Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Wednesday 21 August 2013

MAHUSIANO BAINA YA WANANDUGU NDANI YA UKOO

Maana ya Mahusiano ni hali ya ukaribu, ujirani, urafiki, umoja au ushirikiano unaojengeka baina ya Ndugu, Jamaa au Marafiki. Mahusiano ni hali ya kuwa pamoja Kifikra, Kimwili, Kimawasiliano, Kiimani, Kiitikadi, Kimaendeleo, Kikazi, Kijamii na Kimichezo.
 
Mahusiano hujengwa kwa misingi/namna mbalimbali. Baadhi ya njia au vitu vinavyosababisha kukawepo na mahusiano ni pamoja na:
Ujirani: Ujirani mara nyingi katika jamii zetu huchangia sana katika kujenga Mahusiano. Mahusiano yenyewe huonekana katika sura mbili tofauti. Yaani Mahusiano Mazuri kwa maana ya Sura Nzuri au Mahusiano Mabaya kwa maana ya Sura ya Ubaya.
 
Undugu: Hii ni aina ya nyingine ya Mahusiano ambapo ndugu wa Damu Moja au wanachangia damu, hujenga Mahusiano ya Moja kwa Moja (Automatic Relationship). Mara nyingi Mahusiano ya aina hii huwa na Sura ya Uzuri zaidi (Mahusiano Mazuri). Japo kuna kipindi Fulani hata Sura ya Ubaya (Mahusiano Mabaya) hujitokeza.
 
Imani: Pia watu huweza kujenga Mahusiano kupitia Imani zao, mfano watu wanaoabudu katika dhehebu moja huweza kujenga mahusiano ya aina yao tofauti na dhehebu jingine. Mara nyingi Mahusiano ya Kiimani huwa na mwelekeo wa Mahusiano memo. Mahusiano mabaya mara nyingine hutokea na hata kusababisha vita vya kiimani (dini).
 
Itikadi: Mahusiano ya Kiitikadi nayo hujengeka kwa kufuata Mlengo wa Vyama Vyao. Na zaidi Mahusiano ya Kiitikadi huegemea zaidi kwenye siasa na hupungua au kutoweka kabisa baada ya mmoja wao kubadili Itikadi yake yaani kuhama toka chama cha kimoja cha siasa na kwenye chama kingine cha siasa. Mahusiano ya Kiitikadi hujengwa kwa misingi ya Chuki, Fitina na Vitisho baina wa watu wa Itikadi moja na wale wa Itikadi nyingine.
 
Maendeleo: Watu wenye hali fulani ya kimaendeleo huweza kujenga aina fulani ya mahusiano yenye nia ya kuinuia hali zao za kimaisha. Na mara nyingi wanaojumuika hapa ni wale ambao tayari wameonesha nia na mwelekeo. Lakini pia hata wale waliopiga hatua kimaendeleo huweza kuja mahusiano yao yakiwa nia ya kuimarisha hali walizonazo. Msingi mkubwa wa mahusiano ya aina hii huwa ni kupeana mbinu na mikakati ya kuleta au kujiimarisha zaidi katika maendeleo ambayo wanayatarajia au ambayo wamekwisha yapata.
 
Pia hata kwa upande wa wale wenye hali duni ya kimaendeleo nao hujenga aina Fulani ya mahusiano kulingana na hali na uwezo wao. Kasoro ambayo hujitokeza hapa huwa ni mahusiano duni baina wenye uwezo (matajiri) na wale na wasio na uwezo (maskini). Katika kujiimarisha zaidi kimaendeleo, maskini huwa mtumishi (kibarua) na tajiri huwa mtumikiwa (mtwana).
 
Elimu: Watu wenye elimu nao mara nyining hujenga mahusiano yao. Mara nyingi katika mahusiano yao huwatenga wale wenye elimu kidogo au wasio na elimu kabisa. Hii hutokea zaidi kwa wale waliobahatika kupata Elimu ya Juu mfano Chuo Kikuu. Mazungumzo na mipango yao huwatenga zaidi wale wenye elimu kidogo. Kuwatenga hujitokeza katika matumizi ya lugha za kigeni, kutowashirikisha katika mawazo mbalimbali ambayo wanadhani yanaweza kuwainua watu wa hali zote (wasomi na wasio wsomi).
 
