MAMBO MBALIMBALI YALIYOJADILIWA KAMA SEHEMU YA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA UKOO
A: Mambo ya Muhimu ya Kuwezesha Mkutano Kufanikiwa
1. Malazi : Kwa Wageni wote watakaokuja kwenye Mkutano Mkuu wa Ukoo Kidamali.
2. Usafiri: Toka Iringa Mjini mpaka Kidamali, Iringa na kutoka Kidamali mpaka Iringa Mjini
3. Chakula: Kwa siku za mkutano na kabla ya mkutano
4. Vinywaji: Kwa siku za mkutano na kabla ya mkutano
· Pombe ya Asili
· Pombe ya Kisasa
5. Burudani
· Muziki wa Asili
· Muziki wa Kisasa
6. Makisio (Makadirio) ya Washiriki wa Mkutano (Tunategemea kuwa na Wanaukoo takribani 200 watakaohudhuria mkutano)
7. Mchango wa Kufanikisha Mkutano
· Waishio Mijini (Kima cha chini kimependekezwa Tsh. 15,000/- lakini njia ni nyeupe kwa wale ambao wataona kuna haja ya kuchangia kwa hali na mali ili kuweza kufanikisha mkutano huo)
· Waishio Vijijini (Kima cha chini kimependekezwa Tsh. 5,000/- pia wanashauriwa kuwa wanaweza kutoa kitu kingine chochote chenye thamani kama kuku wawili, mbuzi au vinginevyo)
8. Mahali pa kufanyia Mkutano: Kuna kumbi mbili zimependekezwa; Kwa Sanga ndiyo umepewa asilimia kubwa. Kwenye ukumbi wa Justin kuna watu wanazungumzia imani zao zinawasuta kufika mahali pale. Pia kibiashara inaweza kumuathiri japo nadhani siyo suala la msingi sana. Majukumu ya ukumbi litashughulikiwa na Kamati ya Kidamali. Lakini maoni na mawazo yanakaribishwa kwa ajili mashauriano zaidi kuhusu sehemu ambayo watadhani inafaa zaidi.
Kuundwa kwa Kamati za Maandalizi
1. Kamati ya Dar es Salaam inaongozwa na:
Kamati ya Dar es Salaam na mikoa ya karibu inayoshirikiana na Kamati ya Kidamali katika kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule ipo chini ya viongozo wafuatao:
1. Mwenyekiti: Christian Kivenule
2. Makamu Mwenyekiti: Athuman Mtono
3. Katibu: Adam Kivenule
4. Mweka Hazina: Innocent Kivenule
5. Mshauri: Edgar Kivenule
2. Kamati ya Kidamali inaongozwa na:
Kamati ya Kidamali inayoshirikiana na Kamati ya Dar es Salaam na Mikoa ya karibu katika kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule ipo chini ya viongozo wafuatao:
1. Mwenyekiti: Faustin Kivenule
2. Makamu Mwenyekiti: Aujen Kivenule
3. Katibu: Jovin Kivenule
4. Mweka Hazina: Justin Kivenule
5. Mshauri: Caroline Kivenule
Donati Mhapa
Daniel Kivenule
Kamati hii itashughulikia majukumu yote ya maandalizi ya mkutano mkuu na shughuli zote za maandalizi ndani ya Kidamali na vijiji vya karibu. Itasimamia usambazaji wa barua za mialiko pamoja na za michango mbalimbali, usambazaji wa kadi za michango, ukusanyaji wa michango pamoja na kutekeleza majukumu mengine ambayo Kamati hizi mbili zitakuwa zimeshauriana. Kamati hii itafanya kazi chini ya uongozi ulioundwa na kutekeleza majukumu waliyokubaliana katika vikao vyao.
B: MAJUKUMU YA KAMATI ZOTE MBILI
1. Kusambaza barua za mwaliko pamoja na maombi mengine kama michango nk. Kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Ukoo pale zitakapohitajika.
