Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Wednesday 7 August 2013

UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI) ULIKOTOKA



UTANGULIZI
Ni mwaka 2005, tarehe 6 Februari, ndipo Wazo la Kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule lilipojadiliwa. Ufuatao ni muhtasari wa Kikao Hicho na maaamuzi yaliyochukuliwa, endelea...
 

MUHTASARI WA MKUTANO WA KWANZA WA KAMATI KUU YA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA UKOO WA KIVENULE, DESEMBA 17 – 18, 2005

Mahali Ulipofanyika: Ubungo - River Side Bar
Tarehe: Februari 06, 2005
Muda: 10:32 Jioni

Waliohudhuria:
Jina Kamili Mahali Anapoishi Namba ya Simu
1. Christian Kivenule Morogoro 0744 031 675
2. Adam A. Kivenule Ubungo, Dar es Salaam 0741 270 364
3. Innocent Kivenule Ubungo, Dar es Salaam 0748 663 315
4. Edgar S. Kivenule Mwenge, Dar es Salaam 0741 215 724
5. Ignas Kivenule Tabata, Dar es Salaam 0744 060 183
6. Raphael Kivenule Mbezi Beach, Dar es Salaam 0745 949 218
7. Philemon Kivenule Buguruni, Dar es Salaam 0744 757 844
8. Priskus F. Kivenule Mbezi, Dar es Salaam
9. Bakhita A. Kivenule Ubungo, Dar es Salaam
10. Tenus F. Kivenule Dar es Salaam
11. Valenia Kivenule Dar es Salaam 0745 555 521
12. Monica Kivenule City Center, Dar es Salaam 0745 409 138
13. Phesto Ngimba Dar es Salaam
14. Hamidu Mtono Mabibo, Dar es Salaam 0748 443 319
15. Athuman Mtono Kibamba, Dar es Salaam 0748 708 708
16. Nuhu Js Mtono Mabibo, Dar es Salaam

KUFUNGUA MKUTANO
Mkutano ulifunguliwa mnamo saa 10:32 jioni kwa Mwenyekiti wa muda wa Kamati ya Muda ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule, ndugu Christian Kivenule, na baadaye kuuombea kwa Sala iliyochukua muda wa dakika mbili hivi. Baada ya Sala, pia Mwenyekiti wa muda aliitumia fursa hiyo kuomba msamaha kwa Ndugu Edgar Kivenule ambaye ni Baba na Mkubwa wa Ukoo wa akina Kivenule wote waishio Dar es Salaam na mikoa ya karibu, kwa kushindwa kumshirikisha kikamilifu katika hatua za awali za Mashauriano na Maandalizi ya Mkutano huo pamoja na suala zima la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa akina Kivenule.

UTAMBULISHO
Mwenyekiti wa muda pia aliitumia fursa hii kumwomba na kumkaribisha Ndugu Edgar Kivenule ambaye ni Mkubwa wa Ukoo wa Kivenule waliishio Dar es Salaam, kutoa utambulisho kwa wajumbe waliojitokeza kuhudhuria mkutano huo.

Utambulisho ulianza kama ifuatavyo:
1. Christian Kivenule (Baba yake John toka Kidamale) anaishi Matombo, Morogoro
2. Adam Kivenule (Baba yake Alphonce toka Kidamale) anaishi Ubungo, DSM
3. Innocent Kivenule (Baba yake Mareh. Samwel toka Ilole) anaishi Ubungo, DSM
4. Edgar S. Kivenule (Baba yake Sigatambule toka Kidamale) anaishi Mwenge, DSM
5. Ignas Kivenule (Baba yake Pangayena toka Ilole) anaishi Tabata, DSM
6. Raphael Kivenule (Baba yake Pangayena toka Ilole) anaishi Club Oasis, DSM
7. Philemon Kivenule (Baba Mareh. Gwelino toka Ilole) anaisha Buguruni, DSM
8. Priskus F. Kivenule (Baba yake Mareh. Francis toka Magubike) anaishi Mbezi, DSM
9. Bakhita A. Kivenule (Baba yake Alphonce toka Kidamali) anaishi Ubungo, DSM
10. Tenus F. Kivenule
11. Valeria Kivenule (Mke wa Innocent Kivenule) anaishi Ubungo, DSM
12. Monica Kivenule (Baba yake Mareh. Francis toka Magubike) anaishi Zanaki, DSM
13. Phesto Ngimba
14. Hamidu Mtono (Baba yake Juma toka Nzihi) anaishi Kibamba, DSM
15. Athuman Mtono (Baba yake Juma toka Nzihi) anaishi Kibamba, DSM
16. Nuhu Js Mtono (Baba yake Juma toka Nzihi) anaishi Kibamba, DSM
 