AINA ZA MAHUSIANO
Kuna aina mbalimbali za mahusiano, lakini tunaweza kugawanya mahusiano haya katika sehemu kuu mbili.
Mahusiano Mazuri; na
Mahusiano Mabaya.
 
Aina mbalimbali za mahusiano ambayo yapo katika jamii zetu ni pamoja na mahusiano ya:
Kikazi;
Kijamii;
Kisiasa; na
Kiuchumi.
 
MAHUSIANO MAZURI
Mahusiano Mazuri ni hali ya kuwa pamoja kwa kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano Mazuri huwa katika shida au raha. Raha hujumuisha hali zozote zenye kuashiria mafanikio na maendeleo katika maisha ya binadamu. Hii ni pamoja na kufaulu mitihani mbalimbali ya darasani na ya maisha; kujenga nyumba, kununua gari, kapata kazi nzuri, kufanikiwa katika kilimo, Jubilei, kupandishwa cheo pamoja na kupata nishani.
 
Shida huwa ni hali ya kuwa na mashaka, kutokuwa na uhakika wa maisha, kutokuwa na kipato, kutofanikiwa katika elimu, ugonjwa, misongamano (Depression), misusuko (stress), kutokuwa na ajira, kutofadhiliwa kwa hali yoyote (Promotion au Scholarship) na kadhalika.
 
MAHUSIANO MABAYA
Mahusiano Mabaya ni hali ya kutokuwa na ushirikiano, huruma au wema katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano Mabaya nayo hali kadhalika huwa katika ubaya au uzuri au shida na raha. Tofauti na katika Mahusiano Mazuri, Mahusiano Mabaya hubaki kuwa ni swa katika shida na raha. Kwa ujumla ushirikiano na mawasiliano hukosekana kabisa. Huwa hakuna huruma, maelewano, kuvumiliana na kuwasiliana.
 
Kikubwa ambacho hujengeka ni chuki, majivuno, wivu, ugomvi na kutakiana shari. Hamna hata mmojawapo ambaye huombewa kheri. Kwa yule aliyenacho, huombea au hutamaini yeye aendelee kuwa nacho peke yake na kutomwombea kheri ya kupata yule ambaye hana kitu.
 
Na kwa yule ambaye hana, humwombea shari, bahati mbaya kupotteza au kwa namna yoyote ambayo haina kheri kwa yule ambaye anacho. Baadhi huomba mfano kama ni gari lipate ajari, nyumba iungue na kama anasoma anafeli. Katika aina hii ya mahusiano hakuna nafasi ya kutakiana mema au maendeleo.
 
MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
Ukoo wa Kivenule ni mkubwa sana na kwa haraka unakadiriwa kuwa na ndugu karibia elfu mbili (2000). Ni ukoo ambao unaweza kufanya mambo makubwa nay a kimaendeleo kama utaungana na kuwa kitu kimoja.
 
Tatizo kubwa ambalo linaonekana kwa wanaukoo ni kuwa na mwamko mdogo. Kwa mfano wanaukoo wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni theluthi au robot u ya wanaukoo wote. Tumaini la Kamati za Maandalizi ya MKutano Mkuu ni kuhudhuriwa na Ndugu pamoja na Wanaukoo wa Kivenule kwa wingi zaidi.
 
Kwa upande wa Dar es Salaam, mwamko wao ni mdogo sana. Tumaini na tegemeo la awali ilikuwa Dar es Salaam ingekuwa ni mfano, lakini imeshindika na hii ndiyo hali halisi. Tunasikitika na Kamati ya maandalizi ya Dar es Salaam inaomba samahani.
 

Kwa wanaukoo toka Ilole, nao wamesema tatizo kubwa kwao ni suala na nauli kuwa ni kubwa. Lakini cha msingi kufanyika ni kuzidi kuwahamasisha na kuwapa mojyo wa kutambua umuhimu wa Mkutano Mkuu wa Ukoo pamoja na mikutano mingine.
 
