TANGAZO LA MKUTANO
MKUTANO MKUU WA 10 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE - KAUKI
KAUKI NI NINI? Ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii inayounda umoja huu; hususani katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga, maradhi na utegemezi.
DIRA YA KAUKI: Ni kuwa na jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa kujitegemea
MAONO YA KAUKI: Ni kujengeana uwezo kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia mafunzo, kongamano, mijadala na mikutano
LENGO KUU LA KAUKI: Ni kuinua na kuboresha maisha ya wanaukoo, kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa kutumia ujuzi, maarifa na raslimali zinazotuzunguka. Mipango ya KAUKI inajikita katika kujiimarisha katika ngazi zote za kiutendaji, kiuendeshaji na kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kielimu, kisiasa, kimaendeleo na kimapinduzi.
MUUNDO WA KAUKI: KAUKI inaundwa na Kanda Sita za Kidamali, Irore, Nduli, Magubike, Mufindi na Dar eS Salaam. Mkutano Mkuu wa KAUKI hufanyika mara moja kila mwaka. Pia kuna mikutano ya Kamati ya Utendaji. Kuna Uongozi wa KAUKI na Viongozi wa Kanda.
MAHALI UNAPOFANYIKA MKUTANO: Kanda ya Kidamali, Iringa Vijijini
TAREHE YA MKUTANO: Jumamosi na Jumapili ya tarehe 28 - 29 Juni 2014
WAALIKWA KWENYE MKUTANO: Ndugu, Wanaukoo, Wageni Waalikwa na Wadau wa Maendeleo
MAHITAJI YA MKUTANO: Chakula, Maji, Kalamu, Daftari, Chati Mgeuzo, Makapeni na Manila
OMBI LA MICHANGO: KAUKI inaomba michango ya Fedha Taslimu, Nafaka (Mahindi, Unga, Maharage, Kunde, Karanga, Mchele); Mifugo (Kuku, Bata, Mbuzi nk); Kuni; Mkaa; Mafuta ya Kula; Mafuta ya Taa; Chumvi, Sukari, Unga wa Ngano Nk.
TAARIFA NA MAWASILIANO: Simu: 0755914505, 0714 146382, 0787 843561, 0713 270364, 0755293193
Tovuti: www.tagumtwa.blogoak.com / www.kauki-kauki.blogspot.com / www.tagumtwafoundation.wetpaint.com / www.facebook.com/tagumtwa Barua pepe: tagumtwa@gmail.com / kauki2006@gmail.com / tagumtwa.kauki@gmail.com
Mawasiliano Kanda ya Kidamali | | UONGOZI WA KAUKI |
Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI 1. George S. Kivenule-Mwenyekiti wa Kamati-0755914505 2. Jovin S. Kivenule - Katibu wa Kamati- 0754026106 3. Faustino Kivenule-Mwenyekiti KAUKI- 0755293193 4. Justin D. Kivenule-Mweka Hazina- 0787 843561 | | Faustino Sigatambule Kivenule -Mwenyekiti 0755293193 |
| Adam A. Kivenule -Katibu Mkuu 0713 270364 | |
| Christian J. Kivenule -Makamu Mwenyekiti 0714 146382 | |
| Justin D. Kivenule -Mweka Hazina-0787 843561 Vitus Nzala -Katibu Msaidizi - 0788282046 E-mail: KAUKI2006@gmail.com www.kauki-kauki.blogspot.com | |
| |
No comments:
Post a Comment