2. Kuratibu shughuli zote za Ukusanyaji wa Michango
3. Kuandaa mikutano mbalimbali za maandalizi kwa kushirikisha ndugu mbalimbali wanaoishi sehemu tofauti. Mfano kwa Dar es Salaam kuna ndugu toka Kidamale, Ilole, Nduli na Ilula nk.
4. Kuhamasisha Wanaukoo waishio kijijini Kidamali, Ilole, Nduli, Ilula na sehemu nyinginezo hapa Tanzania kuhusiana na umuhimu wa kuwepo kwa mkutano huo pia kutoa ushirikiano wa hali na mali katika zoezi zima la maandalizi.
5. Kuandaa Mpango wa Kazi wa Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo
- Kufanya vikao mbalimbali vya Kamati ya Maandalizi vitakavyoshirikisha Kamati zote mbili ya Kidamali na Dar es Salaam.
- Kuwajulisha walengwa (Ndugu) umuhimu wa kujali muda wa kukusanya michango. Kwa mfano kuwaeleza Mwisho wa Ukusanyaji wa Michango (Mara baada ya kupata Barua na Kadi).
- Kuwashirikisha wadau wengine wasio ndugu katika kampeni za kukusanya michango. Mfano kuwaomba michango Wabunge, Madiwani, Maaskofu na watu wengine muhimu katika jamii zetu.
C: ORODHA YA UKOO WA AKINA KIVENULE WAISHIO DAR ES SALAAM
1. Edgar Kivenule (Mwenge Flats)
2. Innocent Kivenule (Ubungo Jeshini)
3. Athuman Mtono (Kibamba)
4. Adam Kivenule (Ubungo Kibangu)
5. Christian Kivenule (Matombo – Morogoro)
6. Philemon Kivenule (Buguruni) 0744 029880
7. Flora Kivenule (Mabibo Sahara)
8. Ignas Kivenule (Tabata Shule)
9. Sabina Mhapa (Buruguruni)
10. Mama Tamasha (Ubungo Kibangu)
11. Raphael Kivenule (Mbezi – Club Oasis)
12. Monica Kivenule (Zanaki Street)
13. Priskusi Kivenule (Mbezi Juu)
14. Michael Mhapa (Ubungo Kibangu)
15. Regina Mapembe (Kinondoni)
16. Evaristo Mapembe (Tabata)
17. Nuhu Mtono (Mabibo)
18. Hamidu Mtono (Mabibo)
19. Sijali Kivenule Kisukuli
20. Alexander Nyangalima (Morogoro)
21. Flomina Kivenule (Mbezi)
22. Fred Mapembe (Tabata)
23. Thabit Mtono (Kigamboni)
D: ORODHA YA UKOO WA AKINA KIVENULE WAISHIO NJE YA DAR ES
SALAAM NA KIDAMALE
1. Alphonce Kivenule (Ludewa)
2. John Kivenule (Kilombero)
3. Zavery Kivenule (Igowole/Sadani)
4. Lizeta Kivenule (Dodoma)
5. Victoria Kivenule (Dodoma)
6. Goretha Kivenule (Mtera)
7. Asia Kivenule (Morogoro)
8. Irene Kivenule ( )
9. Furaha Kivenule ( )
10. Bakita Kivenule (Mafinga)
11. Emmanuel Kivenule ( )
12. Agatha Kivenule (Dodoma)
13. Florian Kivenule (Mafinga)
E: RATIBA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
Mahali pa kufanyia Mkutano: _____________________________________
Tarehe: 17 – 18 Desemba 2005
Washiriki: Ukoo Wote wa Kivenule na Wageni Waalikwa
Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE | ||
Muda | Shughuli/Jukumu | Wahusika |
12:00–12:45 | Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano | Wote |