Katika suala zima la mahusiano, ukaribu wa wanandugu na wanaukoo linaangaliwa kwa karibu zaidi. Mahusiano yanagusa mambo muhimu katika maisha ya kila siku mfano Elimu, Ugonjwa, Vifo pamoja na Starehe (Harusi, Send-Off, Kipaimara na Komunio). Elimu ni muhimu sana kwani inaongeza upeo na ufahamu wa kuweza kukabiliana na matatizo ya maisha ya kila siku.
 
Suala jingine ni ushirikiano katika nyanja mbalimbali mfano Biashara, kazi na kilimo. Hapa tunamaanisha kuunda kikundi ambacho kitakuwa na mfuko utakaokuwa unachangiwa na watu mbalimbali kulingana na shughuli na kipato.
 
Katika kujenga mahusiano imara, kutembeleana ni muhimu sana. Faida ya kutembeleana ni kujuliana hali, kusaidiana, kushauriana na kupeana mbinu na mwongozo wa kufauli katika maisha. Pia katika kutembeleana huwapa fursa wanaukoo/ndugu kuangalia mazingira mapya anayotembelea kama yanaweza kumfaa kuishi akilinganisha na mazingira aliyotoka.
 
Pia katika kushirikiana kuna haja ya kuwashawishi na kuwabembeleza wale wasio na uwezo ikiwa ni pamoja na kuwapa moyo, kuwashauri waondoe aibu na wajenge tabia ya kushirikiana. Katika kushirikiana inakuwa ni rahisi kuweza kutatua matatizo mbalimbali baina ya wenye nacho na wasionacho.
 
Kwa mfano katika shughuli nzima ya kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, inakuwa kitu kizuri na mfano kwa wengine kama tutaonyesha kwa vitendo haya tunayozungumza hapa. H
 
SIKU YA KWANZA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE, DESEMBA 17, 2006
 
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ulifunguliwa na Mgeni Rasmi Ndugu Daima Luvanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidamali.
 
Awali kabla ya yote, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mkuu wa Ukoo Ndugu Faustino Kivenule, aliwakaribisha ndugu, jamaa na wanaukoo kwa ujumla kwenye mkutano huo.
 
Kabla ya kusoma hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ukoo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo, alimkaribisha Ndugu George Kivenule, kuuombea Mkutano Mkuu kwa sala.
 
Baada ya Sala ya kuuombea Mkutano Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo, alitumia fursa hiyo kuisoma Hotuba ya Ufunguzi.
 
Alianza kwa kuwajulisha ndugu, wanaukoo na wageni waalikuwa kuwa, lengo la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni kuwaunganisha wanaukoo wote, wanaoishi sehemu mbalimbali hapa Tanzania, ili wafahamiane, waelimishane na kupeana ujuzi katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kupeana uzoefu.
 
Pia, lengo jingine la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni kutolewa na kufundishwa kwa Mada kadhaa zenye nia ya kuujengea ukoo na kuwa na msimamo imara. Kwa kuwakusanya ndugu pamoja, Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu, iliamini itasaidia kuujenga Ukoo katika misingi ya Ushirikiano na Upendo na hiyvo kuwa na ukoo wenye umoja.
 
Lengo jingine la kufanya mkutano mkuu wa ukoo ilikuwa ni kufanya senza ili kujua idadi ya wanaukoo na mwishoni kufanya uchaguzi wa viongozi, watakaunda Uongozi wa Ukoo na pia watashirikiana na Kamati ya Ukoo wa Kivenule katika kutekeleza majukumu mbalimbali.
 
Kamati itakayoundwa itakuwa na jukumu la kuratibu mambo mbalimbali na matatizo yanayohusu ukoo.
 
Jumla ya Mada Tano ziliwasilishwa na kufundishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Mada zilizowasilishwa ni pamoja na:
<![if !supportLists]>1.        <![endif]>CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO;
<![if !supportLists]>2.      <![endif]>MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO;
<![if !supportLists]>3.      <![endif]>ELIMU NA MUSTKABALI WA UKOO;
<![if !supportLists]>4.     <![endif]>UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE; NA
<![if !supportLists]>5.      <![endif]>DINI KATIKA UKOO.
 