DHUMUNI LA MKUTANO
Mwenyekiti alianza kuwaeleza wajumbe kwa kusema kuwa Wazo la Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule, lilibuniwa na Ndugu Faustin Kivenule ambaye ni Baba yake mdogo pamoja na yeye mwenyewe Christian Kivenule, alipokuwa likizo kijijini, Kidamali mwishoni mwaka jana (2004). Mtu wa tatu kulipata wazo alikuwa ni ndugu Adam Kivenule, anayeishi Ubungo, mjini Dar es Salaam kutoka kwa Christian Kivenule mwaka huo huo wa jana.

Mambo mbalimbali yalijitokeza kutokana na wazo (kusudio) la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, Desemba 17-18, 2005 kijijini Kidamale. Kati ya mambo hayo ya msingi ni pamoja na suala nzima la mahusiano ndani ya wana ukoo, suala la elimu, suala la UKIMWI, kufahamiana na kuujua ukoo kwa ujumla, kufanya senza ili kujua idadi ya ndugu na mahali wanapoishi pamoja na mambo mbalimbali ambayo tunayategemea yatajitokeza.
 
Suala la Ukoo pamoja na Mahusiano baina ya wanandugu ndani ya ukoo, suala la elimu na gonjwa hatari la UKIMWI ni mambo ya msingi pia ni kiini na changamoto ya mambo mengi ambayo yatajitokeza katika mkutano huo mkuu. Mahusiano duni baina ya wana ndugu, kukosa kwa ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo, kiuchumi na kijamii, matatizo ya kifamilia na kiukoo ni kati ya masuala msingi yaliyofikiriwa sana kabla ya kuletwa kwa wazo hili katika kikao hiki.

Mwelekeo wa ukoo wa Kivenule kuhusiana na suala nzima la Elimu hasa katika dunia hii ya Utandawazi (Globalization) ambapo dunia imekuwa kama kijiji kisicho na mipaka na kila mtu anaruhusiwa kuingia na kutoka, kuongezeka kwa viwanda vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu, kuongezeka kwa teknolojia ya mawasiliano, kupanuka na kujengeka kwa miji, pamoja na soko huria. Mambo yote haya ndiyo yanayoweza kuonyesha mustakabali na nafasi ya ukoo wa Kivenule kwa maisha ya baadaye. Ilionekana kuwa ukoo wetu upo nyuma sana katika suala nzima la elimu, hii linajidhihirisha kutokana na kuwa na ndugu wachache sana ambao wameweza kupata elimu kwa kiwango kinachostahili. Hii ni hatari kwa sababu tunajenga ukoo tegemezi ambayo baadaye utakosa mwelekeo. Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayojitokeza kila kukicha yanaibadili dunia na hivyo kutulazimisha nasi katika ukoo wa Kivenule kubadilika. Matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika simu za mikononi, computer, radio na satellite ni changamoto kwetu.

Maambukizo ya ugonjwa wa UKIMWI ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiri familia nyingi zikiwemo familia zetu sisi wana ukoo, yanapaswa kutopuuzwa bali kuwekewa mikakati madhubuti. Ufahamu kuhusiana na gonjwa lenyewe livyoenea na madhara yake katika jamii, njia mbadala za kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wenyewe pamoja na kuitikia mialiko mbalimbali ya wanajamii wanaopambana na janga hili ni mambo ya msingi sana ambayo yatajadiliwa kwenye mkutano huo.

Ilipendekezwa kuwa, wakati wa mkutano huo kutakuwa na nafasi kutoa uzoefu katika mambo mbalimbali ya kitaalum pamoja na mada ambazo tutazijadili kwenye agenda za mkutano huu wa leo, nazo zitawasilishwa kwenye mkutano huo.

Maandalizi ya mkutano mkuu wa ukoo yameanza mapema ili kutupa nafasi kubwa zaidi ya kujadili, kuandaa pamoja na kuwasilisha michango yetu ndani ya wakati unaotakiwa.