12:45–1:45 | Kupata Kifungua Kinywa | Wote |
1:45 – 2:45 | Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili | Wote |
2:45 – 3:15 | Ufunguzi wa Mkutano na Mgeni Rasmi | Mgeni Rasmi |
3:15 – 4:00 | Utambulisho baina wa wana Ndugu | Wote |
4:00 – 4:45 | Pumziko la Chai / Kahawa/Maji | Wote |
4:45 – 5:30 | Mada ya Kwanza: HISTORIA YA UKOO | Mtoa Mada na Mkubwa wa Ukoo |
5:30 – 6:00 | Majadiliano katika Makundi | Makundi 4 |
6:00 – 6:20 | Murejesho na Majumuisho | Mwezeshaji |
6:30 – 8:00 | CHAKULA CHA MCHANA | Wote |
8:00 – 8:45 | Mada ya Pili: MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO WA KIVENULE | Mtoa MADA (…………………) |
8:45 – 9:15 | Majadiliano katika Makundi | Makundi 4 |
9:15 – 9:45 | Murejesho na Majumuisho | Mwezeshaji |
9:45– 10:45 | Pumziko la Chai/Kahawa/Maji | Wote |
10:45-1:30 Usiku | Mapumziko Marefu (Kusalimiana na Kufahamiana zaidi) | Ndugu na Wageni Wote |
1:30 – 2:30 | Chakula cha Usiku na Vinjwaji | Ndugu Wote |
2:30 – 6:30 | Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili) | Wote |
Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE | ||
Muda | Shughuli/Jukumu | Wahusika |
12:00– 12:45 | Kuamuka na Kufanya Maandalizi ya Mkutano | Wote |
12:45 – 1:45 | Kifungua Kinywa | Wote |
1:45 – 2:15 | Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili | Ndugu wote |
2:15 – 2:45 | Mada Ya Tatu: ELIMU NA MUSTAKABILI WA UKOO WA KIVENULE | Mtoa Mada |
2:45 – 3:15 | Majadiliano kwenye Makundi | Makundi 4 |
3:15 – 3:45 | Murejesho na Majumuisho | Kiongozi wa Kundi na Mwezeshaji |
3:45 – 4:30 | Pumziko la Chai/Kahawa/Maji | Wote |
4:30 – 5:00 | Mada ya Nne: UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE | Mtoa Mada |
5:00 – 5:30 | Majadiliano kwenye Makundi | Makundi 4 |
5:30 – 6:00 | Murejesho na Majumuisho | Kiongozi wa Kundi na Mwezeshaji |
6:00 – 7:15 | CHAKULA CHA MCHANA | Wote |
7:15 – 7:45 | Mada ya Tano: DINI KATIKA UKOO | Mtoa Mada |
7:45 – 8:15 | Majadiliano kwenye Makundi | Makundi 4 |
8:15 – 8:45 | Murejesho na Majumuisho | |
8:45 – 9:45 | Majumuisho:1. Yote Yaliyojitokeza2. Matarajio 3. Tarehe ya Mkutano Mwingine | Mwezeshaji |
9:45 – 10:15 | Shukurani toka kwa Ndugu Mbalimbali | |
10:15–11:00 | KUCHAGUA VIONGOZI WA KUUNDA KAMATI YA UKOO | Ndugu Wote |
11:00 | Kufunga Mkutano | Viongozi wa Kamati ya Ukoo |
F: WAWEZESHAJI WA MADA (FACILITATORS)
1. Agatha Mhapa
2. Alphonce Kivenule
3. Lizeta Kivenule
4. Ignas Kivenule
5. Siha Kivenule
6. Christian Kivenule
7. Adam Kivenule
8. Justin Kivenule
9. Donath Mhapa
10. John Kivenule
11. Victoria Kivenule
12. Edger Kivenule
13. Piera Kivenule
14. Florian Kivenule
15. Innocent Kivenule
16. Stephen Mhapa
17. Severin Nyangalima
