI
No comments:
Post a Comment