AGENDA ZA KIKAO
Agenda mbalimbali zilijadiliwa kwenye kikao zikiwa na mwelekeo na malengo mahususi ya kufanikisha kufanyika kwa mkutano mkuu wa ukoo. Agenda zilizojitokeza ni:-
1. Kuunda Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo itakayoratibu shughuli mbalimbali za wanaukoo wanaoishi Dar es Salaam.
2. Kulitoa kwa wajumbe wazo la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule unaotegemewa kufanyika kijijini Kidamale, Desemba 17 – 18, 2005.
3. Mashauriano baina ya Ndugu wa Ukoo wa Kivenule waishio ILOLE, NDULI, ILULA NA ENEO LA KIDAMALI kama wanakubali kuwepo na kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza Ukoo wa Kivenule, hapo Desemba 17 hadi 18, 2005.
4. Kupitia viwango vya michango vilivyopendekezwa.
5. Kuweka Mikakati mbalimbali ya kufanikisha mkutano huo.
6. Kupitia Mada zilizopendekezwa kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu.

KUJADILI AGENDA ZA MKUTANO
1. Kuunda Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo itakayoratibu shughuli mbalimbali za wanaukoo wanaoishi Dar es Salaam
Ndugu Ignas Kivenule alianza kwa kutoa mapendekezo kuwa Kamati iliyoandaa kikao cha kwanza cha maandalizi ya mkutano mkuu wa ukoo wa Kivenule iendelee kufanya kazi kwani imeshaonyesha nia. Pia Ndugu Edgar Kivenule alipendekezwa awepo mbele kwa waongoza mkutano kama kiungo muhimu cha wana ukoo waishio Dar es Salaam. Pia aliuliza swali, je kutakuwa na vikao vingapi kabla ya mwezi wa kumi (12) wakati wa Mkutano Mkuu?

Ndugu Edgar Kivenule alipendekeza kuwa kuundwe Kamati. Alipendekeza yeye awe mshauri tu katika masuala mbalimbali ambayo yatakuwa yanajitokeza kuhusiana na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, Desemba 17-18, 2005 kijijini Kidamale. Pia alishauri kupata viongozi ambao wataunda Kamati itakayokuwa na kazi ya kuyaratibu yote ambayo yatakuwa yanajadiliwa na wajumbe kuhusiana na maandalizi ya mkutano. Kazi nyingine ya kamati itakuwa kuwaunganisha ndugu wote wa ukoo wa Kivenule wanaoishi mjini Dar es Salaam na mikoa ya karibu pamoja na kushughulikia majukumu mbalimbali kama itakavyotakiwa kufanya hivyo. Alipendekeza achaguliwe Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina.

Wajumbe waliochaguliwa kuunda Kamati ni:
1. Christian Kivenule Mwenyekiti
2. Athuman Mtono Makamu Mwenyekiti
3. Adam Kivenule Katibu
4. Innocent Kivenule Mweka Hazina
5. Edgar Kivenule Mshauri Mkuu wa Kamati

Ndugu Edgar Kivenule alipendekezwa kuwa Mshauri na Kiungo cha wanaukoo wa Kivenule wanaoishi Dar es Salaam na mikoa ya karibu.

Kuhusu suala vikao vingapi vitafanyika hadi mwezi wa kumi na mbili! Ilikubaliwa kuwa umuhimu wa vikao utatokana na mahitaji ya kamati ambayo ndiyo yenye jukumu kubwa la maandalizi ya mkutano mkuu. Kuchangamka au kudorora kwa maandalizi ya mkutano huo ndio kutakako amua ni vikao vingapi vifanyike.

2. Kulitoa kwa wajumbe wazo la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule unaotegemewa kufanyika kijijini Kidamale, Desemba 17 – 18, 2005
Wazo la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule lilikubaliwa na wajumbe wote.

3. Mashauriano baina ya Ndugu wa Ukoo wa Kivenule waishio ILOLE, NDULI, ILULA NA ENEO LA KIDAMALI kama wanakubali kuwepo na kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza Ukoo wa Kivenule, hapo Desemba 17 hadi 18, 2005
Wajumbe wote toka Ilole, Nduli, Ilula, Kidamali na Dar es Salaam walikubali kwa kauli moja umuhimu wa kuwepo kwa mkutano huo, pia waliaahidi kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.