Harakati za maandalizi ya Mkutano Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, zilianza toka mwezi Februari 05, 2005. Harakati hizi zilifanyika Kijijini Kidamali kwa upande mmoja na kwa upande mwingine jijini Dar es Salaam.
 
Kamati zote mbili zilizoundwa zilijipa majukumu mbalimbali, likiwemo lile la kuwaalika na kuwashirikisha ndugu na wanaukoo katika suala zima la maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo katika vikao, na pia utoaji wa michango.
 
Katika harakati za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa UKoo wa Kivenule, kamati zote mbili zilizipata vikwazo mbalimbali likiwemo tatizo la mwitikio duni katika kulipokea wazo hili. Kwa ujumla, katika kuliuza suala/wazo hili la kuandaa na kuwa na Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, kamati ilibidi zitumiea nguvu na mbinu za ziada ili kuweza kufanikiwa.
 
Mahudhurio duni yalitoa changamoto kwa Kamati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu, kuongeza juhudi/jitihada na kutafuta njia mbadala za kufikia lengo. Kwa upande wa Kijijini Kidamali, ushawishi ulizaa matunda, kwa sababu ongezeko la wanaukoo na ndugu kuliunga mkono wazo la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo lilivuna washiriki wengi.
 
Kwa upande wa Dar es Salaam, suala la mahudhurio duni, liliendelea kuwa ni kikwazo kwa kipindi chote cha maandilizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Wapo waliodiliki kusema Mkutano Mkuu wa Ukoo ufanyike kwanza Dar es Salaam na ndipo ufanyike na kijijini Kidamali. Licha ya kupewa sababu na maelezo ya kina ya kuufanya Mkutano huo ufanyike Kijijini Kidamali, hawakutilia maanani.
 
Katika suala la utoaji wa michango, watu wamekuwa na ari na mwitikio wa hali ya juu hapa Kijijini Kidamali, na kwa kiwango kikubwa ndio waliosaidia kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
 
Licha ya wanaukoo waishio Dar es Salaam kuchangia, lakini mchango wao umesaidia kidogo sana, kwa sababu kiwango kikubwa cha fedha pamoja na mahitaji mengine, yamepatikana hapa.
 
Sehemu nyingine, nje ya Kidamali, utoaji wa michango hapo mwanzo ulikuwa wa wastani, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakaribia, ari na kasi mpya ilijitokeza na kuwa kubwa hasa toka sehemu za Magubike pamoja na Nyamihuu.
 
Majirani na watu wengine wasio wanaukoo wamejitolea kutoa michango katika kuusaidia Ukoo wa Kivenule, kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Majirani na marafiki waliojitokeza kwa hali na mali katika kutoa fedha, vyombo na vifaa mbalimbali.
 
HOTUBA YA MGENI RASMI
Mgeni Rasmi aliishukuru Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa kumwalika kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule. Alisisitiza kwa kusema kuwa, kuna watu wengi muhimu ambao tumewaacha na kuamua kwenda kumwalika yeye.
 
Mgeni Rasmi alisema amefarijika sana kutokana na kuwashirikisha jamaa/wanaukoo wote. Pia alisisitiza kuwa anahisi yupo karibu na ukoo wa Kivenule kutokana na baadhi ya jamaa zake wa karibu kuwepo kwenye mkutano huo. Pia hata rafiki zake nao waliohudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Ukoo; hii ilimpa faraja sana.
 
Kutokana na ukoo kuwa na mtandao mkubwa sana, ni muhimu kuwa na shughuli za pamoja kama hizi. Wakati anakuongea na Mwenyekiti, amefurahi sana kusikia mikakati ya wanaukoo hasa lile la kufanya senza na pia mkakati wa kufahamiana zaidi.
 
Mgeni Rasmi aliwashukuru wale wote waliotoa wazo la kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule na jinsi walivyoshirikisha wanaukoo katika shughuli hii.
 
Katika shughuli yoyote ile, vikwazo vipo, suala la msingi ni kuelimishana na kuwashawishi wale ambao hawakuhudhuria ili kuwepo na umoja na mshikamano. Suala mshikamano na umoja ni muhimu sana katika jamii yetu kwani itasaidia kuleta maendeleo na wanandugu wawtakuwa karibu.
 
