Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Wednesday, 30 January 2013

CHANGAMOTO YA KUWA NA MAKAZI BINAFSI

SEHEMU YA KWANZA
Watanzania wengi wamejenga makazi yao ya kudumu kwa namna ambayo hata ukielezwa huwezi kuamini kuwa mtu wa kawaida anaweza kujenga. Uzoefu unaonesha kuwa, ujenzi wa nyumba hufanyika kwa kupata mkopo toka benki, mahali pa kazi au kwa kwa mtu yeyote mwingine mwenye pata kubwa.

Mishahara ya wafanyakazi walio wengi ni aghalabu kumudu gharama za ujenzi wa nyumba. Kwa mara nyingi mishahara hiyo ni midogo sana. Ukiangalia tu kima cha chini cha mshahara ni kweli kabisa mtu hawezi kununua kiwanja au kujenga nyumba. 

Mathalani, thamani ya kiwanja kilichopimwa na serikali ni kubwa mno, achilia mbali viwanja ambavyo vinauzwa na watu binafsi. Ukigusa kiwanja unaambiwa mamilioni ya pesa. Kwa wengi wetu tumekata kabisa tamaa ya kuendelea kutafuta viwanjwa au kufikiria kununua viwanja. Unajiuliza, kula tu ni kwa shinda, kweli nitamudu kununua kiwanja na kujenga?

Kila mmoja wetu hujiuliza. Binafsi nimepatwa na changamoto kubwa katika kufikiria hatua ya kufikiria kuwa na kiwanja changu, na pengine kuwa na nyumba kabisa. Kwa jamii ya Kitanzania ambayo kwa kiwango kikubwa imegubikwa na umaskini wa kupindukia, wanajitahidi kupambana ili angalau waweze kupata mahali pa kudumu pa kuishi. Mchakato wa kutafuta kiwanja hadi kujenga huchukua miaka kadhaa kuanzia miaka mitano hadi kumi na pengine kuzidi kumi. Inategemea aina ya shughuli ambayo inamwingizia kipata mtu yule. 

Kwa sasa kuna mambo mengi ambayo yanawanya watu kuyafikiria katika mchakato wa ujenzi au ununuzi wa viwanja. Mmojawapo ni kujiunga na vikundi vya mikopo. Wapo wengine ambao hufikiria dili au safari za kikazi ambapo wana fursa ya kupata kipata kikubwa kidogo ambacho mara nyingi huwa nje ya bajeti. 

Sehemu ijayo, nitaendelea kuelezea changamoto mbalimbali ambazo zinawapata wananchi wa kawaida (maskini katika kutafututa viwanja na kujenga; pia tutaangalia hatari ya mwongezeko wa msongamano katika makazi haya mapya).







































































TUZIPENDE MBUGA ZETU JAPO TUDHULUMIWA NA WENYE MAMLAKA

Tanzania ni nchi ambayo kwa miaka mingi ilijaliwa kuwa na raslimali nyingi na za kuvutia zikiwemo mbuga za wanyama. Kwa sasa hali ni tofauti kwa sababu ujangili unaofanywa na watendaji na viongozi wa nchi ya Tanzania unaendelea kuziangamiza mbuga zetu. Mfano mzuri tu kuendelea kukamatwa kwa nyara za serikali zinazojumuisha pembe na meno ya Tembo, hali inayotishia kutoweka kwa viumbe hawa wa kuvutia.

PINDA AONGEA NA MAIMAMU MTWARA



WAZIRI MKUU PINDA MKONI MTWARA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizunguma na Maimamu wa mkoa wa Mtwara kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa veta mjini Mtwara Januari 27, 2013

HATIMAYE LULU AACHIWA HURU KWA DHAMANA



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba Aprili 7, 2012 bila kukusudia baada ya kukamilisha taratibu zote za dhamana

Angalia picha Matukio Jana Hiyoooo!!!
Lulu kushoto akiwa na mama yake ndani ya gari baada ya kupata dhamana jana, Januari 29, 2013

Lulu (katikati) akitoka eneo la mahakama baada ya kukamilisha dhamana yake.

Kutoka kushoto ni mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, wakili wa Lulu bwana Kibatala na Dk. Cheni wakijadili jambo wakati wakisubiri dhamana ya Lulu.

Lulu akiingia katika chumba cha msajili wa mahakama ili kukamilisha dhamana yake.

Gari lililombeba Lulu likiondoka mahakamani.

Lulu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata dhamana leo.

Add caption

  


WAZIRI MKUU PINDA MKONI MTWARA



Mheshiwa Pinda Ziarani Mtwara Kutafuta Suluhu ya Mgogoro wa Raslimali Gesi na Wananchi wa Huko

Je atamudu kunasua kitendawili hiki, Gesi Kwanza, Uhai Baadaye!!!


Angalia Picha za Matukio




 

MGOGORO WA GESI MTWARA, NINI CHANZO CHAKE



Kwa kile kinachoaminika kuwa ni kukua kwa MGOGORO WA GESI Mkoani Mtwara na Kusini kwa ujumla, usiku wa kuamkia leo Mahakama ya Mwanzo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani imeteketezwa kwa moto huku nyumba ya Mbunge Hawa Gasia ikivunjwa vioo na kuchomwa motto wakati ile ya Mwenyekiti wa CCM Mtwara, ndugu Sinani ikiwa imevunjwa tu vioo.

Chanzo hasa cha vurugu hizo haziko wazi lakini wengi wanazihusisha na sakata la GESI kwani Hawa Gasia na Sinani wamekuwa kwa Muda Mrefu wakishutumiwa kwa kuchochea na kuridhia usafirishaji wa gesi hiyo kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam. Uchomaji huo wa moto uliambatana na vurugu na ulipuaji wa mabomu ya machozi kutoka kwa polisi na hadi wakafanikiwa kuzima jaribio la uchomaji wa Kituo cha Polisi cha Shangani.

Wakati huohuo kuna taarifa kutoka Masasi zikieleza nako kuibuka tukio la chomachoma mchana huu wa leo ikihusisha uchomwaji wa Offisi za Serikali, Polisi, nyumba za Wabunge na Offisi za CCM. Hali ya Masasi inaelezwa kuwa ni tete zaidi kuliko ilivyokuwa hapa Mtwara Mjini usiku wa jana ingawaje napo palikuwa na kimuhemuhe cha mabomu ya machozi kutoka kwa polisi.

Bado mpaka sasa haileweki ni nini hasa hatma ya mgogoro huu, maana kwa upande wake Serikali inaonekana kushikilia msimamo wake uleule wa kutaka kusafirisha gesi hiyo wakati upande wa raia wakiwa na msimao wao wa GESI KWANZA MAISHA BAADAYE, kwa maana kutoridhia usafirishaji wa gesi hiyo ikiwa ghafi kupelekwa Dar es Salaam.

PICHA ZA MATUKIO SIKU HIYO YA MAPAMBANO YA KUDAI GESI





 







 salaam.