G: WAHUDUMU: CHAKULA, CHAI/KAHAWA NA VINYWAJI
1. Rahel Chambula
2. Asia Kivenule
3. Germana Mhapa
4. Mrs. Justin
5. Mrs. Jovin
6. Stewart Kivenule
7. George Kivenule
8. Janeth Kivenule
9. Frola Kivenule (Supervisor)
10. Jovin Kivenule
11. Mama Tamasha (Supervisor)
H: MAANDALIZI YA VIFAA VYA KUTUMIA
Vifaa | Idadi | Bei | Jumla |
1. Sahani: Bati (150) na Udongo (50) | 200 | | |
2. Vikombe: Plastiki (150) na Udongo (50) | 200 | | |
3. Vijiko | 200 | | |
4. Biki | 100 | | |
5. Mark Pen | 15 | | |
6. Glasi | 200 | | |
7. Radio + 2 MIC | 1* | | |
8. Flip Chart | | | |
9. Meza | 5 | | |
10. Viti + Fomu/Benji | 100 | | |
11. Video Picture Camera | 1 | | |
12. Still Picture Camera | 2 | | |
13. Tissue Paper | 20 | | |
14. Opener | 10 | | |
Jumla | | | |
I:CHAKULA
Vifaa | Idadi | Bei | Jumla |
15. Mchele | | | |
16. Mahindi (Unga) | Gunia 2 | | |
17. Viazi Mviringo | Gunia 1 | | |
18. Unga wa Ngano | | | |
19. Mafuta ya Kula (Alizeti) | Lita 40 | | |
20. Chumvi | Kgs 4 | | |
21. Appetizer (Kiongeza Mate) | Kopo 12 | | |
22. Maharage | Kgs 50 | | |
23. Mbuzi wa Nyama | 2 | | |
24. Nyama ya Ng’ombe | Kgs 100 | | |
25. Mboza Majani | Maf. 20 | | |
26.Sukari | Kgs 25 | | |
27. Majani+Iliki | ½ Dazani | | |
28. Viungo: Nyanya | Tenga 3 | | |
29. Viungo: Vitunguee | Debe 1 | | |
Jumla | | | |
J: VINYWAJI
Vifaa | Idadi | Bei | Jumla |
25. Soda | | | |
26. Bia | Kreti 10 | | |
27. Maji (Madogo) | Katoni 50 | | |
28. Pombe ya Kienyeji | Plastiki 10 | | |
29. Sufuria | | | |
30. Plastiki za Maji | | | |
31. Pipa | | | |
32. Bakuli za Mboga | | | |
33. Miiko | | | |
34. Kuni | Tela 1 | | |
35. Mkaa | Gunia 2 | | |
Jumla | | | |
K: MENGINEYO
Vifaa | Idadi | Bei | Jumla |
29. Kutangaza Mkutano | Poster 2, Vipeperushi | | |
30. Kutangaza Mkutano | Mwandishi wa Habari 1 | | |
31. Maua na Mapambo | | | |
| | | |
Jumla | | | |
L: MADA ZITAKAZOWASILISHWA KWENYE MKUTANO MKUU
1. HISTORIA YA UKOO
- Ukoo ni Nini na Unapatikanaje?
- Dhana ya Kuenea na Kukua kwa Ukoo.
- Mgawanyiko wa Ukoo (Chora Mchoro Kuonyesha Ukoo unavyoundwa).
- Kupotea kwa Ukoo.
2. MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
- Ukaribu wa Wana Ndugu.
- Ushirikiano Katika Nyanja Mbalimbali.
- Kutembeleana kama Sehemu ya Kudumisha Mahusiano.
- Kuondoa Tofauti na Kusaidiana.
3. ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
- Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu.
- Umuhimu wa Elimu.
- Dunia ya Utandawazi.
- Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika Ukoo Wetu.
4. UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
- UKIMWI ni nini?
- Namna gani UKIMWI unavyoenea/kuambukizwa?
- Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi?
- Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI.
5. DINI KATIKA UKOO
- Maana ya Dini
- Umuhimu wa Kuwa na Imani
- Maadili na Dini
- Ukoo Uliojengeka katika Misingi ya Dini
M: MADA ZA KUJADILI KWENYE MAKUNDI
Mada ya Kwanza: HISTORIA YA UKOO
· KUNDI LA KWANZA: Ukoo ni Nini na Unapatikana
· KUNDI LA PILI: Kuenea na Kukua kwa Ukoo
· KUNDI LA TATU: Mgawanyiko wa Ukoo (Chora Mchoro Kuonyesha Ukoo unavyoundwa)
· KUNDI LA NNE: Kupotea kwa Ukoo
Mada ya Pili: MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
· KUNDI LA KWANZA: Ukaribu wa Wana Ndugu
· KUNDI LA PILI: Ushirikiano Katika Nyanja Mbalimbali
· KUNDI LA TATU: Kutembeleana
· KUNDI LA NNE: Kuondoa Tofauti na Kusaidiana
Mada ya Tatu: ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
· KUNDI LA KWANZA: Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu
· KUNDI LA PILI: Umuhimu wa Elimu
· KUNDI LA TATU: Dunia ya Utandawazi
· KUNDI LA NNE: Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika Ukoo Wetu
Mada ya Nne: UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
· KUNDI LA KWANZA: UKIMWI ni nini?
· KUNDI LA PILI: Namna gani UKIMWI unavyoenea/kuambukizwa?
· KUNDI LA TATU: Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi?
· KUNDI LA NNE: Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la
UKIMWI.
Mada ya Tano: DINI KATIKA UKOO
· KUNDI LA KWANZA: Nini Maana ya Dini?
· KUNDI LA PILI: Umuhimu wa Kuwa na Imani
· KUNDI LA TATU: Maadili na Dini
· KUNDI LA NNE: Ukoo Uliojengeka katika Misingi ya Dini
N: MAAZIMIO YA MKUTANO
Licha ya kuwa na malengo na makusudia mbalimbali, pia tunategemea mwisho wa mkutano kutakuwa na mambo kadhaa ambayo yatakuwa ni makubaliano kutoka pande mbalimbali za ukoo wa Kivenule. Yote hayo kwa pamoja yatakuwa ni maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Kati ya Maazimio ambayo tunayategemea katika mkutano huo ni:
1. Kufanya Senza ya Ukoo wa Kivenule ili kupata idadi kamili ya ndugu.
2. Kuanzisha Mfuko wa Ukoo
3. Kuchagua Viongozi wa watakaounda Kamati ya Ukoo ya Kuratibu mambo mbalimbali ya ukoo. (Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina pamoja na viongozi wengine ambayo wana umuhimu na kupewa majukumu kuwepo).
4. Uongozi utakaoundwa kufanya mashauriano na usuluhishi wa matatizo mbalimbali ya ukoo yaliyojitokeza.
5. Kukusanya taarifa mbalimbali za ukoo
6. Kuangalia na Kutathmini usalama wa mali mbalimbali zinazomilikiwa na ukoo nk.
O: KAMATI MBALIMBALI ZITAKAZOUNDWA KUFANYA KAZI KABLA NA
WAKATI WA MKUTANO
1. Kamati ya Mapokezi
2. Kamati ya Malazi
3. Kamati ya Chakula
4. Kamati ya Vinywaji
5. Kamati ya Burudani
6. Kamati ya Usafiri
7. Kamati ya Ulinzi na Usalama
8. Huduma ya Kwanza
9. Kamati ya Uratibu wa Shughuli za Mkutano
P: VITAMBULISHO KWA AJILI YA MKUTANO MKUU WA UKOO
Kitambulisho kitakuwa na:
· Jina la Mkutano
· Jina:
· Tarehe Mkutano:
· Mahali Anapoishi:
No comments:
Post a Comment