Pia, kuwa pamoja kunasaidia kushirikiana katika magonjwa, furaha na matatizo mbalimbali ya kila siku. Mgeni Rasmi, alitoa mfano wa Abraham na Lutha katika ugomvi wao wa mifugo, lakini mwisho walijaliana licha ya kutengana. Ndugu ni muhimu sana na hawawezi kutengana.
 
Mkutano huu unatoa changamoto ya kuwa na mshikamano na kuwa na nguvu zaidi katika kuleta maendeleo.
 
Mgeni Rasmi aliushukuru Ukoo wa Kivenule kwa kuelimishana kuhusu umuhimu wa kuwa na ushirikiano wakati wote nasi tu wakati wa matatizo. Huu ni mfano mzuri kwa jamii nyingine.
 
Mgeni Rasmi aliutakia kila la kheri Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, na kuahidi kuwa yuko nyuma ya wanaukoo sambamba wakati wote wa Mkutano huo.
 
Baada ya hotuba ya Mgeni Rasmi, MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE, ulifungulia Rasmi mnamo saa 4:45, tarehe 17 Desemba 2005.
 
UTAMBULISHO WA WANAUKOO
Kwa mujibu wa ratiba ya siku ya kwanza ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, utambulisho wa Wanaukoo ulifanyika kwa kila ndugu/mwanaukoo kujitambulisha. Mwenyekiti aliwaelewesha washiriki wote jinsi ambavyo wanapaswa kujitambulisha.
 
Kila anajitambulisha alipaswa/alitakiwa kutaja jina lake la mwanzo, jina la baba yake, babu na jina la mwisho la ukoo. Lakini, pia wanaukoo walijitambulisha kwa kutaja majina ya Mama zao, Waume au Wake zao.
Kila mshiriki katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, alipewa kitambulisho cha kumtambulisha kwa ndugu wengine. Kitambulisho hicho kilionyesha jina lake kamili, mahali anapoishi, namba ya simu pamoja na sanduku la posta. Hii ilifanyika makusudi ili kupunguza kuulizana majina kutokana na washiriki kuwa wengi.
 
Yafuatayo hapa chini ni majina ya wanaukoo waliojitambulisha siku kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. (refer registration forms).
 
UWASILISHAJI WA MADA
Katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, jumla ya Mada Tano ziliwasilishwa. Mada ya kwanza kuwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni “CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO”. Wawasilishaji wa Mada hii walikuwa ni ndugu:
<![if !supportLists]>1.        <![endif]>Christian     J.        Kivenule
<![if !supportLists]>2.      <![endif]>Augustino            Kivenule
 
 
VIAMBATANISHO (ANNEXTURE)
Wawezeshaji wa Mada Mbalimbali
<![if !supportLists]>1.        <![endif]>Christian           J.        Kivenule
<![if !supportLists]>2.      <![endif]>Augustino                 Kivenule
<![if !supportLists]>3.      <![endif]>Stephan                     Mhapa
<![if !supportLists]>4.     <![endif]>Maria                        Milimo
<![if !supportLists]>5.      <![endif]>Adam              A.      Kivenule
<![if !supportLists]>6.     <![endif]>Jovin                D.      Kivenule
<![if !supportLists]>7.      <![endif]>George             S.       Kivenule
<![if !supportLists]>8.      <![endif]>John                 S.       Kivenule
<![if !supportLists]>9.     <![endif]>Ignas                P.      Kivenule
 
Wawezeshaji Wasaidizi
<![if !supportLists]>1.        <![endif]>Lesandu                    Mhapa
<![if !supportLists]>2.      <![endif]>Adam              A.      Kivenule
<![if !supportLists]>3.      <![endif]>Faustin            S.       Kivenule
<![if !supportLists]>4.     <![endif]>Christian          J.        Kivenule
 
Msimamizi wa Vyombo vya Matangazo
<![if !supportLists]>1.        <![endif]>Lesandu                    Mhapa
<![if !supportLists]>2.      <![endif]> 
 
 

No comments:

Post a Comment