4. Kupitia viwango vya michango vilivyopendekezwa
Hapo awali ilipendekezwa kuwa kila mjumbe anayeishi mjini na wale wanaoishi vijijini wenye uhakika wa kipato pia watoe kiasi cha Tsh. 15,000.00; na vijijini watoe kiasi cha Tshs. 5,000. Kwa upande wa vijijini pia ilipendekezwa kuwa kwa wale wasio na uwezo wanaweza kutoa mifugo mfano kuku wawili au mifugo yoyote mingine. Na mwisho wa kutoa michango ilipendekezwa iwe mwezi wa tisa mwaka huu.

Kati ya wajumbe waliotoa/waliochangia mawazo yao alikuwa ni Priskus Kivenule wa Magubike ambaye aliahidi kutoa kiasi hicho licha ya kuwa na hali ngumu ya kiuchumi, lakini anadhani mkutano una umuhimu sana. Naye Rafaeli Kivenule toka Ilole, alihoji ni kiasi gani cha fedha kinakadiriwa kugharimu Mkutano huo mkuu? Mwenyekiti wa Kamati alifafanua kwa kusema, kiasi cha shilingi laki tisa na elfu kumi (910,000.00) kinakadiriwa kutumika baada ya kuchambua gharama za mahitaji na vitu mbalimbali ambavyo ni muhimu kuwepo kwenye mkutano huo mkuu.

Pia Rafaeli Kivenule aliuliza kama kutakuwa na wawakilishi wowote toka Dar es Salaam au kuna utaratibu gani wa kwenda kwenye mkutano huo? Mwenyekiti alimjibu kuwa toka Dar es Salaam au sehemu yoyote nyingine hakutakuwa na usafiri wa moja kwa moja. Ila kuna utaratibu umepangwa wa kuwa na usafiri kuanzia Iringa Mjini mpaka Kidamali kwa wageni mbalimbali wanaishi nje ya Kidamali. Kiasi cha Tshs. 50,000.00 kimewekewa bajeti kuwasafirisha wageni to ka Iringa mjini hadi Kidamali na 50,000 nyingine kuwarudisha toka Kidamali hadi Iringa mjini. Hakutakuwa na mwakilishi yeyote toka Dar es Salaam kwenye kwenye kikao hicho, ila kila ambaye atachanga kiasi cha Tshs. 15,000 atakuwa amejipa tiketi ya kushiriki na itabidi agigharamie nauli toka hapa hadi Iringa Mjini na toka Iringa Mjini hadi Dar es Salaam.

Swali jingine lilikuwa ni kigezo gani kimetumika kupitia viwango vya michango? Swali hili lilijibiwa na Mwenyekiti pamoja na Mshauri Mkuu, huduma mbalimbali zilizopendekezwa kuwepo kwenye mkutano mkuu ndiyo kigezo na utaratibu mahsusi uliotumika kupendekeza viwango vya michango. Pia Adam Kivenule, Katibu wa Kamati aliongeza kwa kusema kuwa makadirio yaliyopendekezwa mwanzo yanaweza yasikidhi haja, kwani kuna mambo mbalimbali yanaweza kujitokeza na hivyo kuongeza gharama. Hata hivyo kiwango cha michango kikizidi lengo hamna ubaya wowote, kuna ununuzi wa vifaa vya kudumu vitakavyotumika wakati wa shughuli. Tunategemea vifaa hivyo vitaendelea kutumika katika shughuli mbalimbali za kiukoo zitakazokuwa zinajitokeza kama misiba na masuala mengine ya kiukoo ambayo yatakuwa yanawakusanya ndugu wengi. Baadhi ya vifaa hivyo ni pamoja na vyombo vya chakula (sahani, vijiko, vikombe, sufuria, visu), viti (vya plastiki na mbao) pamoja, meza pamoja na magodoro.

5. Kuweka Mikakati mbalimbali ya kufanikisha mkutano huo
Mikakati mbalimbali imewekwa ili kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Kamati imepanga kuandaa kadi za kuchangisha michango ndani ya wanaukoo na nje ya wanaukoo. Mwenyekiti aliahidi kuwapelekea kadi ya kuomba michango Askofu wa Jimbo la Iringa Ngalaleku Mtwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Pia kwa makadirio ya haraka haraka kama watapatikana watu 50 toka Dar es Salaam na wakalipa shilingi 15,000.00 kila mmoja, tunategemea kupata Tsh. 750,000.00. Kwa hiyo tutakuwa tunatakiwa kukamilisha kiasi cha Tshs. Tshs. 160,000.00. Kwa hiyo Kamati imeona ni vyema kama tarehe ijayo ya Februari 26, 2005 ya kufanya kikao, pia itumike kusambaza kadi za kuomba michango.

