Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Wednesday 21 August 2013

KIVENULE CLAN-AUGUST 2013.pdf

CHIMBUKO NA HISTORIA YA

UKOO WA KIVENULE

 

 

Toleo la Kwanza - 2013

 

 

 

 

 

Kwa mawasiliano:

Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)

Kando ya Barabara ya Hifadhi ya Ruaha

Sanduku la Posta 193

Kidamali, Iringa

Simu: +255 713 270364 (Katibu Mkuu-KAUKI)

Barua-pepe:     kauki2006@gmail.com

                                   kivenule@gmail.com

                                   tagumtwa.kauki@gmail.com

Blogu: http://www.kauki-kauki.blogspot.com


UTANGULIZI

UKOO NI NINI?

Ukoo ni muungano wa familia kadhaa zenye utambulisho fulani. Unaweza kuwa utambulisho wa jina, alama au mwelekeo mmoja. Utambulisho wowote kati ya hizo nilizotaja, unaufanya ukoo utambulike miongoni mwa jamii mbalimbali. Mara nyingi utambulisho ambao huufanya ukoo utambulike baina ya jamii za Kiafrika ni Jina. Pamoja na jina, halikadhalika kuna tunu (values) mbalimbali ambazo huheshimiwa na ukoo husika na jamii kwa ujumla.

 

Tunu hubeba mambo mengi, ikiwa ni pamoja na miiko, maadili, heshima, vyakula na tamaduni. Sambamba na tunu, pia kuna Mila na Desturi, ambazo huzingatiwa sana katika masuala ya kijamii, mfano wakati wa kuoa au kuoza, misiba, sherehe za jadi mfano matambiko na masuala ya kimila.

 

Ukoo wa Kivenule ni mmojawapo wa koo nyingi kubwa zilizopo katika Himaya ya Uhehe katika Mkoa wa Iringa. Ukoo wa Kivenule ulianza kutambulika toka Karne ya 18. Historia inaonesha kuwa Ukoo huu asili yake ni kutoka kwa Wabena-Manga, waliopo Kusini mwa Mji wa Iringa; yaani maeneo ya Mufindi na Njombe. Ni mchanganyiko wa Wahehe na Wabena wanaojulikana kama Wabena-Manga.

 

Wahehe ni moja kati ya makabila makubwa hapa Tanzania ambalo kiasili linaishi katika Wilaya za Kaskazini mwa Mkoa wa Iringa, yaani Iringa Vijijini, Iringa Mjini, Kilolo na Mufindi. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinazopatikana na kutafitiwa, inasemekana kuwa ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji; yaani Wahehe wenye Asili ya Ungazija. Pengine hata ile sababu ya kuzika wafu wao wakielekea mashariki inapewa uzito.

 

Lugha ya Kabila hili ni Kihehe na limegawanyika kiasi fulani katika lahaja (matamshi) tofauti tofauti kutokana na maeneo ambayo huzungumzwa. Inafanana kimatamshi na kimaana na lugha ya Kibena iliyopo wilayani Njombe. Pamoja na Wabena wanaohesabika kuwa zaidi ya watu milioni moja. Wengi wao ni wafuasi wa Ukristo, hasa wa Kanisa Katoliki (Jimbo Katoliki la Iringa). Kihistoria Wahehe ni maarufu kwa jinsi walivyopambana na Wajerumani walioteka maeneo yao, kama katika mapigano ya Lugalo mwaka 1891. Kiongozi wao alikuwa Chifu Mkwawa.

 

Katika kuenzi na kutunza tunu za asili za Uhehe, Ukoo wa Kivenule hauli nyama ya Mbawala (kwa lugha ya Kihehe Mato/Imato). Imani kubwa imejengeka miongoni mwa jamii ya Ukoo wa Kivenule kuwa kula Mbawala ni kuvunja miiko ya Ukoo ambayo iliyowekwa na Waasisi wetu (Babu zetu). Mara mwanaukoo anapokiuka miiko hii na kula nyuma ya Mbawala (Imato) basi huweza kufikwa na matatizo mbalimbali, mfano kudhurika afya yake. Mara nyingi huwapata matatizo kama ya kuvimba miguu na pengine kuoza kabisa.

 

Tunu nyingine ambazo Ukoo wa Kivenule unazienzi kama zilivyo koo nyingine katika Uhehe ni Miitikio (Midikiso). Tunu hii huutambulisha Ukoo wa Kivenule miongoni mwa Koo za Wahehe. Mwitikio (Mwidikiso) wa Ukoo wa Kivenule ni 'MLIGO'. Mwitikio huu hutumika katika maeneo mbalimbali mfano katika salamu, kuapa (kufanya viapo) na pia kujitofautisha na koo nyingine. Miitikio (Midikiso) huutambulisha Ukoo wa Kivenule katika koo nyingine katika ardhi ya Uhehe.

 

CHIMBUKO LA UKOO WA KIVENULE

Historia ya Chimbuko la Ukoo wa Kivenule limetoka mbali zaidi hata kabla ya Jina la sasa la KIVENULE kupatikana. Utafiti unaonesha kuwa BABU NYAKUDIRA BALAMA ndiye aliyemzaa BABU KANOLO BALAMA. Hapa tunauangalia Ukoo wa Balama. Hali kadhalika, BABU KANOLO BALAMA, akamzaa BABU MTENGELINGOMA BALAMA. Maelezo haya yote tunayoyazungumzia ni katika Karne ya 17 kabla ya kuja kwa BABU TAGUMTWA BALAMA, ambaye aliuleta Jina la KIVENULE.

 

BABU MTENGELINGOMA BALAMA ndiye Baba Mzazi wa TAGUMTWA BALAMA. Wakati huu Babu Tagumtwa Balama alikuwa hajaenda kwenye Vita za LIGALU.

 

Kwa Asili, Ukoo wa Balama na baadaye Kivenule ni maarufu kama Wapiganaji wa Vita. Ukoo wa Balama (Kivenule) ulikuwa hodari sana katika vita vya msituni ambavyo viliwahusisha Babu zetu akina TAGUMTWA. Enzi hizo za Mababu zetu vita za Koo na Kabila zilipiganwa maeneo mengi ya himaya ya Uhehe kwa lengo la kupata mali, mifugo na heshima.

No comments:

Post a Comment