Mikakati mingine ni kuwahamasisha wale wenye uwezo kuchangia zaidi, na pia tunashauri wajumbe waangalie baadhi ya maeneo ambayo wanadhani kuna uwezekano wa kusaidiwa kama wakipeleka barua, miniti, kadi za michango pamoja na wazo zima la mkutano. Kupatikana kwa wingi wa michango kutasaidia pia kuboresha baadhi ya mambo/huduma ambazo zimeminywa kutokana na ufinyu wa bajeti.

Pia kamati itakayochaguliwa itakuwa na jukumu la kwenda kijijini Kidamali na vijiji vingine wanakoishi wana ukoo kwa lengo la kuwahamasisha jamii nzima ya ukoo ya Kivenule ione umuhimu wa mkutano huo, na pia ichukue jukumu la kuuchangia kwa namna moja au nyingine. Pia tutaandaa vipeperushi mbalimbali ambavyo vitakuwa ni sehemu ya hamasa pamoja na mabango ya kubandika sehemu mbalimbali vijijini yakiwa yamejaa ujumbe mzito kuhusiana na mkutano huo.


6. Kupitia Mada zilizopendekezwa kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu
Mada zote zilizopendekezwa kuwasilishwa na kufundishwa kwenye mkutano mkuu, zilikubaliwa na wajumbe wa mkutano. Mwenyekiti wa Kamati alizitaja mada na wawezeshaji waliopendekezwa kusaidia ufanikishaji wa ufundishaji kuwa ni:-

Mada zilizopendekezwa:-
1. HISTORIA YA UKOO
• Ukoo ni Nini na Unapatikanaje?
• Dhana ya Kuenea na Kukua kwa Ukoo.
• Mgawanyiko wa Ukoo (Chora Mchoro Kuonyesha Ukoo unavyoundwa).
• Kupotea kwa Ukoo.

2. MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
• Ukaribu wa Wana Ndugu.
• Ushirikiano Katika Nyanja Mbalimbali.
• Kutembeleana kama Sehemu ya Kudumisha Mahusiano.
• Kuondoa Tofauti na Kusaidiana.

3. ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
• Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu.
• Umuhimu wa Elimu.
• Dunia ya Utandawazi.
• Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika Ukoo Wetu.

4. UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
• UKIMWI ni nini?
• Namna gani UKIMWI unavyoenea/kuambukizwa?
• Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi?
• Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI.

Wawezeshaji Waliopendekezwa:-
1. Agatha Mhapa
2. Alphonce Kivenule
3. Christian Kivenule
4. Donath Mhapa
5. Edger Kivenule
6. Florian Kivenule
7. Ignas Kivenule
8. Adam Kivenule
9. Innocent Kivenule
10. John Kivenule
11. Justin Kivenule
12. Lizeta Kivenule
13. Piera Kivenule
14. Siha Kivenule
15. Victoria Kivenule
16. Zavery Kivenule

Rafael Kivenule aliuliza kuhusiana na mada zilizopendekezwa kwenye mkutano mkuu wa Kidamale kama zitahusika na kwenye vikao vyetu vitakavyokuwa vinafanyika huku? Jibu lilikuwa kuwa Mada zinahusika kote kwani malengo ya mkutano mkuu ni yale yale ya kudumisha mahusiano, elimu, UKIMWI, kujuana na kusaidiana.

Mshauri Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo uliufunga mkutano kwa kutoa nasaha mbalimbali ikiwemo kuujali na kuona umuhimu wa mikutano mbalimbali itakayokuwa inaitishwa na Kamati hii iliyoundwa. Pia alipendekeza kikao kingine kinachofuata kisiwe mbali sana na hiki cha mwanzo. Alisisitiza umuhimu wa kuwajulisha ndugu wengine ambao hawakuhudhuria waje na washirikiane na wajumbe wengine ambayo tayari wana taarifa.

Kikao cha pili cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kilipendekezwa kifanyika tarehe 26 Februari 2005, saa 9.00 Ubungo, River Side Bar.

Kikao cha kwanza kilifungwa saa 12:58 jioni
Imetiwa Saini na:
____________________ _________________
Christian Kivenule Adam Kivenule
Mwenyekiti wa Kamati Katibu wa Kamati

_______________________
Edgar Kivenule
Mshauri Mkuu wa Kamati

http://www.kauki-kauki.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment